Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Sio chama mbadala ambacho kinavunja katiba; ni mbadala kutawala na kuwapa asali na maziwa WATZ; sio ajenda yao; CCM iliiba kadhi kwa CUF; so ndio maana wao wanashindania hoja hiyo; waache wafu wawazike wafu wenzao; chadema kaa hivyo hivyo now wasipate mahala pa kukimbilia; time will tell soon

HAPO NI SAWA, maana hao CUF hiyo ni ajenda yao tangu miaka ya 90, sasa kuhitaji jibu ktk hoja ilio andaliwa kwa muda mrefu hivyo lazima uwe kimya ukitafakari, ikibidi un anyamaza maana sikushabikia tu. safi Malundi.
 
Junius,
Mbona hiyohabari kwa sehemu kubwa inawahusu NCCR-Mageuzi na wewe unaleta kichwa cha kuonesha kama ni habari ya CHADEMA? Ni uchokozi au?
Kama chama chochote kikiamua kujibu ni suala lao la ndani. Hata Freeman akiongea bado yanaweza kuwa mawazo binafsi kama ya hawa viongozi waliotajwa. Tusubiri kama wanataka kutueleza misimamo ya vyama vyao basi watafanya hivyo. Au waandishi wawahoji hao ili kuona kama vyama vyao tayari vimeshaweka misimamo kwenye hayo mambo. Kama ningekuwa na maamuzi, basi nisingetia mguu kwenye hzo hoja. Labda CCM kwa vile ni chama tawala basi wanatakiwa kutoa msimamo kuhusu hoja y akadhi na wanaweza kusema lolote kuhusu waraka ingawa siyo lazima. Wanaotakiwa kutoa tamko ni serikali ambayo pia iko kimya kwenye suala la waraka wa Wakatoliki. Hapa naona anatafutwa mtu wa kununua kesi kama ilivyomtokea Kingunge.
 
Mjadala kuhusu waraka umekuzwa kwa kuwa watu wa dini ya kiislamu wanataka justification za mahakama ya kadhi na nchi kusilimishwa kwa sababu sio mara ya kwanza kwa kanisa katoliki kutoa waraka kama huo! Jaribu kuchunguza hata kuwepo kwa ubalozi wa Vatican nchini kwa nini mjadala huu upo sasa wakati ubalozi huu umekuwapo muda mrefu! Watu wameanza hata kuhoji kuhusu uwepo wa ubalozi wa Iran, nchi ya Kiislamu! Kwa ujumla tutasikia mengi sana wakati wa utawala wa JK, ambaye ni mwislamu na ambaye aliingia madarakani kwa kofia isiyoonekana ya kishekhe, kama mambo yataachwa yaende kwa mtindo huu!
 
Buchanan,
Mkuu wangu dini ni choice yako, kama vile wewe CCM na mimi Chadema kesho unaweza kabisa kubalidilisha chama. lakini Usitake kunilazimisha mimi nikubaliane na waraka wa CCM kwa sababu una maslahi ya wananchi hali utunzi wake umetokana na mfumo wa siasa zake.. KUBEBANA.. Hivyo, kama Mkataba utamhusisha Rostam kwa sababu ni member wa CC hata uwe na picha nzuri kiasi gani mimi siwezi kukubaliana nao..
Kanisa Katoliki halini represent mimi na sitaki representation yao ktk maswala ya siasa..washughulike na waraka unaolenga matakwa ya waumini wake.. I can easily fit in..

Kutoikubali kwako kuwa Muislaam hakukufanyi wewe kuwa mbaguzi, vile vile Musilaam kutokubaliana na Ukristu hakumfanyi kuwa mbaguzi, wewe panga mipango yako inayokuhusu wewe na mimi nitapanga yangyu after all nchi hii haikuunganishwa kwa dini zetu bali makabila..
Hizi habari za dini KUINGIA siasa ndizo zilizotufanya tukatawaliwa kwa miaka mingi wakoloni wakitaka kueneza dini zao... Mtindo unaotumika sasa hivi hauna tofauti kabisa na kufundisha dini wakitumia vyombo vya serikali.
Kuhusu Vatican inatakiwa wewe uwashukuru Waislaam kwani kama ingekuwa ndio Waislaam wana kiongozi mmoja kama Papa akiongoza nchi..msingekubali kushirikiana nayo hata kwa Ubalozi..
 
