Kama una ndoto ya kwenda Ulaya, Marekani, Canada n.k, pitia uzi huu

Jebel

JF-Expert Member
Jul 10, 2021
306
2,041
Salamu kwenu nyote.

Kikwetu tunasema, “ndege asiyeruka hawezi kujua wapi ulezi umekomaa”.
Leo ninapenda kuwapa ABC za namna ya kufika nchi za wenzetu kwa wale wenye ndoto za kubadili mazingira ya Tanzania na kwenda nje kutafuta.

Binafsi nimeishi nchi kadhaa za wenzetu kwa vipindi tofauti na kwa sababu tofauti. Nimeishi UK(3yrs), Italy(3yrs), Spain(1yr), UAE(1.5yr). Lakini pia nimefanya kazi za mda mfupi katika nchi anuai kama Germany, France, Portugal na Austria. Nimetembelea pia nchi nyingi, Europa, Middle East, Far East(S. Korea), USA na visiwa vya St. Lucia.

Katika uzi huu nitakupeni nchi chache ambazo ni nzuri kutoboa kama ukifika, nitakupeni mbinu za kufika huko na nitakupeni shughuli za kuweza kufanya kama ukifika huko.

Hapa chini nimekuwekea nchi kadhaa ambazo ni tija sana kwa mtu ambaye anawaza kwenda nje. Nchi nzuri kiutafutaji, usalama na wepesi wa maisha.

1. South Korea. Nchi hii kama mtu ana ndoto ya kwenda nje kutafuta maisha basi nafasi ya kwanza kuwaza na Kusini mwa Korea.
-Nchi hii nimeiweka nafasi ya kwanza kwa sababu zifuatazo
1. Nchi yenye viwanda vingi
2. Uchumi wake ni mzuri sana
3. Uhaba wa nguvu kazi shauri ya jeografia yake
4. Malipo mazuri kwa wafanyakazi
5. Nchi salama kuishi na ubaguzi siyo mkubwa
6. Rahisi sana kupata kazi/Lazima kupata kazi
South Korea ni nchi ambayo kwa jeografia yake ipo mbali sana na “labour zone countries” ambazo ni bara lote la Africa, India, Bangladesh, Pakistan, Srilanka na Latin America.
Uhamiaji katika nchi hii ni mdogo sana ukikinganisha na nchi za Ulaya, USA na Canada
Malipo kwa kazi nyingi za nguvu yaani non professional jobs au manual works ni kuanzia $50/hr.
Changamoto; namna ya kuingia katika nchi hii. Zipo namna mbili au tatu za kukusaidia kufika Korea Kusini ambazo ni
A. Uende kama mwanafunzi- hapa utahitaji kupata udhamini wa kimasomo, na student visa. Kama bado upo shule au chuo unaweza kujaribu bahati yako

B. Uende kama mtalii- hapa itakupasa kuwa na tourist visa ambapo utatakiwa ku prove uwezo wako kiuchumi kama kweli unaweza ku afford kwenda na kurudi na kulipia gharama za accomodation ukiwa katika ardhi ya Korea; uthibitisho huu utautoa katika embassy ya Korea kusini nchini Tanzania.

C. Uende kama mkimbizi- hii ndo njia rahisi ambayo nimeona watu kadhaa wanautumia na imewasaidia kufanikisha ndoto zao kuingia ktk nchi hii ya Korea. Katika njia hii mkimbizi utatakiwa uombe hifadhi ktk nchi ya Korea kwa kutoa sababu ya kukimbia nchi yako. Wachache niwajuao wamewahi kutoa sababu za kiusalama kwamba wanawindwa ktk jamii kutokana na sexual orientation zao. Lakini hao niwajuao wote ni straight hivyo njia hii imetumika kiujanja tu. Hapa sintaingia ndani sana kuepusha maswali lakini binafsi nakubaliana na Machiavelli anaposema “la fine si giustifica il mezzo” yaani “the end justifies the means”.

Kazi za kufanya: kutokana na wingi wa viwanda na uhaba wa nguvu kazi kuna kazi nyingi za kufanya kwenye viwanda, supermarkets, car wash n.k. Kazi zote malipo ni mazuri sana.

NB: LUGHA KTK TAIFA HILI NI CHANGAMOTO KWANI WACHACHE WANAONGEA KI ELIZABETH

2. Canada. Hii nchi ndo namba mbili kufikiria kama kweli mtu unafikira ya kwenda nje kusaka tonge. Lugha mbili zinatumika sana ktk nchi hii; KiElizabeth na Kifransa.

