Wassira amtaka Sitta "kujiuzuru".

HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
7,149
3,817
Wassira amemwambia Sitta "kama unaona serikali inaendeshwa kwa rushwa jiuzuru", akaendelea kusisitiza, "huwezi kuwa kwenye serikali hiyo hiyo bado unaisema ni serikali ya kifisadi wakati na wewe ni sehemu ya serikali."

Wassira pia aliongeza yafuatayo, "huwezi kuisema serikali vibaya wakati na wewe ni sehemu ya serikali hiyo, vinginevyo ndugu Sitta aachie ngazi la sivyo huu utakuwa utapeli wa kisiasa".

Aidha, katika kuimalizia hoja yake hii aliuliza swali, "samaki mmoja akioza, wote wanaoza, sasa yeye (akimaanisha Sitta) atasalimika vipi?"

My take;

Mhe. Sitta nadhani ana hitaji kukopeshwa busara kidogo, katika hatua hii huwezi kujifanya una chukizwa na madudu ya serikali ambayo kwa kipindi chote hiki amekuwa akiitumikia, amekuwa sehemu ya serikali hiyo na kama akisema kuna madudu, na yeye tuseme ni miongoni mwa wazalisha madudu hayo.

Mhe. Sitta, kiu ya urais isikufanye uonekane kituko mbele ya watanzania, kuwa mpole na usubiri wakati muafaka, kwani tabia hizi za kuropoka ropoka ndani ya CCM hatunazo, tuwaachie hii tabia wasaka dola bila mbinu (CHADEMA).
 
Ngoja WaChaga wakiamka utaona majibu yao asubuhi
Acha propaganda zako za kitoto.

Nani amekwambia Chadema ni chama cha wachaga?

Hivi sugu amechaguliwa ubunge Mbeya mjini,hilo si eneo la wanyakyusa?

Na je Mwanza nako,walikompa kura Wenje na Kiwia,nako utasema ni kwa wachaga?

Nako Kigoma kaskazini,aliokopata kura nyingi sana za ubunge,Zitto Kabwe,nako utasema kuna wachaga wengi kuliko waha?!

Hizo buku saba saba,mnazolambishwa hapo Lumumba,kwa kutangaza propaganda za magamba humu JF,zinawafanya mshindwe kabisa kupambanua mchele na pumba?!
 
Yaan hauwezi kumaliza siku bila kuitaja CHADEMA una matatizo ehee... Haya nenda lumumba ukaingize cku
 
Unapoleta mada jaribu kutoa wasiwasi na mashaka ya wasomaji ukieleza mazingira na nafasi ambayo Wasira ametamka hivyo. Hata kama kuna ukweli na hoja yako tatizo haijajitosheleza na hivyo kuzua maswali kama baadhi wafanyavyo hapa. Jaribu kututoa mashaka ya ujumbe wako mzuri.
 
Yaan hauwezi kumaliza siku bila kuitaja CHADEMA una matatizo ehee... Haya nenda lumumba ukaingize cku

Ushawahi kumlahumu padre/mchungaji au shekhe kumaliza ibada kwa kumkemea/kumtaja shetani?
 
Sitta ndani ya ccm atakuwa na wakati mgumu sana, sababu kubwa ni kujifanya tofauti na wenzake! Yeye anajifanya msafi kuliko wenzake ndani ya ccm wakati ni tofauti, ni huyuhuyu sitta aliyejenga ofisi ya spika urambo kwao,kana kwamba siku zote spika atatoka urambo!

SIASA ZA Mh 6 SIJUIKAMA ATALAMBA DUME! Mara CCJ! Mara atajejiunga Chadema! Mara anaikosoa Serikali aliomo! Mara atangaza Marafiki zake ambapo mda ukifika watajadiliana nani agombe Urais! Daah! "NAMSHAURI ASTAAFU SIASA"
 
Alichongea wassira yupo sahihi kwa 100% kwani Sitta miongon mwa wajenga dola sasa anapotoa shutuma kama hzo then aonyeshi suluhisho juu ya tatizo 2namuona n mnafki pia mbinu yake ambayo anatumia ili apate urais aje ku2mikia kanisa kama Nyerere ajue ameshndwa.
 
SIASA ZA Mh 6 SIJUIKAMA ATALAMBA DUME! Mara CCJ! Mara atajejiunga Chadema! Mara anaikosoa Serikali aliomo! Mara atangaza Marafiki zake ambapo mda ukifika watajadiliana nani agombe Urais! Daah! "NAMSHAURI ASTAAFU SIASA"

Kwani huyo Sitta ni Mpinzani wa Chama gani ?
 
Wassira amemwambia Sitta "kama unaona serikali inaendeshwa kwa rushwa jiuzuru", akaendelea kusisitiza, "huwezi kuwa kwenye serikali hiyo hiyo bado unaisema ni serikali ya kifisadi wakati na wewe ni sehemu ya serikali."

Wassira pia aliongeza yafuatayo, "huwezi kuisema serikali vibaya wakati na wewe ni sehemu ya serikali hiyo, vinginevyo ndugu Sitta aachie ngazi la sivyo huu utakuwa utapeli wa kisiasa".

Aidha, katika kuimalizia hoja yake hii aliuliza swali, "samaki mmoja akioza, wote wanaoza, sasa yeye (akimaanisha Sitta) atasalimika vipi?"

My take;

Mhe. Sitta nadhani ana hitaji kukopeshwa busara kidogo, katika hatua hii huwezi kujifanya una chukizwa na madudu ya serikali ambayo kwa kipindi chote hiki amekuwa akiitumikia, amekuwa sehemu ya serikali hiyo na kama akisema kuna madudu, na yeye tuseme ni miongoni mwa wazalisha madudu hayo.

Mhe. Sitta, kiu ya urais isikufanye uonekane kituko mbele ya watanzania, kuwa mpole na usubiri wakati muafaka, kwani tabia hizi za kuropoka ropoka ndani ya CCM hatunazo, tuwaachie hii tabia wasaka dola bila mbinu (CHADEMA).

Kiwewe cha kuukosa uwaziri mkuu na uspika bado kinamsumbua.

Nakumbuka baada ya kupokwa uspika, huyu Mheshimiwa aliiomba serikali hiyo hiyo anayoituhumu aendelee kutumia gari ya spika na kuishi kwenye nyumba ya spika iliyokuwa inalipiwa na serikali $10,000/= kwa mwezi.
 
Back
Top Bottom