benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Serikali inatarajiakupata dola za Marekani bilioni 20 sawa na takribani Shilingi trilioni 50 kutokana na biashara ya hewa ya ukaa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki amesema yapo mazungumzo yanaendelea kati ya serikali na kampuni 22 kwa ajit ya biashara hiyo. Alisema hayo Dar es Salaam jana katika mkutano wa fursa zilizopo katika mabadiliko ya tabianchi ikiwamo biashara ya hewa ukaa.
Alisema serikali ina misitu inayosimamiwa na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na mingine ikiwa chini ya Mamlaka ya Hifadhi ya Misitu na Mamiaka ya Wanyamapori (TAWA).
"Ni fursa kwetu na sasa tupo katika hatua ya mashauriano na kampuni hizo na makubaliano yapo hatua mbalimbali kama yakifanikiwa tunaweza kupata dola bilioni 20 kama wizara na taasisi zake," alisema Kairuki.
Alisema baadhi ya maeneo yametanikiwa katika biashara hiyo akitoa mano wa vijiji vinane vya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi kwa kipindi cha baada ya miaka sita hadi saba vimepata Sh bilioni nane ambazo zimesaidia kujenga huduma za kijamii.
"Wameweza kutumia mapato yao kujenga vituo vya afya, kujenga ofisi za vijiji na kata, wamepata bima za afya, wamejenga shule pamoja na miundombinu nyingine na huduma za kijamii," alisema.
Alisema wanachukua hatua kutekeleza afua kukabili mabadiliko ya tabianchi na kwamba wizara inaingia kwa upande wa misitu ikiwamo uhifadhi na kupanda miti.
"Tumeanza na tunashukuru sasa watu wanapanda miti kadiri unavyopanda unapunguza hewa ukaa na wanapima na wanalipwa na pia nashukuru kwa mkutano huu wa kaboni Tanzania unaendelea kujenga uelewa kwa Watanzania, kuna wamiliki wa misitu, halmashauri, misitu ya kijamii na binafsi au mtu mmoja mmoja na wizara tunasimamia," alisema.
Alisema Watanzania watakaopata fursa ya biashara hiyo washirikishe taasisi za serikali kufahamu hatua gani
wachukue kufanikisha mikataba.
"Katika mchakato wa kila hatua kuanzia mawazo hadi namna ya kupima, tuwe na mamlaka inayohusika kujua namna ya kupima, tuwe macho kila hatua na kujijengea uwezo kila eneo kuwe na wabobevu kupata mikataba ambayo ina manufaa," alisema Kairuki.
Meneja uendeshai wa Wakala wa Kaboni Afrika (ACA), Cosmas Tungaraza alisema miradi ya hewa ya ukaa ni fursa kwenye sekta tofauti ikiwamo ya misitu, misitu ya bahari, takataka zinazozalisha umeme na nishati jadidifu.
Tungaraza alisema biashara ya kaboni ni shughuli zote zinazolenga uhifadhi wa mazingira na kupunguza kiwango cha hewa ukaa katika anga. Balozi wa Uswisi nchini, Didie Chassot alisema wamejipanga kukabili mabadiliko ya nchi na watashirikiana na Tanzania kufanikisha hilo.
"Mabadiliko ya tabianchi ni mada kuu Uswisi na tumeona matokeo yake, watu wanakufa kwa magonjwa, mafuriko, hakuna usalama wa chakula na pia kuna ongezeko la joto, haya yote ni matokeo yake," alisema Balozi Chasso.