Canada nayo kama ilivyo Korea Kusini, ina uchumi mzuri, pesa ina thamani, ubaguzi hakuna, wakimbizi wachache, fursa bado zipo, nchi salama na gharama ya maisha ktk miji mingi ipo chini sana.

Ajira bado ni nyingi sana kwa profesional personales na non professionals. Kuna shughuli nyingi za kutunza wazee, mashambani, viwandani, usafi n.k.

Namna ya kufika katika nchi hii.

Kwenda Canada ni rahisi nadhani kuliko kwenda nchi nyingine yoyote ile duniani. Wepesi wa kufika Canada unatokana na ukweli kwamba hii nchi inatoa nafasi nyingi kwa watu wanaopenda kwenda kusoma katika taifa hili.

Ni rahisi sana kama mtu unaweza kupata kiasi kidogo cha pesa cha kufanya maombi ya kujiunga na chuo kikuu chochote kinachopokea international students. Hapa ni lazima ujue programs na courses ambazo ni rahisi kupata nafasi ambapo nyingi sana ni zile zinazohusiana na Elimu Ahera. Ukishapata nafasi utatumiwa documents za kuprocess visa, kisha utakata ticket na kutinga Toronto au Vancouver. Simple sana.

Lakini pia unaweza kwenda kama tourist na kishafika kule unaprocess visa ya kuishi na kufanya kazi Canada.

Kwa leo naishia hapa kwanza, nitaendela na kuangazia mataifa ya USA, Germany na UAE.

“La Aquila non capit muscas”.

:::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::

SEHEMU YA PILI.

Namna kufika Germany na UAE na shughuli za kufanya.

Germany- Kwanza kwa asiyefahamu, Ujerumani ni nchi inayoongozwa na maneno ya Paulo Mtume aliyowaandikia Wathesalonike katika barua ya 2; 3:10. “Asiyefanya kazi na asile”.
Ukiwa Germany ni mwiko kuishi bila kufanyakazi yoyote. Sijui kama sera imeshabadilika lakini wakati naenda kupiga kazi wakati wa kiangazi, ilikuwa mhamiaji akikamatwa anazurula....anakamatwa na kupewa kazi yoyote ili ale chakula kwa kukifanyia kazi. Kuombaomba na kupewa bure katika nchi hii ni dhambi. Napendekeza mtu kwenda katika nchi hii kwani kupata kazi ni rahisi.
Kwa Ulaya au nje ya nchi hakuna kitu cha muhimu Kama kuwa na kazi. Hii ndo sababu nashauri sana kuangalia nchi ambazo itakuwa rahisi kupata kazi.
-Namna ya kufika Germany. Nchi hii ni mojawapo ya nchi zinazounda Umoja wa Ulaya(European Union).
-Kwa hiyo ukiweza kupenya mojawapo ya taifa linalounda umoja huu basi inakuwa rahisi sana kuingia Germany.
-Unaweza kwenda kama mtalii wa nchi mojawapo ya taifa la EU kisha ukazamia Germany kusaka sega la asali.
NB: Ukikamatwa Germany na passport lazima urudishwe nchini mwako mara moja kwa gharama zao. Sera hii ipo pia Switzerland and Netherlands.
-Kwa hiyo cha kufanya, ukifika nenda Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani, wapatie passport yako halafu utakapoamua kurejea nchini tena itakubidi kuifuata ubalozini.
-Germany pia inatoa nafasi za masomo kwa hiyo unaweza kujaribu bahati yako kuomba udhamini.
-Kiingereza kinaongelewa lakini ukifahamu Kijerumani utakuwa katika nafasi nzuri sana.
(Nakumbuka namna nilivyopata chance ya kuwa naenda kupiga kazi Germany, ni baada ya siku moja kuwa na mazungumzo na Mjerumani mmoja ambaye alikuwa ni visiting lecturer chuoni kwetu. Aliponiuliza natokea wapi nikamjibu Tanzania halafu nikaongezea, moja ya nchi iliyotawaliwa na babu yako...nilifanya hivyo in an amazing casual way kiasi kwamba aliniona mtu cheerful nisiye na resentments. Tulitokea kuwa mabest sana na hata kuwa ananifanyia michongo ya kazi zenye malipo matamu).
Mwisho ukiwa Ujerumani-fanya kosa lolote lakini siyo kuchelewa chelewa. Uchelewaji ni kitu Mjerumani hawezi kuvumilia. “Be obedient to Kantian punctuality”.

