Wataalamu wa IT wa Tanzania ni 'zero' kabisa

Wataalamu wa IT wa Tanzania ni 'zero' kabisa

Umeshaambiwa ni mwanasheria kazi yake ni kumeza..
Hata kama kasoma zote 12, language alizofanyia project sidhani kama zinafika nne.
Na kusoma language 12 kwa ajili ya vyeti na si project ni rahisi b'coz
ukijua c(structual programing language)na Java(or any oop language) ni rahisi kusoma
language yeyote hata mia na si maajabu.. maajabu ni kama zote 12 amefanyia project za kueleweka.
Alikuwa anakodi wakati anasoma Sheria.
 
Sio kwaba siwezi ingia advanced. Mimi sio mtaalamu wa IT nina general knowledge tu ya vitu. That time natafuta vyuo nilijiuliza kwanini website ya chuo ifichwe wakati website za CIA naingia nasoma kilichopo. Vipi hapa sio mapungufu kwenye security ya system?
Haijafichwa. Ni SSL cerificate ime expire na hawajlipia ku renew. So browser yako inajaribu kukulinda maana imeshindwa ku verify cerificate ambayo ina security implications
 
Wewe jamaa wewe ulitafuta cheap labour ndio maana. Mbona kuna kampuni kibao hapo bongo wanatoa program/product bora kabisa. Nafikiri ubahili umewapa kazia hiyo...kuna kampuni hadi za kihindi ziko poa...ungekosa ungeenda kwa wataalamu UDOM, UDMS au DIT wangekuunganisha na watu wa uhakika
 
Wewe jamaa wewe ulitafuta cheap labour ndio maana. Mbona kuna kampuni kibao hapo bongo wanatoa program/product bora kabisa. Nafikiri ubahili umewapa kazia hiyo...kuna kampuni hadi za kihindi ziko poa...ungekosa ungeenda kwa wataalamu UDOM, UDMS au DIT wangekuunganisha na watu wa uhakika
UDSM/UDOM/DIT developer? Una utani wewe. Hao wote wanalalamikiwa si wa huko huko? Yaani tha max sasa ivi naweza lipa kwa IT wa TZ ni 200,000 tu ya bando ya kugoogle na soda.
 
UDSM/UDOM/DIT developer? Una utani wewe. Hao wote wanalalamikiwa si wa huko huko? Yaani tha max sasa ivi naweza lipa kwa IT wa TZ ni 200,000 tu ya bando ya kugoogle na soda.
IT wa Kenya malipo unaweza kumlipa ngapi
IT wa Rwanda?
IT wa India?

Nataka kufanya tu comparison ya IT wa Bongo aka zero na ma IT wenye akili zao huko!
 
Naandika kwa uchungu sana. Nilipewa instructions ya kutafuta kampuni ya IT hapa Tz kudisign app na web kwa ajili ya masuala fulani fulani. Nikawacheck jamaa fulani ni IT wazuri tu (kwa mjibu wao na ka kampuni kao uchwara) na mmoja kasoma US mwingine China. Nikawapa 15,000,000/= waanze kazi. Hii ni baadhi ya malipo ya awali.

Miezi mi4 hakuna feedback. Tukasema tusubiri labda jamaa wako kazini. Miezi 6 hola. Miezi 12 hola. Huku na huku nikapigiwa simu kazi tayari. Nikasema poa. So nilikuwa mbali. Nikamtafuta software engineer ni mkenya afanye testing. Aisee jamaa alicheka sana. Ikasema hao vijana wamegoogle templates wameedit na kupachika na ni bogus development.

Idea ilikuwa kuwa na software inayotrace magari ya kumpuni, yako wapi, yametembea kilo ngapi and other staffs-Real time data.

Wakaishia kutengeneza utopolo tu. I guess wako humu pia. Ilibidi tulipe upya tukapeleka project Rwanda. Vijana wamedesign from scratch na within 4 month wamekabidhi kazi.

Sasa naelewa kwa nini watu hawataki kuwekeza kwenye IT Bongo. Ujinga mtupu. Hawa vijana wetu wafuge tu kuku kwa kweli. Hivi nyie ndo mtaweza hata kushindana na Bolt+uber?.

Anyway sijui CS/IT mnafundishwa nn huko vyuoni. Natamani kujua mitaala yenu.

100% disappointed.
Kutengeneza Barabara DSM mpaka Mwanza hawezi kupewa MTU mmoja.. na kwenye programming ni hivyohivyo
 
Labda alitumia madalali?
Wataalamu wa IT wapo, tatizo lao labda hawajitangazi na tatizo lingine la wateja ni kutumia single source pekee badala ya kutangaza tender ili wachague wenye weledi.
Mfano ni kuwa Project ya mleta Mada ilihitaji combination ya IT experts na pengine cost yake ni kubwa kuliko alivyopatana na IT wake,hivyo kupata product nusu/robo..
 
Je ukitumia hiyo "reuse" usalama wake upoje?
Kwenye software development model zipo tatu..
Waterfall model hii ina tumika kwa critical software i.e kwenye ndege, hospital, car break system nk.
Agile model hii nayo inatumika kwa software zinazo evolve na zinahitaji freuntly feedback from user kama windows nk,
Kutumia Intergration and configuration model haina maana kwamba hutafanya modification.
Utaimodify kulingana na mahitaji yako katika angle yeyote ile hata kwenye security ndio maana ya configuration.
 
UDSM/UDOM/DIT developer? Una utani wewe. Hao wote wanalalamikiwa si wa huko huko? Yaani tha max sasa ivi naweza lipa kwa IT wa TZ ni 200,000 tu ya bando ya kugoogle na soda.
Shida ya watu wengi wanadhani kila IT ana interest au anatakiwa kufanya programming.
Kuna watu hata class wanakomaa na Network tu, Graphics, webmaster, system developer, troubleshooting and mantainance wengine security na wengine kupata degree au diploma tu amalize chuo kama zilivo course nyingi.
Mtu anataka IT awe nondo kote hicho kitu ni kigumu.
Ukimwambia huwezi kimoja kati ya hivo anakuona mzururaji.
 
Ni ipi tofauti kati ya Ku-Code from Scratch na ku-out sources templates kutoka sehemu...katika out put ya platform husika si vilevile tu.

Sasa si bora uchukue templates sehemu.
 
Kuna mambo kadhaa yanayotufanya wasomi wa Tz tufike Huku
1.kudharau taaluma za wengne ( hapa unakuta Mtu anakwambia u-IT Kwan unadhan mgumu basi ukijua code na app flan kaz yyte unafany…)
2.kutokuheshimu taaluma yako,
3.Tamaa ya pesa za haraka ( shortcuts)na
4.Ujuaji mwingi ( unakut mtu hajasomea mambo ya hospitality lakin naye anajifanya anatak kupokea watalii mwisho wasiku tunawapoteza )…jmn kila kaz ina ethics zake angalau pata basics ya kile unachotaka kufanya .

Hivi vyote vimetufanya watanzania nje ya nchi tutambulike wasanii (watu waongo) na hata hapa ndan tumekua tukifanya kazi za hovyo ..na sio passion ya kuendelea mbele.
Ni ngumu sana kumpa mtu kazi akasema haiwezi aidha atakwambia anaiweza au atakutafutia mtu anayeiweza na nyuma ya pazia wanaenda kuoogle huko bila kutambua u-serious wa kazi. .
 
12 programming languages namashaka nayo. Developer hata awe senior, language ambazo anazozijua comprehensively zikiwa nyingi ni 5-6. Ukizidisha hapo unakua half baked, unazijua lakini juu juu sana.

Naweza nikarekebishwa kwasababu mimi ni junior dev.
For average serious developer kujua language zaidi ya 3 ni uongo, but it possible kua na vyeti hata vi nne for single language.
mfano unaweza kuta language moja ina level ya associate ambayo inahitaji 2 exams, professional ina 2 exam na master ina exams. kila exams ina cheti chake, kwahiyo hapo kuimasta hiyo language unaihitaji 5+ certificates. mfano mwingine watu wa networking e.g. Cisco unakuta mtu ana certification kama 8 hivi lakini for Cisco tu, ukimpa Juniper, huawei et al. ni mweupe
 
Shida ni ccm imeharibu vijana siku hizi wanashinda mitandaoni kutengeza urafiki na viongozi ili wapate kujulikana na uteuzi.(uchawa).
 
Mimi naona unawalaumu IT wa bongo bure.. maana hao ulio wapa kazi elimu yao wameichukulia China na USA. Huenda huko ndo walifundishwa utopolo hoja yako ingekuwa na mashiko kama kweli kijana wetu wa Udsm au UDom kashindwa kufanya hiyo kazi . Mm naona ungelaumu elimu ya china na usa ila sio wabongo
 
Mimi naona unawalaumu IT wa bongo bure.. maana hao ulio wapa kazi elimu yao wameichukulia China na USA. Huenda huko ndo walifundishwa utopolo hoja yako ingekuwa na mashiko kama kweli kijana wetu wa Udsm au UDom kashindwa kufanya hiyo kazi . Mm naona ungelaumu elimu ya china na usa ila sio wabongo
Hao vijana CV zao ni kuwa digrii wamesomea bongo. Wanahusika vile vile.
 
Back
Top Bottom