Dodoma: Yaliyojiri kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)


B

Boniphace Kichonge

Verified Member
Joined
Jul 31, 2017
Messages
1,105
Likes
1,346
Points
280
B

Boniphace Kichonge

Verified Member
Joined Jul 31, 2017
1,105 1,346 280
Wadau,

Matangazo Mubashara yanarushwa kutoka ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma kupitia ITV, Star TV, Channel Ten, Clouds TV, ZBC na TBC na pia kupitia jumls ya Redio 19.
Karibuni.
Viva CCM
Viva JPM

Kuwasili kwa Mwenyekiti
Mwenyekiti wa Chams cha Mapinduzi Mh Dk John Pombe Magufuli tayari ameshawasili kwenye ukumbini unaotumika kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa 9 wa CCM.

Wageni maarufu waliohudhuria
Wake wa Viongozi Wastaafu
1.Mama Maria Nyerere 2. Mama Sitti Mwinyi 3.Mama, Khadija Mwinyi, 4.Mama Fatuma Karume 5.Mama Salma Kikwete, 6.Mama Janeth Magufuli.

Marais Wastaafu waliohudhuria

1.Mh. All Hassan Mwinyi 2.Mh. Benjamin William Mkapa3.Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.

Mawaziri wakuu wastaafu
1.Mh Cleopa David Msuya 2. Mh Salim Ahmed Salim 3.Mh John Samweli Malecela 4. Mh Mizengo Pinda

Wakuu wote wa Mikoa nchini wamehudhuria
Mabalozi kutoka nchi mbalimbali na wawakilishi kutoka vyama rafiki ndani na nje ya nchi
Spika wa Bunge mstaafu Anna Makinda
Mh Pius Msekwa
Augustino Mrema & John Cheyo

Wajumbe waliohudhuria mkutano mkuu 1,871
JPM sasa anazungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu
Ushindi katika uchaguzi wa madiwani unatokana na CCM kuungwa mkono na watanzania wengi nchi nzima, kutekeleza kwa vitendo ilani ya uchaguzi na umoja uliopo kwa Wana CCM.
CCM ni chama cha kipekee.

Agenda za Mkutano Mkuu
1. Kupokea na kujadili taarifa ya kazi za chama - Mh.A. Kinana

2.Kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa Serikali zote mbili - Mh.Kassim Majaliwa

3.Kufanya Uchaguzi wa Viongozi Wakuu na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa.

=>Amewaomba wasichague Viongozi wala rushwa.

=>Amesema maamuzi ya Mkutano Mkuu wa CCM ni yana umuhimu mkubwa kwani yana matokeo ya moja kwa moja kwa Watanzania wote.

=>Ameomba matokeo ya uchaguzi ndani ya Jumuiya za CCM yasiwagawe Wana CCM bali yazidi kuimarisha umoja.

=>Ameagiza kuwa makundi yote yaliyokuwapo wakati wa uchaguzi yavunjwe mara moja kwani uchaguzi umeshamalizika.

=>Amesema Chama hakitamvumilia mtu yoyote atakayejaribu kuvuruga umoja uliopo.

=>Amesema CCM imefanya mageuzi mbalimbali tokea kuanzishwa kwake kwa ajili ya maslahi ya WanaCCM wote na Watanzania kwa ujumla.

Majukumu ya Viongozi Wapya

1.Kuongeza idadi ya wanachama wenye mapenzi na chama

2.Kuhakikisha kuwa Chama kinajitegemea kiuchumi. Ada zilipwe kwa wakati na wanachama. Pia ameagiza viongozi watembelee wanachama badala ya kukaa tu maofisini. Aidha ameagiza kuwepo na uwazi katika matumizi ya fedha na usimamizi mzuri wa rasilimali za Chama.

Amesema kuwa chama tayari kimeidhinisha mfumo mpya wa kielectronic utaotumika kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Chama. Viongozi wote wapya wamehimizwa kubuni miradi mipya ikiwamo Viwanda.

Ameongeza kuwa CCM inazo mali nyingi ikiwemo jumla ya viwanja vikubwa 3,000 nchi nzima.

3. Viongozi wapya wawe kiungo kati ya Serikali na wananchi. Wasikilize na kuyachukua matatizo ya wananchi na wayapeleke Serikalini kutatuliwa.

Ameagiza kuwa Viongozi wa CCM hawapaswi kuwaogopa Watendaji wa Serikali kwani wako pale kutekeleza ilani ya CCM.

JPM - Nyinyi ndio chama tawala na wote tupo chini cha CCM.

4. Uadilifu kwa Viongozi

Wawe mfano wa kuigwa kwa wananchi na wanachama wote.

Masuala ya Uchumi
Akizungumzia ukuaji wa uchumi Mh mwenyekiti amesema kuwa uchumi wa nchi yetu unakua kwa kasi ya kuridhisha.

Mfumuko wa bei umepungua

Amesema kuwa akiba ya Taifa iliyopo inaweza kutulisha Watanzania wote kwa muda wa miezi mitatu bila ya kufanya kazi.

Viwanda zaidi 3000 vimeshajengwa

Viwanda vilivyokufa vinafufuliwa.

JPM anawashukuru Wajumbe wote

Anawashukuru sana Makamo wawili ( Mzee Shein & Mzee Mangula) wamemsaidia sana. Mzee Mangula anapewa shukrani za kipekee.

Wazee ni muhimu sana kwa chama.

Mzee Kinana nae anapewa shukrani za kipekee kwa kumsaidia JPM hasa kufanya reforms. JPM anasema kuwa Mh. Kinana anaamini ataendelea kumsaidia sana na Wajumbe wanashangilia kwa nguvu.

Wanachama wapya wanatambulishwa
=>Wapo wengi wanaotaka kujiunga na CCM akiwemo Mbunge mmoja anayetaka kuhamia na madiwani wake 8.

=>CCM inafanya tathmini kabla ya kuwapokea ili wasipokee mamluki.
JPM amemaliza kufungua kikao.

Katibu Mkuu Mh Kinana anaongea

=>Anamshukuru JPM KWA KUENDELEA KUMUAMINI NA ANATOA AHADI YA KUENDEKEA KUMSAIDIA MWENYEKITI WAKE.

Kwanini CCM inapendwa?

1. Demokrasia ya kuchagua na kuchaguliwa

2. Uhuru wa kutoka mawazo bila woga.

3. Kutenda haki

=>Waliokiuka taratibu za chama wakati wa uchaguzi walichukuliwa hatua km kupewa onyo, onyo kali au kufukuzwa uanachama n.k

>Mageuzi ya CCM yasipotoshwe

>Ilani ya CCM ni bora

CCM ataendelea kupambana na rushwa.

Uwajibikaji ufanyike kwa vitendo

Mafunzo kutolewa kwa Viongozi wote wapya

Uhakiki wa Mali za Chama umekamilika.

Mali zote za CCM kuwekwa kwenye mfuko mmoja ili utumike kwa uwiano kwa mikoa yote.

Kinana amemaliza kuwasilisha.

Kinana kuendelea kuwa Katibu Mkuu wa CCM

Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa anawasilisha taarifa kwa Wajumbe

Sekta ya kilimo inaendelea kuboreshwa

Serikali kuendelea kushirikiana na Sekta binafsi

Uzalishsji wa zao la Korosho umeongezeka

Sekta ya ushirika kuzidi kuboreshwa nchini.

Sekta ya Utalii kuzidi kuimarishwa k.m kuongeza bajeti, kutoa mafunzo, kutatua migogoro mbalimbali, kuimarisha miundo mbinu, kuongeza matangazo ya Utalii nk. Matokeo ya hatua hizi ni kuongezeka kwa idadi ya watalii nchini.

Serikali kuimarishwa nidhamu kwa watumishi

Mashamba yasiyoendelezwa kutaifishwa na kisha kurejeshwa kwa wananchi.

Zaidi ya Vijiji 11,000 vimepimwa na hati kutolewa

Serikali kuendelea kuimarishwa ujenzi wa Barabara

Serikali kuendelea kujenga na kukarabati viwanja vya ndege

Serikali imeanza ujenzi wa Reli ya kisasa.

Usafiri wa majini kuzidi kuimarishwa

Taratibu za kunua meli mpya kubwa wakamilika

Miradi ya umeme kwa kutumia gesi asilia Kinyerezi 1 & 2

Mradi wa REA kuimarishwa

Serikali kuimarisha sekta ya Afya kwa kuongeza bajeti ya dawa(2.6) billioni.
Wananchi watakiwa kujiunga na Bima ya Afya.

Walimu zaidi ya 4,600 wameajiriwa na wengine zaidi kuajiriwa.

Idadi ya Wanafunzi darasa la kwanza yaongezeka nchini.

Serikali kuboresha sekta ya maji kwa kukamilisha miradi mikubwa ya maji. (Mini zaidi ya 17 kunufaika)

Watumishi zaidi 2,800 tayari wameshahamia Dodoma.

Serikali kuendelea kusimamia utawala bora.

Ofisi za Ubalozi zaombwa kuhamia Dodoma.

Waziri Mkuu Mh Kassimu Majaliwa amemaliza kuwasilisha.
More Updates From Dodoma

Utambulisho wa Wageni

Mh Kinana anatoa utambulisho wa Wageni

Nchi zilizowakilishwa na Mabalozi;

1. Comoro 2. Msumbiji 3. Cuba 4. China 5. DPRK 6.Palatine 7. Burundi 8.

Nchi zilizowakilishwa na Wawakilishi wa Mabalozi

1.Zimbabwe 2. Rwanda 3. Kenya 4. Saudi Arabia 5.Urusi 6. DRC Congo 7. Japan 8. Afrika Kusini 9. Somalia 10. Angola

Vyama vilivyoalikwa na kutuma wawakilishi

1. UDP 2.SAU 3.UPDP 4. DP 5.TADEA 7.CUF 8. CCK 9. AFP 10. DEMOKRASIA MAKINI 11. ADC 12.TLP

Utambulisho wa Wagombea
Mwenyekiti wa CCM anawatambulisha wagombea wa nafasi 30 za Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kwa kuwaita mbele ya Mkutano Mkuu. Mh Steven Masatu Wassira kada mkongwe ni miongoni mwa wagombea. Tanzania bara itatoa nafasi 15 na Zanzibar itatoa nafasi 15.

Zoezi la Kupiga Kura
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wanaendelea kupiga kura.

Burudani Kidogo
=>Sebene la nguvu linapingwa sasa wakati kura zikipigwa
"CCM ni ileile Tumejipanga mwaka huu wataisoma"

=>Mh.John Shibuda Mwenyekiti wa Tadea amuomba JPM Tshs milioni 20 ili chama chake kiweze kushiriki vema katika uchaguzi wa wabunge unaotarajia kufanyika mapema mwakani. Ameshangazwa na vyama vinavyopewa ruzuku na Serikali na kuamua kususia kushiriki chaguzi.

Mapumziko
=>Wajumbe wa Mkutano Mkuu sasa wanapumzika ili kujipatia chakula cha mchana.

>>>>More updates From Dodoma

=>Wajumbe wamerudi kwenye ukumbi wa Mkutano

=>Mh John Pombe Magufuli amejiuzulu Uenyekiti ili kupisha mchakato wa Uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti wawili.

=>Mh Benjamin Mkapa amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa muda na msimamizi wa uchaguzi.

=>Wajumbe wanapiga kura kuchagua Viongozi wa juu wa CCM.
Masanduku ya kura sasa yanakusanywa.

Burudani
=>Sebene la nguvu kutoka TOT linapigwa sasa na Wajumbe wote ni furaha kwenda mbele

"Waacheni waandamane eehh CCM mbele kwa mbele"

" wacha waisome namba eeh CCM mbele kwa mbele"

"Harambeee eeh harambeee Mama harambee"

>>>Zoezi la kuhesabu kura linaendelea

=>Wasanii wa kizazi kipya waliohudhuria wanatambulishwa na Mh Humphrey Polepole

=>Mwanamuziki wa nyimbo za Injili Rose Mhando na kikundi chake wanatoa burudani kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa kuimba wimbo maalumu.( "Magufuli tubebe tuna imani nawe")

=>Baada ya wimbo wameomba kukabidhiwa kadi za Chama cha Mapinduzi.
JPM anaenda kumtunza Rose Mhando.

Mwenyekiti wa muda Mh Benjamin William Mkapa

=>Ameahirisha Mkutano kwa muda wa saa moja ( Wajumbe wanatakiwa kurejea ukumbini saa 11 jioni)

=>Matokeo ya uchaguzi wa Viongozi wa CCM yatatangazwa mara tu Wajumbe watakaporejea ukumbini saa 11

>>>Wajumbe wa Mkutano Mkuu wamerejea ukumbini tayari kupokea matokeo

=>Burudani inaendelea huku Wajumbe wakisubiri matokeo

=>Mh JPM amejiunga na kikundi cha TOT kwa kupiga ngoma.

=>Mwenyekiti WS muda anawakaribisha wazee Wastaafu.

Mzee Jakaya Kikwete anazungumza na Wajumbe kwa niaba ya Marais Wastaafu.

=>Anatoa shukrani kwa Wajumbe, Mwenyekiti wa muda na Mwenyekiti wa sasa.

=>Anapongeza kazi nzuri iliyofanywa hadi sasa ya utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM

=>Amewapongeza Viongozi kwa ujasiri mkubwa walio nao.

=>Amewapongeza kwa kuwa na mipango mizuri.

=>Anasema watoe muda kwa Viongozi waliopo sasa ili waweze kutekeleza au kutatua kero mbalimbali.

=>Anasema kazi ya Urais ni ngumu sana na haina shule

=>Anampongeza JPM kwa hotuba nzuri inayothibisha kuwa sasa amekamilika.

=>Kwamba anatamani sana JPM apate 100%

=>Anasema kuwa kura nyingi zitampa nguvu kubwa ya kumfanya aweze kujituma zaidi.

=>Anamaliza kwa kumtakia kila la kheri Mh JPM na pia kuongoza wimbo wa "Tuna Imani na Magufuli"

=>"Rais Mstaafu Zanzibar Mh Abeid Karume anatoa salaam zake kwa Wajumbe"

=>Kwamba mipango ya maendeleo inaleta matumaini

=>Kwamba Wanachama/ Viongozi wapya wanaleta mawazo mapya

=>Awapongeza Viongozi wapya waliochaguliwa

=>Anampongeza JPM kwa kazi nzuri

Mh John Samweli Malecela anawasalimu Wajumbe

=>Anamshukuru JPM kwa kufanya Mkutano Mkuu wa kwanza Dodoma ikiwa pia makao makuu.

=>Kwamba atakumbukwa daima

Mh Salim Ahmed Salim anazungumza na Wajumbe

=>Amkumbusha JPM kuwa CCM ni muhimu kwa bara la Afrika na ni chama kinachotegemewa. Ni chama chenye majukumu ya ndani na majukumu ya nje pia.

=>Anaomba wana CCM na Watanzania wote wamsaidie JPM

Mh Mizengo Pinda anazungumza na Wajumbe

=>Aipongeza CCM kwa kazi nzuri

=>Aipongeza Serikali kwa mapambano dhidi ya rushwa.

Anasema Viongozi wa CCM safi

=>Yusuph Nakamba anazungumza na Wajumbe

Waliojenga msingi wa nchi hii ni Mwalimu Nyerere na Mzee Karume

Awapongeza JPM na Marais wote Wastaafu bara na visiwani kwa kazi nzuri.