UAE (United Arab Emirates)
Kwa asiyefahamu, unaposema una maanisha muunganiko wa vinchi saba ambavyo makao makuu yake yapo Abu Dhabi. Kiongozi Mkuu pia yupo Abu Dhabi huku msaidizi wake akiishi Dubai.
Abu Dhabi ndiyo imeshikilia uchumi mkubwa kwa sasa ikifuatiwa na Dubai kisha Sharjah.
Umoja huu, mbali na Abu Dhabi, Dubai na Sharjah, unajumuisha pia Ajman, Umm Al Quwain, Fujairah na Ras Al Khaimah.
-Wale vijana wa Ilala wanaofuata spea za magari Dubai, chimbo lao lipo Sharjah.

Namna ya kufika- Wepesi wa kufika Dubai ni kwamba kama unatokea Tanzania unaweza kwenda bila visa na ukakata visa on arrival. Kwa maana hii Mtanzania yeyote anaweza kutinga Dubai bila shida yoyote.
-Unaweza kwenda kama mtalii kwa kukata visa ya miezi3 au 6 na kishafika kule ukaprocess working na resident permit. Visa hii utahitajika kukata ticket mbili yaani go and return lakini kwa sasa technology itakusaidia kwa kukata ticket moja ya go na return unaweza kupata “DUMMY TICKET”.
-Pamoja na kuwa una vinchi saba, binafsi napendekeza Dubai kwa sababu zifuatazo;
  • Mchanganyiko wa watu wa mataifa mengi
  • Ni mji ambao ni very westernized
  • Uchumi ni mzuri na kazi bado zipo japo competition ni kubwa sana kutokana na kuzungukwa na labor-zone states yaani Africa, India, Pakistan, Afghanistan, Srilanka, Bangladesh, Lebanon, n.k.
  • Gharama ya maisha ipo chini sana ukilinganisha na nchi nyingi zilizoendelea
  • Thamani ya pesa ni nzuri sana (1AED=630Tsh)
  • Ni karibu sana hivyo panafikika(nauli inafika hadi chini ya laki5 za Kitanzania)
  • Ni rahisi sana kutuma pesa nyumbani kutokea Dubai
  • Kuna sehemu za kuabudi za wahindi ambapo wanatoa breakfast, lunch na dinner bure kabisa hivyo kwa mzamiaji unaweza kuishi kwa kuvizia mlo sehemu hizo.
>Ukiwa Dubai unaweza kufanya kazi za kuajiliwa kama vile Ulinzi, Usafi, Ujenzi n.k au unaweza kujiajili mwenyewe kwa kufanya shughuli zifuatazo
>Unaweza kuingia mjini kati yaani Deira City Centre na ukapiga kazi ya kupakia na mizigo kwenye magari.
>Unaweza kufanya kazi ya kusukuma toroli la mizigo katikati ya mji hasa hasa Deira
>Unaweza pia kujiajili kuuza nguo, mikoba ya wanawake, Viatu nk, ambapo itakubidi ujue machimbo ya wachina unapoweza kupata mzigo kwa bei nafuu...sehemu kama Baniyan Square shughuli hii inapigwa sana na waafrica.
>Kuna wa Wabongo wengi pia maeneo kama Etisalat wanapiga shughuli ya kuuza mishikaki, vitumbua nk.
>Kama wewe ni risk taker unaweza pia kupiga deal la kuuza pombe; kikubwa ni kujua chimbo la kupata mzigo zaidi Sharjah na sehemu ya kuuzia. Hii kazi inalipa sana.

Mwisho kwa mtu anayewaza kutoka nje ya nchi Dubai ni sehemu ya kufikiria kuanzia kabla ya kuwaza kwenda kuishi katika taifa kubwa kama .
Maisha ya Dubai na Bongo binafsi sikuuona utofauti mkubwa sana.

Next time nitakuelezeeni namna ya kufika USA na naamini kila mtu anapenda sana. Kwa kila mwaka huwa nasaidia walau watu 2 kufika USA na huu ni mwaka wa 3 nafanya hivyo.

“Aquila non capit muscas”
 
Nyumbani ni nyumbani bongo ndio home, kiwanja nikafanye nini/ maharage nayapeda sana kuliko nyama, jomba hasani washa koroboi humu ndani mbu wamezidi, wanang'ata mpaka visigino

Shibe shibe hainogi
Shibe shibe hainogi
Nyumbani ni nyumbani
Hainogi
Hata kama kichakani
Hainogi
Wanaume?
 
Nchi zote ulizotaja watu wake wanajanaza USA kila leo wewe huiweki US namba moja how?

Wabongo wanaosoma kimombo hadi chuo kikuu na bado kinawashinda leo unataka waende SK ambako hawajui hata salam zao!

Mtu yeyote anayetaka kwenda nje should first shoot for the stars (USA) if they fail ndo waende huko vichochoroni huko. There's a reason US ni superpower.

Aidha SK haina wageni wengi sio sababu ya its geographical location bali hawana utamaduni wa kujichanganya na wageni. This is also true kwa Japan. Watu wanaenda Greenland huko ndo iwe Sk tu hapo? Ukienda SK jiandae kwa maisha ya kipweke na box tu.
 
Kweli lakini km per hour unakula $50 si bora uendelee tu huku unajaza kibubu,

Mfano let say ukifanya kazi kwa masaa 10 means una $500 per day unahisi ni ndogo hio?

$500×30=15000
Mwezi mmoja unaingiza $15000

Sio kidogo hio?

Za kuambiwa changanya na zako. There's more to life than money.

There's a reason wakorea wenyewe na watu wa mataifa mengine wanakimbilia US. Kuna Korean towns kibao in the USA na Canada.

View: https://youtu.be/M7TNP2OTY2g?si=RbDSSUh1ewm6hMTa
 
Sawa mkuu tunashkuru kwa taarifa.
Mimi elimu yangu ni kidato Cha nne, ( non professional) nawezaje kwenda nchi yoyote ya UAE au Qatar kufanya kazi ya ulinzi? Nisaidie kwenye eneo hili kama una uzoefu unipe msaada

Hauwezi kupata kazi kule bila wakala, maana ukipata matatizo wakala ndo anasimamia show. Wakala anataka hela kama laki sita hivi
 
SEHEMU YA PILI.

Namna kufika Germany na UAE na shughuli za kufanya.

Germany- Kwanza kwa asiyefahamu, Ujerumani ni nchi inayoongozwa na maneno ya Paulo Mtume aliyowaandikia Wathesalonike katika barua ya 2; 3:10. “Asiyefanya kazi na asile”.
Ukiwa Germany ni mwiko kuishi bila kufanyakazi yoyote. Sijui kama sera imeshabadilika lakini wakati naenda kupiga kazi wakati wa kiangazi, ilikuwa mhamiaji akikamatwa anazurula....anakamatwa na kupewa kazi yoyote ili ale chakula kwa kukifanyia kazi. Kuombaomba na kupewa bure katika nchi hii ni dhambi. Napendekeza mtu kwenda katika nchi hii kwani kupata kazi ni rahisi.
Kwa Ulaya au nje ya nchi hakuna kitu cha muhimu Kama kuwa na kazi. Hii ndo sababu nashauri sana kuangalia nchi ambazo itakuwa rahisi kupata kazi.
-Namna ya kufika Germany. Nchi hii ni mojawapo ya nchi zinazounda Umoja wa Ulaya(European Union).
-Kwa hiyo ukiweza kupenya mojawapo ya taifa linalounda umoja huu basi inakuwa rahisi sana kuingia Germany.
-Unaweza kwenda kama mtalii wa nchi mojawapo ya taifa la EU kisha ukazamia Germany kusaka sega la asali.
NB: Ukikamatwa Germany na passport lazima urudishwe nchini mwako mara moja kwa gharama zao. Sera hii ipo pia Switzerland and Netherlands.
-Kwa hiyo cha kufanya, ukifika nenda Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani, wapatie passport yako halafu utakapoamua kurejea nchini tena itakubidi kuifuata ubalozini.
-Germany pia inatoa nafasi za masomo kwa hiyo unaweza kujaribu bahati yako kuomba udhamini.
-Kiingereza kinaongelewa lakini ukifahamu Kijerumani utakuwa katika nafasi nzuri sana.
(Nakumbuka namna nilivyopata chance ya kuwa naenda kupiga kazi Germany, ni baada ya siku moja kuwa na mazungumzo na Mjerumani mmoja ambaye alikuwa ni visiting lecturer chuoni kwetu. Aliponiuliza natokea wapi nikamjibu Tanzania halafu nikaongezea, moja ya nchi iliyotawaliwa na babu yako...nilifanya hivyo in an amazing casual way kiasi kwamba aliniona mtu cheerful nisiye na resentments. Tulitokea kuwa mabest sana na hata kuwa ananifanyia michongo ya kazi zenye malipo matamu).
Mwisho ukiwa Ujerumani-fanya kosa lolote lakini siyo kuchelewa chelewa. Uchelewaji ni kitu Mjerumani hawezi kuvumilia. “Be obedient to Kantian punctuality”.

UAE (United Arab Emirates)
Kwa asiyefahamu, unaposema una maanisha muunganiko wa vinchi saba ambavyo makao makuu yake yapo Abu Dhabi. Kiongozi Mkuu pia yupo Abu Dhabi huku msaidizi wake akiishi Dubai.
Abu Dhabi ndiyo imeshikilia uchumi mkubwa kwa sasa ikifuatiwa na Dubai kisha Sharjah.
Umoja huu, mbali na Abu Dhabi, Dubai na Sharjah, unajumuisha pia Ajman, Umm Al Quwain, Fujairah na Ras Al Khaimah.
-Wale vijana wa Ilala wanaofuata spea za magari Dubai, chimbo lao lipo Sharjah.

Namna ya kufika- Wepesi wa kufika Dubai ni kwamba kama unatokea Tanzania unaweza kwenda bila visa na ukakata visa on arrival. Kwa maana hii Mtanzania yeyote anaweza kutinga Dubai bila shida yoyote.
-Unaweza kwenda kama mtalii kwa kukata visa ya miezi3 au 6 na kishafika kule ukaprocess working na resident permit. Visa hii utahitajika kukata ticket mbili yaani go and return lakini kwa sasa technology itakusaidia kwa kukata ticket moja ya go na return unaweza kupata “DUMMY TICKET”.
-Pamoja na kuwa una vinchi saba, binafsi napendekeza Dubai kwa sababu zifuatazo;
  • Mchanganyiko wa watu wa mataifa mengi
  • Ni mji ambao ni very westernized
  • Uchumi ni mzuri na kazi bado zipo japo competition ni kubwa sana kutokana na kuzungukwa na labor-zone states yaani Africa, India, Pakistan, Afghanistan, Srilanka, Bangladesh, Lebanon, n.k.
  • Gharama ya maisha ipo chini sana ukilinganisha na nchi nyingi zilizoendelea
  • Thamani ya pesa ni nzuri sana (1AED=630Tsh)
  • Ni karibu sana hivyo panafikika(nauli inafika hadi chini ya laki5 za Kitanzania)
  • Ni rahisi sana kutuma pesa nyumbani kutokea Dubai
  • Kuna sehemu za kuabudi za wahindi ambapo wanatoa breakfast, lunch na dinner bure kabisa hivyo kwa mzamiaji unaweza kuishi kwa kuvizia mlo sehemu hizo.

    -Ukiwa Dubai unaweza kufanya kazi za kuajiliwa kama vile Ulinzi, Usafi, Ujenzi n.k au unaweza kujiajili mwenyewe kwa kufanya shughuli zifuatazo

    -Unaweza kuingia mjini kati yaani Deira City Centre na ukapiga kazi ya kupakia na mizigo kwenye magari.
    -Unaweza kufanya kazi ya kusukuma toroli la mizigo katikati ya mji hasa hasa Deira
    -Unaweza pia kujiajili kuuza nguo, mikoba ya wanawake, Viatu nk, ambapo itakubidi ujue machimbo ya wachina unapoweza kupata mzigo kwa bei nafuu...sehemu kama Baniyan Square shughuli hii inapigwa sana na waafrica.
    -Kuna wa Wabongo wengi pia maeneo kama Etisalat wanapiga shughuli ya kuuza mishikaki, vitumbua nk.
    -Kama wewe ni risk taker unaweza pia kupiga deal la kuuza pombe; kikubwa ni kujua chimbo la kupata mzigo zaidi Sharjah na sehemu ya kuuzia. Hii kazi inalipa sana.

    Mwisho kwa mtu anayewaza kutoka nje ya nchi Dubai ni sehemu ya kufikiria kuanzia kabla ya kuwaza kwenda kuishi katika taifa kubwa kama .
    Maisha ya Dubai na Bongo binafsi sikuuona utofauti mkubwa sana.

    Next time nitakuelezeeni namna ya kufika USA na naamini kila mtu anapenda sana. Kwa kila mwaka huwa nasaidia walau watu 2 kufika USA na huu ni mwaka wa 3 nafanya hivyo.

    “Aquila non capit muscas”
 
Sawa mkuu tunashkuru kwa taarifa.
Mimi elimu yangu ni kidato Cha nne, ( non professional) nawezaje kwenda nchi yoyote ya UAE au Qatar kufanya kazi ya ulinzi? Nisaidie kwenye eneo hili kama una uzoefu unipe msaada

Tafuta passport na fedha at least 1 M nenda kajilipue kama mtalii utapata 90 visa.
Ndani ya hizo siku 90 jitahidi upate kazi ukikosa itabidi urudishwe kama mtalii uliyefilisika
 
Back
Top Bottom