Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
- Labda wewe mkuu ndiye ungeanza kuelewa nilichoandika kwamba kwa kufanya haya Kanisa linawapa kila dini Tanzania kujiingiza kwenye siasa kwa visingizio vya kueilmisha waumuni siasa na kupiga kura, hiyo ni hatari sana kwa amani ya taifa kwa sababu sio dini zote zina-preach amani, ndio point yangu ya msingi, kwamba kama Pengo anahusika he is wrong! atatuchafulia amani na ninaamini sasa hivi watamuita CC na kumpa onyo zito.

- Tayari kwa wale wenye uchungu na taifa hili tumeshalifikisha kwa wahusika huko CC, tumepokea malalamiko mengi sana kuhusu hii ishu na tumewapelekea huko serikali na CCM, hili kanisa ni lazima liambiwe na kuonywa vikali sana.

FMEs!
FMEs!

Mazee mbona unajichanganya, hapo juu umesema eti Pengo alimchimba biti Membe ishu ya OIC ikasizi, sasa hivi unabadilisha kibao unasema eti CC watamuita Pengo na kumpa onyo kali..lol..Sasa nani mwenye power juu ya mwingine hapo..Duh.

Mazee back kwenye kuitana sijui kwenye CC, you are alarmed for nothing. Masuala ya kanisa kuhamasisha watu kushiriki kwenye uvchaguzi kikamilifu hayakuanza leo labda tu watu wengi mankurupukia hii ishu kwa kuwa sasa everyone is alarmed with ufisadi na ruling part is trying to defend and na kufight everyoneelse anayeonekana anataka kuwanyang'anya tonge mdomoni.

Program ni kuwahusu waumini kuhusu kuwahamasisha waparticipate fully kwenye machakato wa 2010. Kuwafanya waone turufu waliyonayo, umuhimu wake na jinsi gani wanaweza kuinfluence maisha yao kwa kufanya maamuzi sahihi. Ninachokiona hapa ni kuwa tabaka tawala linafeel the heat na ku-feel threatened, na hivyo kuanza kutapatapa.Hao CC kama wapo clever enough wangeanza kuweka mitigative measures za jinsi ya kushinda hizo kura badala ya kuanza kuitana kupeana maonyo. That will be useless.

Ninachoweza kusema kwa kumalizia, hii elimu ya uraia hata kama itapigwa vita 2010, time will come ambapo kila mwananchi ataamka na wale wote waliokuwa wakichukua advantage ya wananchi maskini vijijini the time has come kuangalia approach mpya na kuwa wawajibikaji na kuacha longolongo.
 
FMES,
Mkuu unaposema sio dini zote zina preach amani una maana gani?..samahani lakini!..

Abdulhalim,
Mkuu nimekusoma na nimeelewa unachojaribu kusema kuwaelemisha wanabodi.. Lakini pia nimeona mara nyingi ukiondoka ktk mada na kuongeza fikra zako binafsi ambazo pia hazijengi kitu zaidi ya kupotosha kabisa..
Mimi nataka kuelewa vitu vichache sana..
1. Hilo kanisa litatumia kipimo gani kuwapata hao wagombea wazuri..
2. Ni misingi ipi ya elimu ya Uraia wataitumia kuwaelimisha hao waumini wake..
3. Kama alivyosema FMES, Askofu Pengo kama askofu ni mwakilishi wa Vatican nchini, kushiriki kwake kunaweza kuleta utata zaidi..

Kifupi nakubaliana sana na hatua hii ya kanisa ikiwa tu elimu hii itatolewa na vyombo vinavyohusika na uchaguzi.. na vikigharamiwa na kanisa..Kama vile tunavyoona shule za kanisa walimu wake ni wale waliofuzu kufundisha elimu husika.. Hivyo kama utanambia kanisa litagharamia elimu hiyo ya uraia na uchaguzi kwa kufuata sheria za katiba ya nchi yetu na sii mafundisho ya kiongozi bora kulingana na matakwa ya kanisa hilo au Vatican..
 
Mimi sio Mkatoliki. Lakini mahubiri ya Padre Baptiste Mapunda ni somo la uraia zuri kwa Watanzania wote: Wakristo, Waislamu , Wahinduu, Budhists na wasiokuwa na dini, hasa wakati huu wa kujiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa 2010.

Aliyoyasema Padre Mapunda yangefaa yafundishwe katika makanisa yote, misikiti yote na mahala pote pa ibada nchi nzima. Hata waalimu wa shule zetu zote na wakufunzi wa vyuo vya elimu ya juu, ambao jukumu lao kuu ni kuendeleza maisha ya vijana wetu waweze kujitegemea kikamilifu, pamoja na kuwaimarisha katika uraia mwema, ingefaa waige huyu Padre na kufundisha yote aliyoyataja.

Nchi yetu inaelekea pabaya; na hatuna budi kama tunajali future ya Tanzania kwa dhati, kufuatilia yaliyosemwa na Padre Mapunda na kujiandaa kwa ujasiri kuleta mabadiliko ktk uongozi wa nchi ili tusiporomoke kabisa. Tumeshaanza kuporomoka!

Ni jukumu la kila asasi inayojali maendeleo mema ya wananchi, ili waondokane na "ujinga, maradhi na umaskini" kuwaelimisha wananchi wote ili wawe jasiri kuchagua viongozi walio hakika nao kwamba watawaletea maendeleo. Wananchi waelimishwe na wakazaniwe wajiandikishe kama wapiga kura. Wananchi waelimishwe kwamba kwa vyovyote vile wasipoteze shahada zao za kupigia kura au wasikubali kutoa shahada zao za kupigia kura kwa kiongozi yeyote kwa gharama yeyote ile. Shahada iwe ni silaha adimu na yenye thamani kubwa ya kumletea mwananchi uhuru kamili wa kuchagua mtu atakayebadilisha maisha yake na kumletea neema.

Wakati wa kampeni za uchaguzi, wananchi waambiwe kwamba Mgombea wa Chama chochote anayetoa hongo la fedha au chakula, nguo au kifaa chochote ili apigiwe kura, hafai; na asipigiwe kura. Waambiwe kwamba huyo akichaguliwa atatumia wakati wake wa uongozi kula mali ya umma kama kodi na fedha nyingine za serikali ili ajirejeshee zile gharama alizotumia kuhonga kupata uongozi. Akumbushwe kwamba viongozi ambao wame-reduce nchi yetu kuwa na umaskini wa kutisha, ni hao hao waliotajirika kwa kukwapua mafedha toka taasisi zetu za fedha.

Ningewasihi wachangiaji ktk blog hii ya JF waone kwamba huyu Padre Mapunda ni Raia mwema tu aliyejitolea mawazo ya kuimarisha umma na kwamba hana chama anachokipigia debe, au kiongozi anayempendelea. Ningegundua hivyo ktk mahubiri yake ningesema, amepotoka.
 
KIilasara,
Mkuu nakuunga mkono mara 100...tatizo ni kwamba Abdulhalim anashindwa kuangalia upande wa pili wanapotoa hoja zao na akawapa jawabu la kitu gani kinachokusudiwa kufanywa..

Kwanza kichwa cha mada hii pekee kinatisha.. Huwezi kuwaanda WAUMINI wako ktk uchaguzi (elimu ya uraia) hii inavuta matabaka baina ya dini na madhehebu yake.. Hatupo Iraq wala US ambako dini zinavutana kupata sera ambazo zinakubaliana na mafundisho ya madhehebu hayo..

Kama lengo kubwa la kanisa ni kutoa elimu kwa wananchi nchini kuhusiana na somo hili inge sound vizuri, lakini unapojitenga na kuchagua kundi la watu fulani kupata elimu ambayo hatufahamu ni vigezo vipi vinatumika inaleta mashaka sana na somo zima..mbona shule zao zinatoa elimu kwa watu wote iweje swala la uraia liwe kwa waumini pekee!
Kama wakifundisha elimu hii ya Uraia ktk shule zao ambapo watu wenye imani tofauti na kanisa hili wanaweza kufaidika na elimu hii, binafsi sioni ubaya lakini wanaposema waumini wake inajenga hisia za kwamba kanisa lina agenda zake.. kuwa elimu wanayokusudia kuitoa haihusiani na katiba ya nchi isipokuwa matakwa ya kanisa.
Ndivyo nilivyoelewa mimi kwa nini watu wengi wamekuwa na mashaka na dhamira ya kanisa hili..Kama Abdulhalim ataweza kuelewa upande wapili wanachofikiria nadhani itakuwa rahisi zaidi kuifikisha point yake.
 
Nadhani wacha wakaangwe na tuone ujasiri wao wa kusema na ndiyo muda wa kujua kama wakuu wa hizi dini wako kwa ajili ya watu ama matumbo yao na kukalia madaraka .Big test wacha tuone kitakacho fuata .Ndiyo muda wa wao ku fight udhalimu kwa nguvu zao na kupunguza kura za CCM kama wayasemayo ni kweli basi wazidi kuonyesha uovu wa CCM kila nyanja.
 
Mazee mbona unajichanganya, hapo juu umesema eti Pengo alimchimba biti Membe ishu ya OIC ikasizi, sasa hivi unabadilisha kibao unasema eti CC watamuita Pengo na kumpa onyo kali..lol..Sasa nani mwenye power juu ya mwingine hapo..Duh.

- Hapana, Membe alitangaza mambo ya OIC akiwa ametumwa na bosi wake kupima maji, akakuta yamejaa na akaishia kuomba sana msamaha kwa Pengo, that has nothing to do na CC ambako membe ni member tu wao wanaweza na ninaamini watamuita na kumpa onyo zito kuhusiana na hii habari, kwa maneno mengine CC ina power over all.

Mazee back kwenye kuitana sijui kwenye CC, you are alarmed for nothing. Masuala ya kanisa kuhamasisha watu kushiriki kwenye uvchaguzi kikamilifu hayakuanza leo labda tu watu wengi mankurupukia hii ishu kwa kuwa sasa everyone is alarmed with ufisadi na ruling part is trying to defend and na kufight everyoneelse anayeonekana anataka kuwanyang'anya tonge mdomoni.
- Kuyafanya kwa siri na kutangaza to the public, politically ina results tofauti, binafsi I am concerned sana na hili tangazo on its impact kwa the future ya amani kwa taifa letu, that is all na mifano ipo mingi sana kwamba amani haunza kuchafuliwa pole pole na ishus kama hizi.

- Taifa ni langu kama lilivyo lako pia, tuendelee kuelemishana mkuu.

Respect.

FMEs!
 
FMES,
Mkuu unaposema sio dini zote zina preach amani una maana gani?..samahani lakini!..

..

- Mkulu Bob, Tanzania imebadilika sana siku hizi tunazo mpaka dini za Satan, hizi hazi-preach ku-deal na ishus kwa amani sasa ninaogopa zikirukia hii agenda ya Pengo, amani inaweza kuchafuka sana.

Respect.

FMEs!
 
Safi sana Padre Mapunda! Tunataka mapadre na masheikh wote waunge mkono jitihada za kuisafisha nchi ili iendeshwe kwa maadili. Kanisa lazima litimize wajibu huu mkubwa wa kuhakikisha kwamba viongozi waadilifu ndio wanaopata nafasi ya kuongoza. Tumeshaona jinsi viongozi wanaoingia madarakani kwa rushwa wanavyoshindwa kukemea rushwa na badala yake wanalipa fadhila kwa wale 'mafisadi' waliowawezesha kuingia madarakani.
Naunga mkono jitihada zote za Kanisa katika kuhakikisha tunapata viongozi waadilifu wanaotanguliza mational interests mbele badala ya matumbo yao. Viongozi wa aina hiyo wapo!
 
Hakuna jipya hapa, wataendelea kuchaguliwa wastaafu, kila baada ya miaka mitano.
 
FEMS anadhani CC ina power juu ya Kardinali! Haina. Haiwezi kumpa amri afanyeje kazi zake za kichungaji. Kwanza hiyo CC ni ya CCM, sio taasisi ya serikali.

CC wakimwita Pengo atakwenda kama ni mwana CCM. Kama sio mwana CCM si lazima aende. Ama CC wanadhani huu ni wakati wa kutawala kwa vitisho vya "preventive detention"?

Wanoweza kuhaha kutokana na nia ya Kanisa kuwaelimisha wananchi ili wachague viongozi wazuri lazima ni viongozi wabaya. Kama wewe ni kiongozi mzuri, hutaogopa kwani wanataka mtu wa aina yako achaguliwe.
 
Inaweza ku-work naona hata Malawi walitumia hiyo approach kuwaelimisha raia juu ya umuhimu wa kuwa makini na kula wanazopiga na impact zake for the coming 5 years.

Kwa kuanzia naona sio mbaya makanisa na misikiti ikatumika. B'se I sometimes wonder watz kama tumelogwa when it comes to election watu hawako serious. Zawadi ya kofia na t-shirt tayari unaruhusu maisha yako kuwa ruined for 5 years.
 