Kwa kuchapisha Ilani hii tunataka kutekeleza haki yetu ya uzalendo ili kujenga maisha
yaliyo mema zaidi kwetu sote katika siku zijazo.​
AskofuMkuu P. Ruzoka (Ukurasa wa utangulizi wa waraka)

Kitendawili msingi cha Tanzania​
Tanzania ni tajiri katika rasilimali na bado watanzania wengi ni maskini. Kwa nini? Hiki
ni kitendawili kikubwa ambacho tunapaswa kukijibu.
Umaskini katika Tanzania sio ugonjwa ambao tiba yake haipatikani kwa urahisi. Kwa
kweli umaskini tulionao huku tukiwa tumejaliwa rasilimali nyingi na utajiri mwingi
unaotokana na mchakato wa mambo mengi yanayokuwepo kwa wakati mmoja.
Hali tuliyo nayo imeletwa na mchanganyiko wa mambo mengi. Tunapaswa kuchunguza
na kuchanganua mambo hayo na hasa tukijiangalia sisi wenyewe, mienendo yetu, na​
kisha tuelewe ukweli wetu, mazuri na kasoro zetu. Kuondokana na umaskini, ni lazima
kufuata mchakato wa kubadilika. Mwenye wajibu katika kuongoza mchakato huo ni sisi
wenyewe. Ni lazima tuwe viongozi wa mchakato huo. Haifai kuwaachia watu wa nje,
wafadhili, ama fedha kutoka kwingine popote. Hatuwezi kufaulu kwa kujifunza na
kupokea njia zilizosaidia nchi nyingine. Kikwazo cha maendeleo yetu ni utegemezi na
kukosa uwajibikaji miongoni mwa mawakala katika jitihada za kuleta maendeleo.
Kukosa uwajibikaji ndio sababu kuu na jambo kuu linalosababisha umaskini wetu. Ni
lazima, kwa hiyo, tujiwajibishe wenyewe katika kujinasua na mtego huu. Lazima
tujisumbue na tuhangaikie kutafuta ufumbuzi wa matatizo yetu tukitumia ubunifu wetu​
wenyewe na rasilimali zetu wenyewe.

Imenukuliwa kama ilivyo Kutoka kwenye waraka ukurasa wa 2
 
Hivi kwa nini Kardilnali Pengo asipewe kiti Bungeni, tumalize ubishi wote!

Tunapendekeza paundwe baraza la wazee, wanaoteuliwa na sekta za kijami, ama
wanaochaguliwa na taasisi mbalimbali za kijamii, kidini na wanazuoni. Chombo
hiki kingechaguliwa na kuhakikishiwa uhuru watendaji wake kulingana na Katiba​
yenyewe. Kiwe huru, na kisibanwe na serikali.

Imenukuliwa kama ilivyo kwenye waraka Ukurasa wa 4
 
Ni kweli kwamba watanzania tunapaswa sasa tubadilike. Tuwe watu wa kutafuta ukweli, wazalendo na wenye kujituma kwa ajili ya maendeleo endelevu. Jamii inabidi ipate uelewa sahihi juu ya elimu uraia ambayo ni wajibu wa kila mwananchi kuelewa na kumwelewesha asiyeelewa zikiwemo taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na mashirika ya Dini. Hivyo waraka huo kama una nia ya kuwapa wananchi elimu waliyoikosa sasa kwa takiribani miaka hamsini sasa tangu uhuru, wanaoupinga wana agenda yao ya siri iliyo kinyume na mstakabili wa ustawi wa jamii ya watanzani. Kubwa na muhimu hapa watanzania wote tunatakiwa kustaarabika. Kustaarabika ni pamoja na kuwajibika kistaarabu katika maisha yetu kwa kadri tunavyotakiwa. Tuko nyuma sana kimaendeleo ukilinganisha na nchi za ulaya ya magharibi na hata tu nchi za Asia.

Sasa hivi niko hapa nchini Ujerumani, kwa kweli inabidi tuamke ili hatimaye tuone siku moja wananchi wetu wanapata huduma muhimu kama: Hospitali, barabara nzuri, Usafiri ya jamii (Public transport), Shule nzuri zilizo na ubora wa kuleta tija na huduma zingine muhumu ambazo zitaleta watanzania wenye afya njema na nguvu ya kulitumikia taifa. Hivyo, watu kama Mzee Kingunge inabidi wabadilike kwa masilahi ya wanachi. Miaka ya (2000-2002) nilikuwa mtumishi katika mgodi mmoja wa dhahabu kanda ya ziwa (Bulyanhulu Gold Mine-KMCL). Najua jinsi mikataba iliyowekwa na viongozi wetu inavyotunyonya na kutuachia ardhi iliyorudishiwa simenti (cement) tu na mali ikapelekwa nchi zilizoendea. Iliniuma sana kuwa nashuhudia wizi mkubwa wa namna hii, na ilibidi niache kazi na kwenda kutafuta elimu mbadala ambayo hadi sasa naendelea nayo kwa ajili ya kulitumikia taifa langu. Kubwa wanachi wa Tanzania inabidi tubadilike sana. Nilishuhudia mwezi wa nne (April) 2002, mzee Mkapa alipokuja kufungua mgodi huo jinsi alivyoshereheka. Aibu!!!!!!
 
