Wasanii "maarufu" wasusia mkutano wa ugawaji wa "viwanja hewa"...

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Jul 3, 2007
5,520
2,091
Mkutano wa ulioitishwa na SHIWATA aka "SHIWATA DESI" ambao waliwaahidi kuwapatia viwanja vya bei ya "mteremko au bwerere" Mkuranga na Kisarawe unaendelea hapa AFRI-CENTRE Ilala umesusiwa na wale wanaojiita "Ma-super star" wa movie bongo, muziki wa dansi na waandishi wa habari...

Mkutano huo ambao umeitishwa na SHIWATA kwa wadau wa burudani, sanaa na habari kwa kiasi kikubwa umehudhuriwa na watu wasio na majina na makanjanja kadhaa wa tasnia ya habari hadi saa tano na nusu ni Lwiza Mbutu mwanamuziki wa Africann stars ndie aliyeonekana maeneo ya hapa AFRI-CENTRE Ilala... Jambo linaloonyesha wasanii "maarufu" wameamua kufunika kombe mwanaharamu apite...
 
Saa 6 kamili mwanmziki nguli Kikumbi Mwanza Mpango anaingia... Naona ule msemo wa "No free lunch" umewapitia pembeni wasanii hawa...
 
Mkutano huo ambao umeitishwa na SHIWATA kwa wadau wa burudani, sanaa na habari kwa kiasi kikubwa umehudhuriwa na watu wasio na majina na makanjanja kadhaa wa tasnia ya habari hadi saa tano na nusu ni Lwiza Mbutu mwanamuziki wa Africann stars ndie aliyeonekana maeneo ya hapa AFRI-CENTRE Ilala... Jambo linaloonyesha wasanii "maarufu" wameamua kufunika kombe mwanaharamu apite...
Si kama ni funika kombe mwanaharamu apite, hawataki kuonekana kuwa wamelizwa! Wabongo ndivyo walivyo, kama inge-turn out kuwa DEAL basi ungewaona wakiuza sura.
 
Kweli kabisa Ivisible...underground walikuwa wengi sana kama 300,na wengi wao...walioacha fun na wamrejea baada ya deal hilo... MAISHA BORA KWA KILA M-TZ...
 
si kama ni funika kombe mwanaharamu apite, hawataki kuonekana kuwa wamelizwa! Wabongo ndivyo walivyo, kama inge-turn out kuwa deal basi ungewaona wakiuza sura.

umejuaje yaani kipindi wanapelekwa kuonyeshwa kibonde alichonga si mchezo ooh wasanii waliradhaulika sana yaani jahazi ikawa kama kipindi cha kuwatukuza wasanii
kazi wanayo hiyo imetoka ...kibonde alikashifu sana deci nae wamemnyoosha
mwosha uwoshwa
 
Mbona mhabarishaji hatajutujuza kilichojiri mkutanoni zaidi ya kutuambia mahudhurio?
lete ishu
 
Wenye habari hebu nifahamisheni: Kwanini wasanii walikuwa "wanatengewa maeneo yao" bila kuchanganyika na wengine... ina maana walikuwa wanataka kutengeneza kama " Holywood" - Mambo ya Tollywood???
 
WOS
wasanii kupitia SHIWATA (shirikisho la wasanii tanzania) waliamua kutafuta maeneo ambapo wasanii watagawiwa kwa gharama nafuu kwa ajili ya kuanzisha makazi ya pamoja na shughuli zao.
Thats all i know
 
Mbona mhabarishaji hatajutujuza kilichojiri mkutanoni zaidi ya kutuambia mahudhurio?
lete ishu

wewe ndio utujuze siulijigamba kwa madaha kuwa ilikuwa effort yako kutuibia no kutupa viwanja hewa kisarawe?
 
Hahaha
ni kweli nipo ktk kamati ya SHIWATA.
kinachojiri sasa ni kwamba wasanii wameshagawia viwanja (waliolipia) na endapo kuna mtu ambaye alilipia hajapata kiwanja chake basi ajitokeze.
Kuhusu kuibiwa sidhani kama kuna NIA hiyo wala tukio hilo. Cha maana kwa kuwa sisi tu wa wazi ktk ishu zetu pitia ofisi ya mkuu wa wilaya MKURANGA kitengo cha ardhi upate data kamili.
Naongea hivyo kwa kuwa ninauhakika na taarifa nipewazo na watendaji wetu pale SHIWATA.
 
Msanii acha usanii
 
Bradha,
Nilikuwa sijajua kwamba na wewe ulikuwemo kwenye dili.
Lakini kama ni kweli viwanja hivi vipo pale Mkuranga, mbona mkuu wa wilaya (DC) na mkurugenzi mtendaji (DED) wa wilaya wame-disclaim kuwa hawagawi viwanja katika wilaya yao? Wamedai kwamba utaratibu wa kugawa mashamba lazima uanzie katika vijiji ndipo vijiji vipeleke muhtasari wilayani, kwa mashamba/viwanja vinazyozidi ukubwa wa ekari 50. Lakini pia, ni kiwanja gani kinauzwa kwa sh. 38,500/-?
 
Well said
Mkuu hapo nilipoweka bold ufafanuzi wake ni gharama za kujiunga na kijiiji na si gharama za kiwanja hivyo baada ya kujiunga na kijiji ndipo kama mtu atapewa kipande cha ardhi atawajibika kugharimia kukipima kama anataka ofa. Pia ni kweli DC hawahusiki kugawa viwanja maana ktk sheria ya Vilage land act kijiji kupitia ngazi husika na mabaraza yake ndiyo vinatoa maamuzi ya kukubali ama kukataa matumizi pendekevu ya ardhi ikiwemo kushughulikia maombi yote yahusuyo ardhi ya kijiji.
Kule wilayani wanapata taarifa na kushirikishwa hatua zote kwa mujibu wa sheria. Ndo maana nasema taarifa zote zipo wilayani maana shiwata inategemea maongozi ya wilaya kama utaratibu umefuatwa ama la.
Sikuwepo ktk kikao cha juzi ila tulipewa ufafanuzi kuhusu suala hilo na hali halisi.
kama kungekuwa na ufisadi walah shiwata ingeshakuwa mahala pake very now.
Mhusika mkuu ktk hili namba yake ni 0712 87 35 09 ambaye ni mwenyekiti wa shiwata. mpigie upate ufafanuzi kisha utujuze hapa jukwaani.
 
Umesomeka!
Let's hope for the best.
 
Sikuwepo ndani ya kikao hicho bali nilikuwa hapo kwa kupata Supu na Tusker Bariiiidi kadhaa!!!
 
Back
Top Bottom