Nadhani Wabongo wanafuata ule msemo:
'better the devil you know than the devil you don't' That's why kila chaguzi wanaendelea kuchaguwa wale wale wanao warudisha nyuma. (Wastaafu)
 
Dini ina role kubwa sana ya ku-play katika kuelimisha jamii kuhusu wajibu wao. Kwa jamii hii ya Kitanzania ambayo bado imefunikwa na blanketi zito jeusi na hata watu hawajui kinachoendelea, elimu hii ni muhimu sana. Afadhali viongozi wa dini watusaidie kuwafunua wana wa nchi hii ili watambue kwamba wanayo haki ya kuwakataa watu wanaong'ang'ania kuwaongoza huku wakifikiria zaidi matumbo yao badala ya kuwaongoza kwa lengo la kuwaletea maendeleo. Mungu awabariki viongozi wetu wa dini kwa kazi hiyo njema na takatifu. Amen!
 
Last edited:
FEMS anadhani CC ina power juu ya Kardinali! Haina. Haiwezi kumpa amri afanyeje kazi zake za kichungaji. Kwanza hiyo CC ni ya CCM, sio taasisi ya serikali.

CC wakimwita Pengo atakwenda kama ni mwana CCM. Kama sio mwana CCM si lazima aende. Ama CC wanadhani huu ni wakati wa kutawala kwa vitisho vya "preventive detention"?

Wanoweza kuhaha kutokana na nia ya Kanisa kuwaelimisha wananchi ili wachague viongozi wazuri lazima ni viongozi wabaya. Kama wewe ni kiongozi mzuri, hutaogopa kwani wanataka mtu wa aina yako achaguliwe.
Mkuu nafikiri watu hapa wanaogopa kusema ukweli wao.. maneno yako yanaweza kuwa sawa kabisa 100% kama navyotazama mimi lakini kumbuka hii ni Bongoland, nchi ya Wadanganyika lolote lisilowezekana duniani hapa huwezekana..

Hofu kubwa ya watu mkuu wangu ni ukweli kwamba viongozi wetu wamejenga uchafu wa nafsi zao.. sii wasafi kama unavyofikiria iwe waislaam, au wakristu.. Kuna hofu kwamba hoja kama hii inaweza kuwa inasukumwa na fedha (kina Lowassa/RA), ama watu kutafuta umaarufu na kijiko au ni nia mbaya ya kuleta utengano baina yetu sote kwa mfano, wanaweza sema msimchague kiongozi Muislaam (ataleta Uislaam) au asiyekuwa Mkatoliki asichaguliwe maanake hana mila zetu.. na kadhalika.

Ni hofu ambayo hata Wakristu walikuwa nayo wakati Kikwete anaingia Ikulu na itaendelea kuwepo kila uchaguzi kwa sababu hatuna imani na watu ktk kuongozi ngazi zote..Toka madhehebu ya dini hadi serikalini hatuna imani na mtu kwa sababu sote ni maskini wa hali na mali..

Na kibaya zaidi mkuu wangu ukifikiria kwa nini tusiwaamini ndipo unapokosea kwani kwa Mdanganyika vionmgozi wetu hutafuta kaimani kadogo kama hako wakatumia kuwajaza mimba walalahoi.

Huo ndio upande wa pili hoja zote zinalenga kuyasema haya lakini wanazunguka tu.. mkuu kumbuka hawa viongozi ni watu kama sisi wenye tamaa za maisha bora kama sisi, kutangulia sii kufika na ujanja ni kupata sii kufika! Hilo neno kuokoka ni swala la akhera na alijuaye ni Mungu pekee kuwa nani kati yetu kweli kaokoka!....

Hapa duniani kila mtu anachunga mzigo wake.
 
Kadinali Pengo ni mkweli au naye ni MSANII TU!?

Na mimi nilikuwa najiuliza hayo. Hivi kwanini viongozi wa dini wa zamani ndio walioleta maendeleo na umoja wetu na hawa wa sasa ghafla wanataka kutugawa na kuturudisha nyuma.

Jibu ninalohisi mimi ni kwamba iwe ni SIASA au DINI zote zina kazi ya kuuliza Nani kapata hiki, wapi, kwanini, kwa namna gani, lini ili mradi wakishapata majibu hayo wao kama 'waacha-Mungu' na 'wanasiohasa' wajue na wao watapata kiasi gani. Tatizo ni tumbo tu. Sasa ukichanganya kwamba jamaa hawa wote wanaweza wakawa na nyumba mbili au tatu inakuwa ni kazi kweli.

Watanzania ninawaomba tusidanganywe na wanasiasa au viongozi wa dini. Wote hawa na walaji na watumiaji tu wa kile tunachokizalisha. Sisi sote tujitahidi kusoma kati ya mistari kila wanachokisema au kukidai. Na mwongo tumuumbue kwa hilo. Na sisi sasa tutangulize maslahi yetu mbele sio kutumiwa na wanasiasa na viongozi wa dini kuwafanya wao na jamaa zao kuishi na kula vizuri wakati sisi tunalala kwenye mbavu za mbwa, tunakula matembere na ugali wa bada na watoto wetu tofauti na hao wakubwa hawasomi nje ya nchi bali kwenye shule ambazo hazina hata uwezo wa menejimenti na utawala bora na ambako watoto wetu lazima wazodolewe na madreva na makonda wa daladala ndio waende au watoke shule ! Chalema! Chakiii ? Kite cha mchili ndao ?

Wakati viongozi wa masikini Tanzania wanang'angania magari ya kifahari....

Viongozi wa Kenya wameamua kuuza magari yote ya kifahari na fedha itakayopatikana itatumika kwa shughuli mbalimbali za kuwasaidia masikini ikiwemo wale walioathirika na kuhama kutokana na mapigano mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Badala ya magari ya kifahari sasa viongozi wa nchi hiyo watapatiwa magari ya kawaida kama vile Volkswagen, Toyota Corolla, Celica, Cresta na mengine kama haya.

Mapinduzi haya inaelekea yanaletwa na mtoto wa Familia ya Kitajiri na wa Rais wa kwanza wa Kenya ambaye sasa kajifunza kuwa yeye kuwa tajiri na kuishi kifahari wakati Wakenya wengi ni masikini wa kutupwa ni sawa na kukufuru.

Wachunguzi wa kisiasa wanajiuliza hivi nchi ambayo ingelifanya jambo hili ni Keny au Tanzania. Majibu ya baadhi yao ni kwamba viongozi wengi wa kItanzania wanatokea familia za Kimasikni na wakiukwaa utajiri kwa njia za halali au wizi inakuwa kama vile kipofu kauona mwezi. Wale wanaotokea familia za Kitajiri hawajawahi kufunzwa lolote na wazazi wao kuhusu maana na sababu ya kuwepo hapa duniani. Na wanachukulia kwamba kuwa na magari ya kifahari, majumba makubwa na kutapanya pesa katika anasa binafsi ni haki yao.
 
he should resign now au alazimishwe kuondoka na sisi waumini wa dini mbali mbali kwa kujali masilahi ya taifa hasa la baadaye.

Respect.

FMEs!

Mimi nadhani ungekuwa wazi zaidi kwa kusema kuwa ni kwa maslani ya ccm na wala siyo ya taifa. Mbona wanapotoa elimu nyingine katika shule zao hamjamtaka ajiuzulu! Serikali ya ccm ndiyo iliyotakiwa kujenga hiyo mashine ya kuhakikisha kuwa wananchi wanaelimishwa ili waweze kuelewa na kushiriki ipasavyo kuwapata viongozi wasafi, sasa hawataki kwani hawataweza kuiba tena kura wala kutoa hongo n.k. Nanukuu hapa "....andikeni mtakavyo,... kwanza busanda yenyewe haina umeme, hivyo wananchi hawana TV ili waone matangazo yenu, wengi hawajui kusoma, hivyo hawawezi kusoma hayo magazeti yenu, na hata kama wanajua kusoma hawana hela ya kununua hayo magazeti yenu.." Hii inaonyesha jinsi serikali ya ccm ilivyodhamiria wananchi waendelea kuwa maskini na wajinga ili iendelee kuwatumia kama mtaji wao wa kuwatawala.

Nadhani kanisa limeliona hili na kufahamu kuwa ni dhambi iliyo kubwa. Nawapa hongera sana na kutoa mwito kwa taasisi zote za kijamii na kidini kuendelea kuwaelimisha wananchi wote juu ya haki zao ikiwemo nafasi yao katika kujipatia viongozi waliobora kwa mustakali mwema wa nchi yetu.
 
Makanisa nchini sasa yamtosa Rais Kikwete

  • Mchungaji amfananisha na Farao
  • Waraka maalumu kuwaelekeza wapiga kura waandaliwa

<font face="Courier New"><font size="4"><font color="Navy">KUNA kila dalili sasa kuwa viongozi wa makanisa nchini hawaridhishwi na mwenendo wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kutokana na kauli za karibuni zinazotolewa na viongozi wa makanisa hayo.

Katika siku za karibuni, viongozi wa makanisa mbalimbali wametumia matukio mbalimbali, zikiwamo ibada, kuelezea kutoridishwa kwao na utendaji wa Serikali ya Kikwete ikiwa ni pamoja na jinsi Serikali inavyowachukulia hatua watuhumiwa wa ufisadi.

Jamapili wiki hii kulitokea matukio mawili ya makanisa kuikemea Serikali, ikiwa ni pamoja na mahubiri ya Kanisa Katoliki na katika kipindi cha dini cha &#8216;Kutoka Makanisani' kilichorushwa kwenye Televisheni ya Taifa (TBC1).

Katika kipindi cha dini cha TBC1, Mchungaji Lawi Mwankuge wa Kanisa la Moravian la Ruaha Kidatu, Morogoro, alitoa mahubiri makali ambayo yaliielekea Serikali ya Kikwete moja kwa moja, akirejea mfano wa Mfalme Farao wa Misri aliyemtumia mfungwa Yusufu kumshauri baada ya washauri wake wote kushindwa.

Mchungaji Mwankuge alitumia mfano huo kuhoji; "yuko wapi Yusufu wetu wa kuwasaidia viongozi wetu"; huku akitaja wazi kwamba uchaguzi ujao wa Serikali za mitaa wa mwaka huu na uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 utumike kuwapata viongozi wenye kujali maslahi ya wananchi wao.

Akiendelea kurejea maandiko ya Biblia, Mchungaji Mwankuge alisema nchi imechukuliwa na wageni na kwamba, "yuko wapi Yusufu" wa kuikomboa nchi na kuongeza:"Mungu awaan
 
TUmeshuhudia lengo zuri la Kanisa Katoliki kuwafundisha waumini wake kuchagua viongozi wazuri hasa uchaguzi ujao. Kwangu hili si tatizo na ninawapongeza.

Lakini hapohapo kanisa hilo halijafanya juhudi kama hizo kwa wakatoliki kuelewa sheria za kanisa na mahakama ya kanisa hilo.

Ni wakatoliki wangapi hata waliomo humu JF ambao wanajua mchakato mzima wa kutafuta haki yao ndani ya kanisa katoliki.

Kuna wanaodhani askofu akisema basi ndiyo mwisho wa dunia. Kwamba alichokisema ndiyo utii.

Ni wangapi wananyimwa huduma ya mazishi kwa sababu ya vikundi hivi vilivyoanzishwa viitwavyo jumuiya ndogondogo ambavyo havimo kwenye sheria za kanisa.

Wenzetu Ulaya muumini kupeleka kesi hadi Roma ni kawaida. Huku Afrika husikii kitu hicho. Hivyo wakatoliki hawajui haki zao ndani ya kanisa eti leo wanafundishwa kutafuta haki zao nje ya kanisa.

Je, mkatoliki ulishawahi kusikia padri au askofu anakuhubiri ununue Sheria za kanisa.

Naweza kukosea lakini nadhani Kanisa Katoliki halifundishi waumini sheria za kanisa ili waendelee kuwa mambumbumbu wasiwasumbue mapadri na maaskofu kwa kesi za mara kwa mara za kuwafikisha Roma.

Hivyo Kanisa linapofundisha muumini haki zake kwa serikali au uchaguzi basi liende sambamba kufunidisha haki kama hizo ndani ya kanisa hilo.

Usishangae kumkutua mkatoliki haju kwamba kuna sheria za kanisa.
kama unabisha basi kama wakatoliki kumi uwaulize sheria za kanisa. Waweza kukuta wengine hawaju kwamba kuna kitu kama hicho.

Waweza kukuta hawajui kwamba askofu unaweza kumfikisha Roma kwa sheria hizo ili asiendelee kutudanganya kwa utii ambao hawajui kuu-define.

Hivyo Katoliki toa kibanzi jichoni mwako kabla ya kwenda kwa mwingine. Fundisha haki za waumini. Fundisha sheria za kanisa waumini wazikariri.

