Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Spika hakumkatisha kwamba alete ushahidi ama kwa kuwa ni CCM basi anasema tu habari za kusikia bila ya ushahidi mezani?

Msambya anasema ni waislam tu kwani hawako Tanzania? Mahakama itaendeshwa kwa pesa zipi hizi hizi za sisi walipa kodi tusio waislam na bado hajaona haja ya mjadala kwa kuwa kodi yetu itawahudumia wao?
 
Mahakama itaendeshwa kwa pesa zipi hizi hizi za sisi walipa kodi tusio waislam na bado hajaona haja ya mjadala kwa kuwa kodi yetu itawahudumia wao ?

Kwani mafundisho ya imani yako yanasema kuwa ni dhambi kodi yako kulipia maendeleo ya watanzania wenzako walio na imani tofauti nawe?

Na hiyo kodi unalipa lakini? Na malipo hayo hufanya kwa dhati ukitekeleza wajibu wako kama raia ama kimbindembine tu?

By the way, bado una uraia wa Tanzania?

Omarilyas
 
huo sasa uchokozi Mkuu
 
Mtu unaweza kuandika kitu kama hiki? Omary vipi tena mkuu? Hivi kwa nini yakija mambo ya DINI, basi watu huwa wanajifanya wana dini kuzidi hata Waizrael au Waarabu wenyewe ambako hawa Yesu na Mtume M. walizaliwa. Utaona mtu ajifanya kufahamu historia hadi mila kuzidi hata Waarabu/Waizrael wenyewe. Hivi mwajua kwa nini hawa watu walizaliwa huko kwenye race ya Wazungu? Sababu ni moja kuwa jamaa wanatenda madhambi hadi yanatisha na sisi ni cha mtoto. Ona walivyouwana kugombea mji wa Jerusalem, na sisi Mipingo tunadandia treni la DINI kwa mbele.

Hapa swali ni KODI YANGU. Hata kama sipo Tanzania, nimechukua uraia wa nchi nyingine kama Gabon, nk si huwa nakuja Tanzania? Kuna ndugu zangu ninaowasaidia na wao wanakatwa hiyo mikodi kwa ajili hiyo? Unafikiri matatizo yao si yangu? Sasa nikianza kuhoji Kodi yangu inaenda wapi inakuwa nongwa? Ndiyo maana wanakuja akina Barrick, Voda, Sheraton na wahuni wengine ambao hata kodi hawalipi, na watu kama wewe mnaona sawa tu. Kumbe acha tu ngozi nyeupe waile hii nchi maana watu wenyewe hatujui hata haki yetu iko wapi. Acha Kikwete asafiri wee na tusihoji maana itasemwa kuwa "kwa kuwa Muislaam basi mwahoji,,,,,,"

Mkuu Omary umeenda too low hadi siamini. Labda wewe na jamaa huwa mnataniana.... hapo basi naondoa maneno yangu na ninajitoa kwenye makala yenu.
 
Huyo Msambya anapigania tu jimbo lake. kama ulivyomsikia PM Pinda watu wanabwatuka tu sasa hivi ili wasikike majimboni mwao.

Suala la kadhi kuhudumiwa na serikali lazima liridhiwe na wakristu pia kwani nchi hii haina dini
 
Msambya nchi hii siyo ya kidini kama iran,wakristo na waislamu na dini zingine ndio wanaopaswa kuamua juu ya kila kitu ktk nchi hii.unaposema suala la kadhi na oic liamuliwe na waislamu ni kutenga jamii nyingine ktk nchi yetu ambayo haina ubaguzi wa dini wala rangi.Hivyo usilaumu makundi mengine yakiwa na mikakati kama hiyo.NYANI HAONI KUNDULE.
 
Wakati wakina Zitto wanazungumzia mambo ya maendeleo kwa nchi kiasi cha kupewa hata barabara za lami wakina Msambya wao wanaona mahakama ya Kadhi na OIC ndiyo maendeleo ya jimbo na taifa.

Huu ujinga utakwisha lini vichwani mwa watu hawa?

Nilisikia akisema Profesor Haroub (Marehemu) alikuwa mwalimu wake. Kumbe na yeye Msambya ni msomi? Lakini pamoja na elimu yake badala ya kutafuta maendeleo anatafuta mahakama ya kadhi? Ama kweli watu aina ya Msambya hata shule hawana sababu, si ajabu alikuwa ni zero tu hata huko university.
 
Huyu Msambya anataka kurudi kwa mlango wa nyuma...alipopewa ulaji wakati ule inatosha.....bado anataka tena?amesahau nini au ndio mfa maji......?
 
Swali ninalojiuliza je ni kweli kuna waraka wa aina hiyo? na kama upo mbona sikuona wanamtaka alete ushahidi? je kwa kutotaka alete ushahidi ni kweli serikali inakili kuwapo kwa waraka huo? Na kama upo basi mwenye kuwa nao naomba aulete hapa jf maana ni vema wote tuuone na kuujadili.

Hakika waraka huo upo. Ebu soma gazeti la Raia Mwema toleo la 088 la july1 - mpaka 7 utaona picha ya waraka huo.

Labda kuna suala dogo napenda kuuliza. hivi kwanini Serikali ilipofuta misamaha a kodi kwa taasisi zote za kidini kwanini wakristu ndio waliolalama zaidi?

Nafikiri sasa Taifa linaelekea kubaya kwani wengi hawajui ruzuku Tuangalie kwene kijitabu cha bajeti ya 2007/2008 na 2008/2009 na pg 236 para iv ya bajeti 2009/2010 utaona ni nani kati ya waislamu na wakristu wanaochota ruzuku kubwa ( kwa hisabu zangu za kingumbaru aislamu wanachukua 7% tu ya pesa zote na zilizobaki zinakenda kanisani.

Sasa vp waislamu hawalalamiki kwa hilo? Nikiangalia hata kama serikali italipia fedha za ofisi a kadhi hawataeza kutumia zaidi ya 32% ya pesa wanazotumia aislamu katika ruzuku.

Inabidi watanzania wavumiliane na isiwe ile Kunya anye bata akinya kuku uchafu

Dr Hamza.
Mapumzikoni
Shanghani, Znz
Nafikiri kijita
 
Nilitaka nishereheshe ni ruzuku gani hizo.

Hapa nilikusudia kueleza zile ruzuku wanazopata taasisi za kidini katika misamaha a kodi na zile za kupea katika kuendesha shughuli binafsi za taasisi kama hospitali, shule ,vyuo vikuu n.k.

Dr Hamza ousuf Al-Naamani.
mapumzikoni
Shanghani. Znz
 
Nadhani huyu jamaa anataka kupandisha C.V. yake tu.
 
Wakati wakina Zitto wanazungumzia mambo ya maendeleo kwa nchi kiasi cha kupewa hata barabara za lami wakina Msambya wao wanaona mahakama ya Kadhi na OIC ndiyo maendeleo ya jimbo na taifa.

Huu ujinga utakwisha lini vichwani mwa watu hawa?

Nilisikia akisema Profesor Haroub(Marehemu) alikuwa mwalimu wake. Kumbe na yeye Msambya ni msomi? Lakini pamoja na elimu yake badala ya kutafuta maendeleo anatafuta mahakama ya kadhi? Ama kweli watu aina ya Msambya hata shule hawana sababu, si ajabu alikuwa ni zero tu hata huko university.
Fikiri kabla ya kuandika isije ikakugeukia!Nijuavyo mimi ukimwita mtu mpumbavu/mjinga kwa mtu ambaye sio mpumbavu/mjinga, basi ile dhana ya upumbavu/ujinga inakugeukia wewe, upo hapo?
 
Hakika waraka huo upo. Ebu soma gazeti la Raia Mwema toleo la 088 la july1 - mpaka 7 utaona picha ya waraka huo.

Barubaru acha upotoshaji, kwa mujibu wa gazeti la Raia Mwema toleo tajwa hakuna waraka unaosema waraka unaowataka Waumini wasichague wabunge ambao si wakristo. Hivyo acha kupotosha jamii tena acha ushabiki wa kidini usioleta maendeleo.

