Wataalam wa Mazingira: Kwanini kuna huduma za kijamii (Shule, Polisi, Hospitali) za kata lakini hakuna hifadhi ya misitu/miti (Mapafu) kwa ngazi hiyo?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,318
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu Watanzania wataalam wa mazingira eti;

Kwanini kuna huduma za kijamii (shule, polisi, hospitali) za kata lakini hakuna hifadhi ya misitu (mapafu ya hewa safi) kwa ngazi ya hiyo?

Au hiyo hifadhi maalum ya misitu kwa ngazi ya kata ipo lakini mimi ndio sijui?

images (1).jpg

KWA UFUPI KUHUSU MSITU WA AMAZON (MAPAFU YA DUNIA)

==========

The Amazon (Msitu wa Amazon) is often referred to as Earth's 'lungs,' because its vast forests release oxygen and store carbon dioxide, a heat-trapping gas that is a major cause of global warming.

Msitu wa Amazon ndio msitu mkubwa zaidi duniani unaopatikana huko America kusini. Msitu huu una eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 5,500,000 ( Milioni 5) yani kwa ukubwa huu nchi ya TANZANIA iingie mara 6 kwenye msitu huo.

images.jpg

Msitu wa Amazon unakadiriwa kuwa na miti billion 400 na aina mbalimbali za miti zaidi ya 160,000 pia kuna miti ya matunda tofauti tofauti elfu tatu katika msitu huo.

Asilimia 20% ya oxygen iliyopo dunia inatengenezwa katika msitu wa amazon ndio maana unaitwa mapafu ya dunia.
==========

Kwanini huduma nyingi za kijamii (shule, polisi, hospitali) zimeteremshwa kutoka ngazi ya Taifa, Mkoa, Wilaya, Tarafa, Kata isipokuwa huduma hii ya kuwa na hifadhi nzuri za msitu (Mapafu ya hewa safi)?

images (3).jpg

Kama watu huwa wanafidiwa mali zao ili kupisha miradi ya maendeleo, kwanini sehemu zenye mbanano kama Magomeni, Manzese, Mbagala, Tandale kusifanyike fidia hizi ili kupata eneo kuwa la kujenga haya mapafu ya hewa safi walau ngazi ya kata tu?

MSAADA PLEASE: Ni miti gani mizuri mtu anaweza kupanda pasipo mizizi yake kuleta madhara kwenye msingi wa nyumba?

WATAALAM WA MAZINGIRA NA MIPANGO MIJI MSIPITE PASIPO KUCHANGIA CHOCHOTE TAFADHALI.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Infantry Soldier 〜 A True Patriot 〜
 
Kuanzia leo jua zaidi ya 70% ya dawa zote duniani inatokana na sumu ya nyoka. Madawa ya kisasa zaidi ya 70% yanatengenezwa na sumu ya nyoka.

Galon (5litres) Sumu ya nyoka kwenye soko la dunia ni karibu 5 billion
 
Kwa level ya kata inatosha kabisa. Au we ulitakaje kwa mfano kata ya Gerezani (kariakoo) pale hifadhi ingekua wapi
 
Zipo kiongozi. .Kwenye Wildlife wanaita WMA (Wildlife management Areas) zinakuwa managed na vijiji na pia wao wanakuwa wanufaika wakuu wa mradi hiyo kama Wamimbiki.

Suala la forests conservation ngaz ya vijiji imefanywa sana na Pinda kwenye masuala ya ulimaji wa asali.

Kingine lazima ujue changamoto ndio uzungumze ufanano.

Huku kuna kipind Norway ilikuwa na mradi wa kulipa kila mti unaopandwa.

Tatuzo likaonekana kutakuwa na ukosef wa chakula watu Waka mute.

Matumizi ya gas asilia na Rea ni moja ya mikakati
 
Infantry soldier huko sawa kabisa. Upandaji miti hautiliwi maanani kwa sasa. Miti inahitajika sana lakini hakuna msisitizo kwa sasa. Chuo Kikuu Dodoma hawajawahi kupanda msitu maeneo yale. Miaka zaidi ya kumi tangu chuo kianzishwe imepita.

Kuna kata nyingi hazina misitu hata kuhamasisha wanaopata viwanja kupanda miri hakuna. Vijiji na mitaa sioni wakiwa na mipango endelevu ya kupanda miti. TUJISAHIHISHE
 
Sawa mkuu, kwa hiyo hizo WMA zinaanzia ngazi ya kijiji na sio kata?...
Hapa sielewi kata inaundwa na vijijiji vingapi.....Tatizo Sheria zetu za umiliki ardhi vijiji na mijini bado ni mali ya waziri na Rais, na mwenye mamlaka ya mwisho ni hao watu... sasa suala la utunzaji mazingira siasa yake ni shida sana... nimewahi fanya kaz vijijini na shirika moja najua migogoro ya hii kitu inavogharim maisha ya watu.. tuishie hapa tafadhali.
 
Moja ya kada inayo dharaulika hapa Tz ni hiyo ya kukifanya mtu wa mazingira.... Kitu kibaya zaid ata pary ya urban planning pia hatujali tz, dsm nafikir zaid ya 70% ya makaz ni unplanned, yaan Tz kumiliki jiwanja kilicho pimwa ni expensive sembuse mazingira
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu Watanzania wataalam wa mazingira eti;

Kwanini kuna huduma za kijamii (shule, polisi, hospitali) za kata lakini hakuna hifadhi ya misitu (mapafu ya hewa safi) kwa ngazi ya hiyo?

Au hiyo hifadhi maalum ya misitu kwa ngazi ya kata ipo lakini mimi ndio sijui?

View attachment 1588612

KWA UFUPI KUHUSU MSITU WA AMAZON (MAPAFU YA DUNIA)

==========

The Amazon (Msitu wa Amazon) is often referred to as Earth's 'lungs,' because its vast forests release oxygen and store carbon dioxide, a heat-trapping gas that is a major cause of global warming.

Msitu wa Amazon ndio msitu mkubwa zaidi duniani unaopatikana huko America kusini. Msitu huu una eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 5,500,000 ( Milioni 5) yani kwa ukubwa huu nchi ya TANZANIA iingie mara 6 kwenye msitu huo.

View attachment 1588819

Msitu wa Amazon unakadiriwa kuwa na miti billion 400 na aina mbalimbali za miti zaidi ya 160,000 pia kuna miti ya matunda tofauti tofauti elfu tatu katika msitu huo.

Asilimia 20% ya oxygen iliyopo dunia inatengenezwa katika msitu wa amazon ndio maana unaitwa mapafu ya dunia.
==========

Kwanini huduma nyingi za kijamii (shule, polisi, hospitali) zimeteremshwa kutoka ngazi ya Taifa, Mkoa, Wilaya, Tarafa, Kata isipokuwa huduma hii ya kuwa na hifadhi nzuri za msitu (Mapafu ya hewa safi)?

View attachment 1588820

WATAALAM WA MAZINGIRA NA MIPANGO MIJI MSIPITE PASIPO KUCHANGIA CHOCHOTE TAFADHALI.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Mapafu ya kata ni muhimu sana kujikinga na kansa.
 
Naamin ngazi ya kata kwa tz bado na pengine hawajalikuwa ktk mpango... Mf. Kama watu wanauza au wanajenga ktk viwanja vya michezo au maeneo ya wazi yaliyotengwa, watakuwa na akili ya kuwa na maeneo ya hifadhi ya miti?

Baadhi ya wilaya hizo hifadhi zipo... Pia maeneo mengi ya shule, hospitali, na maeneo ya ofisi za serikali walikuwa na utaratibu wa kupanda miti ktk siku ya miti Sina uhakika Kama huo utaratibu bado upo..
 
Back
Top Bottom