Fundisha mahakama ya kanisa waumini wako waijue. Na wasiishie kufundisha sheria za ndoa tu kana kwamba maonevu ndani ya ukatoliki ni kwenye ndoa tu.

Salaam
 
TUmeshuhudia lengo zuri la Kanisa Katoliki kuwafundisha waumini wake kuchagua viongozi wazuri hasa uchaguzi ujao. Kwangu hili si tatizo na ninawapongeza.

Lakini hapohapo kanisa hilo halijafanya juhudi kama hizo kwa wakatoliki kuelewa sheria za kanisa na mahakama ya kanisa hilo.

Ni wakatoliki wangapi hata waliomo humu JF ambao wanajua mchakato mzima wa kutafuta haki yao ndani ya kanisa katoliki.

Kuna wanaodhani askofu akisema basi ndiyo mwisho wa dunia. Kwamba alichokisema ndiyo utii.

Ni wangapi wananyimwa huduma ya mazishi kwa sababu ya vikundi hivi vilivyoanzishwa viitwavyo jumuiya ndogondogo ambavyo havimo kwenye sheria za kanisa.

Wenzetu Ulaya muumini kupeleka kesi hadi Roma ni kawaida. Huku Afrika husikii kitu hicho. Hivyo wakatoliki hawajui haki zao ndani ya kanisa eti leo wanafundishwa kutafuta haki zao nje ya kanisa.

Je, mkatoliki ulishawahi kusikia padri au askofu anakuhubiri ununue Sheria za kanisa.

Naweza kukosea lakini nadhani Kanisa Katoliki halifundishi waumini sheria za kanisa ili waendelee kuwa mambumbumbu wasiwasumbue mapadri na maaskofu kwa kesi za mara kwa mara za kuwafikisha Roma.

Hivyo Kanisa linapofundisha muumini haki zake kwa serikali au uchaguzi basi liende sambamba kufunidisha haki kama hizo ndani ya kanisa hilo.

Usishangae kumkutua mkatoliki haju kwamba kuna sheria za kanisa.
kama unabisha basi kama wakatoliki kumi uwaulize sheria za kanisa. Waweza kukuta wengine hawaju kwamba kuna kitu kama hicho.

Waweza kukuta hawajui kwamba askofu unaweza kumfikisha Roma kwa sheria hizo ili asiendelee kutudanganya kwa utii ambao hawajui kuu-define.

Hivyo Katoliki toa kibanzi jichoni mwako kabla ya kwenda kwa mwingine. Fundisha haki za waumini. Fundisha sheria za kanisa waumini wazikariri.

Fundisha mahakama ya kanisa waumini wako waijue. Na wasiishie kufundisha sheria za ndoa tu kana kwamba maonevu ndani ya ukatoliki ni kwenye ndoa tu.

Salaam
Kazi ya wachungaji/mapadri/askofu ni kufundisha neno la Mungu na kuweza kusaidia roho kufika mbinguni, na hili linatoka kwenye Biblia ambayo inaeleweka vizuri tu. Mafundisho ya kanisa ni kuweza kumfanya mwanadamu kuwa na uhusiano na Mungu na wala si na roma.

Ni wajibu wa kanisa kufundisha waumini wake ni nini maana ya utawala wa haki na usawa mbele za mwenyezi Mungu na kiongozi wa namna hiyo anatakiwa awevipi, na ni wajibu wa kanisa kuhakikisha waumini wake hawawajachagua viongozi wadhalimu na wasiofaa mbele ya Mungu na kanisa.

Waumini wa kanisa wanajua nini misingi ya dini yao kwani hakuna kilichojificha, na kupeleka madai Roma sio kiini cha kuijua dini husika kwani kila mmoja ana mpango wake na Mungu wake Roma haiwezi kukufikisha mbinguni hata ukilala huko. Fuata amri za Mungu na utende mema siku zote usiwe fisadi na umendee kila binadamu haki na kumheshimu, usiwe chanzo cha dhuluma, rushwa, upendeleo na utawala wa kisasi.
 
Kipindi cha je tutafika kinachorushwa na runinga ya channel Ten,walikuwa na mjadala unaoshabihiiana na huu kuhusu maandalizi ya uchaguzi wa 2010 na maelekezo kwa waumini.

Kati ya wachangiaji waliokuwepo Studio za Ch. ten wapo waliokuwa na nakala ya barua ya baraza la maaskofu husika na hilo.
kama yupo mwenye nayo naiomba hapa JF.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom