Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
King Zzenji,
Mkuu wangu Mtume Muhammad alikuja na Kuran ikiwa na nia njema kwa binadamu wote.. lakini sii lazima Kuran hiyo ifundishwe, itukuzwe na ikubalike kwa binadamu wote pamoja na kwamba ndio lengo lake..Hivyo hivyo kwa biblia, Na vitabu vinginevyo vyote hivi vimetangulia mwongozo wa dini moja na waraka hutolewa kwa wote ila hupokewa na waumini wake na sii kila mtu...

Mawazo ya kanisa yabakie kama ujumbe kwa viongozi na hakika kanisa lina kila haki kuwahamasisha waumini wake kuchagua viongozi bora kwani sote tunaitaka Pepo, lakini waraka huo hauwezi kuishirikisha serikali nzima kukaa nao kitako kuandika mwongozo wa kitaifa ambao tayari upo na ndio tunaufuata. yanayotokea leo ni uvunjaji wa mwongozo na sheria za nchi, hivyo kazi ndogo tu.. wahusika wachukuliwe hatua, hizi habari za kusamehe tuanze upya, sijui kutunga mwongozo mpya wa kutochagua viongozi mafisadi na kadhalika ni kupoteza muda.
Waraka mzuri ni ule unamtaka JK na vyombo vya sheria kuwasimamisha Mafisadi mahakamani..Binafsi sintaona haki ikianza kesho na kuwaacha kina Mkapa, Lowassa, Ro, Yona na wengineo wakipeta kwa sababu hawatachaguliwa tena na tunaanza upya na sheria mpya..
Kifupi, sisi wote tunajua Ufisadi ni kitu gani bila ushauri wa Padre wala Sheikh..Na itakuwa vizuri sana hawa Masheikh na Mapadre wazidi kuifundisha neno la Mungu kwa sababu Ufisadi unatoikana na watu kutofanya ibada..Ufisadi ni dalili kubwa ya kuonyesha kwamba dini zetu zimeshindwa kuwaokoa wananchi wake, aidha mafundiisho ni hafifu au wao viongozi wa dini ni mifano mibaya, hivyo wananchi hawaogopi tena kutenda madhambi..

Swadakta Mkandara,
Mawazo yako yamechungulia darasa. Wote tunataka kuona wezi wetu Ben Mkaa Hapa and co wanajibu uharamia wao. Kwa viongozi tulionao hilo linawezekana? Nitajijibu kuwa haiwezekani kamwe. Hawa viongozi ambao ndio wanatakiwa kuwapeleka mahakamani ndio wamekuwa watetezi wao wakuu. Unaona ANBEN inatakiwa ilipwe fidia!!!!
Suluhisho la kuwa shughulikia hawa ni pale tutakapopata viongozi na sio watawala waadalifu ndipo hawa jamaa watajibu ufedhuli wao. Hawa waliopo wote dhamira zinawasuta maana ni wanufaika wa huu wizi.
 
Mimi nilimjua siku nyingi makwaia kama mdini wa kutisha kupitia makara zake katika magazeti mbalimbali, Hana tofaoti na mwandishi mdini mwingine ambaye sijui yuko wapi siku hizi, Khalid Mtwangi. niliwahi kuwasiliana na makwaia kwa email nikimueleza maoni yangu juu ya uandishi wake, alinijibu kwa kunitukana matusi ya nguoni, nikamsamehe kwa kujua kuwa hayo ndiyo malezi aliyopata ya kutukana, chuki, wivu, manungunuko yanayopelekea watu kufikia kujilipua. Hakuwahi kupata malezi ya kuenzi amani na msamaha.
Kuhusu waraka naomba wanaoupinga watueleze kanisa linapojenga shule, vyuo vikuu, hospitali, visima nk. linakua linachamganya dini na siasa tukemee?
 
Ee bwana ndiyo. Ulitakiwa kuihifadhi hiyo e mail kisha uianike umu jamvini. Kama unayo e mail address yake ianike humu ni mtupie ndoanona kwa kuwa hana hoja ataimeza bila shaka.
 
Gulwa,
Mkuu wangu mimi ni mmoja kati ya watu wanaopinga waraka kwani hatuuhitaji toka sehemu yoyote ile..
Nachojaribu kusema hapa ni kwamba Mafisadi wote wanajulikana -Wakamatwe! waraka wowote ule unaovuka au kuruka hatua hii sii waraka mzuri kiutendaji kwa wananchi kwani waraka huo unaepa kuwawajibisha wale waliokwisha tenda madhambi..
Mkuu kumbuka tu kwamba hawa wote viongozi Mafisadi ni waumini wa dini zote, ni Waislaam na Wakristu iweje makanisa na misikiti inashindwa kuwasema wazi watu hawa wanapokuja misikitini na makanisani kwa machafu au waovu wanayoyafanya?..Je, huu hautakuwa waraka mzuri kwetu sisi ikiwa viongozi wa dini watachukua nafasi ya kazi yao kwa kuitumia dini kuwaambia ukweli hawa waumini Mafisadi badala ya miskiti na makanisa hayo kuchukua misaada na sadaka za hawa hawa watu wanaendelea kufanya madhambi..

Hivyo hitimisho langu nitarudia kusema ni kwamba hawa viongozi wa dini ndio walezi wakubwa wa Mafisadi... laa sivyo wangeisha fanya kazi yao kukataa sala wala sadaka za hawa watu kisha baada ya hatua hizo ndio watuletee waraka..
Tukirudi ktk maswala ya shule, Hospital, na huduma nyinginezo bila shaka makanisa na misikiti walifanya kwa hatua zinazotakiwa kusajili hizo shule..Kisha hii ni biashara kwao na wanafuata sheria za serikali kama Taasisi nyinginezo zisizo za kidini. Hivyo mfumo wa shule binafsi haukuandikwa na kanisa wala msikiti na hata hakuna Sheikh wala Padre aliyejumuishwa kuunda au kutunga waraka wowote unaohusiana na elimu, Afya nchini isipokuwa vyombo vyote hivi vinaendesha shughuli zao kutokana na sheria za taasisi zao.

Tunashukuru sana kwa kanisa kuandika waraka, ni ujumbe mzuri sana tena una kila maana lakini kanisa sio chombo kinachowakilisha wananchi wote kuweza kuitaka serikali wajumuishwe wao ktk kuunda Mwongozo..Wangetusaidia sana kama wangeongeza somo la Uraia ktk masomo ya shule zao kwani sidhani kama walihitaji kukaa kitako na serikali ili wapate kuongeza somo lolote, ila wao wanafuata utaratibu ulowekwa na serikali..Na binafsi ningewaunga mkono sana tu kama serikali ingekataa shule zisifundishe somo la Uraia..hapo mkuu tungekuwa pamoja na tungeipelekesha serikali hadi ikubali somo hili liwepo..

Kifupi mkuu wangu hakuna mtu anayepinga waraka huu kama ni mawazo yenye manufaa kwa jamii yetu isipokuwa nguvu hiyo wangeitumia kanisani kuwanasa hao Mafisadi na kuwapa neno la Mungu..Kama nilivyosema Ufisadi ni dalili kubwa ya kuonyesha makanisa na misikiti wameshindwa kazi yao.. Hawa Mafisadi ni sawa na mashetani na ikiwa kanisa au msikiti inawapokea na kuwatukuza, iweje leo wawe na nguvu ya kutuambia sisi kuwa mchezo mpya uanze uchaguzi 2010 wakati sisi tunataka hawa Mafisadi washughulikiwe leo - wkaose marafiki, sehemu za ibada na kila adhabu leo hii..Mkuu kama ni fedha wameisha zichuma sana ni matajiri wa kutupa yaani wana hela hadi ktk truck za magari yao..na wanaendelea kupeta na mali zenu, hiyo 2010 wanaisubiri kwa hamu sana na pengine hutatawaona wakijiandikisha kabisa ktk uchaguzi.. wa nini..Fedha wanayo, huo Ubunge wa nini tena! wakati kilichowapeleka Chimwaga ni kuzoa mahela yetu!
 
Jamani , naona hii issue imenipita kidogo kwani huo waraka ulilengwa kwa watu gani ? Jee ni watanzania wote, wakristo wote au wakatoliki tuu ?
 
Rufiji,
Mkuu unaposema walengwa bila shaka ni - Mafisadi na viongozi wabovu, wabaya, U name it.
Tatizo langu sii waraka wenyewe, kwani vitabu vya dini zote zinatufundisha kuepukana na hawa watu..tatizo ni pale tunnapowakumbatia na kufikiria kwamba tunaweza kubadilisha mwongozo kuwafichua wakati hawa viongozi ambao hadi sasa hivi wanakaribishwa misikitini na makanisani..

Kisha kuna swala la Uraia ambalo ni muhimu sana kwa Wadanganyika ambao hadi leo baada ya miaka 48 ya Uhuru bado tupo kizani..Pamoja na kuwa kizani sijui kanisa hilo limelenga Tanzania nzima au bara tu kwa sababu haikuzungumziwa Muungano na haki ya Wazanzibar kama nchi..
Waraka umelenga zaidi viongozi wachafu na kusema kweli ni tishio kubwa sana kwa CCM, lakini wakati huo huo kundi kubwa la Mafisadi hawapo ktk ngazi za Uongozi wa nchi..
Kutomchagua Rostam kama mbunge wa Igunga haiwezi kusaidia kwa sababu mabaya yote anayoyafanya Rostam sii kwa sababu ni mbunge! ila kashindwa kumpokea bwana au niseme ni sawa na mtu asiyekuwa na dini.. Hivyo njia bora sana ya kumwongoza mtu kama huyu ni kumpa neno la Mungu waislaam wanasema DAWA!..Rostam, Lowassa, Mkapa Karamagi, Kingunge na wengine wote wanamhitaji YESU, waongoke! na hii ngekuwa kazi ya kanisa na misikiti badala ya waraka!
Nje ya hapo ni mahakamani tu..Hizi habari za kuchagua wabunge ambao binafsi sioni mazuri yao (toka CCM) hata kwa wale wasafi ni kupoteza focus yetu ktk kuwashughulikia Mafisadi. We know them tuufikishe ujumbe kwao direct bila kupindapinda..
 
Huyu makwaia anataka ku fool all ze pipo all ze time,2naloose so many calories 2nazozipata kwa jasho toka kwa mama lishe,just siting down and sikilizaling his non sense talks!!!!
 
Rufiji,
Mkuu unaposema walengwa bila shaka ni - Mafisadi na viongozi wabovu, wabaya, U name it.
Tatizo langu sii waraka wenyewe, kwani vitabu vya dini zote zinatufundisha kuepukana na hawa watu..tatizo ni pale tunnapowakumbatia na kufikiria kwamba tunaweza kubadilisha mwongozo kuwafichua wakati hawa viongozi ambao hadi sasa hivi wanakaribishwa misikitini na makanisani..

Kisha kuna swala la Uraia ambalo ni muhimu sana kwa Wadanganyika ambao hadi leo baada ya miaka 48 ya Uhuru bado tupo kizani..Pamoja na kuwa kizani sijui kanisa hilo limelenga Tanzania nzima au bara tu kwa sababu haikuzungumziwa Muungano na haki ya Wazanzibar kama nchi..
Waraka umelenga zaidi viongozi wachafu na kusema kweli ni tishio kubwa sana kwa CCM, lakini wakati huo huo kundi kubwa la Mafisadi hawapo ktk ngazi za Uongozi wa nchi..
Kutomchagua Rostam kama mbunge wa Igunga haiwezi kusaidia kwa sababu mabaya yote anayoyafanya Rostam sii kwa sababu ni mbunge! ila kashindwa kumpokea bwana au niseme ni sawa na mtu asiyekuwa na dini.. Hivyo njia bora sana ya kumwongoza mtu kama huyu ni kumpa neno la Mungu waislaam wanasema DAWA!..Rostam, Lowassa, Mkapa Karamagi, Kingunge na wengine wote wanamhitaji YESU, waongoke! na hii ngekuwa kazi ya kanisa na misikiti badala ya waraka!
Nje ya hapo ni mahakamani tu..Hizi habari za kuchagua wabunge ambao binafsi sioni mazuri yao (toka CCM) hata kwa wale wasafi ni kupoteza focus yetu ktk kuwashughulikia Mafisadi. We know them tuufikishe ujumbe kwao direct bila kupindapinda..
Mkandara, Habari za leo?
Nadhani waraka uliotolewa haulengi mafisadi wala viongozi wabovu. Bali unatoa matamanio ya nini serikali yenye nia njema kwa watu wake inavyotakiwa iwe. Wanaelezea mmomonyoko wa maadili, ufisadi n.k. kwa nia ya kuelezea tulipo sasa na endapo tusipobadilika tunaweza kuwa na Taifa la namna gani. Waraka huu pia unalizungumzia Taifa kwa ujumla wake bila kujali muungano. Kwani Tanzania ni Taifa linalotakiwa kuwa na umoja ambao pia unahusu Bara na visiwani.
 
Gombera,

We muulize kwanza huyo Mkandara.....je, ameshaupita waraka ule au anaupinga tu kama Mh.Kingunge na mwenzie Makwaia?

Vinginevyo umetoa mtazamo halisi wa waraka ule just can't understand why people wanaupinga tu bila kusema kipengere kipi kina matatizo!
 
Naungana na Said Sabke kuwa "Ilani ya Wakatoliki" ni mpango dhidi ya Serikali ya sasa iliyopo madarakani. Kama ukisema Kadhi na OIC ni masuala yanayokiuka katiba, je, kuwepo kwa Ubalozi wa Vatican nchini kumekubalika na katiba ipi? Ubalozi huo upo kwa minajili gani kama siyo kundeleza Ukristo? Ukitaka kubisha, thibitisha kwa kusoma Katiba ya Vatican: Dogmatic Constitution of the Church: Lumen Gentium, solemnly promulgated by his holiness Pope Paul VI, on Nov. 21, 1964...."Christ is the Light of nations. Because this is so, this sacred Synod gathered together in the Holy Spirit eagerly desires, by proclaiming the Gospel to every creature, to bring the light of Christ to all men, a light brightly visible on the countenance of the Church...The present day conditions of the world add greater urgency to this work of the Church so that all men, joined more closely today by various social, technical and cultural ties, might also attain fuller unity in Christ...". Hii ndiyo Vatican, ambayo ina ubalozi wake Tanzania, kuhitimisha kazi ya Kanisa. Ni vile tu Waislamu ni wavumilivu, ndiyo maana kuna amani! Na Ilani ya Kanisa Katoliki nchini, kuhusu uchaguzi wa viongozi na kutaka kubadilisha Katiba ya nchi, ni sehemu ya kazi hiyo iliyomo kwenye Katiba ya Vatican! Mnashanga nini? Waislamu wakitaka Mahakama ya Kadhi, OIC n.k. ni udini na ni kinyume cha Katiba!

Bwassa
 
Last edited:
Katoliki: Kingunge amepwelea (Mwananchi news paper)
Waandishi wetu

MALUIMBANO kuhusu waraka wa Kanisa Katoliki (RC) yanaendelea kuwa makali, baada ya waumini wa kanisa hilo kumuelezea mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru kuwa amepwelea.

Mbali na kauli hiyo iliyotolewa jana na Baraza la Walei, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana, Valentino Mokiwa amemtaka Kingunge kuliomba radhi kanisa badala ya kuombwa radhi kama alivyotaka.

Matamko hayo mazito yalitolewa kwa nyakati tofauti jana wakati wahusika hao walipokuwa wakizungumza na gazeti hili kuhusu utashi wa Kingunge kuwa Kanisa Katoliki limuombe radhi na kuungama kutokana na kumwita kuwa ni mkongwe.

Mwenyekiti wa Baraza la Walei, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Balozi Nicholas Kuhanga alisema baraza limewataka maaskofu wa kanisa hilo, kutoendelea kujibishana na Kingunge badala yake kazi hiyo sasa itafanywa na baraza hilo. Kuhanga, ambaye amewahi kuwa waziri, alisema wamefikia uamuzi huo kwa kuwa baraza linamjua kwa undani mwanasiasa huyo kwa kuwa wanaishi naye.

Balozi Kuhanga alisema anamshangaa Kingunge kuupinga waraka huo wakati unawasisitizia wananchi kuwachagua viongozi waadilifu na wanaojali maslahi ya wananchi. Alisema kanisa haliwezi kumwomba radhi Kingunge kwa kuwa hana tofauti na mafisadi kutokana na kitendo chake cha kupinga waraka unaowapinga mafisadi.

"Yeye anaingia katika kundi hilo, (Mafisadi) kutokana na msimamo wake wa kuupinga waraka huo unaopinga ufisadi nchini," alisema Kuhanga. "Wale ambao hawana hulka za kifisadi wanaunga mkono waraka wakati wale ambao wana hulka za kifisadi wanaupinga, kwa sababu unatishia maslahi yao." Alifafanua kuwa waraka huo umetolewa kama somo la uraia ambalo limeonekana kufifia na kusababisha mmomonyoko wa maadili katika jamii.

Naye Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo, Joseph Selasini alisema kwamba kauli ya Kingunge inamfanya aonekane kwamba upeo wake wa kufikiri umekwisha na sasa hana tena cha kuweza kuwasaidia Watanzania. "Upeo wake wa kuelewa umeshuka baada ya miaka mingi ya siasa, akili yake imechoka, imechakaa, na haina tena uwezo wa kuwasaidia Watanzania," alisema Selasini.

Selasini alisema Kingunge angekuwa na hoja iwapo angewaeleza Watanzania kifungu cha Katiba ya Tanzania ambacho kimevunjwa na waraka huo. Alifafanua kuwa kilichofanywa na maaskofu ni kutumia uhuru wao wa kikatiba kutoa mchango wao wa mawazo kwa jamii ili mradi hawavunji sheria.

"Ingekuwa ni maajabu kama maaskofu wangesimama makanisani na kukemea maovu, lakini wakaacha kuwakemea watenda maovu ambao wapo hata serikalini. Waraka unawakumbusha Watanzania kukemea maovu na kukataa wasiongozwe na watenda maovu.

Hili si kosa." Kuhusu madai ya Kingunge kuwa waraka huo unachanganya dini na siasa, Selasini alisema huwezi kutenganisha dini na siasa kwa sababu vitu hivyo ni sawa na mwili na roho, lakini akasisitiza kuwa ungekwenda kinyume iwapo waraka ungeelekeza wachaguliwe watu wa dini fulani au kabila fulani pekee.

Alisema Kingunge, ambaye jina lake la awali ni Caetan Maurice Ngombare Mwiru, haujui ukatoliki kwa sababu ulimshinda na kukimbilia ukomunisti ambao pia umemshinda na sasa anakimbilia ubepari.

Selasini amemwelezea Kingunge kuwa yupo njia panda kwa sababu amekimbilia ubepari akiwa amechelewa. Hata hivyo, alisema Wakatoliki wangependa kuona madhehebu ya dini mbalimbali na mashirika yasiyo ya kiserikali yakitoa waraka kama huo kuelimisha wananchi namna ya kupata viongozi waadilifu.

Alisema kwa kutumia hayo, serikali ingeyakusanya, kuyaratibu na kutoa muongozo kwa manufaa ya taifa zima ukiwakilisha maoni ya wote.

Aliitahadharisha CCM na serikali kuwa macho na kauli za Kingunge kwa sababu zinaweza kutafsiriwa kwamba anayoyatamka yana mkono wao baada ya mwanasiasa kutoa matamshi dhidi ya RC katika mkutano na waandishi ulioratibiwa na chama hicho tawala.

Katika kuonyesha jinsi tabia ya mwanasiasa huyo inavyoweza kuleta madhara kwa jamii, Selasini alimfananisha Kingunge na ndege aitwaye lipyoto ambaye ana kawaida ya kusababisha mifarakano.

Alifafanua kuwa lipyoto huchafua maji ya kisima kilicho katikati ya vijiji viwili na kusababisha wanavijiji wa maeneo hayo mawili kugombana kwa tuhuma kuwa kijiji kimoja ndicho kilichochafua maji.

Wakati huo huo, Umoja wa Wanawake Wakatoliki Tanzania (Wawata) Jimbo Kuu la Dar es Salaam umetoa msimamo kuwa unaunga mkono waraka na msimamo wa maaskofu wa kanisa hilo na hakuna kitakachowafanya kubadili msimamo huo. Katibu wa Wawata, Yusta Chacha alisema: "Tunaunga mkono kwa nguvu zote waraka na msimamo wa maaskofu wetu."

Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Mhashamu Valentino Mokiwa alisema mwanasiasa huyo ndiye anayepaswa kuliomba radhi kanisa Katoliki na si maaskofu wa kanisa hilo kumwomba radhi yeye. Alisema Kingunge ana siasa za kizamani na kwamba RC haikukosea kutoa waraka huo.

"Huu ni waraka wa kanisa, hivyo halijakosea kuutoa ni wajibu wake, ninachokiona hapa ni kuwa Kingunge anataka kutumia siasa za kizamani," alisema askofu huyo. Waraka haukuwasema viongozi wa serikali bali baadhi ya viongozi wake waliokaa katika hali ya rushwa na ndio maana rushwa imetawala nchi."

Kabla ya kuzungumzia tena suala hilo juzi, Kingunge aliibuka bungeni katika mkutano wa 16 uliomalizika Julai 31 mwaka huu na kulisihi kanisa hilo liuondoe waraka huo, akieleza kuwa unaligawa taifa. Kauli hiyo ya Kingunge iliamsha hisia tofauti miongoni mwa jamii huku kanisa lenyewe likimpinga na kufafanua kuwa wanaoogopa waraka huo uliotolewa kupinga ufisadi, ni mafisadi.
Juzi katika mkutano wake na waandishi wa habari nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, Kingunge aliibuka upya na kulitaka kanisa hilo limwombe radhi na maaskofu hao watubu kwa kumwita fisadi. Habari hii imeandaliwa na Exuper Kachenje, Leon Bahati na Minael Msuya
 
wakatoliki wanataka kuifanya hii nchi ni yao peke yao ukweli ni kuwa tumekubaliana tusichanganye dini na siasa

wao wasimamie mambo ya imani na kama wanajiona wanahitaji ya siasa basi waanzishe chama waache ujinga wao na kutaka kuingiza tanzania katika mambo yasio na faida

suala la kadhi wao walikuwa mbele kusema ni la kisiasa na litatugawa hali ni suala la kijamiii, hawa watu ni ovyo sana
 
Naungana na Said Sabke kuwa "Ilani ya Wakatoliki" ni mpango dhidi ya Serikali ya sasa iliyopo madarakani. Kama ukisema Kadhi na OIC ni masuala yanayokiuka katiba, je, kuwepo kwa Ubalozi wa Vatican nchini kumekubalika na katiba ipi? Ubalozi huo upo kwa minajili gani kama siyo kundeleza Ukristo? Ukitaka kubisha, thibitisha kwa kuoma Katiba ya Vatican: Dogmatic Constitution of the Church: Lumen Gentium, solemnly promulgated by his holiness Pope Paul VI, on Nov. 21, 1964...."Christ is the Light of nations. Because this is so, this sacred Synod gathered together in the Holy Spirit eagerly desires, by proclaiming the Gospel to every creature to bring the light of Christ to all men, a light brightly visible on the countenance of the Church...The present day conditions of the world add greater urgency to this work of the Church so that all men, joined more closely today by various social, technical and cultural ties, might also attain fuller unity in Christ...". Hii ndiyo Vatican, ambayo ina ubalozi wake Tanzania, kuhitimisha kazi ya Kanisa. Ni vile tu Waislamu ni wavumilivu, ndiyo maana kuna amani! Na Ilani ya Kanisa Katoliki nchini, kuhusu uchaguzi wa viongozi na kutaka kubadilisha Katiba ya nchi, ni sehemu ya kazi hiyo iliyomo kwenye Katiba ya Vatican! Mnashanga nini? Waislamu wakitaka Mahakama ya Kadhi, OIC n.k. ni udini na ni kinyume cha Katiba!
Bwassa

Bwassa,

Si busara sana kuingia jamvini na kuongelea vitu ambavyo wewe mwenyewe huvijui utaishia kuwapotosha na raia wengine hapa!

Kama wewe ni mgeni hapa bisha ufunguliwe na uonyeshwe chumba cha kulala ni kipi, store ni ipi, jiko ni lipi etc etc! Mambo ya Vatican /Holisee/Papa tulishayajadili sana hapa na ikaelezwa vizuri uhusiano kati ya Italy na Vatican na uhusiano wa Vatican na nchi nyingine duniani kufuatana na prouncement za UN!....Kama unahitaji details zaidi, sema uonyeshwe wapi utazipata hapa JF!

Post yako hapo juu inakuonyesha ni jinsi gani huelewi namna gani nchi yako Tz inahusiana na nchi nyingine na nini msingi wa mahusiano hayo. Hadithi ulizoleta hapo juu umezitoa kwenye vijiwe vya kahawa na bao vya kule uswazi manzese, vingunguti, buguruni, tandika etc!

Omba msaada usaidiwe kuelewa mambo usiyoyajua kuliko kukurupuka na kuandika vitu ambavyo havipo mkuu wangu!
 
Kinachomtia hofu Mzee wetu Caetano Maurice Kingunge Ngombale Mwiru ni MTANDAO wa WAKATOLIKI ambao upo kila kona ya Nchi hii. Ukienda kila kijiji au mtaa wa nchi hii utakuta kuna PAROKIA au KIGANGO au JUMUIA NDOGO ya kikatoliki. Watu hawa wanakutana kila wiki sio chini ya mara mbili au zaidi. Nidhamu na utii kwa viongozi wao ni ya hali ya juu. Wakielimishwa yote yaliyomo kwenye waraka huu CCM na akina KINGUNGE watabaki kweli?
 
wakatoliki wanataka kuifanya hii nchi ni yao peke yao ukweli ni kuwa tumekubaliana tusichanganye dini na siasa

Kivipi RC wanataka waifanye nchi hii ya kwao? kwani umeambiwa ule waraka ni wa wakatoliki pekee? Na je, niambie kny waraka ule kuna mambo gani yanazungumzia dini.....kuonyesha kuna kuchanganya dini na siasa?

wao wasimamie mambo ya imani
Unafahamu unachokisema lakini? we unafikiri wakatoliki wote ni viongozi wa dini? Waraka ule umeandaliwa na wasomi (CPT) wa kikatoliki....kwa hiyo unataka kuniambia wakatoliki hawana haki ya kuzungumzia au kutoa elimu ya uraia coz of the imani yao eeh? ....try to think out side of the box!

na kama wanajiona wanahitaji ya siasa basi waanzishe chama
Hilo ndo mnalisema nyie, technical issues mnazigeuza siasa.....no wonder why hamna maendeleo!

waache ujinga wao
Acha jazba bro......kama vipi tutakusaidia mabomu ujilipue nayo...isiwe tabu!

na kutaka kuingiza tanzania katika mambo yasio na faida
Elimu ya uraia kweli si jambo jema kwa Tz au kwakuwa limetolewa na RC?

suala la kadhi wao walikuwa mbele kusema ni la kisiasa na litatugawa hali ni suala la kijamiii

Unashangaza kweli....RC ndio ni kinara wa kupinga Mahakama ya Kadhi mkuu? na kwanza kabisa nijuavyo mimi issue ya kadhi hakuna mtu kakukatalieni kuanzisha mahakama hiyo, ila tatizo nyie mnataka vya dezo dezo, eti suala la imani yenu mnataka lifadhiwe na serikali why? hapo ndipo kny utata mkuu!

hawa watu ni ovyo sana
Wanaotoa Elimu, mnawaita HOVYO, je wanaotaka mahitaji ya dini zao zigharimiwe na serikali unawaitaje?
 
Balozi Kuhanga alisema anamshangaa Kingunge kuupinga waraka huo wakati unawasisitizia wananchi kuwachagua viongozi waadilifu na wanaojali maslahi ya wananchi. Alisema kanisa haliwezi kumwomba radhi Kingunge kwa kuwa hana tofauti na mafisadi kutokana na kitendo chake cha kupinga waraka unaowapinga mafisadi.

"Yeye anaingia katika kundi hilo, (Mafisadi) kutokana na msimamo wake wa kuupinga waraka huo unaopinga ufisadi nchini," alisema Kuhanga. "Wale ambao hawana hulka za kifisadi wanaunga mkono waraka wakati wale ambao wana hulka za kifisadi wanaupinga, kwa sababu unatishia maslahi yao." Alifafanua kuwa waraka huo umetolewa kama somo la uraia ambalo limeonekana kufifia na kusababisha mmomonyoko wa maadili katika jamii.

Naye Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo, Joseph Selasini alisema kwamba kauli ya Kingunge inamfanya aonekane kwamba upeo wake wa kufikiri umekwisha na sasa hana tena cha kuweza kuwasaidia Watanzania. "Upeo wake wa kuelewa umeshuka baada ya miaka mingi ya siasa, akili yake imechoka, imechakaa, na haina tena uwezo wa kuwasaidia Watanzania," alisema Selasini.

Safi sana Baraza la walei! Huyu babu Ukatoliki ulimshinda, ukomunisti umemshinda.....now anakimbilia Ubepari! Akatuke tulonge bana!
 
Next Level,

Kwamba suala la Vatican lilijadiliwa katika JamiiForums kwa kina na kwa kirefu zamani, haliondoi ukweli huu kuwa Vatican kazi yake ni kuendeleza Ukristo, basi! Soma katiba yake! Hizi siyo hadithi, wala upotoshaji, ila ndiyo ukweli ulivyo, hata kama baadhi yenu hamtaki kuukubali! Pimeni mambo kwa uyakinifu wake na siyo kwa upendeleo tu mliouzoea. Kubalini hoja za kweli za wengine pia!

Bwassa
 
Next Level,

Kwamba suala la Vatican lilijadiliwa katika JamiiForums kwa kina na kwa kirefu zamani, haliondoi ukweli huu kuwa Vatican kazi yake ni kuendeleza Ukristo

Vatican mzee sio taasisi Vatican ni nchi mzee ambako ni makao makuu ya RC. Huko kuna Holisee ambayo hiyo inaongozwa na Pope pamoja na wajumbe wengine, chombo ambacho kama ilivyo kwa say BAKWATA au CCT au TEC kipo kwaajili ya kuimarisha imani ya Kikatoliki kwa waumini wake. So sikuelewi unaposema eti VATICAN kazi yake kubwa ni kuendeleza Ukristo kivipi?

, basi! Soma katiba yake!

Katiba inasema kuwa Vatican itakuwa inaingilia mambo ya kisiasa kny nchi ilizo na uwakilishi eeeh? Vatican kama ilivyo nchi kama Iran, Libya, Saudia...ni nchi ya Kikisto so sheria zake pamoja na katiba ya nchi ile yes, lazima itakuwa na misingi ya kidini....nini cha ajabu hapo?

Hizi siyo hadithi, wala upotoshaji, ila ndiyo ukweli ulivyo, hata kama baadhi yenu hamtaki kuukubali!

Ulichokiandika pale mwanzo kuwa eti Waraka wa kanisa ni mpango wa VATICAN dhidi ya serikali iliyopo madarakani nitaendelea kuuita hadithi na upotoshaji kutoka vijiwe vya bao na kahawa za uswahilini na wewe unajua hilo kwani umelishwa tu sumu hiyo bila kufanya jitihada kidogo kuutafuta ukweli halisi!

Pimeni mambo kwa uyakinifu wake na siyo kwa upendeleo tu mliouzoea.

Ebu kuwa mkweli kidogo hapa, nani kazoea upendeleo hapa? nyie tu sahivi mnalialia mpendelewe mahakama ya kadhi etc....hawa wengine walishapendelewa nini toa ushahidi bro....sio kuongea tu!

Kubalini hoja za kweli za wengine pia!

Hoja zikiwa na nguvu zinakubaliwa, lakini sio hoja zako za nguvu....kamwe haziwezi kukubalika!
Stay blessed!
 
King Zzenji,
Mkuu wangu Mtume Muhammad alikuja na Kuran ikiwa na nia njema kwa binadamu wote.. lakini sii lazima Kuran hiyo ifundishwe, itukuzwe na ikubalike kwa binadamu wote pamoja na kwamba ndio lengo lake..Hivyo hivyo kwa biblia, Na vitabu vinginevyo vyote hivi vimetangulia mwongozo wa dini moja na waraka hutolewa kwa wote ila hupokewa na waumini wake na sii kila mtu...

Mawazo ya kanisa yabakie kama ujumbe kwa viongozi na hakika kanisa lina kila haki kuwahamasisha waumini wake kuchagua viongozi bora kwani sote tunaitaka Pepo, lakini waraka huo hauwezi kuishirikisha serikali nzima kukaa nao kitako kuandika mwongozo wa kitaifa ambao tayari upo na ndio tunaufuata. yanayotokea leo ni uvunjaji wa mwongozo na sheria za nchi, hivyo kazi ndogo tu.. wahusika wachukuliwe hatua, hizi habari za kusamehe tuanze upya, sijui kutunga mwongozo mpya wa kutochagua viongozi mafisadi na kadhalika ni kupoteza muda.
Waraka mzuri ni ule unamtaka JK na vyombo vya sheria kuwasimamisha Mafisadi mahakamani..Binafsi sintaona haki ikianza kesho na kuwaacha kina Mkapa, Lowassa, Ro, Yona na wengineo wakipeta kwa sababu hawatachaguliwa tena na tunaanza upya na sheria mpya..
Kifupi, sisi wote tunajua Ufisadi ni kitu gani bila ushauri wa Padre wala Sheikh..Na itakuwa vizuri sana hawa Masheikh na Mapadre wazidi kuifundisha neno la Mungu kwa sababu Ufisadi unatoikana na watu kutofanya ibada..Ufisadi ni dalili kubwa ya kuonyesha kwamba dini zetu zimeshindwa kuwaokoa wananchi wake, aidha mafundiisho ni hafifu au wao viongozi wa dini ni mifano mibaya, hivyo wananchi hawaogopi tena kutenda madhambi..
Kwa hayo hapo juu niliyo highlight kwa wino mwendu naomba kupingana na wewe, na kusema si kweli, bali walimkatalia wakiwa na sababu za msingi kabisa kwani hakuja na nia njema.
Kwa kuwa si jukwaa lake na reserve more comments.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom