Wassira amtaka Sitta "kujiuzuru".

pilau

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
1,582
1,500
...Nani wa kujiuzulu kati yao........Hivi wakisimama na kuonyeshana ubabe kati ya 6 na tyson ... ghafla wakachenjiana .. wakaamua kuchapana makonde..... unalionaje hilo.
 
mtotowamjini

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
4,531
0
alichoongea wasira ni kweli..huwezi lalamikia serikali ambayo unaitumikia...kama hapendi inavyoendeshwa aachie ngazi..
 
idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
23,575
2,000
@KYAMTUMBU, hayo uyasemayo ni kweli na nukuu yako ni sahihi, lakini tatizo linakuja kwenye kuipenda CHADEMA, kama kweli kingekuwa mbadala wa ccm, basi muda mrefu tu ningekuwa mkereketwa wake. Tatizo lilipo ni kwamba Chadema wameonyesha mapungufu mengi wakiwa nje ya dola, sasa tukiwapa dola itakuwaje?

hamy.
Unaweza kutwambia ukamilifu wa ccm.?
hivyo wanavyozodoana Wassira na Sitta hadharani ndio ukamilifu.?

kuiba pesa zetu, kama alivyosema Wassira "samaki mmoja akioza wote wameoza" ndio ukamilifu.?

kuua wanawake wenye mimba na kuchoma moto nyumba za raia ndio ukamilifu.?

kuwapelekea wananchi vifaru ndio ukamilifu?

kumaliza Tembo wetu ndio ukamilifu.?
 
Last edited by a moderator:

Galapagos

JF-Expert Member
Nov 26, 2012
252
195
Wassira amemwambia Sitta "kama unaona serikali inaendeshwa kwa rushwa jiuzuru", akaendelea kusisitiza, "huwezi kuwa kwenye serikali hiyo hiyo bado unaisema ni serikali ya kifisadi wakati na wewe ni sehemu ya serikali."

Wassira pia aliongeza yafuatayo, "huwezi kuisema serikali vibaya wakati na wewe ni sehemu ya serikali hiyo, vinginevyo ndugu Sitta aachie ngazi la sivyo huu utakuwa utapeli wa kisiasa".

Aidha, katika kuimalizia hoja yake hii aliuliza swali, "samaki mmoja akioza, wote wanaoza, sasa yeye (akimaanisha Sitta) atasalimika vipi?"

My take;

Mhe. Sitta nadhani ana hitaji kukopeshwa busara kidogo, katika hatua hii huwezi kujifanya una chukizwa na madudu ya serikali ambayo kwa kipindi chote hiki amekuwa akiitumikia, amekuwa sehemu ya serikali hiyo na kama akisema kuna madudu, na yeye tuseme ni miongoni mwa wazalisha madudu hayo.

Mhe. Sitta, kiu ya urais isikufanye uonekane kituko mbele ya watanzania, kuwa mpole na usubiri wakati muafaka, kwani tabia hizi za kuropoka ropoka ndani ya CCM hatunazo, tuwaachie hii tabia wasaka dola bila mbinu (CHADEMA).
Ni vema na haki unapoleta uzi kama huu humu JF ukatupa na source ya hiyo habari, hii itasaidia kututoa wasiwasi kuhusu itikadi yako, vinginevyo tutalazimika kuamini kuwa unatiririka kwa nguvu za hizo buku saba saba.
 
Gefu

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
6,945
1,500
....wamekula ya ng'ombe sasa wanaota mapembe,hayafichiki...teh tehehhh....
 
Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,307
2,000
Wassira amemwambia Sitta "kama unaona serikali inaendeshwa kwa rushwa jiuzuru", akaendelea kusisitiza, "huwezi kuwa kwenye serikali hiyo hiyo bado unaisema ni serikali ya kifisadi wakati na wewe ni sehemu ya serikali."

Wassira pia aliongeza yafuatayo, "huwezi kuisema serikali vibaya wakati na wewe ni sehemu ya serikali hiyo, vinginevyo ndugu Sitta aachie ngazi la sivyo huu utakuwa utapeli wa kisiasa".

Aidha, katika kuimalizia hoja yake hii aliuliza swali, "samaki mmoja akioza, wote wanaoza, sasa yeye (akimaanisha Sitta) atasalimika vipi?"

My take;

Mhe. Sitta nadhani ana hitaji kukopeshwa busara kidogo, katika hatua hii huwezi kujifanya una chukizwa na madudu ya serikali ambayo kwa kipindi chote hiki amekuwa akiitumikia, amekuwa sehemu ya serikali hiyo na kama akisema kuna madudu, na yeye tuseme ni miongoni mwa wazalisha madudu hayo.

Mhe. Sitta, kiu ya urais isikufanye uonekane kituko mbele ya watanzania, kuwa mpole na usubiri wakati muafaka, kwani tabia hizi za kuropoka ropoka ndani ya CCM hatunazo, tuwaachie hii tabia wasaka dola bila mbinu (CHADEMA).
Naomba Mungu awazidishie nguvu ya kubomoana! Mbomoke vizuri tumeona Ghasia vs Membe na sasa Wassira vs Sitta....cabinet hiyohiyo na bado
 
mdeki

JF-Expert Member
Mar 28, 2011
3,304
1,225
Si kila mwenye mvi anabusara wengine ni mvi za ukoo tu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Gefu

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
6,945
1,500
...always wageni wengi kuliko wenyeji(members),nahisi vijana wa mzee 6 wanatasmini maoni ya great thinkers..hahahhh...
There are currently 543 users browsing this thread. (69 members and 474 guests)
 
Kite Munganga

JF-Expert Member
Nov 19, 2006
1,614
1,500
mkuu mzee 6, mnafiki sana!
Huyu Six ni mnafiki sana na anafikiri watu tumesahau ushenzi wake alipokuwa Spika?

Wabunge wanapolilia mkia wa kondoo
Joseph Mihangwa
Toleo la 049
1 Oct 2008
Hoja yao ilizimwa na kelele za wananchi kupitia vyombo vya habari. Hiyo ikimfanya Rais Jakaya Kikwete aliambie Taifa kuwa “Wabunge bila shaka ni watu wazima, lazima wamesikia”.
Lakini Spika Samuel Sitta, alifunga hoja hiyo kwa kuwapa matumaini Wabunge hao akisema, “kwa vyovyote vile, maslahi ya wabunge yataendelea kushughulikiwa na taasisi zinazohusika serikalini, kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa”, akaongeza kwamba, hizo ndizo siasa na gharama za kuwa mwanasiasa,
Wakati wabunge hawa wanadai mkia wa kondoo, zaidi ya Watanzania milioni 18 wanaishi kwa kipato duni chini ya 400/= kwa siku; watano kati ya sita hawana hakika ya mlo wa siku, na mmoja kati ya watatu hapati mahitaji muhimu ya maisha. (Mr Six hana huruma na watanzania kama anavyojipambanua)
…..Bunge limevamiwa na wafanyabiashara walioingia si kwa lengo la kutumikia, bali kuendeleza na kulinda biashara zao kwa nguvu za kisiasa? Hawa wanataka mishahara mikubwa na marupurupu manono kufidia muda na biashara zao walizoziacha?
Bunge limevamiwa na wasomi na wanataaluma walioziacha taaluma zao kukimbilia mkia wa kondoo? Wanadai vinono kufidia posho nono, pensheni na “ten per cent” zilizoua mashirika na taasisi za umma walikotokea kwa kuipa jina baya Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Ni utamaduni huu ulizaa kashfa za EPA, Richmond / Dowans na nyingine. Makundi yote mawili yameingia bungeni bila wito bali kwa lengo la kujinufaisha na kutumikiwa?
Wabunge wetu wangeonyesha busara na kuweza kuheshimiwa, kwa kupeleka muswada bungeni kuongeza mishahara ya wafanyakazi, au kwa lengo la kuwapunguzia wakulima ukali wa maisha, kuonyesha kwamba wanawajali wapiga kura wao.

Tuangalie toka Mwanahalisi

Nyuma ya pazia la posho za wabunge(Mr Six alikomalia mpaka wakajiongeza posho wakati watanzania wakifa na njaa)

Na Joster Mwangulumbi - Imechapwa 22 June 2011

Nyuma ya pazia
Hata hivyo, kuna sababu zilizofichika ambazo Waziri mkuu hawezi kuweka wazi. Uamuzi wa kuwapa posho wabunge, wanajeshi na hata polisi ni mpango wa nchi nyingi duniani hasa za Afrika kupunguza uwezekano wa serikali zilizoko madarakani kukataliwa na kuondolewa.
Katika nchi ambazo demokrasia bado ni changa kama Tanzania, wabunge wote wa chama tawala, kazi kubwa bungeni ni kuunga mkono hoja na kudhoofisha hoja za upinzani. Wao hujiweka nafasi ya mawaziri kuzima hoja za wapinzani.
Wanadhani kuwa wakikosoa kwa uhuru wao watakuwa wamesaidia serikali kuondolewa madarakani; wanahofu wasipounga mkono wanaweza kukosa nafasi za uteuzi. Hivyo wanaipa tuzo serikali kwa kuipigia makofi kwa kila jambo ili nayo ilipe fadhila kwa kuwapa wabunge posho kwa kazi ambayo wanalipwa mshahara.

Ujinga wote huu ulibarikiwa na Mr Six
 
Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
11,371
2,000
tuwaachie hii tabia wasaka dola bila mbinu (CHADEMA).
Mkuu hivi ikipita Siku Bila Jina CHADEMA kutoka Kinywani Mwako Siku yako Haiishi Kabisa!!!!!
Yaani Katika ----- wa CCM unaingiza CHADEMA.
Nadhan hata Siku ukijikuta Mjazito bado utakurupuka na Kusema Huu Ujauzito ni wa CHADEMA
 
MTK

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
8,255
2,000
Wassira amemwambia Sitta "kama unaona serikali inaendeshwa kwa rushwa jiuzuru", akaendelea kusisitiza, "huwezi kuwa kwenye serikali hiyo hiyo bado unaisema ni serikali ya kifisadi wakati na wewe ni sehemu ya serikali."

Wassira pia aliongeza yafuatayo, "huwezi kuisema serikali vibaya wakati na wewe ni sehemu ya serikali hiyo, vinginevyo ndugu Sitta aachie ngazi la sivyo huu utakuwa utapeli wa kisiasa".

Aidha, katika kuimalizia hoja yake hii aliuliza swali, "samaki mmoja akioza, wote wanaoza, sasa yeye (akimaanisha Sitta) atasalimika vipi?"

My take;

Mhe. Sitta nadhani ana hitaji kukopeshwa busara kidogo, katika hatua hii huwezi kujifanya una chukizwa na madudu ya serikali ambayo kwa kipindi chote hiki amekuwa akiitumikia, amekuwa sehemu ya serikali hiyo na kama akisema kuna madudu, na yeye tuseme ni miongoni mwa wazalisha madudu hayo.

Mhe. Sitta, kiu ya urais isikufanye uonekane kituko mbele ya watanzania, kuwa mpole na usubiri wakati muafaka, kwani tabia hizi za kuropoka ropoka ndani ya CCM hatunazo, tuwaachie hii tabia wasaka dola bila mbinu (CHADEMA).
I think your take in this case is not entirely erudite enough!! The concept of collective responsibility does not translate into Homogenity or call it blind royalty aka robotic thinking; it does not in any way make Sitta a mere cheer leader! concept ya collective responsibility haiwezi kumfanya Sitta au waziri mwingine yoyote anayejiheshimu asiwe na independent opinion!

At least Sitta deserves credit for the courage to stand up to be counted! self criticism is a virtue! do not read so much katika kauli za Wassira; yule ni mmoja kati ya re-cycled politicians ambao hawawezi kuisaidia serikali kujisahihisha ili kuwasaidia watanzania kupiga hatua za haraka kimaendeleo; Wassira ana mind set mgando, kwake ni swala la survival, umimi na kufikiri kwa kutumia tumbo badala ya ubongo, na kajaliwa analo tumbo kubwa kweli kweli!!!

No wonder at least for once JK got it right! news has it that Wabunge wa CCM walipotaka kuwachinjia chini Kina Kangi Lugola, Luhaga Mpina na Deo Filikunjombe kwa kuishutumu serikali wazi wazi bungeni, tunaambiwa JK aliwaasa wabunge kwamba "Kazi ya kuisahihisha serikali wasiwaachie wapinzani peke yao, kufanya hivyo ni kuwapa ujiko wapinzani"

Your take leaves a lot to be desired
 
Kamili Gado

JF-Expert Member
Jan 10, 2013
386
0
Huwezi kukaa kwenye uchafu halafu ukabaki kulalamika tu kwamba hii sehemu ni chafu bila hata kuchukua hatua za kutoka.

Kwa hili namuunga mkono mzee Tyson, kimsingi ili tuone kwamba kweli mzee 6 anachukia ufisadi ambao anadai upo kwenye serikali ambayo yeye ni sehemu ya hiyo serikali anatakiwa ajiondoe , hapo ndipo tutaamini kwamba kweli yeye ni mzalendo otherwise hizi ni siasa za majitaka.

huo ni "Uchichidodo" kwa wale waliowahi kusoma kitabu cha "A man of the people" watakua wanamfahamu ndege anaeitwa "chichidodo". Ndege huyu anapenda kula funza wanaopatikana kwenye kinyesi lakini pia anachukia sana kinyesi.
 
HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
6,955
2,000
Huyu Six ni mnafiki sana na anafikiri watu tumesahau ushenzi wake alipokuwa Spika?

Wabunge wanapolilia mkia wa kondoo
Joseph Mihangwa
Toleo la 049
1 Oct 2008
Hoja yao ilizimwa na kelele za wananchi kupitia vyombo vya habari. Hiyo ikimfanya Rais Jakaya Kikwete aliambie Taifa kuwa “Wabunge bila shaka ni watu wazima, lazima wamesikia”.
Lakini Spika Samuel Sitta, alifunga hoja hiyo kwa kuwapa matumaini Wabunge hao akisema, “kwa vyovyote vile, maslahi ya wabunge yataendelea kushughulikiwa na taasisi zinazohusika serikalini, kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa”, akaongeza kwamba, hizo ndizo siasa na gharama za kuwa mwanasiasa,
Wakati wabunge hawa wanadai mkia wa kondoo, zaidi ya Watanzania milioni 18 wanaishi kwa kipato duni chini ya 400/= kwa siku; watano kati ya sita hawana hakika ya mlo wa siku, na mmoja kati ya watatu hapati mahitaji muhimu ya maisha. (Mr Six hana huruma na watanzania kama anavyojipambanua)
…..Bunge limevamiwa na wafanyabiashara walioingia si kwa lengo la kutumikia, bali kuendeleza na kulinda biashara zao kwa nguvu za kisiasa? Hawa wanataka mishahara mikubwa na marupurupu manono kufidia muda na biashara zao walizoziacha?
Bunge limevamiwa na wasomi na wanataaluma walioziacha taaluma zao kukimbilia mkia wa kondoo? Wanadai vinono kufidia posho nono, pensheni na “ten per cent” zilizoua mashirika na taasisi za umma walikotokea kwa kuipa jina baya Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Ni utamaduni huu ulizaa kashfa za EPA, Richmond / Dowans na nyingine. Makundi yote mawili yameingia bungeni bila wito bali kwa lengo la kujinufaisha na kutumikiwa?
Wabunge wetu wangeonyesha busara na kuweza kuheshimiwa, kwa kupeleka muswada bungeni kuongeza mishahara ya wafanyakazi, au kwa lengo la kuwapunguzia wakulima ukali wa maisha, kuonyesha kwamba wanawajali wapiga kura wao.

Tuangalie toka Mwanahalisi

Nyuma ya pazia la posho za wabunge(Mr Six alikomalia mpaka wakajiongeza posho wakati watanzania wakifa na njaa)

Na Joster Mwangulumbi - Imechapwa 22 June 2011

Nyuma ya pazia
Hata hivyo, kuna sababu zilizofichika ambazo Waziri mkuu hawezi kuweka wazi. Uamuzi wa kuwapa posho wabunge, wanajeshi na hata polisi ni mpango wa nchi nyingi duniani hasa za Afrika kupunguza uwezekano wa serikali zilizoko madarakani kukataliwa na kuondolewa.
Katika nchi ambazo demokrasia bado ni changa kama Tanzania, wabunge wote wa chama tawala, kazi kubwa bungeni ni kuunga mkono hoja na kudhoofisha hoja za upinzani. Wao hujiweka nafasi ya mawaziri kuzima hoja za wapinzani.
Wanadhani kuwa wakikosoa kwa uhuru wao watakuwa wamesaidia serikali kuondolewa madarakani; wanahofu wasipounga mkono wanaweza kukosa nafasi za uteuzi. Hivyo wanaipa tuzo serikali kwa kuipigia makofi kwa kila jambo ili nayo ilipe fadhila kwa kuwapa wabunge posho kwa kazi ambayo wanalipwa mshahara.

Ujinga wote huu ulibarikiwa na Mr Six
Mkuu Kite Munganga, umeleta hoja nzuri sana, nadhani hii itadhihirisha ukigeu geu wa huyu mzee Sitta. Kila siku, mimi ni miongoni mwa wana CCM tunao pinga maslahi ya wabunge kuwa yalivyo sasa.

Ni mzigo mzito kwa taifa, ndio maana huwa namkubali Zitto kwenye hili la kukataa posho za viti, ni ufujaji mkubwa sana wa fedha za umma.

Lakini pia sababu za wabunge kung'ang'ania kuongezwa posho sio reasonable kabisa, mara watakwambia gharama za maisha Dodoma ni kubwa, mara wamegeuzwa ATM na wapiga kura wao, sasa kweli hizi nazo sababu?

Sitta kwenye hili aliniudhi kwa kweli.
 
Last edited by a moderator:

Manyi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
3,254
1,195
Dah, haya makundi yatawafanya mlishane sana sumu mwaka huu, mpaka 2015 mtakuwa mmevuana nguo hadharani!
 
Elineema J Mosi

JF-Expert Member
May 17, 2013
809
195
Wassira amemwambia Sitta
"kama unaona serikali inaendeshwa kwa rushwa jiuzuru", akaendelea
kusisitiza, "huwezi kuwa kwenye serikali hiyo hiyo bado unaisema ni
serikali ya kifisadi wakati na wewe ni sehemu ya serikali."

Wassira pia aliongeza yafuatayo, "huwezi kuisema serikali vibaya wakati
na wewe ni sehemu ya serikali hiyo, vinginevyo ndugu Sitta aachie ngazi
la sivyo huu utakuwa utapeli wa kisiasa".

Aidha, katika kuimalizia hoja yake hii aliuliza swali, "samaki mmoja
akioza, wote wanaoza, sasa yeye (akimaanisha Sitta) atasalimika vipi?"

My take;

Mhe. Sitta nadhani ana hitaji kukopeshwa busara kidogo, katika hatua hii
huwezi kujifanya una chukizwa na madudu ya serikali ambayo kwa kipindi
chote hiki amekuwa akiitumikia, amekuwa sehemu ya serikali hiyo na kama
akisema kuna madudu, na yeye tuseme ni miongoni mwa wazalisha madudu
hayo.

Mhe. Sitta, kiu ya urais isikufanye uonekane kituko mbele ya watanzania,
kuwa mpole na usubiri wakati muafaka, kwani tabia hizi za kuropoka
ropoka ndani ya CCM hatunazo, tuwaachie hii tabia wasaka dola bila mbinu
(CHADEMA).
Nyie tafunaneni tu wala usimalizie uzi wako kwa kuchokonoa majipu ya CHADEMA.sasa naamini CCM wanalaana
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom