Mombo Wetu
JF-Expert Member
- Aug 5, 2008
- 377
- 38
Kuhusu jina langu ..inashangaza kidogo umeishiwa na hoja kiasi cha kutaka kuyaingiza hata majina ya mtoa hoja ktk mada. Ok, nasikitika kuwa hapa si mahala pake kuanza kuongelea majina.
Ama kuhusu kanisa kujenga au kutokujenga ufalme wa dunia hiyo ni tafsiri yako potofu kuhusiana na maandiko uliyoitengeneza wewe mwenyewe kichwani mwako. Nitapenda kuliongelea hili siku nyingine na mahali muafaka hapa sio mahala pake.
Pili naona unaongea tu kwa hisia bila ya kuwa na vitu tangibles. Unadai neno la lina nguvu, sasa sijui ulitaka watu waache kufanya kazi wakae chini wafanye maombi tu bila kujishughulisha na kila kitu kitatelemka kutoka mbinguni kama mana? Kuna usemi unaosema sala na kazi. Kukaa tu madhabahuni na kuhubiri huku hujali kinachoendelea mitaani ni kutokuwa mchungaji mwema. Uchungaji wa kweli wa kondoo walikabidhiwa wawatunze ni lazima uangalie maendeleo ya mwili na roho kwa pamoja. Huo ndo uchungaji wa kweli na hata Yesu aliwaponya watu shida zao za mwili na kuwaponya na roho zao pia, hakufanya kimoja tu na kuwaacha watu njia panda.
Hayo mengine niliyoya-bold ni yako na sijui yanakoanzia wala yanakoishia na yanakusudia nini na yanalenga kufanya nini.
Unaongelea kuwa suspicious..Kuwa suspicious ni one thing na kukishutumu kitu au kukipinga baada ya kujua undani wake ni suala jingine. Unaruhusiwa kuwa suspicious provided unaonesha some kind of efforts kuutafuta undani wa unachokitilia mashaka. Kukitilia tu kitu mashaka na kutoendelea kutafuta undfani wa jambo lenyewe ndio hasa wengi wenu mnachokifanya hapa.
Unauliza kama ningesikia watu wa imani nyingine wanafanya utaratibu wa kuelimisha watu wao, jibu langu ni kuwa chochote kilicho chema kwao ni chema kwangu provided hakina lengo baya.
Mwishoni naona una-recycle hoja zilezile. Inaonekana hauna taarifa ya ukweli wa mambo ulivyo. Wengi wetu tunayo mazoea ya kutupia tu shutuma na lawama bila ya kuchukua muda kuona tunachokilaumu ni nini na iwapo tuna sababu za msingi kulaumu. Kwa taarifa tu, kwa nyakati tofauti kanisa limekuwa likishirikiana na serikali kwenye mambo ya afya, elimu na kampeni mbalimbali, na wakati mwingine wataalamu wa serikali huja mpaka madhabahuni kuhamasisha kampeni mbalimbali za kijamii. Hili hulijui au hutaki kuliona, inashangaza.
Nakushauri uangalie thread nyingine kama mbili hivi, nadhani kuna moja ipo attachment kuhusiana na hii plan. Unaweza kusoma na mawazo ya wenzio kuona wanachoongea na kukipima badala tu ya kushikilia cha kwako.
I concur!
BUT
Ijue kweli nayo itakuweka huru. Adui yangu namba moja ni devil na wapili ukiondoa d kwenye neno devil huyo hata aje Kwakupitia sura yangu ndani yangu lazima nita m-cast out in the name of Jesus. Kwahuyo sina msamaha wala ushirika and am powered to do so. It does not matter which object it will use either dini, chama, elimu, wanyama, binadam, mimea or any other object it will try to hide in sura yake ni moja tu "uwongo" with the aim of Kiling, destroying and stealing. Lakini my best friend and I always fellowship with is "Ukweli" huyo hata aje kwa the above mentioned objects nitampokea na kuunga ushirika nae kwani huja kuleta uhai tena ulio tele katika jambo lolote kama maendeleo, mahusiano, afya kwani sura yake huwa na mwanga na haijifichi iwazi na rahisi kueleweka na mtu yeyote. Sasa rafiki inawezekana tunatofautiana katika kutafsiri ipi ni kweli na upi ni uwongo lakini najua kabisa hata wewe unapenda ukweli na unachukia uwongo. Taarifa tu hivi vitu viwili hupatikana ndani ya objects na object hiyo hiyo moja inaweza kutumiwa na wote wawili kwa ridhaa ya hiyo object although at different times lakini kuna saa nyingine huyo moja anaweza kujidai kuwa ni mkweli kumbe ndani it is the opposite na hii ni tabia ya uwongo na hao objects wanitwa hypochrites. Sasa hapo sina mjadala tena maana hatuwezi kufanana ndo maana mimi ni mimi na wewe ni wewe ila ukinijia kwa sura ambayo siipendi nitaku cast out kwasababu hiyo capacity ninayo na wewe vilevile nikikujia kwasura ambayo huipendi kama uwezo unao ni cast out!