Mkandara,ccm imekuwa kama nyani anayekufa,kama unavyojuwa,huwa nyani huyo hujaribu kukamata matawi ya miti ili kujiepusha kwenda chini kwenye safari hiyo ya kifo.
CCM,imeamuwa kuwatumia waislam kama matawi ya miti ya kujishikilia inapoanguka kwenye kifo chake.Ni wajibu wetu kuangalia ni kivipi hilo halitotokea.Ni wazi wata capitalize kwenye maeneo ya waislam ili kuzidi kuleta ile chuki pamoja na kuhaikisha wanakufa na wengine.Nguvu zao zote watazielekeza kwenye kushikilia matawi hayo(waislam).
Wanachotakiwa kufanya chadema,ni kuendeleza mapambano haya kama kawaida.Kama kunawatakaokuja na waje(waislam,wakristo,wakristu,wapagani etc),ila si vyema wajikite kwenye kujaribu kuonyesha hili ama lile ili kupata sura ya kuwafurahisha watu wa imani hii ama ile.
Kama chadema inapita nchi nzima,na kusikiliza matatizo ya watanzania,basi watakutana na maoni hayo kama yapo.
Ushahidi upo wazi kabisa na kama unakumbuka,JK kwa kupitia yule Rashid Shamte,walituma zile message zilizopanda chuki hizi.Na funny enough,kuna waliozinunuwa na kuziamini
Halafu kuna maopportunist kama mh Zitto,yeye nadhani anasikia raha sana kufikia hapo alipo bila kutumia dini yake,lakini anataka kufanikisha malengo yake ya juu zaidi kwa kutumia hilo hilo la dini.Na nilishasema huko nyuma kuwa chadema ina waislam wengi tu,la muhimu ni kuwarecruit wale ambao wana sifa za uongozi na pia wenye kuijali Tanzania na utaifa wao.Hao wako wengi tu.Cha muhimu,ni kuhakikisha si wabinafsi,maana kuna watu wanaitumia sana karata ya udini kufanikisha malengo ya binafsi na ya kisiasa.
Kwa kifupi,aliyoyasema
Semilong,nilishayasema vilevile,
kama chadema tayari ina waislam,basi ianze nao na si kwenda kujaribu kuwatafuta hao wasiokuwa na imani ama walioaminishwa hayo ya mafisadi wa ccm.
Ninakuhakikishia kabisa kuwa kama harakati hizi za ukombozi tutakuwa tunataka kubalnce viongozi based on religion affiliation,basi hilo linaweza kukwamisha ukombozi.Kwasababu kama tutawaondoa viongozi wenye uwezo na kupachika wasiokuwa na uwezo ili tu kuweka balance ya dini,basi hapo ni kupotoka na itakuwa sawa na kuondoa "eye on the prize",ama kwa kifupi ukombozi wa mtanzania unaweza ukawa jeorpodized,unapoweka viongozi kwa misingi hiyo.
Na kiongozi huyo akijuwa kuwa amewekwa hapo kwa misingi hiyo,basi sitoshangazwa kuona akitaka kubaki hapo kwa misingi hiyohiyo hata kama amevurunda,huko sidhani kama chadema inataka kwenda.
I'm just saying.