Tusker Bariiiidi
JF-Expert Member
- Jul 3, 2007
- 5,520
- 2,091
Mkutano wa ulioitishwa na SHIWATA aka "SHIWATA DESI" ambao waliwaahidi kuwapatia viwanja vya bei ya "mteremko au bwerere" Mkuranga na Kisarawe unaendelea hapa AFRI-CENTRE Ilala umesusiwa na wale wanaojiita "Ma-super star" wa movie bongo, muziki wa dansi na waandishi wa habari...
Mkutano huo ambao umeitishwa na SHIWATA kwa wadau wa burudani, sanaa na habari kwa kiasi kikubwa umehudhuriwa na watu wasio na majina na makanjanja kadhaa wa tasnia ya habari hadi saa tano na nusu ni Lwiza Mbutu mwanamuziki wa Africann stars ndie aliyeonekana maeneo ya hapa AFRI-CENTRE Ilala... Jambo linaloonyesha wasanii "maarufu" wameamua kufunika kombe mwanaharamu apite...