Ni ndefu lakini vumilia hivyo hivyo
SEHEMU YA PILI
28.Ndivyo ilivyokuwa katika siku za
Lutu: Watu walikuwa wakila na kuinywa,
wakinunua na kuuza, wakilima na kujenga.
29Lakini siku ile Lutu alipoondoka Sodoma,
ikanyesha mvua ya moto na kiberiti kutoka
mbinguni ukawaangamiza wote. 30Hivyo ndivyo
itakavyokuwa siku ile Mwana wa Adamu
atakapofunuliwa. 31Siku hiyo, mtu ye yote
aliyeko kwenye dari ya nyumba yake, vitu vyake
vikiwa ndani ya hiyo nyumba asishuke
kuvichukua. Vivyo hivyo mtu aliyeko shambani
asirudi nyumbani kuchukua cho chote.
32Mkumbukeni mke wa Lutu! (Luka 17:28-32).
Haya ni maneno yaYesu Kristo alipokuwa akieleza
kuhusu mambo yatakayotokea kabla ya kurudi
kwake. Sodoma inatajwa kama mji ambao watu
wake walikuwa wenye kutenda dhambi nyingi sana
(Mwanzo 13:13). Na Lutu anatajwa kama mtu
aliyekuwa akiishi katika mji huo.
WAGENI WALIOMTEMBELEA IBRAHIMU
BWANA akamtokea Abrahamu karibu na
mialoni ya Mamre wakati alipokuwa ameketi
kwenye ingilio la hema lake wakati wa adhuhuri.
2Abrahamu akainua macho akaona watu watatu
wamesimama karibu naye. Alipowaona,
aliharakisha kutoka kwenye ingilio la hema lake
kuwalaki na kuwasujudia hadi nchi (Mwanzo
18:1-2). Wageni hawa watatu, wakiwa
wameongozana na Bwana(Yesu Kristo),
walipokarimiwa na Abrahamu Na baada ya
kumbariki Sarah mke wa Abrahamu(Mwanzo
18:10) waliaga na walipoelekeza nyuso zao
Sodoma, Abrahamu akiwa anawasindikiza
(Mwanzo 18:16), ndipo Bwana akawaza ya
kwamba hatamficha Ibrahimu kuhusu kile
alichokuwa amekusudia kutenda fungu la 17.
Kumbe basi, ugeni huo haukuwa kwa ajili ya
kumtembelea Abrahamu, bali ulikuwa ni ugeni
uliomtembelea kwa kusudi maalumu, na kusudi
lenyewe likiwa ni kutangama MAMBO
YALIYOKUWA MBIONI KUIPATA MIJI YA SODOMA
NA GOMORA. Sasa tuangalie jumbe ambazo
malaika wale pamoja na Bwana walikuwa
wamepeleka kuhusiana na Sodoma na Gomora.
UJUMBE WA
KWANZA
Bwana alipobaki na Abrahamu kabla ya
wale malaika wawili kwenda Sodoma, akafunua
juu ya kusudio lake kwa miji ile kwa rafiki yake
Abrahamu, 20Basi BWANA akasema, Kilio dhidi
ya Sodoma na Gomora ni kikubwa sana na
dhambi yao inasikitisha sana, 21kwamba
nitashuka nione kama waliyoyatenda ni mabaya
kiasi cha kilio kilichonifikia. Kama sivyo,
nitajua (Mwanzo 18:20-21). Ndipo malaika
wawili wakaondoka na kumwacha Abrahamu
akiwa na BWANA, na ndipo Abrahamu akatamuka
25Hilo na liwe mbali nawe, kufanya jambo kama
hilo, kuwaua wenye haki pamoja na waovu,
kuwatendea wenye haki sawasawa na waovu. Iwe
mbali nawe! Je, Mwamuzi wa dunia yote
hatafanya lililo sawa?(Mwanzo 18:25), ndipo
Abrahamu akaanza kumuuliza BWANA kama
wakiwemo watu waaminifu kadha wa kadha ndani
ya mji kama atawaangamiza, alianza na 45,40,
hadi 10. Hapa ujumbe tunaoupata hapa ni
TANGAZOLA HUKUMU
UJUMBE WA PILI
Katika Mwanzo 19:1 tunasoma Malaika
wale wawili wakafika Sodoma wakati wa jioni,
,
Lutu aliwakaribisha, na wakamwambia atoe kila
mtu wake katika mji maana wapo karibu
kuuharibu(Mwanzo 19:12), naye Lutu alipoenda
kutoa taarifa kwa wakweze waliokuwa wameposa
binti zake, Biblia inasema, 14Kwa hiyo Loti alitoka
ili kuzungumza na wakwe zake, waliokuwa
wamewaposa binti zake. Akawaambia, Fanyeni
haraka kuondoka mahali hapa, kwa kuwa BWANA
ni karibu kuangamiza mji huu! Lakini wakwe
zake walifikiri kwamba alikuwa akitania. (Mwanzo 19:14). Ujumbe waliofikisha malaika wale ni
TANGAZO LA UHARIBIFU WA
MIJI ILE
UJUMBE WA
TATU
Mwanzo 19:15-16 tunasoma 15Kunako
mapambazuko, malaika wakawahimiza Loti,
wakamwambia, Fanya haraka! Mchukue mke
wako na binti zako wawili walioko hapa,
vinginevyo utaangamizwa wakati mji
utakapoadhibiwa. 16Alipositasita, wale watu
wakamshika mkono wake na mikono ya mke
wake na binti zake wawili na kuwaongoza salama
nje ya mji, kwa kuwa BWANA alikuwa na huruma
kwao. 17Mara walipokwisha kuwatoa nje, mmoja
wao akawaambia, Mkimbie kwa usalama wenu!
Msitazame nyuma, wala msisimame popote
katika tambarare! Kimbilieni milimani, ama sivyo
mtaangamizwa! kwa hiyo hapa ujumbe
uliopelekwa na ale malaika kabla ya kuharibiwa
kwa Sodoma ni ONDOKA.
JUMBE HIZO TATU
KATIKA NYAKATI ZA LEO
Katika kitabu cha ufunuo 14:6-12 tunasoma
6Kisha nikamwona malaika mwingine
akiruka juu angani, naye alikuwa na Injili ya
milele ya kuwatangazia wale waishio duniani,
yaani, kwa kila taifa, kabila, lugha na jamaa.
7Akasema kwa sauti kubwa, Mcheni Mungu na
kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake
imewadia. Mwabuduni Yeye aliyeziumba mbingu,
dunia, bahari na chemchemi za maji.
8Malaika wa pili akafuata akisema,
Ameanguka! Ameanguka Babeli aliye mkuu, yeye
aliyeyafanya mataifa yote kulewa kwa mvinyo wa
ghadhabu ya uasherati wake.
9Malaika wa tatu akawafuata hao wawili
akisema kwa sauti kubwa, Kama mtu ye yote
anamwabudu huyo mnyama na sanamu yake na
kutiwa chapa yake kwenye kipaji chake cha uso
au kwenye mkono wake, 10yeye naye, atakunywa
mvinyo wa hasira kali ya Mungu ambayo
imemiminwa katika kikombe cha ghadhabu yake
pasipo kuchanganywa na maji. Naye atateswa
kwa moto uwakao na kiberiti mbele ya malaika
watakatifu na mbele za Mwana-Kondoo. 11Nao
Moshi wa mateso yao hupanda juu milele na
milele. Hakuna mapumziko, mchana wala usiku,
kwa wale wamwabuduo huyo mnyama na sanamu
yake, au kwa ye yote anayepokea chapa ya jina
lake. 12Hapa ndipo penye subira na uvumilivu
wa watakatifu, yaani, wale wanaozishika amri za
Mungu na kudumu kuwa waaminifu kwa Yesu
Tunapata jumbe tatu katika mafungu hayo
juu
i/. HUKUMU ikiwa ni tangazo toka kwa
malaika wa kwanza(Ufu 14:7).
ii/. TANGAZO LA ANGUKO(UHARIBIFU) WA
BABELI huu ni ujumbe toka kwa malaika wa pili
(Ufunuo
14:8)
Iii/. Onyo kwa wale wasiotii agizo la kutoka
BABELI ambalo linatolewa katika Ufunuo 18:4
4Kisha nikasikia
sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema:
Tokeni katikati yake, enyi watu wangu, ili msije
mkashiriki, dhambi zake,ili usije
ukapatwa na pigo lake lo lote
Jumbe zote hizi ni sawa kabisa na jumbe zile
zilizotolewa kabla ya anguko la sodoma. Kumbe
kabla Yesu kristo kurudi hapa duniani, jumbe hizi
zitatangulia, watu waandaliwe kuhusu hukumu,
wajue BABELI NI NINI ili wajihadhari wasije
wakaingia huko, na pia wakimbie kutoka huko
BABELI (walio watu wa Mungu). Cha kujiuliza leo
hii makanisani na misikitini, jumbe hizi
zinahubiriwa?