Warioba: CCM ijiandae kuwa chama cha Upinzani

Unajua mkuu, kuna watu ni wagumu kuelewa ukweli na kuona vitu halisi, badala yake wanajilazimisha kuona vivuli tu..! Yaani pamoja na madudu yote ya CCM, bado kuna watu, tena bahati mbaya wengine hawana hata chembe ya ufisadi, kuhongwa au majinamizi ya siasa; ambao bado wanaamini kuwa CCM bado iko hai (it exists)!!

Tumewaleza muda mrefu ila hawataki kusikia...CCM ilikufa na akina Kolimba. Limebaki ghost fulani hivi ambalo watu kama hao niliowataja hapo juu wanadhani ndiyo CCM. CCM ambayo tuliiamini na kuitumikia ilizikwa siku nyingi tena kabla ya Mwalimu!

Wasiotaka kuamini hayo ama wana-motives zao za kifisadi au wanasumbuliwa na illusions!

Ngoja waendelee kujidanganya!

Nimekusoma mkuu, ikae ikifaamika kuwa CCM sio chama tena bali ni mfumo wa biashara.
 
Habari yenyewe nimeisoma yote sijaona mahali kasema hayo..

Wishing zako mkuu..endelea ku--dream
we nae unatakiwa ubadirike sasa uko so much in love na CCM.
Huyu jamaa kasema amesikiliza mahojiano na TBC1 wewe unasema
umesoma habari, huoni kama unarefer kwenye different source.

why, sababu tu uko in love.
Mapenzi yanaua
 
Naomba kutoa mawazo yangu hapa ktk jukwaa hili!,Mimi binafsi hakuna siku nitakayokuwa na raha ka siku CCM Kitakuwa chama cha upinzani nchini!
Kitakacho nifurahisha ni kuitwa jina hambalo hawajalizoea!
Pili watakavyokuwa wanyonge na kutoisha mahakamani!
Tatu watakapo pokonywa viwanja walivyovichukua kwajimilikisha wakati ilikuwa ni mali yaumma wakati wa chama kimoja!
Nne viongozi wake watakapo ambiwa warudishe nyumba za serikali!
Tano ni ukata utaokikabili chama hicho!
Sita wabunge wake waliopo kwa ajili ya matumbo yao watakavyo kihama nakubaki kikiwa kama yatima..
 
ccm kwa ilipofikia haiwezi kuwa chama cha upinzani.
kikishaondolewa madarakani kinakufa kabisa,sasa hivi si chama tena bali ni kampuni.

nashangaa ukienda brela hukuti usajili wake wakati inafanya biashara na viongozi wake ni wajasiriamali.

mwisho wao ni siku itakapoondolewa madarakani.
 
ccm kwa ilipofikia haiwezi kuwa chama cha upinzani.
kikishaondolewa madarakani kinakufa kabisa,
sasa hivi si chama tena bali ni kampuni.

nashangaa ukienda brela hukuti usajili wake wakati inafanya biashara na viongozi wake ni wajasiriamali.

mwisho wao ni siku itakapoondolewa madarakani.
Ni kweli kabisa. Siku waking'olewa madarakani, itawachukua miaka mingi sana kujipanga upya ukizingatia kuwa kuna vitegauchumi vingi walivyojimilikisha isivyo halali ambavyo itabidi virejeshwa serikalini km viwanja vya michezo Kirumba, Majimaji na majengo mengi tu. Upungufu wa mapato utawasambaratisha ukizingatia kuwa hakuna tajiri atakayeona umuhimu wa kuwachangia tena watakapokuwa nje ya serikali.
 
CCM kikiondoka madarakani ndo kitakuwa kimekufa rasmi maana CCM si chama cha siasa bali chama dola, kama hakina dola basi kinasambaratika.
 
Kwanza wanasubiriana kama sio kutegeana nani aanze kujitoa na kujiunga na vyama vingine........siku si nyingi hili litatokea na ndio utakuwa mwisho wake
 
Kila chenye mwanzo hakiachi kuwa na mwisho, tusome alama za nyakati. Kweli hili linawezekana na sio siku nyingi sana
 
kinadhalia ccm nichama tawala,kivtendo nichama cha upnzani.ikiwa mbunge 1 wa cdm nisawa na wabunge 30 wa ccm kuna nni hapo!
 
Back
Top Bottom