Wasafi FM Unguja yapigwa faini Milioni 5 kwa kuvunja masharti ya Leseni

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Tume ya Utangazaji imeitaka WASAFI FM Radio kulipa faini ya Tsh. Milioni 5 kwa kuvunja masharti ya leseni kwa kuidanganya Tume juu ya Studio zao za Unguja kutotumika kwa vipindi vya aina yoyote kwa karibu miezi mitatu sasa

Tume imeitoza ZBC Faini Tsh. Milioni 1 kwa kipindi cha MICHAPO kuonyesha maudhui yasiyozingatia Mila Silka na Maadili ya Mzanzibari kupitia miziki yenye picha zilizokuwa hazina maadili

Aidha, Tume imeipiga Redio Mjini FM 92.5 Faini Tsh. Milioni 10 kwa kurusha matangazo kutoka Dar kwa 90% badala ya Mlandege (Unguja) kinyume na Leseni yao.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (1)_page-0001.jpg

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (1)_page-0002.jpg
 
Chanel ten ya CCM mnaiachaje?
 

Attachments

  • 20231127_075049.jpg
    20231127_075049.jpg
    72.5 KB · Views: 3
studio zikiwa Dar wazanzibar wanakosa ajira maana hawawezi kushindana na soko la hapo DSM.
 
Inaonekana zanzibar vituo vya redio havipati mapato kutokana na masharti ya urushaji wa matangazo kwa kujifanya mnaendesha nchi kidini. Hii itafanya zanzibar mbaki na ZBC yenu pekeyake.
 
Kuna mpemba hapa kijiweni anasema Dimondi ashukuru muungano vinginevyo Milioni 5 ya Kizanzibari ingekuwa sawa sawa na milioni 500 ya Kitanganyika🐒
 
“Maadili ya Mzanzibari”, Kuna kila sababu za kuvunja huu muungano maana wenzetu wanavyakwao ila vya huku Tanganyika ni vyetu wote,
 
Inaonekana zanzibar vituo vya redio havipati mapato kutokana na masharti ya urushaji wa matangazo kwa kujifanya mnaendesha nchi kidini. Hii itafanya zanzibar mbaki na ZBC yenu pekeyake.
Tatizo nchi hii ni unafiki.
Wanajifanya kulinda maadili huku wanapumuliana visogoni aah
 
Back
Top Bottom