YALIYOJIRI: Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni za CCM - Viwanja vya Jangwani, Dar-es-Salaam

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,536
2,264
Kwa wale wapenzi, washabiki, wanachama na wananchi kwa ujumla wanaopenda kufahamu kinachoendelea katika mkutano wa ufunguzi wa Kampeni za CCM katika viwanja vya Jangwani watapata update hapa.

Mkutano utarushwa LIVE kupitia TBC, ITV, Azam TV pamoja na Star TV.

Tujumuike kwa pamoja kama kaulimbiu ya CCM katika Uchaguzi Mkuu inayosema, Umoja ni Ushindi.

===================================
VIDEO NA PICHA:

30.jpg

attachment.php


Jangwa.png
Picha zaidi: PICHA UZINDUZI WA KAMPENI KWA CHAMA CHA MAPINDUZI


Sasa Nape ameomba watu wenye uwezo wa kusimama, wasimame kuimbia wimbo wa Taifa. Baada ya wimbo wa taifa, wameitwa kikundi cha yamoto band kuimba wao wa Magufuli pia ameimba Bushoke. Sasa ameitwa mwenyekiti wa masoko soko la Ilala.

Ameitwa Mapinduzi Mpema ambae ni mwenyekiti wa waendesha bodaboda wilaya ya Ilala amesema watu wanaoshirikiana na UKAWA sio viongozi wa bodaboda na anamshukuru Kikwete kwa kurasimisha biashara ya bodaboda kupitia bunge kwa sababu bunge linaloongozwa na CCM ndio lililopitisha bungeni biashara ya bodaboda kuwa vyombo rasmi vya usafiri.

Amon Mpanju(Mwenyekiti walemavu): Ukiona mtu anajiunga na anasema anaenda kuwasaidia walioshindwa, jana amesema UKAWA hawana uwezo wa kuondesha serikali, wale ni wababaishaji. Tumpeleke Magufuli Ikulu na tuache wababaishaji.

Makongoro Nyerere: Magufuli nilikaa nae na ndio aliniambia mna maombi niwe kampeni meneja wake, nimejiandaa maana ni rahisi kuzunguka kwa sababu unachosema ni kweli na kipo, lakini uongo unahitaji maandalizi kwelikweli. Leo umesema na kesho unausahau, tabu tupu.

Kuna yule kaka yangu mmoja nasikia afya yake sio nzuri tumuache kwanza. Kuna yule wa jana kajileta kwenye chandimu. Miaka kumi iliyopita Sumaye aliingia kwenye tano bora lakini akashindwa na Jakaya. Miaka kumi baadae tano bora hakuingia.

Sumaye yeye mkali, akatuambia mkimpa Lowassa hiki chama kugombea Urais mimi nitahama, shida ya uongo kuusema rahisi, kuukumbuka tabu. Mbona sasa yeye ameenda kumkumbatia Lowassa, tumueleweje! Nawaheshimu lakini sio rafiki zangu, kama wanaongopea watu, mimi lazima nikuambieni ukweli.

Jaji Warioba: Kama alivyosema Makongoro, hatutasema mengi, tutakutana huko. Leo siku ya uzinduzi, Magufuli na Samia watatoka hapa na Ilani. Mafanikio tuliyopata, matatizo tuliyopata na jinsi tulivyojipanga taarifa ipo hapa(Ilani). Katika miezi miwili hii nitashiriki kikamilifu kueneza Ilani hii.

Wagombea wetu wataeleza sera lakini sisi tutawaeleza wao wenyewe.

Mkutano mkuu wa CCM ulisikiliza maombi yetu na kuchagua watu wachapakazi, Magufuli mnafahamu. Miaka ishirini aliyokuwa kwenye serikali mmeona kazi yake. Sio kusimamia tu bali kuwafanya watanzania pia waelewe haki zao. Kazi aliyofanya matunda yake yanaonekana. Mimi natoka Mara, miaka si mingi watu wa Mara tulikuwa tunapitia Nairobi, leo mnapita huko, ni kazi ya Magufuli, siku hizi unaweza ukatoka Mtwara na ukafika Bukoba kwa barabara ya lami na ikiwa Mbovu anaikataa. Nyie watu wa Mbagala mtakua mnajua, alienda kuangalia barabara na kuikataa, wakandarasi wakairudia kwa pesa yao.

