Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Makwaia ni mwandishi mzuri isipokuwa ni very prejudicual. Kwa mfano akiandika kitu kinachohusu dini yake anakuwa biased kupita kiasi. Katika makala kuhusu Wapelesitina haangalii upande mwingine wa shilingi wa wayahudi pamoja na matatizo yao! Mtu unaweza ukawa na udini lakini ukionyesha chuki wazi wazi katika maandiko na mazungumzo yako unajiteremsha hadhi yako kama Makwaiya wa Kuhenga anavyofanya. I used to respect him lakini baada ya haya mambo ya udini udini wake nimeacha.

Makwaiya angekuwa fair kwa anagalau kumualika mtu kama Mzee Nicholas Kuhanga, Mweyekiti wa Walei (Katoliki), Tanzania ili kupata maoni ya wakatoliki kuhusu waraka wao na pengine angeweza kumshawishi aongee na TEC(Baraza la Maaskofu) kusitisha Waraka wao. TEC ina taratibu zake za kutoa na kusitisha maagizo yake kwa waumini wake sio kutokana kelele za watu kama Kingunge na Makwaiya.
 
huyu mzee nandhani anazeeka vibaya, pia anaanza kukosa sifa za kuwa mwandishi bora wa habari, anachofanya ni kulazimisha fikra na mtazamo wake uwe ndio msimamo wa jamii, pia anaharibu sifa yake na hata sifa ya kipindi pia, namshauri awe na proffesional ethics ili jamii iweze kumpa heshma stahiki
 
Mimi nitamwona Makwaia ni muungwana na anayetenda haki akiwaleta maasikofu wa kikatoliki walitoa waraka kwenye kipindi chake cha je tutafika kuliko kila siku analeta watu anaojua hawakubaliani na waraka huo.
 
Huyo Makwaia ni very BIAS. Nasema na nitasema. Nimeangalia kipindi chake well ni kizuri lakini hayuko independent kama muendesha mada. Kwanza Mialiko yake haija balance between two sides zinazo support na zinazopinga.Every time he brings the same side people. Sasa kwa hilo mjadala hauwi fair. Alafu the way anapolead mijadala anaonesha kusukuma uende kule anakoamini yeye. That is VERY WRONG and UNPROFESSIONAL. Ningefurahi sana kama angejaribu kubalance ili nasi tuweze kupata mchanganuo yakinifu. Otherwise kama ulivyosema awali naye anazeeka VIBAYA. Siwapendi watu wa namna hiyo.

Yaap Mkuu Shapu,

Wewe hakika umekuwa mfuatiliaji mzuri wa vipindi vya bw.Makwaiya na nina kubaliana na mchango wako hapo juu.

Kama ulivyosema hapo juu, binafsi sielewi kama this guy kama uandishi wa habari or mambo ya habari kama professional anajua maadili yake au la! Huyu jamaa ameekuwa akiendesha vipindi vyake very subjectively and ina very biased way kwa kweli. Panelists anowaleta kwenye vipindi ni wale tu anaona wanashabihiana kimawazo na pia wanashabihiana na mawazo na mtazomo wake pia juu ya mada zinazozungumzwa.

Kuna siku walikuwa wanajadili mambo yanayohusu mahakama ya Kadhi na OIC....Panelists wake walikuwa Mr.Mrema Augustino, Kulikuwa na Shekhe (sikumbuki jina lake) na muumini mwingine wa Kiislam alijitambulisha kama katibu wa kupigania haki za waislam(something like that) na pia kulikuwa na mama mmoja wa Kikristo.

Kwenye panel ile wote walikuwa na mawazo sawa yanayounga mkono kujiunga na OIC pamoja na uanzishwaji wa mahakama ya Kadhi. To me ule mjadala angetaka uwe na wakilishi wa kutosha na ulete maana, ilitakiwa aalike na makundi yanayopinga OIC na Kadhi pia angeleta watu wa serikali na wanaharakati labda.....so ule mjadala was too biased and the man was asking very leading questions na huwa analazimisha uende kule yeye anataka.....this is very bad!

Yaani this guy kwa kweli when it comes maada zinazozungumzwa zinahusu watu wadini......clearly you can see upande anaochukua tangia mwanzo wa mjadala, hakubali kupokea mawazo mapya...he is very mechanical & conservative!

Channel ten should do something to stop that kwa kweli!
 
Nina matatizo makubwa tu na vipindi anavyoendesha Makwaia wa Kuhenga. Kama ni mtazamaji wa vipindi vya mijadala (hard talk cha BBC, straight talk africa, ulimwengu on monday etc) utaona upeo wa MwK ulivyo chini. Vipindi vyake havina kiwango kuanzia katika muonekano hadi hoja. Tatizo alilonalo ni kuwa kama mtu anaweza kuwa mwandishi mzuri wa makala basi anaweza pia kuongoza vipindi vya mijadala katika luninga!
 
Mimi nitamwona Makwaia ni muungwana na anayetenda haki akiwaleta maasikofu wa kikatoliki walitoa waraka kwenye kipindi chake cha je tutafika kuliko kila siku analeta watu anaojua hawakubaliani na waraka huo.
Maana yake...amemleta kingunge aendelee kusisitiza na kuulisha sumu yake umma wa wadanganyika.Ndio maana hakuwaita wanaosupport ili wasimunyime nafasi

Hii haina tija..
 
Nina matatizo makubwa tu na vipindi anavyoendesha Makwaia wa Kuhenga. Kama ni mtazamaji wa vipindi vya mijadala (hard talk cha BBC, straight talk africa, ulimwengu on monday etc) utaona upeo wa MwK ulivyo chini. Vipindi vyake havina kiwango kuanzia katika muonekano hadi hoja. Tatizo alilonalo ni kuwa kama mtu anaweza kuwa mwandishi mzuri wa makala basi anaweza pia kuongoza vipindi vya mijadala katika luninga![/QUOT
hii Jenerali on monday,eti siku hizi inaitwa c10 on monday?hakuna hujuma hapo kweli,maana jenerali alikuwa anagusa mpaka sehemu nyeti...simuoni tena
 
Nimeusoma waraka wa kanisa katoliki na sijaona tatizo lake, na sielewi watu wanaposema kuwa Kilaini anachanganya dini na siasa. Kanisa lina wajibu wa kuelimisha jamii katika kutoa eliku hii inatakiwa kugusa nyanja zote ikiwamo siasa. Sasa watu wanajuaje wajibu wao kama raia wa nchi kama wasipoelimishwa? Ukiangalia raia wengi hawajui wajibu wao kikatiba na hii inatokana na mfumo mbovu wa elimu miaka ya nyuma. Watu walifundishwa propaganda ya siasa (somo la siasa) ambalo lilijikita katika katiba na kiongozo ya CCM na hata leo ni raia wachache tu wanajua au wameisoma katiba.
Pili, katika waraka huu unaeleza vipaumbele vya nchi. Nchi lazima iwe na dira na majukumu ambayo yanaweza kupimwa ktk kila awamu. Nchi yetu inahitaji mipango kama hii ya kuhainisha na kutekeleza mipango kutokana na vipaumbele muhimu. Sasa udini hapa umeingiaje? Kwanini tumekuwa wafia siasa na ushabiki usio na maana? Masheikh nao walisema watatoa warak wao nao mtasema ni udini (kama haugusi masuala imani za watu)?. Tatizo kubwa walio wengi wetu hatupendi kusoma na kuchanganua kwa kina mambo, tunapenda vitu rahisi vya kijiweni, blah blah tu!
 
Hapana ila kanisa katoliki lina agenda ya siri ya kutaka kuing'oa SISIM madarakani na hili limethibitishwa leo katika gazeti la majira kwa tamko la kilaini.Kilaini badala ya kuongelea uoza unaofanywa na mapadre anaongelea siasa.Ukweli wote wanaodai kuna ufisadi wanaongelea njozi kwani ukiacha wachache kama mama kilango hakuna anaeeleza ufisadi upi na nani kafanya isipokuwaRostama aliyeweza kuonyesha vielelezo.hizi ni propaganda ambazo tangu zamani CIA ilikwisha andaa mpango wa kuviondoa vyama vyote vilivyopigania uhuru afrika na kuviweka madarakani vyama ambavyo havina uchungu na nchi.kanisa katoliki ni moja ya taasisi inayotumika kama ilivotumika kuondoa utawala wa kikomunist nchini poland.

Wewe inaonekana una tatizo kubwa la uelewa. Hakuna agenda yoyote ya siri kwenye waraka wa Kanisa. Kuna ubaya gani kwa viongozi wa dini kuwasisitiza wananchi kuchagua viongozi waadilifu? Unaposema wanataka kuiong'oa CCM madarakani unakiri kwamba chama hicho tawala hakina watu waadilifu, sio? Hayo mengine unayoyaeleza hapo ni ya kufikirika na sijui kama hata wewe mwenyewe unayaamini.
 
Huyu mzee Makwaia kushney,

Nafikiri ana ajenda fulani anaitengeneza akifikiri watu hawamwelewi kumbe ni utoto tu anafanya. Kwa nini ajenda yake ni waraka wa wakatoliki , udini na ukabila.

NAFIKIRI HUYU ANA MKATABA NA CUF

Jana pioa mzee Kingunge alielezea vizuri saana kuhusu udini kwamba ni mambo aliyoyasimamia kidete Mwl Nyerere yasiingie kwenye siasa.

Swali: Mwalimu Jk pia alichukia rushwa, ufisadi na kujilimbikizia mali haswa kwa viongozi. Hayo mbona Kingunge hajatia neno kukemea au ndio stori ya Ubungo Bus Terminal inamsuta?

KINGUNGE: TUKUMBUSHE YOOOTE ALIYOKEMEA MWALIMU NA UYAKEMEE KWA VITENDO TUIGE MFANO NA SIO KUWA KIBARAKA CHA MAFISADI
 
Kwanza kabisa nawapongeza wa Tanzania walio5towa mawazo yao aidha kuunga mkono waraka wa Kanisa kAtoliki au kupinga hoja za mzee Kingunge na Kakwaia. Kwani wametumia fursa yao ya kikatiba ya kutoa maoni yao ambayo kwamtazamo wao yatasaidia kuleta amani na utulivu ndani ya taifa letu. Hata hivyo, napenda kuwafahamisaha ndugu hao kwamba hata mzee Kingunge na Makwai ni wa-Tanzania kama wao na waliyosema ni sehemu ya uhuru wa matumizi ya demokrasia ya kutoa maoni yao kwa madhumuni sawia ya kuleta amani na utulivu wa Taifa letu. Wala isije ikaeleweka bibaya kuwa ati wana agenda ya siri. Kwani kuwa na nia njema kwa Taifa ni lazima watu wote wakubaliane na Kanisa KATOLIK? Kuhusu swala la Mahaka ya Kadhi kwandugu zetu Waislam, napenda ifahamike kwamba mahakama hiyo iwapo itaanzishwa haito muhukumu mkristo bali waislamu wenyewe. Sasa pilipili iko shamba wa mjini yakuwashia nini? Kama kuzungumzia Mahakama ya kiislam maana yake ni kuislimsha Tanzania, basi vivyo hivyo kukubaliana na matakwa ya Kanisa Katolik ni sawa na TO CATHOLISIZED OUR COUNTRY AS WELL!!! Ya kaisaili tumuachie kaisali na ya Mungu tumpe Mungu. Mpo hapoo washikaji?!!!!!!!
 
Makwaia atatetea jambo lolote linazo wagusa waislam na si maslahi ya Nchi .Mie nashangaa mnapoteza kumjadili jamaa ni makapi ya mwisho.Elimu sijui ya Urusi sijui ya wapi ya miaka hiyo .Mwangalie hata uvaaji wa kale kakofia kake .Huwa na points bali kugombana na sometimes names calling msikilzeni kwa makini .Lakini mwisho wa siku anakuwa kaganga njaa maana akishuka pale Waislam ama anao watetea lazima waingie mfukoni kusema asante .
 
Oooohhh! yale yale imerudishwa tena..
Ama kweli - MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO!
 
Kupitia Chanel 10, Makwaia wa Kuhenga kama alivyo Kingunge Ngombale Mwiru, wameendeleza ngojera na propaganda zao dhidi ya waraka wa Katoriki kuhusu elimu ya uraia.

Ni kitu cha kushangaza Makwaia wa Kuhenga na Kingunge Ngombale Mwiru wanapouona waraka wa Kanisa Katoriki kuwa unaleta udini. Waraka ambao ni kwa manufaa ya taifa na unaendana na uhuru wa kutoa mawazo kama ulivyoainishwa na Katiba ya Jamhuri wa Muungano ya mwaka 1997 ibara ya 18 na sheria juu ya uhuru wa maoni, Sheria ya mwaka 1984 Na. 15 ibara ya 6.

Cha kushangaza zaidi ni kuwa waraka huo wa taasisi ambayo ni moja ya asasi zisizo kuwa za serikali (AZISE) ambao unasaidia kutoa elimu ya uraia, unaonekana kwa macho ya Makwaia na Kingunge kuwa wa kidini, lakini wakati huohuo wazee hawa hawaoni uvunjaji wa katiba uliofanywa na CCM kwa kuingiza suala ya kadhi kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM. Tena wanaona sawa tu, pale katiba inaponyemelewa kuvunjwa kwa kutaka Tanzania iwe mwanachama wa taasisi ya kidini, tofauti na matakwa ya katiba ya Tanzania ya mwaka 1997. Hapa nashawishika kuamini kuwa Makwaia wa kuhenga kama alivyo Kingunge ama wanazeeka vibaya, au wametumwa au wana ajenda zao binafsi. Na bahati mbaya, kwa makusudi wanaonekana kujenga chuki dhidi ya kanisa na kushawishi watanzania wengine kwa nia yao mbaya. Kama wasingekuwa na nia mbaya wasingetumia nguvu nyingi kupinga waraka halali na badala yake wangepinga nia ya CCM ya kuvunja katiba juu ya kadhi na wangekemea mawazo ya nchi yetu kuwa mwanachama wa taasisi ya kidini. Kwa nini Makwaia na Kingunge hawasemi chochote kuhusu masuala haya?

Bila kuona haya wala aibu, kwanza Makwaia ya kuhenga alianza kupinga waraka wa kanisa kupita gazeti moja la hapa nchini. Mara ya pili akaalika watu kwenye kipindi chake chanel 10, akiwemo mchungaji mmoja ambaye kanisa lake linasemekana kukagua sadaka mikononi ambazo watu wanatoa. Akawatumia watu hawa kulazimisha mawazo yake potofu juu ya waraka. Mara ya tatu Makwaia akaalika tena mashehe nao akawatumia kulazimisha mawazo yake ya kueneza chuki juu ya kanisa. Mara ya nne akamwalika Seif Sharrif ambaye naye wanaendana mawazo yao. Na jana tu, kwa mara ya tano Makwaia wa Kuhenga katika kuendeleza mawazo yake hasi kuhusu waraka wa kanisa kanisa alimleta Kingunge ambaye kama yeye wakaungana kuuona waraka huo kuwa unachanganya dini na siasa. Cha ajabu watu hawa wote aliowatumia Makwaia hawasemi lolote juu ya Kadhi wala OIC, kama ni mambo ya kidini na ambayo hayapaswi kufikiriwa kuingiza kwenye katiba ya nchi.

Je Makwaia wa Kuhenga na Mzee Kingune wametumwa, wanazeeka vibaya au wana ajenda yao binafsi ya siri? Watanzania tunawashauri wazee hawa waache kueneza uongo na chuki, waache elimu ya uraia iendee. Tena Kingunge ambaye inasemekana alihusika kuandaa ilani ya CCM yenye udini wa Kadhi afukuzwe uanachama na CCM na Makwaia naye apewe karipio na mwajiri wake aache kueneza chuki zake dhidi ya sehemu ya jamii ya watanzania.

Mtanzania:

Waraka wa kanisa ni mzuri sana. Lakini kanisa katoliki limechemsha. Na sio kanisa katoliki tu bali viongozi wa dini zingine pia.

Mafisadi ni watanzania na waumini wa dini. Na viongozi wa dini wanawajua hao watu. Kama viongozi wa dini wanatakia mema taifa, basi waambie watu na kutaja majina yao waziwazi.

Mbona Nyerere alisema Lowasa ni mla rushwa? Mbona mwanakijiji anasema JK unaboronga?

Wakara hautasaidia iwapo viongozi wa dini wanawakumbatia wahalifu.
 
Nilitegemea kuona akiitisha simu za maswali toka kwa wasikilizaji lakini sikuona.
Kumbe wasikilizaji walitakiwa wasikilize na kukubaliana na ngumbaru wawili hawa eti!
 
kila mtu aachiwe ku-comment ,km wacatholic wana haki ya kutoa waraka kwanini kingunge na makwaia wasiwe na haki ya ku-comment?
 
Nilitegemea kuona akiitisha simu za maswali toka kwa wasikilizaji lakini sikuona.
Kumbe wasikilizaji walitakiwa wasikilize na kukubaliana na ngumbaru wawili hawa eti!

,,,,,sio hivyo tu, kipindi kinaenda hakina mtiririko maalum,mara mzee KINGU anaanza kuleta stori zake za kutoroka chuo huko Liberia na kwenda kumalizia masomo yake kwenye nchi nyingine hukohuko West africa,Mzee nikicheki muda naona unaenda tu,dakika 10 za mwisho ndio wanaibuka na hoja iliokuwa imeletwa mahsusi kabisa kwa ajili ya kipindi kile nadhani,Mzee KINGU anashindilia,,,"Haiwezekani Wakatoloki watoe Ilani ya Uchaguzi eti kwa sababu wao sio Chama cha Siasa",sasa Akina Makwaia hawatuambii ndani hasa ya huo WARAKA kuna nini(manake mimi sijauona wala kuusoma),ili na sisis tujue uBAYA wake.😱
 
Last edited:
King Zzenji,
Mkuu wangu Mtume Muhammad alikuja na Kuran ikiwa na nia njema kwa binadamu wote.. lakini sii lazima Kuran hiyo ifundishwe, itukuzwe na ikubalike kwa binadamu wote pamoja na kwamba ndio lengo lake..Hivyo hivyo kwa biblia, Na vitabu vinginevyo vyote hivi vimetangulia mwongozo wa dini moja na waraka hutolewa kwa wote ila hupokewa na waumini wake na sii kila mtu...

Mawazo ya kanisa yabakie kama ujumbe kwa viongozi na hakika kanisa lina kila haki kuwahamasisha waumini wake kuchagua viongozi bora kwani sote tunaitaka Pepo, lakini waraka huo hauwezi kuishirikisha serikali nzima kukaa nao kitako kuandika mwongozo wa kitaifa ambao tayari upo na ndio tunaufuata. yanayotokea leo ni uvunjaji wa mwongozo na sheria za nchi, hivyo kazi ndogo tu.. wahusika wachukuliwe hatua, hizi habari za kusamehe tuanze upya, sijui kutunga mwongozo mpya wa kutochagua viongozi mafisadi na kadhalika ni kupoteza muda.
Waraka mzuri ni ule unamtaka JK na vyombo vya sheria kuwasimamisha Mafisadi mahakamani..Binafsi sintaona haki ikianza kesho na kuwaacha kina Mkapa, Lowassa, Ro, Yona na wengineo wakipeta kwa sababu hawatachaguliwa tena na tunaanza upya na sheria mpya..
Kifupi, sisi wote tunajua Ufisadi ni kitu gani bila ushauri wa Padre wala Sheikh..Na itakuwa vizuri sana hawa Masheikh na Mapadre wazidi kuifundisha neno la Mungu kwa sababu Ufisadi unatoikana na watu kutofanya ibada..Ufisadi ni dalili kubwa ya kuonyesha kwamba dini zetu zimeshindwa kuwaokoa wananchi wake, aidha mafundiisho ni hafifu au wao viongozi wa dini ni mifano mibaya, hivyo wananchi hawaogopi tena kutenda madhambi..
 
Last edited:
King Zzenji,
Mkuu wangu Mtume Muhammad alikuja na Kuran ikiwa na nia njema kwa binadamu wote.. lakini sii lazima Kuran hiyo ifundishwe, itukuzwe na ikubalike kwa binadamu wote pamoja na kwamba ndio lengo lake..Hivyo hivyo kwa biblia, Na vitabu vinginevyo vyote hivi vimetangulia mwongozo wa dini moja na waraka hutolewa kwa wote ila hupokewa na waumini wake na sii kila mtu...

Mawazo ya kanisa yabakie kama ujumbe kwa viongozi na hakika kanisa lina kila haki kuwahamasisha waumini wake kuchagua viongozi bora kwani sote tunaitaka Pepo, lakini waraka huo hauwezi kuishirikisha serikali nzima kukaa nao kitako kuandika mwongozo wa kitaifa ambao tayari upo na ndio tunaufuata. yanayotokea leo ni uvunjaji wa mwongozo na sheria za nchi, hivyo kazi ndogo tu.. wahusika wachukuliwe hatua, hizi habari za kusamehe tuanze upya, sijui kutunga mwongozo mpya wa kutochagua viongozi mafisadi na kadhalika ni kupoteza muda.
Waraka mzuri ni ule unamtaka JK na vyombo vya sheria kuwasimamisha Mafisadi mahakamani..Binafsi sintaona haki ikianza kesho na kuwaacha kina Mkapa, Lowassa, Yona na wengineo wakipeta kwa sababu hawatachaguliwa tena na tunaanza upya na sheria mpya..
Kifupi, sisi wote tunajua Ufisadi ni kitu gani bila ushauri wa Padre wala Sheikh..Na itakuwa vizuri sana hawa Masheikh na Mapadre wazidi kuifundisha neno la Mungu kwa sababu Ufisadi unatoikana na watu kutofanya ibada..Ufisadi ni dalili kubwa ya kuonyesha kwamba dini zetu zimeshindwa kuwaokoa wananchi wake, aidha mafundiisho ni hafifu au wao viongozi wa dini ni mifano mibaya, hivyo wananchi hawaogopi tena kutenda madhambi..

Mkandara:

Hizo longo longo tu. Kama viongozi wa dini wanahitakia nchi mema, watoe mfano kwa kuwakemea waumini wao ambao wanafahamika.

Shehe mkuu aseme JK unaboronga. Au Padri aseme Mkapa ulituibia. Wakiweza kufanya hivyo, the rest is history.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom