GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,646
- 109,034
"Nilipokuwa Mdada na kuona Maisha yangu hayaeleweki niliamua kupambana ili niende Nje ya nchi nikiamini huko ndiko kuna Maisha mazuri ila najuta kwani niliishia kuwa Kahaba ( Malaya ) kwa Miaka miwili hadi kuamua kurejea nchini Tanzania ambako nimegundua kama ukijipanga hapa kuna Maisha mazuri kuliko huko Nje za nchi ambako huwa tunakimbilia na Wengi wetu huishia kuwa Makahaba ila huwa tunaficha na tunawaficha Ndugu, Jamaa na Marafiki zetu huku Nyumbani Tanzania" amesema Waridi wa BBC Suzana Michael leo katika Amka na BBC.
Bora amesema huyu Dada ( Suzana Michael ) labda sasa mnaweza mkamsikiliza na kubadilika kwani Sisi akina GENTAMYCINE tukiwaambia acheni Kuhangaika kwenda huko Ng'ambo kwani hapa hapa Kwetu Tanzania ukiwa tu na Mipango, Mikakati na Ukijiamini Kuna Maisha mazuri zaidi ya yale yaliyoko huko ambako huwa mnadanganyika nao kuanzia katika Sinema ( Movies ) zao mnazozitizama Kutwa.