Amfananisha JPM na Yohane Mbatizaji.

Aufananisha ushindi wa CCM kwenye kata 42 za udiwani na Ubatizo wa Moto.

Anasema JPM ni mkweli, hana makuu wala majivuno.

Amuomba JPM ateua Kamati ya ufundi bora.

MATOKEO YA UCHAGUZI
Mh Job Ndugai anatangaza matokeo
1. Matokeo kundi la Zanzibar
Kura zilizopigwa 1,770
Kura zilizoharibika 99
Kura halali 1,671
Waliochaguliwa
1.Ndg Bajari Juma
2.Ndg C.J Antony
3.Ndg Laila Ngozi
4.Ndg Nasiri Juma
5.Ndg Amin Salmin Amour
6.Ndg Juma Juma
7.
8.
9.
10.
11.
12.
13.
14.
15.

2. Kundi la Bara
Kura zilizopigwa 1800
Kura zilizoharibika
Kura halali 1779
Waliochaguliwa
1. Ndg.Ibrahim Msengi
2. Ndg Angel Akilimali
3. Ndg Mwantumu Zoddo
4. Ndg Burton Kihaka
5. Ndg William Sarakikya
6. Ndg Deo Ruta
7. Ndg Ernest Sungura
8. Dr Fenera Mkangara
9. Ndg Jerry Slaa
10.Ndg Theresia Mtewele
11.Ndg Steven Masatu
Wassira
12.Ndg Anna Msuya
13.Ndg Richard Charles
14. Charles Shanda
15. Jackson Msome

3. Makamo Mwenyekiti Tanzania Zanzibar
*Kura zilizopigwa 1,819
*Kura zilizoharibika 0
*Kura halali 1,819
*Kura za ndiyo 1,819
*Kura za hapana 0

4. Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara.
*Kura zilizopigwa. 1827
*Kura zilizoharibika 0
*Kura halali 1,826
*Kura za ndiyo 1,826
*Kura za hapana 0

5. Mwenyekiti wa CCM Taifa
*Kura zilizopigwa 1821
*Kura zilizoharibika 0
Kura halali 1,821
*Kura za ndiyo 1,821
*Kura za hapana 0

Mwenyekiti wa CCM Dkt John Pombe Magufuli anazungumza
Anasema mwajiri Mkuu wa Watendaji wa Serikali ni CCM

Ameagiza kuwa asitokee Kiongozi yeyote wa Serikali akashindwa kutambua/ kutekeleza hilo.

Viongozi wa Serikali waheshimu sana Viongozi wa CCM

Amesema Katibu Mkuu na Sekretarieti iliyopo itaendelea kuwepo.

Watanzania waelezwe ukweli wote ule uwe mtamu au mchungu.

Ameagiza wana CCM waende kutetea chama chetu

Tujibu hoja zinazoletwa dhidi ya CCM na Serikali

Vyama vingine vijifunze demokrasia iliyopo ndani ya CCM. Wenyeviti wa vyama hivyo wajifunze kuachia madaraka bafala ya kung'ang'ania madaraka kwa miaka mingi.

CCM inataka vyama vya upinzani vya ukweli vyenye uwezo wa kujibu hoja.
Amehimiza vyama vya siasa kujenga umoja.

Mwenyekiti amemaliza na anawaaga na kuwashukuru Wajumbe wote.
Mkutano Mkuu wa 9 wa CCM umefungwa rasmi.

ccm-simiyu-jpg.653409

ccm-jpeg.653410
 
Iza

Iza

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2009
Messages
1,905
Likes
171
Points
160
Iza

Iza

JF-Expert Member
Joined Jan 8, 2009
1,905 171 160
Boniface Kichonge
Wako laivu wanaonesha nini ama kuna jambo gani, tufafanulie!
 
K

KIM JOHN UN

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2017
Messages
512
Likes
695
Points
180
K

KIM JOHN UN

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2017
512 695 180
leo kuna kitu gani hapo mkuu?
 
gemmanuel265

gemmanuel265

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2016
Messages
7,478
Likes
15,127
Points
280
gemmanuel265

gemmanuel265

JF-Expert Member
Joined Feb 16, 2016
7,478 15,127 280
Tushawachoka hawana jipya zaidi ya kulishana upuuzi wa kuligawa taifa kwa misingi ya kiitikadi ya kisiasa, mwambieni huyo baba ubaya nchi imekwama tofauti na anavyodanganywa na hao washauri wake maana wanaogopa kumwambia ukweli kwa tahadhari ya kuonekana wabaya.
 
Mulhat Mpunga

Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Messages
26,836
Likes
14,380
Points
280
Mulhat Mpunga

Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2010
26,836 14,380 280
img-20151025-wa0053-jpg.653405
Wadau
Matangazo Mubashara kutoka Ukumbi wa Jakaya Kikwete
Karibuni.
Viva CCM
Viva JPM
Hahaha hakuna cha viva wala makanyagio...

Tunahitaji viwanda, elimu, ajira, sio mambo ya kujipigia promo kama kina diamond wakitoa nyimbo mpya!!!
Kitu pekee watanzania tunahitaji ni maendeleo,

Muda huu wa kazi watu tupo kazini mpo kwenye tv mnahubiri kitu gani ?Wakati mnasisitiza tufanye kazi nyie vipi?..........Hii siyo kazi tuliyowapa kazi ni kutupatia kazi na kubadilisha mambo haya yaliyopo ambayo chanzo ni nyie nyie CCM
 
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Messages
14,151
Likes
1,773
Points
280
Age
48
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined Feb 1, 2013
14,151 1,773 280
Hayawi hayawi sasa yamekuwa, CCM wanafanya mkutano mkuu wa chama chao leo Makao Makuu ya Nchi mjini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine watafanya uchaguzi wa mwenyekiti na makamu wenyeviti wawili wa chama hicho. pia watachagua wajumbe wa halmashauri kuu taifa. wageni mbalimbali wakitaifa na kimataifa wanazidi kuhudhuria. fuatilia uzi huu kwa live updates
 
F

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Messages
14,551
Likes
5,058
Points
280
F

FUSO

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2010
14,551 5,058 280
Hivi jamaa wanamchagua au wanampitisha mwenyekiti maana unachaguaje mtu anaewania kitu na yupo peke yake...
ukoloni mamboleo ndiyo huo; unashiriki uchaguzi wa mtu aliyekwisha kujichagua then unasema chama kina demokrasia - waafrica tuna safari ndefu.
 
Elli

Elli

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2008
Messages
29,954
Likes
15,448
Points
280
Elli

Elli

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2008
29,954 15,448 280
Huu ni muda wa kazi, si ruhusa kuangalia matangazoo ya moja kwa moja. Tafadhali wakumbushe wasisahau jambo hilo ni muhimu saaaana
 
Mulhat Mpunga

Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Messages
26,836
Likes
14,380
Points
280
Mulhat Mpunga

Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2010
26,836 14,380 280
ukoloni mamboleo ndiyo huo; unashiriki uchaguzi wa mtu aliyekwisha kujichagua then unasema chama kina demokrasia - waafrica tuna safari ndefu.
wanatumia kodi za wananchi hahaha
 
Ambiele Kiviele

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2014
Messages
14,462
Likes
26,061
Points
280
Ambiele Kiviele

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2014
14,462 26,061 280
Mwenyekiti Anagombea Na Nan Iyo Nafasi
 
M

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,509
Likes
963
Points
280
M

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,509 963 280
ukoloni mamboleo ndiyo huo; unashiriki uchaguzi wa mtu aliyekwisha kujichagua then unasema chama kina demokrasia - waafrica tuna safari ndefu.
Safari ndefu ya kwenda wapi mkuu?
 

Forum statistics

Threads 1,251,881
Members 481,931
Posts 29,789,104