Labda kuna suala dogo napenda kuuliza. hivi kwanini Serikali ilipofuta misamaha a kodi kwa taasisi zote za kidini kwanini wakristu ndio waliolalama zaidi?

Si kwamba Wakristo ndo walilalama zaidi bali taasisi zinazotoa huduma kwa jamii ndiyo zililalamika pamoja na wananchi wanaotegemea huduma hizo. Ni ajabu kwamba hujui kuwa taasisi za Kikristo zinazotoa huduma za jamii ni nyingi kuliko za dini nyingine. Fanya utafiti kidogo tu juu ya hospitali, shule, vituo vya huduma za ushauri, kulea yatima, vyuo vikuu, Vyuo vya ufundi na huduma za maji vijijini. Mao alisema 'no research no right to speak'.

Nafikiri sasa Taifa linaelekea kubaya kwani wengi hawajui ruzuku Tuangalie kwene kijitabu cha bajeti ya 2007/2008 na 2008/2009 na pg 236 para iv ya bajeti 2009/2010 utaona ni nani kati ya waislamu na wakristu wanaochota ruzuku kubwa ( kwa hisabu zangu za kingumbaru aislamu wanachukua 7% tu ya pesa zote na zilizobaki zinakenda kanisani.

Hivi kunamashindano ya kuchota ruzuku? mshikaji upo low sana! i am sorry to say that
fuatilia ujue kwanini ruzuku inatolewa.

Sasa vp waislamu hawalalamiki kwa hilo? Nikiangalia hata kama serikali italipia fedha za ofisi a kadhi hawataeza kutumia zaidi ya 32% ya pesa wanazotumia aislamu katika ruzuku.

waulize kwanini, maybe watakuelewesha vizuri zaidi, wewe ndo upo hapo unalalamika.

Inabidi watanzania wavumiliane na isiwe ile Kunya anye bata akinya kuku uchafu

Kwa watu wa aina yako, ni vigumu nchi kupata maendeleo, maana inaonekana umejaa mawazo ya kuonewa tu.

Dr Hamza.
Mapumzikoni
Shanghani, Znz
Nafikiri kijita

ebo kumbe ni Doctor! salalei! mapumziko mema mzee.
 
Nijuavyo mimi, ule waraka wa kanisa haujasema wakristu wawapigie kula wakristu wenzao tuu.Wanasema imefika mahala sasa wapiga kura wawachague viongozi wenye kufaa bila kujali dini.Inawezekana huku kuweweseka kwasababu nyingine za kisiasa lakini sio kweli ni za kidini. Mbunge naona anakosea anaposema suala la IOC na kadhi lijadiliwe na waislamu tu halafu nchi ndiyo iingie mkataba. Ingekuwa rahisi kama mkataba ukaingiwa na chombo cha waislamu lakini sio nchi maana katiba inasema wazi serikali haina dini.
Ni muhimu watanzania wenzangu tungeusoma huo waraka unasema nini ili tupinge yale yenye nia kweli za kuleta udini, badala ya kuuchukia tu eti kwasababu umeletwa na baraza la maaskofu. Kumbukeni maaskofu nao ni watanzania kama mimi na wewe na ni viongozi na wanao wajibu wa kurekebisha mambo pale yanapoonekana hayaendi sawa. Nchi imejaa kashfa ambazo nyingi zinawahusisha baadhi viongozi wa dini zote. Waraka wa kanisa utakuwa na makosa kuwakumbatia waumini wake wenye matatizo ya aina hiyo kama hivyo ndivyo.
Wabunge aina ya huyu jamaa ni watu hatari maana huwa anapenda kushupalia mambo yenye utata kwa nguvu zote. Asije akafikiri tumesahau ushirika wake mtukufu wa siku za nyuma na watuhumiwa mbalimbali.Sasa kwasababu wapiga kura wanapewa elimu ya kuangalia ni aina gani ya viongozi wachaguliwe anabadili issue iwe kama ya uislamu na ukristu. Hii nchi ni yetu sote asisahau hilo.Na nikiangalia tuhuma za ubadhilifu au ukiukwaji ya maadili ya uongozi, yapo majina ya aina zote. Suala hapa sio kuelimisha watu kuchagua mtu wa dini yao...suala ni kuchagua kiongozi atakayefaa.
 
Nziku,

Ahali yangu sio vizuri kutoa lugha mbaya kwa wengine kwani kila mtu ana haki sawa katika kutoa maoni na wewe kama una hoja basi jaribu kutafuta hoja na kujibu hoja kuliko kutumia lugha ya kukera au dhihaki kwa wengine.

Nafikiri msingi mkuu ni huu kama ulivyobainisha wee mwenyewe ' 'no research no right to speak'.

Sasa usikurupuke kutoa hoja bila kufana tafiti. Sasa soma gazeti la leo la RAIA MWEMA utakiona kijitabu hicho picha yake ni kisha kitafute kwenye bookshop ( mimi nimemwagiza mtu aninunulie huko Dar kipo Cathedral bookshop pale opp forodhani sec ,posta.

Elewa kuwa ndio maana Hata spika hakuhitaji kuthibitisha kani kitabu bila shaka kitakua kimeeleza mengi.

Sasa labda nije na suala dogo tu kwako. Hivi kwanini waislamu haana miradi mingi ya kijamii kama shule, hospitali, na vyuo vikuu? Kwanini wawe wakristu kwa kila kitu? hebu fanya utafiti kidogo.

Labda kwa kukusaidia kwanini SM Tanzania haitaki kuwaruhusu waislamu waingie katika OIC?

Ukiangalia na kutafiti kidogo utaona Roman Cath ndio wenye miradi mikubwa a kijamii na ndio wanaopata ruzuku na misamaha mikubwa ya kodi.
Je unajuwa kwanini balozi wa Vatican yupo TZ, anamwakilisha nani? na yupo kwa maslahi ya nani?

naomba ufikirie hayo kisha uje na hoja na wala sio kejeli.

Dr Hamza

'
 
hivi watanzania wenzangu....hii nchi mnadhani inahitaji dini na viongozi wake ili iendelee?....sioni nafasi ya dini yoyote katika kutatua matatizo yetu kama ufisadi sugu, umasikini na uporaji wa rasilimali..ndiooo
TUANZE na hawa ROman Catholic...Mkapa ni muumini wao na PENGO mpaka leo ANAMTETEA KUWA NI MTAKATIFU NA ASIGUSWE,...njoo kwa EDWAD L...yeye alipotimuliwa uwaziri mkubwa akapokelewa na ASKOFU WAKE WA KKKT HUKO KWAKE...na kumpongeza ..."MWIZI"...hao hao viongozi wetu wa dini ....LEO WANALETA WARAKA SIJUI HATA WA KAZI GANI???....wanatakiwa waige kwa DESMOND TUTU
Haya kwa wenzangu WAISLAM....sijui wanatetea vipi maadili ya waumini wao AKIWAMO HUYU Vasco da-GAMA...kila siku kiguu na njia kama kala miguu ya kuku...UFISADI UNATOKEA na yeye hachukui hatua yoyote ...KAMA KWELI KUNA VIONGOZI WA DINI NA WAWE KAMA AYATOLLAH WA IRAN...akitoa neno rais anamuheshimu..na anafuata.
HAWA VIONGOZI WETU WA DINI HAWANA MENO NA HIZI ZOTE PROPAGANDA ZA KIJINGA IOC, KADHI, WARAKA NI UPUUZI WAO TU.....HATA WAPEWE UNO...hawatakuwa na lolote la kubadilisha kwa wananchi wa kawaida kama sie na hata kwa mabwana wakubwa wao....
 
Kama kuna wabunge vichefu chefu basi Msambya ni kinara wao!!!
 
Sasa usikurupuke kutoa hoja bila kufana tafiti. Sasa soma gazeti la leo la RAIA MWEMA utakiona kijitabu hicho picha yake ni kisha kitafute kwenye bookshop ( mimi nimemwagiza mtu aninunulie huko Dar kipo Cathedral bookshop pale opp forodhani sec ,posta.

nani aliyekurupuka? kama bado hujasoma hicho kitabu mbona unatoa hoja kuwa kinasema asipewe kura mgombea asiye Mkristo? picha iliyopo mbele ya gazeti la Raia Mwema haisemi hayo unayoyasema! Hiyo picha unaweza kuiona hata hapa: 100_1654.JPG (image)
 
Nziku,

Ahali yangu sio vizuri kutoa lugha mbaya kwa wengine kwani kila mtu ana haki sawa katika kutoa maoni na wewe kama una hoja basi jaribu kutafuta hoja na kujibu hoja kuliko kutumia lugha ya kukera au dhihaki kwa wengine.

Nafikiri msingi mkuu ni huu kama ulivyobainisha wee mwenyewe ' 'no research no right to speak'.

Sasa usikurupuke kutoa hoja bila kufana tafiti. Sasa soma gazeti la leo la RAIA MWEMA utakiona kijitabu hicho picha yake ni kisha kitafute kwenye bookshop ( mimi nimemwagiza mtu aninunulie huko Dar kipo Cathedral bookshop pale opp forodhani sec ,posta.

Elewa kuwa ndio maana Hata spika hakuhitaji kuthibitisha kani kitabu bila shaka kitakua kimeeleza mengi.

Sasa labda nije na suala dogo tu kwako. Hivi kwanini waislamu haana miradi mingi ya kijamii kama shule, hospitali, na vyuo vikuu? Kwanini wawe wakristu kwa kila kitu? hebu fanya utafiti kidogo.

Labda kwa kukusaidia kwanini SM Tanzania haitaki kuwaruhusu waislamu waingie katika OIC?

Ukiangalia na kutafiti kidogo utaona Roman Cath ndio wenye miradi mikubwa a kijamii na ndio wanaopata ruzuku na misamaha mikubwa ya kodi.
Je unajuwa kwanini balozi wa Vatican yupo TZ, anamwakilisha nani? na yupo kwa maslahi ya nani?

naomba ufikirie hayo kisha uje na hoja na wala sio kejeli.

Dr Hamza

'
Je unafahamu Vatican ina status ya nchi kama ilivyo Iran au Saudi Arabia? Na hao wenye jamuhuri za kiislamu balozi zao ni za nini TZ?
Jamani tusipoteze malengo kwenye suala hili. Kwa mfano, mi nimekutana na waislamu wengi ambao kwa matendo yao ninawaheshimu kama waungwana na marafiki zangu.
Tuwe wakweli. Maendeleo ya nchi yetu hayana mjomba wa kuyasaidia. Kanisa na misikiti ina uhuru sawa wa kuanzisha huduma za kijamii. Tutafanya makosa makubwa kuamua kuziba macho tusione mambo yaliyo wazi na kuleta hoja kama hii ya kuwa na balozi wa Vatican Tanzania iwe kama nalo ni kosa. Unless unihabarishe wewe unajua balozi wa Vatican anafanya kazi gani TZ tofauti na ile iliyokusudiwa ntakuelewa.
 
nani aliyekurupuka? kama bado hujasoma hicho kitabu mbona unatoa hoja kuwa kinasema asipewe kura mgombea asiye Mkristo? picha iliyopo mbele ya gazeti la Raia Mwema haisemi hayo unayoyasema! Hiyo picha unaweza kuiona hata hapa: 100_1654.JPG (image)
.

Nziku,

Mi naona kuna lingine lakin sio hoja.

Nafikiri niliandika tokea awali kuwa mimi nimesoma habari hizo katika mada husika la Mchukia Fisadi

Swali ninalojiuliza je ni kweli kuna waraka wa aina hiyo? na kama upo mbona sikuona wanamtaka alete ushahidi? je kwa kutotaka alete ushahidi ni kweli serikali inakili kuwapo kwa waraka huo? Na kama upo basi mwenye kuwa nao naomba aulete hapa jf maana ni vema wote tuuone na kuujadili.
.

Nimesherehesha kwa kusema Yalioelezwa bungeni ni sawia na ndio maana hata wabunge hawakuomba MWONGOZO. kwani ndani ya bunge haipaswi kusema uongo.

Upande wangu nimekiagiza kitabu hicho nikisome kujiridhisha lakini sijakihukumu kijitabu hichi. Ebu nisome vizuri maandiko yangu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom