Mbunge Reuben Nhamanilo Aiomba Serikali Kuongeza Nguvu kwa Wananchi katika Ujenzi wa Shule za Msingi Handeni Mjini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942
"Je, ni lini Serikali itamaliza mgogoro wa mpaka kati ya Handeni na Kilindi katika eneo la Bondo" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini

"Serikali imekwishatatua mgogoro wa mpaka kati ya Halmashauri ya Handeni na Kilindi katika eneo la Bondo kwa maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga kwenye kikao cha tarehe 25 Julai, 2023" - Mhe. Dkt. Festo Dugange, Naibu Waziri TAMISEMI

"Timu ya Wataalam wa Ardhi, wajumbe wa Kamati za ulinzi na usalama wa Wilaya na viongozi ngazi ya Tarafa, Kata na Vijiji wa Halmashauri ya Handeni na Kilindi walikutana tarehe 08 - 09 Oktoba, 2021 kwaajili ya kupitia tangazo la Serikali ili kuhakiki idadi ya watu, upatikanaji wa huduma za kijamii na kutoa ushauri wa Kitaalamu ambapo taarifa iliwasilishwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwaajili ya utekelezaji" - Mhe. Dkt. Dugange, Naibu Waziri TAMISEMI

"Wakurugenzi wa Halmashauri ya Kilindi na Handeni wameelekezwa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa uhifadhi wa Misitu, kuheshimu mpaka ulioainishwa kutokana na tafsiri sahihi ya matangazo ya Serikali, kurekebisha usajili wa Shule za Msingi Bondo na Palakwio ili zisomeke ndani ya Wilaya husika" - Mhe. Dkt. Festo Dugange, Naibu Waziri TAMISEMI

"Mara baada ya mgogoro kutatuliwa Shule ya Msingi Bondo iliyokuwa Handeni Mjini tumeikabidhi Kilindi na Shule ya Msingi Palakwio iliyokuwa Kilindi imekabidhiwa Handeni Mjini, ni lini Serikali itaweka utaratibu wa Walimu wa Shule hizi mbili kuhamasishiwa kwenye Halmashauri husika?" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini

"Waziri yupo tayari kuambatana na mimi mara baada ya Bunge hili kwenda Kata ya Kwamagome kwenye eneo linaloitwa Kolubakamba ambako baada ya kuikabidhi Shule ya Msingi Bondo kwenye Kilindi tumeanza jitihada za kujenga Shule nyingine ili aone jitihada za Wananchi waone Jinsi gani Serikali itatusaidia?" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini

"Niwapongeze wananchi wa Halmashauri ya Handeni Mjini na Kilindi kwa kutatua mgogoro na Mbunge kwa kusimamia suala hilo kwa Umakini mkubwa. Nimuhakikishie kwamba tumeshatoa maelekezo kwa Katibu Tawala Mkoa wa Tanga kuhakikisha ifikapo tarehe 30 Desemba, 2023 watumishi wa Shule ya Msingi Bondo na Palakwio wawe wamepewa barua zao za uhamisho kutokana na eneo wanalotakiwa kuwa kwenye Halmashauri" - Mhe. Dkt. Festo Dugange, Naibu Waziri TAMISEMI.

maxresdefaultwe3.jpg
F-acdCnbEAA4A5Z.jpg
 
Back
Top Bottom