Kwa professionals mara nyingi kama unajua unachofanya na kazi yako inaeleweka pia utakuwa unajua thamani yako kwenye soko kwa hiyo ni vigumu sana kumpata mtu anayajua anachifanya kwa bei chee, now sijui size ya hiyo kazi na sijui kama hiyo hela ni ndogo au kubwa lakini tunasema "You get what you pay for".
Hela ndogo pia inamweka hata mtu ambaye ni competent kwenye hali ngumu, atumie muda wake kwenye project yako ambayo hailipi au afanya minimum effort huku akiendelea kutaffuta na kufanyia kazi project za maana zaidi.
Kosa kubwa zaidi ni jamaa ametoa kazi bila kufanya due diligence yake mwenyewe, hao jamaa aliwatoa wapi? Alichunguza kazi gani ambayo walifanya previously? Alipata recomendations zozote kutoka wateja wa hao jamaa ambao walifanyiwa kazi before etc.
Na cha muhimu zaidi labda hajamanage hiyo project vizuri, sio sawa kuwapa watu kazi na hela kisha kukimbia miezi sita, alitakiwa aweke "milestones" katika utekelezaji wa hiyo kazi mpaka iishe, na nakuhakikishia baada ya kuchemka mara ya kwanza hakuenda Rwanda na kugawa tu kazi kisha kupotea miezi, lazima alijipanga vizuri zaidi katika kuwachagua na kuwasimammia hao watu.