Wasiokujua kwa utamu wako ni wachache sana

Hii ni mboga flani tamu sana hasa ikikutana na mpishi anaejua kuipika kwa kuchanganya viungo flan..

JE KWA KABILA Lenu MNAIITAJE HII MBOGA?

naanza: lisebho (wangoreme na wakurya)

View attachment 2028804
hii mboga ina vitamini sana, nakumbuka mamangu kijijini alikuwa aidha anaiweka karanga, au alizeti zilizotwangwa, au tetere zilizotwanga au makweme, yanachemka vizuri na inakuwa tamu mno kwa ugali wa mchana, pembeni kuna matunda pori, maembe na maziwa ya mgando dah.
 
Duh mkuu utakua na afya sana sio kwa mlo huo😄😄😅😅
mama yenu aliwapenda sana
 
Duh mkuu utakua na afya sana sio kwa mlo huo😄😄😅😅
mama yenu aliwapenda sana
aisee, huwezi amini, nimezaliwa kijijini kabisa, kijiji cha kitanzania, mamangu hakuwa na uwezo kabisa wa kifedha ila alitulisha mboga hizi na viuongo hivyo (tetere,alizeti,ufuta,karanga) sio kwamba tulikuwa tunapenda, bali alikuwa hana hela ya kununua mafuta ya kupikia na sisi tulikuwa tunalalamika sometimes kwamba mama nunua mafuta tupumzike na hivi vya kutwanga.

ajabu yake, tangu nianze darasa la kwanza (sikusoma chekechea), nimekuwa nashika namba moja hadi Form six. huku mjini nilikuja kukutana na wenzangu wa Dsm na kwengine wanakunywa uji wa sukari mimi natumia chumvi au uji mkavu. na hakuna hela ya maandazi, ila akili bado nilikuwa nazo.

wenzangu wakirudi likizo wanasimuliana wamesoma tuition mwezi mzima, mimi izo tuition sijawahi kusoma maisha yangu yote, nilikuwa nashangaa tu na kutamani laiti na mimi ningesoma tuition, ajabu yake, wote waliokuwa wanasoma tuition nilikuwa nawazidi wanakuja kuomba ufafanuzi kwangu, na mimi nikirudi likizo sikumbuki lini niliwahi kushika daftari, daftari zinabaki kwenye begi hadi nitakaporudi shule, but kwenye mitihani nawaongoza. hata nilikuwa sijui ni nini.

ninaamini Mungu akiweka mkono juu yako haijalishi mazingira, wale waliokuwa wananinyima sukari na wengine kunifulisha nguo ili wanipe sukari, wengine nimekutana nao wanakuja kuomba kazi kwangu hata ya kuendesha gari tu. siwezi kusema vyakula bora na vya asili ndio vilisaidia kuwa na akili, kwa jinsi ninavyoishi nikiongozwa na Mungu, na kwa mapito niliyopitia, naamini Mungu kuna kitu aliweka kwangu hata ningeishi maisha ya namna gani lazima angenifikisha kwenye destiny yangu tu. sifa na Utukufu kwa Mungu.
 
hii mboga ina vitamini sana, nakumbuka mamangu kijijini alikuwa aidha anaiweka karanga, au alizeti zilizotwangwa, au tetere zilizotwanga au makweme, yanachemka vizuri na inakuwa tamu mno kwa ugali wa mchana, pembeni kuna matunda pori, maembe na maziwa ya mgando dah.
Nitamu Sana hata mizizi yake ni dawa nzuri Sana na makonyo yake,kwa aliyeumwa na nyoka yanamtibu
 
Back
Top Bottom