KYAMTUNDU
JF-Expert Member
- Mar 7, 2013
- 1,820
- 294
KYAMTUNDU, hayo uyasemayo ni kweli na nukuu yako ni sahihi, lakini tatizo linakuja kwenye kuipenda CHADEMA, kama kweli kingekuwa mbadala wa ccm, basi muda mrefu tu ningekuwa mkereketwa wake. Tatizo lilipo ni kwamba Chadema wameonyesha mapungufu mengi wakiwa nje ya dola, sasa tukiwapa dola itakuwaje?
Sasa tumeelewana ndugu yangu!Sasa tuwape dola tuone kama watafanya usanii,tuwapige chini!Kitu ambacho watanzania wanapaswa kufahamu ni kutokuwa na urafiki na watawala!Hata kama ni CHADEMA, wakiingia madaraka wanaweza kuwepo watu waliokosa fursa wakataka kujinufaisha mapema..
Tutawapima CHADEMA kwa jinsi watakavyokuwa tayari kuwashughulikia watu wa jinsi hiyo!
Tatizo la CCM ni kulindana! Mimi siseme CHADEMA ina malaika, ILA naamini wakiwekewa presha watakuwa tayari kutii!CCM hawaofii kupoteza madaraka ndo maana kwao liwalo na liwe,maana wamejenga urafiki wa kinafiki na watawaliwa kwa kutumia elimu hafifu na umaskini wetu! Mwisho, huwa sielewi nnaposikia mtu anasema CHADEMA si mbadala wa CCM na wakati huo huo hasemi mbadala ni chama kipi! Kutosema maanake tuendelee na CCM! Chama Kimoja kushika madaraka kwa muda mrefu ni sawa na nchi kuwa na chama kimoja! Tuwape likizo CCM ili wajifunze kwamba wananchi ndo msingi wa utawala...Hata wakirudi madarakani (jambo ambalo ni afya ya demokrasia), watakuwa wamejifunza mambo mengi!
Kuanzia leo utakuwa rafiki yangu! Tehe!