Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Wewe unavyowaona wachungaji hawa ni wakweli, kwa kutuchanganyia dini na siasa? Wachague moja, ya Caessar wampe Caessar na ya Mungu wampe Mungu. Tanzania ni secula state hatuwezi kuwapa fursa viongozi wa dini watuchgulie watu wa kutuongoza
 
Kupitia Chanel 10, Makwaia wa Kuhenga kama alivyo Kingunge Ngombale Mwiru, wameendeleza ngojera na propaganda zao dhidi ya waraka wa Katoriki kuhusu elimu ya uraia.

Ni kitu cha kushangaza Makwaia wa Kuhenga na Kingunge Ngombale Mwiru wanapouona waraka wa Kanisa Katoriki kuwa unaleta udini. Waraka ambao ni kwa manufaa ya taifa na unaendana na uhuru wa kutoa mawazo kama ulivyoainishwa na Katiba ya Jamhuri wa Muungano ya mwaka 1997 ibara ya 18 na sheria juu ya uhuru wa maoni, Sheria ya mwaka 1984 Na. 15 ibara ya 6.

Cha kushangaza zaidi ni kuwa waraka huo wa taasisi ambayo ni moja ya asasi zisizo kuwa za serikali (AZISE) ambao unasaidia kutoa elimu ya uraia, unaonekana kwa macho ya Makwaia na Kingunge kuwa wa kidini, lakini wakati huohuo wazee hawa hawaoni uvunjaji wa katiba uliofanywa na CCM kwa kuingiza suala ya kadhi kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM. Tena wanaona sawa tu, pale katiba inaponyemelewa kuvunjwa kwa kutaka Tanzania iwe mwanachama wa taasisi ya kidini, tofauti na matakwa ya katiba ya Tanzania ya mwaka 1997. Hapa nashawishika kuamini kuwa Makwaia wa kuhenga kama alivyo Kingunge ama wanazeeka vibaya, au wametumwa au wana ajenda zao binafsi. Na bahati mbaya, kwa makusudi wanaonekana kujenga chuki dhidi ya kanisa na kushawishi watanzania wengine kwa nia yao mbaya. Kama wasingekuwa na nia mbaya wasingetumia nguvu nyingi kupinga waraka halali na badala yake wangepinga nia ya CCM ya kuvunja katiba juu ya kadhi na wangekemea mawazo ya nchi yetu kuwa mwanachama wa taasisi ya kidini. Kwa nini Makwaia na Kingunge hawasemi chochote kuhusu masuala haya?

Bila kuona haya wala aibu, kwanza Makwaia ya kuhenga alianza kupinga waraka wa kanisa kupita gazeti moja la hapa nchini. Mara ya pili akaalika watu kwenye kipindi chake chanel 10, akiwemo mchungaji mmoja ambaye kanisa lake linasemekana kukagua sadaka mikononi ambazo watu wanatoa. Akawatumia watu hawa kulazimisha mawazo yake potofu juu ya waraka. Mara ya tatu Makwaia akaalika tena mashehe nao akawatumia kulazimisha mawazo yake ya kueneza chuki juu ya kanisa. Mara ya nne akamwalika Seif Sharrif ambaye naye wanaendana mawazo yao. Na jana tu, kwa mara ya tano Makwaia wa Kuhenga katika kuendeleza mawazo yake hasi kuhusu waraka wa kanisa kanisa alimleta Kingunge ambaye kama yeye wakaungana kuuona waraka huo kuwa unachanganya dini na siasa. Cha ajabu watu hawa wote aliowatumia Makwaia hawasemi lolote juu ya Kadhi wala OIC, kama ni mambo ya kidini na ambayo hayapaswi kufikiriwa kuingiza kwenye katiba ya nchi.

Je Makwaia wa Kuhenga na Mzee Kingune wametumwa, wanazeeka vibaya au wana ajenda yao binafsi ya siri? Watanzania tunawashauri wazee hawa waache kueneza uongo na chuki, waache elimu ya uraia iendee. Tena Kingunge ambaye inasemekana alihusika kuandaa ilani ya CCM yenye udini wa Kadhi afukuzwe uanachama na CCM na Makwaia naye apewe karipio na mwajiri wake aache kueneza chuki zake dhidi ya sehemu ya jamii ya watanzania.
 
Nafikiri Makwaia na Kingunge wana agenda yao ya siri na propaganda za kikomonisti
 
Nilimwona jana Mzee Kingunge pale C10. Anachokumbuka na kukieleza vizuri ni elimu yake ya kuungaunga na mambo mengi ya zamani kama mwongozo wa 71 na CCM ya Mwalimu. Makwaia alimwonea tu kumtundika pale ajibu mambo yalivyo sasa nchini. Umri umemtupa mkono na afya inaonekana kama ni mgogoro kwake.
 
Huyo Makwaia ni very BIAS. Nasema na nitasema. Nimeangalia kipindi chake well ni kizuri lakini hayuko independent kama muendesha mada. Kwanza Mialiko yake haija balance between two sides zinazo support na zinazopinga.Every time he brings the same side people. Sasa kwa hilo mjadala hauwi fair. Alafu the way anapolead mijadala anaonesha kusukuma uende kule anakoamini yeye. That is VERY WRONG and UNPROFESSIONAL. Ningefurahi sana kama angejaribu kubalance ili nasi tuweze kupata mchanganuo yakinifu. Otherwise kama ulivyosema awali naye anazeeka VIBAYA. Siwapendi watu wa namna hiyo.
 
Well the catholic church started to influence politics about 1800 years ago... nani atawashika... waraka wakinafiki tuu
 
Nafikiri Makwaia na Kingunge wana agenda yao ya siri na propaganda za kikomonisti
Hapana ila kanisa katoliki lina agenda ya siri ya kutaka kuing'oa SISIM madarakani na hili limethibitishwa leo katika gazeti la majira kwa tamko la kilaini.Kilaini badala ya kuongelea uoza unaofanywa na mapadre anaongelea siasa.Ukweli wote wanaodai kuna ufisadi wanaongelea njozi kwani ukiacha wachache kama mama kilango hakuna anaeeleza ufisadi upi na nani kafanya isipokuwaRostama aliyeweza kuonyesha vielelezo.hizi ni propaganda ambazo tangu zamani CIA ilikwisha andaa mpango wa kuviondoa vyama vyote vilivyopigania uhuru afrika na kuviweka madarakani vyama ambavyo havina uchungu na nchi.kanisa katoliki ni moja ya taasisi inayotumika kama ilivotumika kuondoa utawala wa kikomunist nchini poland.
 
Ukiangalia argument nyingi za Makwaia utaona kuwa hazina substance. Mengi ya anayozungumza ni kama maneno matupu ambayo yanasukumwa na wimbi la story za mitaani.Sio mtu anayefanya utafiti kabla kama Hamza kassongo au Ulimwengu. I wonder why anaendelea na kipindi chake, Channel 10 wanatakiwa kuwa makini. Hoja makini na nzito zinahitaji watu makini
 
C10 wajaribu kuweka laivu baadhi ya vipindi vyake ili watu wamsaidie kuhoji. Vinginevyo anajirekodi na kujitazama akidhani anafanya kazi nzuri tu.
 
Nafikiri Makwaia na Kingunge wana agenda yao ya siri na propaganda za kikomonisti

kitu Pekee kuhusu Makwahiya ninachokijua ni kwamba hajui kuendesha vipindi vya mahojiano. kwenye kipindi huongea yeye zaidi kuliko wale aliowaita. kwa maana nyingine mwisho wa kipindi unaona hakuna haja ya kuwaalika aliowaaalika.
 
Anachofanya huyu bwana ni kutaka ku-prejudge conclusion ya mjadala. Anapotezea watu muda bure kuuza sura kwenye luninga, mtu makini ni Jenerali Ulimwengu. Huyu jamaa namkubali yupo independent sana katika kuendesha mijadala. Haogopi "Mbwa" kumwita "Mbwa" badala ya mfugo.
 
wakati fulani nilishangaa kwa nini aling'ang'ania kuwaita kina Kitine na Ntagazwa, nikajagundua kuwa wale wazee wanakubali kupelekeshwa kirahisi na Makwaiya.
 
We jamaa bana....ulivyoandika natamani nikuone.Una mawazo ya kizamani sana!!We unafikiri CCM ndo wana machungu na nchi hii?Fumbua macho!
 
Hapana ila kanisa katoliki lina agenda ya siri ya kutaka kuing'oa SISIM madarakani na hili limethibitishwa leo katika gazeti la majira kwa tamko la kilaini.Kilaini badala ya kuongelea uoza unaofanywa na mapadre anaongelea siasa.Ukweli wote wanaodai kuna ufisadi wanaongelea njozi kwani ukiacha wachache kama mama kilango hakuna anaeeleza ufisadi upi na nani kafanya isipokuwaRostama aliyeweza kuonyesha vielelezo.hizi ni propaganda ambazo tangu zamani CIA ilikwisha andaa mpango wa kuviondoa vyama vyote vilivyopigania uhuru afrika na kuviweka madarakani vyama ambavyo havina uchungu na nchi.kanisa katoliki ni moja ya taasisi inayotumika kama ilivotumika kuondoa utawala wa kikomunist nchini poland.
We jamaa unanichekesha sana.Unafikiri CCM ndo wana uchungu na nchi hii?Acha mawazo ya 1970s!Fumbua macho
 
Jamaa (makwaia ) anakujaga kufanya conclusion ya mambo ya kijiweni, huo mjadala wake mara nyingi unaonekanaga kamawanazungumzia mambo ya kijiweni tu mjadala gani watu wote wanasupport kitu kimoja tu
 
Kupitia Chanel 10, Makwaia wa Kuhenga kama alivyo Kingunge Ngombale Mwiru, wameendeleza ngojera na propaganda zao dhidi ya waraka wa Katoriki kuhusu elimu ya uraia.

Ni kitu cha kushangaza Makwaia wa Kuhenga na Kingunge Ngombale Mwiru wanapouona waraka wa Kanisa Katoriki kuwa unaleta udini. Waraka ambao ni kwa manufaa ya taifa na unaendana na uhuru wa kutoa mawazo kama ulivyoainishwa na Katiba ya Jamhuri wa Muungano ya mwaka 1997 ibara ya 18 na sheria juu ya uhuru wa maoni, Sheria ya mwaka 1984 Na. 15 ibara ya 6.

Cha kushangaza zaidi ni kuwa waraka huo wa taasisi ambayo ni moja ya asasi zisizo kuwa za serikali (AZISE) ambao unasaidia kutoa elimu ya uraia, unaonekana kwa macho ya Makwaia na Kingunge kuwa wa kidini, lakini wakati huohuo wazee hawa hawaoni uvunjaji wa katiba uliofanywa na CCM kwa kuingiza suala ya kadhi kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM. Tena wanaona sawa tu, pale katiba inaponyemelewa kuvunjwa kwa kutaka Tanzania iwe mwanachama wa taasisi ya kidini, tofauti na matakwa ya katiba ya Tanzania ya mwaka 1997. Hapa nashawishika kuamini kuwa Makwaia wa kuhenga kama alivyo Kingunge ama wanazeeka vibaya, au wametumwa au wana ajenda zao binafsi. Na bahati mbaya, kwa makusudi wanaonekana kujenga chuki dhidi ya kanisa na kushawishi watanzania wengine kwa nia yao mbaya. Kama wasingekuwa na nia mbaya wasingetumia nguvu nyingi kupinga waraka halali na badala yake wangepinga nia ya CCM ya kuvunja katiba juu ya kadhi na wangekemea mawazo ya nchi yetu kuwa mwanachama wa taasisi ya kidini. Kwa nini Makwaia na Kingunge hawasemi chochote kuhusu masuala haya?

Bila kuona haya wala aibu, kwanza Makwaia ya kuhenga alianza kupinga waraka wa kanisa kupita gazeti moja la hapa nchini. Mara ya pili akaalika watu kwenye kipindi chake chanel 10, akiwemo mchungaji mmoja ambaye kanisa lake linasemekana kukagua sadaka mikononi ambazo watu wanatoa. Akawatumia watu hawa kulazimisha mawazo yake potofu juu ya waraka. Mara ya tatu Makwaia akaalika tena mashehe nao akawatumia kulazimisha mawazo yake ya kueneza chuki juu ya kanisa. Mara ya nne akamwalika Seif Sharrif ambaye naye wanaendana mawazo yao. Na jana tu, kwa mara ya tano Makwaia wa Kuhenga katika kuendeleza mawazo yake hasi kuhusu waraka wa kanisa kanisa alimleta Kingunge ambaye kama yeye wakaungana kuuona waraka huo kuwa unachanganya dini na siasa. Cha ajabu watu hawa wote aliowatumia Makwaia hawasemi lolote juu ya Kadhi wala OIC, kama ni mambo ya kidini na ambayo hayapaswi kufikiriwa kuingiza kwenye katiba ya nchi.

Je Makwaia wa Kuhenga na Mzee Kingune wametumwa, wanazeeka vibaya au wana ajenda yao binafsi ya siri? Watanzania tunawashauri wazee hawa waache kueneza uongo na chuki, waache elimu ya uraia iendee. Tena Kingunge ambaye inasemekana alihusika kuandaa ilani ya CCM yenye udini wa Kadhi afukuzwe uanachama na CCM na Makwaia naye apewe karipio na mwajiri wake aache kueneza chuki zake dhidi ya sehemu ya jamii ya watanzania.

Hawa jamaa wako wengi na nia yao ni moja kupotosha ujumbe mzuri kwa kuwachanganya wananchi ili mambo yaendelee kuwa mabaya. Na huyo Makwaiya ana nia mbaya ya kutaka kuwepo machafuko. Maana mara nyingi anayataja hayo machafuko.

Lakini ngoja tuone. Nasikia hata Waislamu wameshaandaa waraka na sijui kama kwa hao atakuwa 'negative' kwa waraka wao au atauunga mkono kwa vile ni mdau wa dini hiyo?

Pili siku hizi kuna mahubiri karibu kila sehemu hapa jijini na ukisikiliza zaidi yanapiga vita Ukristo au Kanisa Katoliki. Hivi mahubiri ya namna hii ya kuacha kuhubiri dini yako na kuanza kukashfu dini za wengine yanaruhusiwa?
 
Hapana ila kanisa katoliki lina agenda ya siri ya kutaka kuing'oa SISIM madarakani na hili limethibitishwa leo katika gazeti la majira kwa tamko la kilaini.Kilaini badala ya kuongelea uoza unaofanywa na mapadre anaongelea siasa.Ukweli wote wanaodai kuna ufisadi wanaongelea njozi kwani ukiacha wachache kama mama kilango hakuna anaeeleza ufisadi upi na nani kafanya isipokuwaRostama aliyeweza kuonyesha vielelezo.hizi ni propaganda ambazo tangu zamani CIA ilikwisha andaa mpango wa kuviondoa vyama vyote vilivyopigania uhuru afrika na kuviweka madarakani vyama ambavyo havina uchungu na nchi.kanisa katoliki ni moja ya taasisi inayotumika kama ilivotumika kuondoa utawala wa kikomunist nchini poland.
SaidSabke+Makwaiya+Kingunge+SISI M....= UDINI
 
hakika makwaia alichemka na huwa nachemka si kiongozi mzuri wa mada aige kwa kina ADAM SEMBEYE,JEN.ULIMWENGU,HAMZA n.k naona anazungumzia ishu ya waraka for more than mwezi sasa huyu mzee kachoka aachie vijana
 
2010 is around.
tutasikia mengi ya kujitetea.
Maana kwanza akisimama majukwaani wanawaomba viongozi wa dini kuwasaidia katika kupiga vita maovu.
Wakiguswa wao viongozi wa dini wanaingilia siasa, maana yao si maovu. Hapa ndipo walipokosea kwanza.
Unafiki umewajaa.

Tutayasema yote tena tutayasema madhabahuni maana Ukristo na serikali zote ni mali ya Mungu mwenyewe. Kingunge hana dini hivyo huko ajitoe mpagani huyu. Nchi anataka kuidhabihu kwa shetani wake?
 
Bado nashindwa kuelewa ni kwanini watu wanaoujadili waraka hawauchambui waraka wenyewe kipengele kwa kipengele badala yake wanalizungumzia kanisa katoliki. Niliona kipindi C10, I ws really bored, Mzee Makwaiya kamuita Comrade mwenzake, kampa mwongozo basi ikawa nikuponda tu mwanzo mwisho, nilitegemea Kingunge angekosoa kipengele kwa kipengele lakini ametoa a blanket statement na hivyo kuungana na watu wanaotoa hoja nyepesi eti itakuwaje na Waislamu, Walutheri, Waanglikana etc nao wakija na waraka wao. Kimsingi siamini kwamba Waislamu au walutheri watakuja na waraka utakaodai eti tuchague kiongozi mla rushwa, mbinafsi, fisadi etc, wote focus yao itakuwa kiongozi anayepinga kwa dhati mambo maovu. Come on guys let's not discuss people, let's discuss and analyse issues!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom