Wabongo nomaaaaa

One time nilienda kwenye ofisi moja ipo pale mlimani (sijui bado wapo) ka laptop kangu kalikua na shda,

ofisi yao yaani ni full A/C, ni imepambwa kweeeeeli, neno solution kila kona, nikawelezea shida ya pc yangu kijana moja pale anaonekana ananiskiliza kwa umakini yaani smart kweliiii

sasa bwana tukawasha ka pc kangu, fundi akaangalia pale, akazunguka zunguka pale weee, nikaona kachukua ka iphone six kake kaingia YOTUBE akanza kusearch ile meseji inayo desplay pale kwenye pc yangu

kafuatilizia maelekezo kaanza kuya apply kwenye pc yangu, ikashindikana, akaendelea ku scrow chini, anaangalia video tofauti tofauti mwisho akanambia we nenda utarudi kesho!!



Nikamwambia haya, nkaondoka. Kesho yake nimerudi shida iko pale pale!! Sasa wakati ananipanga mwenzie akamwambia hem cheki hii video (yotube)
Akajalibu ile meseji ikapotea,



nikalipa nikazima nikaondoka, nimefika nyumbani kuwasha tu, meseji hiyoooo


nikaona isiwe tabu nikaingia youtube na mie


mpaka nikatibu mwenyewe. So bongo tunamafundi IT wa YOUTUBE kibao