Magufuli ni mzalendo na hana makundi, ni mzalendo haswa, kuna umuhimu katika kipindi hiki kuimarisha umoja watu. Wanaozungumzia mabadiliko, CCM tumefanya mabadiliko makubwa hayo. Kwa mara ya kwanza tumemuweka mama katika nafasi hiyo, tuhakikishe Samia hasa kina mama anapita. Tunayo timu nzuri ya uongozi, tuna sera nzuri na tutaelezana huko mtaani.

Sina wasiwasi na hoja zinazotolewa, tutazijibu tu.




UPDATES ZAIDI: YANAYOJIRI UFUNGUZI WA KAMPENI CHAMA CHA MAPINDUZI

MWISHO:
CCM inatoa shukrani ambazo hazina kipimo kwa wale wote wameungana nayo kwa njia moja au nyingine katika kufanikisha tukio hili la kihistoria kama ambavyo viongozi wa CCM wamesema.

CCM inawashukuru wale wote wameungana nayo katika hii thread kwa kutoa mchango/michango au kusoma michango ambayo kwa njia moja au nyingine ni chachu ya kuifanya CCM iendelee kuwa imara zaidi kwa faida ya ushindi katika uchaguzi ujao.

CCM inawashukuru sana MOD'S wa Jamiiforums kwa kuisimamia ipasavyo hii thread bila kujali kelele ambazo hazina msingi wa hoja na ukweli.
 

Attachments

  • SAM_2168.JPG
    SAM_2168.JPG
    105.9 KB · Views: 4,572
  • CNGW-C3WgAAmMZv.png
    CNGW-C3WgAAmMZv.png
    309.5 KB · Views: 5,051
  • SAM_2164.JPG
    SAM_2164.JPG
    218.3 KB · Views: 4,704
  • 2.jpg
    2.jpg
    54.9 KB · Views: 4,787
  • 12.jpg
    12.jpg
    63.7 KB · Views: 4,770
  • magufuli1.jpg
    magufuli1.jpg
    155.2 KB · Views: 35,168
Viongozi kadhaa wameshawasili na sasa ameingia mwenyekiti wa chama cha mapinduzi, Mheshimiwa Jakaya Kikwete. Wengine waliowasili ni Mzee Mwinyi, mzee Mkapa na wengineo.

Wanaingia mgombea urais kwa tiketi ya chama cha mapinduzi, John Magufuli na mgombea mwenza Samia Suluhu.

Sasa Nape ameomba watu wenye uwezo wa kusimama, wasimame kuimbia wimbo wa Taifa. Baada ya wimbo wa taifa, wameitwa kikundi cha yamoto band kuimba wao wa Magufuli pia ameimba Bushoke. Sasa ameitwa mwenyekiti wa masoko soko la Ilala.

Ameitwa Mapinduzi Mpema ambae ni mwenyekiti wa waendesha bodaboda wilaya ya Ilala amesema watu wanaoshirikiana na UKAWA sio viongozi wa bodaboda na anamshukuru Kikwete kwa kurasimisha biashara ya bodaboda kupitia bunge kwa sababu bunge linaloongozwa na CCM ndio lililopitisha bungeni biashara ya bodaboda kuwa vyombo rasmi vya usafiri.

Amon Mpanju(Mwenyekiti walemavu):
Ukiona mtu anajiunga na anasema anaenda kuwasaidia walioshindwa, jana amesema UKAWA hawana uwezo wa kuondesha serikali, wale ni wababaishaji. Tumpeleke Magufuli Ikulu na tuache wababaishaji.

Makongoro Nyerere: Nitoe kofia ee! Na miwani eeh! Na shati eeh! Niliesimama mbele yenu naitwa Makongoro Nyerere, ni mbunge wenu na mwenyekiti wa wabunge watanzania katika bunge la Afrika Mashariki, katika timu ya kampeni urais nami nimo. Nasikia wenye uzoefu wanajua hizi nafasi wakaziombe wape, lakini mimi sijui, nashukuru viongozi wangu. Naomba mniwie radhi kwa sababu leo ni ufunguzi na una taratibu zake, sitaongea sana.

Magufuli nilikaa nae na ndio aliniambia mna maombi niwe kampeni meneja wake, nimejiandaa maana ni rahisi kuzunguka kwa sababu unachosema ni kweli na kipo, lakini uongo unahitaji maandalizi kwelikweli. Leo umesema na kesho unausahau, tabu tupu. Kuna watu wanajidai wa mafuriko, sio unahutubia Mnazi mmoja alafu unaleta watu kutoka Masasi.

Naomba tuelewane, kundi zima la wenzangu ambao tumechaguliwa wote tumelelewa vizuri. Tukumbushane, kuna mchezo unaitwa chandimu na kawaida huchezwa na vijana, wazee wakija kwenye chandimu wameyataka wenyewe, kina taratibu zake. Ukija mzee kucheza na sisi vijina ukiachia miguu tunakupiga mpra wa tobo, ukigeuka nakupiga kanzu. Naenda kumi na nane shuti moja tu ndani. Ohh tumeibiwa kura, una kura za kuibiwa wewe. Mimi kusema uongo siwezi.

Kuna yule kaka yangu mmoja nasikia afya yake sio nzuri tumuache kwanza. Kuna yule wa jana kajileta kwenye chandimu. Miaka kumi iliyopita Sumaye aliingia kwenye tano bora lakini akashindwa na Jakaya. Miaka kumi baadae tano bora hakuingia.

Sumaye yeye mkali, akatuambia mkimpa Lowassa hiki chama kugombea Urais mimi ntahama, shida ya uongo kuusema rahisi, kuukumbuka tabu. Mbona sasa yeye ameenda kumkumbatia Lowassa, tumueleweje! Nawaheshimu lakini sio rafiki zangu, kama wanaongopea watu, mimi lazima nikuambieni.

Jaji Warioba:
Kama alivyosema Makongoro, hatutasema mengi, tutakutana huko. Leo siku ya uzinduzi, Magufuli na Samia watatoka hapa na Ilani. Mafanikio tuliyopata, matatizo tuliyopata na jinsi tulivyojipanga taarifa ipo hapa(Ilani). Katika miezi miwili hii nitashiriki kikamilifu kueneza Ilani hii.

Wagombea wetu wataeleza sera lakini sisi tutawaeleza wao wenyewe.

Mkutano mkuu wa CCM ulisikiliza maombi yetu na kuchagua watu wachapakazi, Magufuli mnafahamu. Miaka ishirini aliyokuwa kwenye serikali mmeona kazi yake. Sio kusimamia tu bali kuwafanya watanzania pia waelewe haki zao. Kazi aliyofanya matunda yake yanaonekana. Mimi natoka Mara, miaka si mingi watu wa Mara tulikuwa tunapitia Nairobi, leo mnapita huko, ni kazi ya Magufuli, siku hizi unaweza ukatoka Mtwara na ukafika Bukoba kwa barabara ya lami na ikiwa Mbovu anaikataa. Nyie watu wa Mbagala mtakua mnajua, alienda kuangalia barabara na kuikataa, wakandarasi wakairudia kwa pesa yao.

Magufuli ni mzalendo na hana makundi, ni mzalendo haswa, kuna umuhimu katika kipindi hiki kuimarisha umoja watu. Wanaozungumzia mabadiliko, CCM tumefanya mabadiliko makubwa hayo. Kwa mara ya kwanza tumemuweka mama katika nafasi hiyo, tuhakikishe Samia hasa kina mama anapita. Tunayo timu nzuri ya uongozi, tuna sera nzuri na tutaelezana huko mtaani.

Sina wasiwasi na hoja zinazotolewa, tutazijibu tu.

Rais wa Zanzibar nae kaongea na kutoa salamu za wazanzibari, kwa sasa ni zamu ya Rais mstaafu, mzee Ali Hassan Mwinyi

Mwinyi: Maneno yaliyosemwa hapa na waliotangulia wote pamoja na waadhi aliotupa mheshimiwa Warioba, tuusikilize sana na mimi nakuombeni nanyi msikilize yaliyosemwa, hakuna haja ya kukumbushana ukubwa wa CCM. Tazama hii leo, kutokana na baadhi ya waliokuwa CCM, wenzetu wapinzani wamepata nguvu zao, inaelekea vyama vya upinzani wameona ili waweze kufanikiwa, shurti waazime.

Wengine wameenda hivi jana wameenda na wamesema wazi wanaenda kuifundisha jinsi ya kuishinda CCM. Kumbe kuna CCM mbili, CCM A na B, A ni hii hapa na B mmeisikia. Kama CCM A ipo, B ya kazi gani. Unawezaje ukaiacha CCM A halafu ukaipe kura CCM B maana yake nini, kuna watu wanaenda kupeleka ufundi alioupata kutoka CCM A, mtu haachi fundi akapokea mwanafunzi.

Mkapa: Katika wagombea waliochaguliwa, hamna timu nzuri kama ya John Magufuli na Samia Suluhu, kuna chama kimoja tu ukombozi, kuna vyama vingine vinadai eti vinataka kuwakomboa watanzania, ni wapumbavu. Nchi hii ilishakombolewa na ASP na TANU. Haitoshi tu kusema unauchukia umasikini bali ueleze mikakati yako. Mshawishi kila mmoja kuipigia kura CCM na timu yake katika ngazi zote.

Kinana: CCM tumejipanga vizuri, kimuundo, kimkakati na kwa hoja na ushindi mkubwa, nimkaribishe mwenyekiti wa chama na rais wa jamhuri ya muungano, Mheshimiwa Jakaya Kikwete.

Kikwete: Shukrani nyingi kwa katibu mkuu, amesema mzee Mkapa hata wakati wake haikuwa hivi, hata wakati wangu haikuwa hivi. Nilisema pale diamond wakanichukia, wanachukua picha za zamani, nyingine za Slaa wanaweka kwenye magazeti lakini sio yaliyotuleta leo. Leo ni mwanzo wa safari ya kukabidhi kijiti na sisi wasiwasi rais huyo atakuwa John Magufuli.

Hatatuki kuchukua mgombea ana makandokando mengi tukatumia muda mwingi kumtetea na kujitetea kabla ya kumnadi kuomba kura, Magufuli hatupi kazi hiyo. Siku anaenda kuchukua fomu aliniaga lakini akasema sitaki kuongea na waandishi wa habari, hakutaka mbwembwe hizo, kweli bwana nasoma gazeti naona kachukua fomu na kutokea mlango wa nyuma.

Magufuli kundi lake lipi! Yeye na dereva wake wamezunguka kupata udhamini. Mimi namuamini, naamini Tanzania chini ya Magufuli iko salama, atapambana na uovu.

Mmoja kaenda jana eti kaenda kuimarisha CCM, mwingine sijamuelewa kabisa. Nawashangaa eti anaenda kwenye chama na kusema hamna mtu wa kuongoza, huyu mtu anawadharau. Kuna mgombea urais ni kama ana sera zake binafsi maana ni kama hazifanani na chama.

SASA NI KITENDO CHA KUKABIDHI ILANI KWA MGOMBEA NA MGOMBEA MWENZA

Samia Suluhu: Nitakuwa msaidizi wa karibu sana kumsaidia Dr John Magufuli kutekeleza ilani, pamoja na mambo mengine ni kuwasaidia kina mama, huduma nzuri za afya, ujenzi wa mabweni kwa ajili ya watoto wetu wa kike. Maji safi na salama baada ya kazi nzuri ya kupeleka maji vijijini. Nimeishi ofisi ya makamu wa rais kwa miaka mitano. Ofisi ya makamu wa rais itasimama vyema kutekeleza ilani na kusimamia muungano, kumaliza kero na kuzuia zile zinazotaka kuibuka. Nimkaribishe kaka yangu mheshimiwa Magufuli.

Magufuli: Nimekaa Dar kwa muda mrefu tangu mwanafunzi mpaka kazi, katika kuishi kwangu sijawahi kuona watu wengi namna hii. Kujitokeza kwa wingi inadhihirisha wazi nia ya watanzania wa kutaka mabadiliko bora na mambo makubwa kwa nchi yetu. Mzee mwinyi amesema kila zama na kitabu chake, katika zama hii natambua mchango mkubwa wa Nyerere, Karume, mzee Mwinyi, mzee Mkapa na mzee mtarajiwa mzee Kikwete. Wamejenga msingi imara kwa ajili ya kuiendeleza nchi yetu. Watanzania natambua kiu yenu kubwa, mnapenda kuona mageuzi makubwa.

Natambua mnataka Tanzania pawe na amani na usalama, ninatambua watanzania wote mnataka maisha mazuri, natambua mnataka swala la rushwa, wizi na utendaji mbovu wa serikali vikomeshwe haraka. Nimejiandaa kwa hilo kama mtanichagua, mgambo watatafuta kazi nyingine lakini sio kusumbua mama ntilie.

Nitafungua mahakama kwa ajili ya majizi na mafisadi ili wajue hapa ni nchi ya kutetea wanyonge, natambua nchi yetu ina vyama vingi, nitajali hata mawazo ya wapinzani. Ninachotaka hapa ni kazi tu ili nchi isonge mbele.
 
Mkitaka Kura Niwape Ni Hadi Hapo MTAKAPOWEKA USAWA KATIKA MISHAHARA YA WAALIMU TULIPWE SAWA NA DAKTARI, MWAL WA DIGRII ALIPWE SAWA NA DAKTARI MWENYE DIGRII.HVY HVY KWA DIPLOMA.SASA HV MWAL MWENYE DIGRII ANALIPWA LAKI SITA KABLA YA MAKATO NA DAKTARI MWENYE DIGRII ANALIPWA MILION MOJA LAKI TANO, HAPO USAWA UPO WAPI? Mwalimu Nae Ni Daktari, Kila Siku Anaingia Opelesheni Ya Kumfanyia Mwanafunzi Asie Na Kitu Kichwani Awe Nacho, Asiejua Kusoma Mpaka Ajue. Na Mwal Anafanya Hayo Kwa Procedure Maalum Ikiwemo Kuandaa Azimio La Kazi, Andalio La Somo, Zana Za Kufundishia, Kumbukumbu La Somo, Shajala, Malengo Mahususi Vyoote Hvy Ni Vifaa Vitakavyotumika Kukarabati Ubongo Wa Mwanafunzi, Vifaa Hvy Ni Sawa Na Mikasi,viwembe, Gozi,mipila Watumiavyo Madaktari Wanapomkarabati Mgonjwa, KWA MSINGI HUO BASI, MWALIMU NAE NI DAKTARI NA KILA SIKU HUINGIA THEATRE KUFANYA UPASUAJI WA UBONGO WA MWANAFUNZI HVY NAE ALIPWE MSHAHARA SAWA NA WA MADAKTARI.
 
Ukiona Ni Shida, Basi Wahi Kwa Fundi UKASHONESHE Hata CHUPI YA NDANI, Kikubwa Hapa Usikose Kabisa Kuwa Na Sare.
 
kwa wale wapenzi, washabiki, wanachama na wananchi kwa ujumla wanaopenda kufahamu kinachoendelea katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za ccm katika viwanja vya jangwani watapata update hapa.

Tujumuike kwa pamoja kama kaulimbiu ya ccm katika uchaguzi mkuu inayosema, umoja ni ushindi.






mbona hao akina mangula na juma simba wamekalia kama vile wako msibani ???
 
Last edited by a moderator:
kakobe alisema mungu amewapaganyisha ndimi zenu msielewane katu ili kudhihilisha kuwa yeye ndo mfalme wa mbingu na ardhi.....
angalieni hapo jangwan hizo ndimi zenu kama nyoka wa kibisa zitasababisha mzidi kuwa wamoja kama mlivyotoka dodoma.....
nawatakia safari yenu njema ya kusindikiza ukawa ikulu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom