Warioba: CCM ijiandae kuwa chama cha Upinzani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Warioba: CCM ijiandae kuwa chama cha Upinzani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dark City, Oct 13, 2011.

 1. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Wakati anaohijiwa na mwandishi wa TBC1 Asumpta Masoi, Jaji Joseph Warioba alisema kuwa kama CCM haitamaliza matatizo yake ya ndani basi ijiandae kukabiliana na hali ngumu huko mbele.

  Amesema kuwa, kwa kuwa tumeukubali mfumo wa vyama vingi na pia kwa kuwa watu wengine wameanza kuichoka CCM na wapo pia wanaotaka mabadiliko, CCM itegemee kuwa mabadiliko yanatatokea tu na yataiweka kando. Na kwamba wasipoiangalia upya dira na itikadi za chama basi itakuwa vingumu kupona!

  Kwa jinsi ninavyowajua CCM, watakurupuka kumtukana Warioba badala ya kuangalia kile alichokisema, ingawa hakusema jambo lolote jipya!
   
 2. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,025
  Likes Received: 3,051
  Trophy Points: 280
  Wenye masikio na wamesikia kasoro Nape
   
 3. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Hata ile alama ya JEMBE NA NYUNDO kwenye bendera yao waiondoe. Waweke alama ya noti na ya mtu anakimbizwa (Mwizi)...

  Warioba huyu kawa kigeugeu sana, juzi alitishiwa kufungwa na dhahabu alizoiba akaja na hoja ya CDM wana fujo, leo kaja na ushauri nasaha. Hawa wazee tumewachoka, hakuna kitu tangible walichotuachia zaidi ya maneno yao ya kinafiki
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  sijui ni mimi tu but i feel like its fate....ccm wako on their way out.......
   
 5. T

  Topical JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Habari yenyewe nimeisoma yote sijaona mahali kasema hayo..

  Wishing zako mkuu..endelea ku--dream
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Nadhani hiyo alama walishaiweka siku nyingi na kila mtu anaiona isipokuwa wale waliokunywa maji ya bendera. Ni hadithi ya mfalme yuko uchi au la!!!
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu umengalia mahojiano ya Warioba na huyo mwandishi kwenye habari za TBC1 saa 2 usiku? Katika hoja ya kwanza alilinganisha vijana wa zamani (enzi zao) na wa sasa...Akasema wa zamani walikuwa makini sana kuliko sisi. Na katika hoja ya pili ndio akaongelea CCM. Kama hujatazama hiyo habari basi fuatilia.

  Sina sababu ya kuwasingizia CCM kwani ni sawa na kuua maiti!
   
 8. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,173
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280

  Kwa hiyo wewe ndiyo ulikuwa unasoma habari TBC1?
   
 9. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,088
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  kazi ipo watanzania tujiandae kwa mabadiliko hakuna wakutuletea isipokua ni sisi wenyewe tusiishie kuonge jamvini tu
   
 10. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Ndo matatizo ya kukurupuka...

  Kalinganisha TBC na gazeti la uhuru
   
 11. Ngadu

  Ngadu Senior Member

  #11
  Oct 13, 2011
  Joined: Oct 10, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  unafiki tu umewajaa hao wazee
   
 12. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  tumeshaambiwa tumhurumie nape kwani ni mbuzi wa kafara yule. Ni kisemeo cha 'mfumo'
   
 13. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ujira wa kutetea majangiri mchezo!!!!
   
 14. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,391
  Trophy Points: 280
  Mkuu miaka 50 hujaichoka tuu ccm?hujaona watoto wa shule sikonge tabora tangu shule ijengwe mwaka 1976 leo ndiyo wanafunzi wamepata dawati la kusomea lililofadhiliwa na wauza bangi sorry tumbaku Alliance company ya mzungu?hembu tafakari kaka usiogope hako ka mrija kako ka ufisadi hakatakatwa ikiwa upinzani utaingia madarakani
   
 15. m

  ma2ngwa Member

  #15
  Oct 13, 2011
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  jamani tusijazane mambo ya kijinga tunalia na maisha magumu na kutaka mabadiliko lakini unafiki ndo unatumaliza kwa kuwa hata ukifika wakati wa kupiga kura watu hawaendi sasa nani alaumiwe wewe ambaye hukupiga kura ya mabadiliko ama kiongozi aliyechaguliwa na wajinga wachache?

  Tafakari!!!!!!!
   
 16. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo kama hujaona kasema ndiyo unajipa matumaini.
   
 17. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #17
  Oct 14, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,763
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwenye red hapo ndo umemaliza kabisa.
   
 18. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #18
  Oct 14, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Unajua mkuu, kuna watu ni wagumu kuelewa ukweli na kuona vitu halisi, badala yake wanajilazimisha kuona vivuli tu..! Yaani pamoja na madudu yote ya CCM, bado kuna watu, tena bahati mbaya wengine hawana hata chembe ya ufisadi, kuhongwa au majinamizi ya siasa; ambao bado wanaamini kuwa CCM bado iko hai (it exists)!!

  Tumewaleza muda mrefu ila hawataki kusikia...CCM ilikufa na akina Kolimba. Limebaki ghost fulani hivi ambalo watu kama hao niliowataja hapo juu wanadhani ndiyo CCM. CCM ambayo tuliiamini na kuitumikia ilizikwa siku nyingi tena kabla ya Mwalimu!

  Wasiotaka kuamini hayo ama wana-motives zao za kifisadi au wanasumbuliwa na illusions!

  Ngoja waendelee kujidanganya!
   
 19. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #19
  Oct 14, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  itakuja kama UDP,hata wakiiba kura haitafika robo
   
 20. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #20
  Oct 14, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mwita 25! Najua huwezi kuona hadi kale kagamba kalikobaki kakutoke! Najiuliza ni kwanini Mods hawakuiunganisha hii ID na ile ya Mwita Mbwa!
   
Loading...