Mambo yanayoweza kuipeleka CCM kuwa chama cha upinzani 2025

koryo1952

JF-Expert Member
Mar 7, 2023
382
764
Sisi wananchi ndo wenye nchi na sisi ndiyo tulioiweka CCM kwenye uongozi lakini kadri mambo yanavyoenda inaonekana CCM haitujali imelewa madaraka. Yafuatayo ni mambo yanayoweza kuipeleka CCM kuwa Chama cha upinzani 2025.

(1) Ukosefu wa umeme. Hili ni tatizo. Umeme ni jawabu la asilimia kubwa katika maiisha ya binadamu. Kule kijijini akina mama wanatumia umeme kwa shughuli nyingi. Mfano mashine za kusaga unga n.k. Juzi nimeshuhudia mama akitoa machozi baada ya kukosa umeme wa kusaga unga. Analia akisema familia itakula nini?

(2) Sukari - Upatikanaji wa sukari umekuwa ni shida. Hakuna anayejali bei elekezi. Wananchi wanateseka na hakuna pa kukimbilia.

(3) Miradi isiyoisha - Kila siku tunaaminishwa kuwa mradi fulani ifikapo mwezi fulani utakuwa umekamilika. Kumbe hii ni danganya toto. Nitoe mifano michache. Mradi wa treni wa mwendokasi toka Dar mpaka Morogoro. Tuliaminishwa mradi utaanza kazi mwaka 2022 mpaka leo hakuna kinachofanyika. Mradi wa JNHHP tuliambiwa mradi utaanza 2022 mpaka leo ni kimya. Tunaambiwa mashine mbili zitawashwa tarehe 16.2.2024 mpaka leo kimya licha ya danadana ya hapa napale. Miradi ya SGR, daraja la Magufuli yote haya yanasuasua. Kwa nini?

(4) Ukosefu wa upatikanaji wa dollar - Chochote tunachotakiwa kuagiza toka nje tunatumia dollar. Sukari inayotakiwa kuagizwa inatakiwa tuwe na dollar za kutosha. Je dollar ziko wapi?

(5) Mikopo - Kila kukicha ni kukopa. Sisi wananchi hatuoni tija inayoletwa na mikoo hiyo. Mfano juzi Serikali imekopa 968bn. Mbona mikopo imekuwa mingi sana?

(6) Watendaji wetu siyo wazalendo. Fuatilia ripoti ya CAG. Kila mahali kuna upotevu wa fedha za Serikali na hakuna hatua inayochukuliwa.

(7) Ziara ya Ndugu Makonda- Ukifuatilia ziara ya Ndugu Makonda utagundua jinsi wananchi wanavyoteseka. Wananchi wananyanyaswa. Hakuna utawala bora. Hii yote Serikali inaona na imekaa kimya.

Kutokana na haya niliyoyataja CCM inaweza kuwa Chama cha upinzani mwaka 2025. Mnatakiwa mjirekebishe vinginevyo wananchi wamechoka.
 
Kwa katiba hii, wananchi hawana uwezo wowote wa kuchagua viongozi, lakini rais awe muungwana akubali matokeo halali, lakini nguvu hiyo ya kura haipo. Nguvu pekee waliyonayo wananchi ni kufanya machafuko kwa ajili ya mabadiliko, lakini sio kwa njia ya kura maana hiyo ni kupoteza muda.
 
Endelea kuota,hamna chama cha kuwaondoa hapo chama twawala.
Wapo mpk siku yakufa kwako.
 
CCM itaendelea kutawala tu kwa sababu ya udhaifu wa vyama vya upinzani, na ujinga wa watanzania walio wengi!

Wewe mtu unaepingana nae kila siku, na unajua anakudharau eti unaenda kufanya nae maridhiano

Mtu ukipewa kipande cha khanga unasahau matatizo yako yote

ACHA CCM ITAWALE TU
 
Back
Top Bottom