Kama tunavyowaambia CCM hii nchi sio yenu peke yenu. Vivyo hivyo na CHADEMA hamna hatimiliki ya Ukweli na Demokrasia peke yenu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
37,375
Reaction score
86,866
Hamjambo!

1. Bado tunawekana Sawa. Tunazungumza. Ili mambo yakae sawa.

2. Kuna vitabia vya ajabuajabu ndani ya nchi yetu. Tabia ya kujimilikisha mambo ambayo hayamilikiwi na yeyote. Mambo ya wote kundi na genge Fulani linahodhi na kujimilikisha. Hiya ni dhulma.

3. Ukweli, uzuri, uponyaji, haki havinaga mmiliki kwa ni halali ya Kila MTU na Kila kiumbe.

4. Mtibeli atatumia kisa cha Yesu na Wanafunzi wake, ambao nao walikuwa na tabia mbaya kama hii. Kujimilikisha mambo ya wote.

5. Wanafunzi wa Yesu walipokuwa kwenye pitapita zao huko mitaani wakiwa wenyewe. Mara wanashuhudia Kundi jingine huko mitaani likiponya na kutoa mapepo watu huku likitaja jina la Yesu.

6.wanafunzi wakapatwa na kihoro, hasira. Wakakimbia mbio wakirudi kushtaki kwa Yesu. Walipofika wakamwambia, Bwana! Bwana tumepita huko Mitaa ya Buza, Nyehunge, na Kaloleni tumeona watu wakitoa Pepo na kuponya watu kwa jina lako. (Wakimaanisha alafu sio wanafunzi wako).

7. Yesu akajibu akawaambia, Wapo kondoo walionje ambao hawapo hapa lakini ni kondoo wa zizi hili.

8. Kisa hiko ni kisa cha umiliki na maslahi.

9. CCM wanaamini kuwa Wao ndio pekee wanahaki ya kumiliki nchi hii huku vyama vingine wakionekana kama wapangaji.
Jambo hili linanyima haki vyama vingine.

10. CCM lazima waelewe vyama vingine navyo vinahaki sawa na wamiliki wa nchi hii.

11. CHADEMA nao wamejikuta katika hali hiyohiyo ya wao kujifanya wamiliki wa ukweli, haki na demokrasia.

12. Chadema wanaamini kwamba huwezi kuwa mpenda Ukweli, demokrasia na mpenda Haki ukiwa nje ya CHADEMA.
Jambo ambalo kama Mtibeli na watibeli wote waliopo siasani na wasio siasani tunalikataa.

13. Wanafunzi wa Yesu waliamini ili uponye na kutoa mapepo lazima uwe mwanafunzi wa Yesu lakini pili waliamini kwamba wao wanammiliki Yesu.
Lakini walipokutana na watu wengine huko duniani ambao hawajawahi hata kuwaona wakiponya, na wakitoa Pepo Kwa jina la Yesu ikawapa kihoro na hasira.

14. Ubaya hauna Kwao. Kama ulivyo wema. Wapo Wabaya Chadema, na wapo Wabaya CCM. Wapo wema Chadema na wapo Wema CCM.

15. Chadema ni chama cha siasa. CCM ni chama cha siasa. Watanzania wanahaki ya kuwa chama chochote Kati ya hivyo au nje ya hivyo. Au wasiwe na Chama Kabisa.

16. CHADEMA pia wanatatizo la wao kutaka kusema Ukweli kwa wengine lakini wao hawataki kuambiwa Ukweli. Jambo ambalo tunarudi kulekule kwamba Ukweli kwao ni ule wanaousema wao sio unaosemwa na watu walionje. Hii kimantiki na masuala ya haki haipo Sawa.

17. Tabia ya kutaka maoni ya watu yafanane na mtazamo wa CHADEMA ni tatizo jingine linalowakabili Chadema.
Katika hilo wanakuwa hawana tofauti na CCM ambao nao unageuka adui yao pale unapowaambia ukweli wanakuhisi wewe ni CHADEMA au adui yao.

18. Demokrasia ni pamoja na kuheshimu maoni ya watu wengine bila kuwashambulia na kuwavunjia haki zao. Kuwatukana, kuwazushia n.k.

19. Unapopigania Demokrasia alafu muda huohuo hutaki mawazo ya wengine au unatukana wenye mawazo kinzani na yako unakuwa hujui maana ya Uhuru wa maoni na demokrasia.

20. Sisi Watibeli Tunajua Ukweli haumilikiwi na mtu, watu au taifa Fulani. Ukweli ni wawatu wote na unaweza kuupata popote.

21. Ukweli kwetu lazima uchunguzwe ili uthibitike.
Ndio maana Watibeli Wote. Unaweza kumkuta Mtibeli ni Muislam lakini hiyo haimaanishi haoni Ukweli na uongo uliopo kwenye Ukristo. Pia ataona kasoro na uongo katika Uislam na haoni shida kusema kasoro na uongo uliopo katika uislam hata kama ni dini yake.

22. Vivyohivyo, Mtibeli Mkristo lazima aone ukweli na uongo uliopo kwenye dini zingine ikiwemo uislam na kasoro zake.
Na pia katika Dini yake.

23. Halikadhalika na mambo ya vyama vya siasa. Watibeli sio mashabiki. Sio watu wakujiendea endea au kupelekwa pelekwa.

24. Sisemi watu wawe kama Watibeli, ila nazungumzia umuhimu watu kuyaangalia mambo vile yalivyo, bila ushabiki. Kutojimilikisha mambo ya watu wore.

25. Mfano kwenye jamii yetu;
Heshima ni haki na mali ya Kila mtu. Lakini utashangaa kundi au tabaka Fulani likijimilikisha heshima, kwamba wao ndio wanastahili kuheshimiwa.
Mfano Wazazi baadhi hutaka kuheshimiwa wao tuu lakini kuheshimu watoto wao wanaona mzigo. Hii sio sawa.

Pia viongozi wa Jamii na taifa baadhi yao hutaka wapewe heshima tuu. Alafu wao kutoa heshima hawataki au wanaona kama ni kujishusha.

26. Sisi Watibeli, Heshima inaanzia juu kwenda chini. Sio chini kwenda juu.
Wajuu akionyesha heshima ataheshimiwa. Sio atake heshima. Nope! Aonyeshe heshima. Mkubwa na wajuu ndio role model.

Kufikia hapo sina la ziada.

Sabato Njema Sana.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi, Chama Cha Mapinduzi CCM ndio chama pekee cha siasa nchini chenye dhamana ya kisheria, ya kusimamia mgawanyo sawa wa matumizi ya rasilimali zote za nchi na kuhakikisha kila mTanzania na mali zake wapo salama.

Wanao tazama dhamana hiyo ya CCM kwa taifa kama sio wajibu wake, wanajifedhehesha tu kwasababu wamekosa agenda.
Lakini hivyo ndivyo ilivyo na hivyo ndivyo itakavyo kua hata ikiwa chama kingine cha siasa kikipewa dhamana hiyo na wananchi 🐒
 
Hii ndiyo tunaita political maturity
Thank you Robert Heriel Mtibeli
Chadema hudhani wao ndiyo bora kuliko vyama vyote 19 vilivyopo na kwamba bila chenyewe vingine vyote 19 vinakuwa useless!
Naomba mjadala wa maridhiano uanze mara moja,wawemo,wasiwemo tusonge mbele,
Kibaya kabisa serekali pia inahusika kwenye kuwapa kiburi hiki,binafsi ni muumini wa vyama vyote 19,vinastahili haki sawasawa,kwa kila hatua bila kuona huyu ni zaidi na yule ni mdogo.
 
Nipe kifungu Gentleman kutoka kwenye Katiba
 
Robert Heriel Mtibel, Unasifa moja kuu na ambayo itakufikisha mbaali sana

Mnafiki na asiye mnafiki unakula naye sahani moja

Ukishakuwa mtu wa haki hili huwezi kuliepuka.

Mtu Fulani anaweza kuwa muovu na mtu mwingine anaweza kuwa Mwema.
Kwenye Haki wote unapaswa kuwasikiliza. Ili Kila mmoja umpe kile anachostahili.
 
Hii ndiyo tunaita political maturity
Thank you Robert Heriel Mtibeli
Chadema hudhani wao ndiyo bora kuliko vyama vyote 19 vilivyopo na kwamba bila chenyewe vingine vyote 19 vinakuwa useless!
Naomba mjadala wa maridhiano uanze mara moja,wawemo,wasiwemo tusonge mbele,
Kibaya kabisa serekali pia inahusika kwenye kuwapa kiburi hiki,binafsi ni muumini wa vyama vyote 19,vinastahili haki sawasawa,kwa kila hatua bila kuona huyu ni zaidi na yule ni mdogo.

Hoja ya Chadema ni kwamba Hatua zote za maridhiano zifuatwe ikiwemo uwajibikaji.
Yeyote anayehusika kwa nanna yoyote awajibishwe kisheria.

CCM wao wanakimbia uwajibikaji. Ni kama wanatetea uhalifu na dhulma iliyofanyika.
 
That's right and am sorry,nilisahau kama kuna tume tayari itakayotuwekea kila kitu wazi wazi,blessed be!..
 
Hii ndiyo tunaita political maturity
Thank you Robert Heriel Mtibeli
Chadema hudhani wao ndiyo bora kuliko vyama vyote 19 vilivyopo na kwamba bila chenyewe vingine vyote 19 vinakuwa useless!
Naomba mjadala wa maridhiano uanze mara moja,wawemo,wasiwemo tusonge mbele,
Kibaya kabisa serekali pia inahusika kwenye kuwapa kiburi hiki,binafsi ni muumini wa vyama vyote 19,vinastahili haki sawasawa,kwa kila hatua bila kuona huyu ni zaidi na yule ni mdogo.
Kipi kinasubiriwa ili "maridhiano" yaanze.Kwenye "uchaguzi" 2025 CHADEMA hawakushiriki.Ni muda muafaka hayo "maridhiano" yakafanyika tu.
 
Hii ndiyo tunaita political maturity
Thank you Robert Heriel Mtibeli
Chadema hudhani wao ndiyo bora kuliko vyama vyote 19 vilivyopo na kwamba bila chenyewe vingine vyote 19 vinakuwa useless!
Naomba mjadala wa maridhiano uanze mara moja,wawemo,wasiwemo tusonge mbele,
Kibaya kabisa serekali pia inahusika kwenye kuwapa kiburi hiki,binafsi ni muumini wa vyama vyote 19,vinastahili haki sawasawa,kwa kila hatua bila kuona huyu ni zaidi na yule ni mdogo.
Huwezi ukafanya maridhiano kama hawapo CHADEMA Huo ndio ukweli…….kila mtu mwenye akili timamu anaelewa hilo

Mwaka jana si mlifanya uchaguzi bila CHADEMA mliona nini kilitokea!?? Kwanini Bado Nchi ipo kwenye mkwamo kama CHADEMA bado haipo kwenye decision making bodies za Nchi hii

CHADEMA ndio chama pekee chenye Wafuasi wengi vijana kuliko vyama vyote

CHADEMA ndio chama pekee chenye uungwaji mkono na Wasomi wengi hapa nchini

CHADEMA ndio chama pekee chenye Wafuasi wengi waishio mijini na vijijini

CHADEMA ndio chama pekee chenye uungwaji mkono na Mataifa mengi ya nje

Unaweza ukaudanganya wajinga wenzako wa ccm lakini huwezi kuudanganya umma na dunia nzima kwa wakati mmoja
 
Hamjambo!

1. Bado tunawekana Sawa. Tunazungumza. Ili mambo yakae sawa.

2. Kuna vitabia vya ajabuajabu ndani ya nchi yetu. Tabia ya kujimilikisha mambo ambayo hayamilikiwi na yeyote. Mambo ya wote kundi na genge Fulani linahodhi na kujimilikisha. Hiya ni dhulma.

3. Ukweli, uzuri, uponyaji, haki havinaga mmiliki kwa ni halali ya Kila MTU na Kila kiumbe.

4. Mtibeli atatumia kisa cha Yesu na Wanafunzi wake, ambao nao walikuwa na tabia mbaya kama hii. Kujimilikisha mambo ya wote.

5. Wanafunzi wa Yesu walipokuwa kwenye pitapita zao huko mitaani wakiwa wenyewe. Mara wanashuhudia Kundi jingine huko mitaani likiponya na kutoa mapepo watu huku likitaja jina la Yesu.

6.wanafunzi wakapatwa na kihoro, hasira. Wakakimbia mbio wakirudi kushtaki kwa Yesu. Walipofika wakamwambia, Bwana! Bwana tumepita huko Mitaa ya Buza, Nyehunge, na Kaloleni tumeona watu wakitoa Pepo na kuponya watu kwa jina lako. (Wakimaanisha alafu sio wanafunzi wako).

7. Yesu akajibu akawaambia, Wapo kondoo walionje ambao hawapo hapa lakini ni kondoo wa zizi hili.

8. Kisa hiko ni kisa cha umiliki na maslahi.

9. CCM wanaamini kuwa Wao ndio pekee wanahaki ya kumiliki nchi hii huku vyama vingine wakionekana kama wapangaji.
Jambo hili linanyima haki vyama vingine.

10. CCM lazima waelewe vyama vingine navyo vinahaki sawa na wamiliki wa nchi hii.

11. CHADEMA nao wamejikuta katika hali hiyohiyo ya wao kujifanya wamiliki wa ukweli, haki na demokrasia.

12. Chadema wanaamini kwamba huwezi kuwa mpenda Ukweli, demokrasia na mpenda Haki ukiwa nje ya CHADEMA.
Jambo ambalo kama Mtibeli na watibeli wote waliopo siasani na wasio siasani tunalikataa.

13. Wanafunzi wa Yesu waliamini ili uponye na kutoa mapepo lazima uwe mwanafunzi wa Yesu lakini pili waliamini kwamba wao wanammiliki Yesu.
Lakini walipokutana na watu wengine huko duniani ambao hawajawahi hata kuwaona wakiponya, na wakitoa Pepo Kwa jina la Yesu ikawapa kihoro na hasira.

14. Ubaya hauna Kwao. Kama ulivyo wema. Wapo Wabaya Chadema, na wapo Wabaya CCM. Wapo wema Chadema na wapo Wema CCM.

15. Chadema ni chama cha siasa. CCM ni chama cha siasa. Watanzania wanahaki ya kuwa chama chochote Kati ya hivyo au nje ya hivyo. Au wasiwe na Chama Kabisa.

16. CHADEMA pia wanatatizo la wao kutaka kusema Ukweli kwa wengine lakini wao hawataki kuambiwa Ukweli. Jambo ambalo tunarudi kulekule kwamba Ukweli kwao ni ule wanaousema wao sio unaosemwa na watu walionje. Hii kimantiki na masuala ya haki haipo Sawa.

17. Tabia ya kutaka maoni ya watu yafanane na mtazamo wa CHADEMA ni tatizo jingine linalowakabili Chadema.
Katika hilo wanakuwa hawana tofauti na CCM ambao nao unageuka adui yao pale unapowaambia ukweli wanakuhisi wewe ni CHADEMA au adui yao.

18. Demokrasia ni pamoja na kuheshimu maoni ya watu wengine bila kuwashambulia na kuwavunjia haki zao. Kuwatukana, kuwazushia n.k.

19. Unapopigania Demokrasia alafu muda huohuo hutaki mawazo ya wengine au unatukana wenye mawazo kinzani na yako unakuwa hujui maana ya Uhuru wa maoni na demokrasia.

20. Sisi Watibeli Tunajua Ukweli haumilikiwi na mtu, watu au taifa Fulani. Ukweli ni wawatu wote na unaweza kuupata popote.

21. Ukweli kwetu lazima uchunguzwe ili uthibitike.
Ndio maana Watibeli Wote. Unaweza kumkuta Mtibeli ni Muislam lakini hiyo haimaanishi haoni Ukweli na uongo uliopo kwenye Ukristo. Pia ataona kasoro na uongo katika Uislam na haoni shida kusema kasoro na uongo uliopo katika uislam hata kama ni dini yake.

22. Vivyohivyo, Mtibeli Mkristo lazima aone ukweli na uongo uliopo kwenye dini zingine ikiwemo uislam na kasoro zake.
Na pia katika Dini yake.

23. Halikadhalika na mambo ya vyama vya siasa. Watibeli sio mashabiki. Sio watu wakujiendea endea au kupelekwa pelekwa.

24. Sisemi watu wawe kama Watibeli, ila nazungumzia umuhimu watu kuyaangalia mambo vile yalivyo, bila ushabiki. Kutojimilikisha mambo ya watu wore.

25. Mfano kwenye jamii yetu;
Heshima ni haki na mali ya Kila mtu. Lakini utashangaa kundi au tabaka Fulani likijimilikisha heshima, kwamba wao ndio wanastahili kuheshimiwa.
Mfano Wazazi baadhi hutaka kuheshimiwa wao tuu lakini kuheshimu watoto wao wanaona mzigo. Hii sio sawa.

Pia viongozi wa Jamii na taifa baadhi yao hutaka wapewe heshima tuu. Alafu wao kutoa heshima hawataki au wanaona kama ni kujishusha.

26. Sisi Watibeli, Heshima inaanzia juu kwenda chini. Sio chini kwenda juu.
Wajuu akionyesha heshima ataheshimiwa. Sio atake heshima. Nope! Aonyeshe heshima. Mkubwa na wajuu ndio role model.

Kufikia hapo sina la ziada.

Sabato Njema Sana.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Thibitisha CHADEMA wanaamini huwezi kuwa mpenda haki, ukweli na demokrasia kama uko nje ya CHADEMA kama hizi sio porojo zako tu na kubwatuka hovyo.
 
Kwenye hiyo namba 15 yako nitatofautiana na wewe kwa kusema eti ccm nayo ni chama cha siasa! Labda wakati wa kuanzishwa kwake. Ila siyo sasa ambapo hiyo ccm imegeuka na kuwa genge la wahuni, mafisadi, wahujumu uchumi, matapeli, machawa, wala rushwa, watekaji, wauaji, na kila aina ya uovu.
 
Back
Top Bottom