Kingunge azidi kubanwa


na Hellen Ngoromera na Datus Bornface


amka2.gif

KAULI iliyotolewa bungeni hivi karibuni na mbunge wa kuteuliwa na rais, Kingunge Ngombale Mwiru, kwamba waraka wa Kanisa Katoliki, utaligawa taifa, jana iliendelea kukosolewa na kupingwa vikali na maaskofu wa kanisa hilo na la Kilutheri (KKKT).
Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania, Mhadhama Kardinali Polycap Pengo, akizungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Chuo cha Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam, alisema kama Kingunge hajui kusoma, ni vema akawauliza wanaojua, ili wamueleze hasa yale yaliyoandikwa katika waraka wa kanisa hilo.
Kauli hiyo ya Pengo dhidi ya mwanasiasa huyo mkongwe, ni mwendelezo wa majibu ya viongozi wa kanisa hilo, dhidi ya hatua ya mbunge huyo.
Aidha, Pengo alisema kuwa kanisa hilo halina mgombea na wala halitakipigia debe chama chochote cha siasa katika uchaguzi mkuu ujao, kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.
Alisema kuwa, anawashangaa baadhi ya watu wanaosema kwamba, kanisa hilo limeandaa waraka kwa wapiga kura ili kumpigia debe mgombea fulani au chama fulani.
“Kingunge kama hajui kusoma, basi awaambie wanaoujua wamueleze kilichoandikwa kwenye waraka wetu na sio kukurupuka kupinga kitu asichokijua vema. Narudia tena, kama Spika alivyosema, waraka uko sawa sawa kabisa.
“Sisi kama kanisa hatuungi mkono mgombea yeyote. Pia hutuungi mkono chama chochote na wala hatutakipigia debe chama chochote cha siasa katika uchaguzi ujao,” alisisitiza Pengo.
Naye, Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC), Mhashamu Askofu Juda Thaddaeus Ruwa’ichi, akizungumza na wanahabari mjini Dodoma, alisema wanaohoji waraka wa Kanisa Katoliki uliotolewa hivi karibuni wana uelewa finyu.
“Mkanganyiko wa mawazo na mawaidha yaliyotolewa na watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa unadokeza wazi kabisa kwamba wapo wanaoijadili ilani hiyo bila kujua kwanza yaliyomo ndani yake.
Hali hii inasababisha upotoshaji, kuwakanganya watu na hata kuzusha hisia za chuki katika jamii.
“Huu si uwajibikaji. Katika hili napenda kuwaasa Watanzania kuwa na tabia ya kuutafuta ukweli na kujenga hoja za msingi wa ukweli na uelewa sahihi,” alisema Ruwa'ichi ambaye pia ni Askofu wa Dodoma.
Alisema waraka huo ambao kwa maneno mengine unajulikana kama Upendo Katika Kweli, ni mhimili wa maendeleo ya kila mwanadamu na jamii.
Kwa mujibu wa Ruwa’ichi, mikataba kama ya rasilimali za madini lazima iangalie hali halisi badala ya kuigawa rasilimali hiyo bure na kukwamisha maendeleo ya taifa.
Alisema hati hiyo ambayo imejikita katika kutoa mafundisho juu ya masuala yanayohusu jamii, inaweka bayana kwamba ilani iliyotolewa na Kanisa Katoliki ni sehemu ya harakati zinazowataka watu wote kujenga uzalendo kwa njia ya elimu ya uraia, masuala ambayo ndiyo mhimili wa uwajibikaji.
Akiendelea kuutetea waraka wa kanisa hilo lenye wafuasi wengi hapa nchini, kiongozi huyo alibainisha kuwa, kanisa hilo lina nia njema ya kuwasaidia wananchi bila ubaguzi, kujizatiti kutambua na kushughulikia maslahi ya wote na pia kuhakikisha nchi na raia wake wanaishi kwa amani, haki, mshikamano, uwajibikaji na maendeleo endelevu.
Alisema viongozi waliochaguliwa na watu na kupewa dhamana, wana wajibu wa kutambua na kujali maslahi ya watu wote kwa kufanya juhudi za dhati na makusudi za kuvielewa na kuvishughulikia vipaumbele halali na sahihi vya wananchi, bila kujiruhusu kutumbukia katika mitego ya ubinafsi, ukabila, udini au ubaguzi wa aina yoyote.
Ruwa’ichi alisema shutuma zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa kuhusiana na hati hiyo iliyotolewa na Baba Mtakatifu Benedicto wa 16, Julai 7 mwaka huu, ni kielelezo cha wanasiasa hao kuwa na uelewa finyu kuhusiana na hati hiyo.
Alisema viongozi wa dini ni sehemu ya jamii na kwamba wao hawashughuliki na viumbe hewa, bali wananchi, hivyo ni lazima kuwapa mafundisho ambayo yanalenga katika kuwawezesha kufikia maendeleo ya kweli. Katika hatua nyingine, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Alex Malasusa, alisema kanisa hilo linaunga mkono waraka wa Kanisa Katoliki na kusema kuwa wanaoupinga ni mafisadi. Awali KKKT kupitia msemaji wake, ilisita kuuzungumzia waraka huo na kudai ingetoa msimamo wake baada ya kufanya vikao vya kuujadili.


Nasubiri kwa hamu sana siku ambayo Kingunge atamjibu Pengo. Nadhani bado anahisi kuwa watanzania wako uisingizini kama enzi zile,
 
Echonza,
Mkuu maelezo yako mazuri sana lakini usivute Ujerumani kuwa mfano wa Tanzania..Wao wanatawaliwa na chama cha Kikristu au sio.. au niseme chama cha dini hiyo kimo ktk vyama vya uchaguzi...Je, Tanzania tunaweza kuwa na chama cha Kiislaam na bado ukaona mfano wa Ujarumani unaweza ku apply kwetu?..

Mkuu ebu turudishe hapa huo waraka maanake tunazungumza tu bila kuangalia vifungu vyake vinasema nini..rudia soma bandiko la mwakijiji kuhusiana na waraka kisha soma zile points walizosisitiza TEC kwa serikali.. Tunachopinga sisi sio swala la elimu kwa wananchi bali kujihusisha kwa kanisa moja kwa moja na serikali..Why serikali ikae nao kupanga mikakati wakati wao sii watawala wala hawawakilishi wananchi wote.

Imani ya dini ni choice ya mtu, ukielewa hivyo utaelewa tunachopinga.. Na kama utakubali mashoga nao wapeleke waraka wao ukashindwa kuelewa kinachowekwa ndani ni zaidi ya elimu unayofikiria basi mkuu una kazi kubwa sana kuelewa... waraka wa kanisa ubakie ni maoni yao na yatatazamwa na vyombo vya serikali bila kushirikishwa kwao kwani wao sii ktk vyombo vinavyotawala nchi.
 
Last edited:
Angekuwepo Einstein angetushangaa!

Johnson Mbwambo
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo​
Julai 29, 2009

MOJA ya nukuu kadhaa zinazonivutia maishani ni ile ya Albert Einstein. Gwiji hilo la zamani la hisabati na fizikia duniani lilisema hivi: The World is a dangerous place to live not because of the people who are evil but because of the people who don't do anything about it."

Kwa tafsiri isiyo rasmi, Einstein anasema hivi : Dunia ni mahali pabaya pa kuishi si kwa sababu ya waovu waliopo, lakini kwa sababu ya kuwepo watu wasiofanya lolote dhidi ya uovu huo."

Hivi karibuni umeibuka mjadala mkubwa kuhusu hati iliyotolewa na Kanisa Katoliki Tanzania (wengine wanaiita Ilani, wengine Waraka, wengine Mwongozo nk). Hati hiyo (sijui niite Ilani, Waraka au Mwongozo) ni mapendekezo ya kanisa hilo kuhusu vipaumbele vya kitaifa.

Niyashukuru magazeti mengine nchini yaliyofikia uamuzi wa kuichapisha hati hiyo yote baada ya gazeti la Raia Mwema kuwa la kwanza kufanya hivyo. Kwa hatua hiyo, magazeti hayo yameupa umma nafasi ya kuisoma, kuitathmini, na kufanya hukumu zao wenyewe dhidi ya hati hiyo.

Kwa bahati mbaya sana; wengine wameijadili hati hiyo kwa jazba za kidini; huku wengine wakiijadili kwa kuongozwa na jazba za kisiasa na wengine wameijadili wakiongozwa na hofu ya kupoteza nafasi zao endapo utawala uliopo utaondolewa madarakani kwenye uchaguzi wa mwakani.

Ni dhahiri kwamba ukiongozwa na jazba za aina hiyo au na hofu ya kupoteza nafasi uliyonayo, huwezi kuyaona manufaa ya hati hiyo kwa umma wa Tanzania.

Wako walioukosoa si kwa yaliyomo ndani; bali kwa kulishutumu Kanisa Katoliki kwamba lina ajenda ya kuandaa viongozi wake kwenye uchaguzi wa mwakani. Hao walinifanya niisome hati hiyo tena na tena nikitafuta ajenda ya siri inayodaiwa kujificha ndani ya hati hiyo – nikitafuta mahala ambapo hati hiyo inatoa maelekezo yoyote mahususi kwa Wakatoliki (au Wakristo kwa ujumla) – sikupaona. Katika hoja zote nilizozisikia au kuzisoma - kuanzia kwa Kingunge Ngombale Mwiru na Seif Sheriff Hamad hadi kwa maofisa wa serikali walioandika kwa kujificha majina, na hadi kwenye wahariri wenye mwelekeo wa kuiunga mkono serikali, sikuona walioichana hati hiyo ya Wakatoliki hoja kwa hoja.
Wengi waliishia kwenye kimbilio rahisi walilolizoea; nalo ni kwamba hati hiyo italeta mgogoro wa kidini. Kama ambavyo serikali inapokosolewa haijibu hoja; bali hukimbilia kwenye kisingizio cha "kuhatarisha amani na utulivu", vivyo hivyo wakosoaji wa hati hiyo ya Wakatoliki wamekimbilia kwenye kututia hofu ya kuibuka kwa mgogoro wa kidini!

Wasichokijua wenzangu hawa (au wanakijua lakini hawataki kukikubali) ni kwamba Watanzania wa leo sio wa jana. Wa sasa wameerevuka na wana uwezo wa kusoma katikati ya mistari kujua pumba ni ipi na mchele ni upi, udini ni upi na maslahi ya taifa ni yapi. Hata kama hawasemi, lakini wanajua. Angalau tuwaheshimu kwa hilo.

Lakini katika wote walioikosoa hati hiyo, aliyenishangaza zaidi ni Maalim Seif. Nilitarajia mwanasiasa huyu mkongwe wa upinzani angeitathmini hati hiyo katika ujumla wake na kupima manufaa yake ya jumla kwa Watanzania masikini wa nchi hii, lakini naye kama wengine ameijadili hati hiyo si kwa kuichana hoja hadi hoja; bali kwa kukimbilia kwenye udini.

Nahisi kwamba wakati Maalim Seif anaisoma hati hiyo, tayari alishajenga fikra zake kuwa ni hati ya kidini, na hivyo wakati akiisoma alikuwa akitafuta vipengele vya kuhalalisha tu msimamo wake huo ambao tayari alishakuwanao.

Kwa bahati mbaya Maalimu Seif hakuona vipengele vyenye hoja nzito vya kuthibitisha mtazamo wake huo aliokwishaujenga. Aliishia kwenye viwili tu vya kulazimisha. Kimoja ni kile katika ukurasa wa sita kinachozungumzia umuhimu wa kuandaa viongozi, kushirikiana nao, kushikamana nao na kuwadhibiti kwa lengo la kuwasaidia kuwa jasiri na kuwa waaminifu katika kazi zao.
Maalim Seif anaona kuna udini katika kipengele hicho. Anasema hivi: "Hii ni hatari kwa sababu hawataandaa viongozi wa kidini hawa, lakini wataandaa viongozi wa dola. Na mimi siamini kwamba Wakatoliki watamwandaa Abdallah au Peter wa Pentekoste au wa Anglican."

Ni dhahiri hofu hiyo ya Maalim Seif imejengwa kutokana na fikra ambazo tayari alikuwanazo, na ndiyo msingi wa tafsiri yake hiyo potofu kwa kipengele hicho cha hati ya Kanisa Katoliki.
Kipengele kinazungumzia kuandaa viongozi bora (basi), na hakisemi kwamba kiongozi bora ni Mkristo, Mwislamu, Mkatoliki au Mlutheri, lakini Maalimu Seif anakimbilia na kusema (bila ushahidi) kuwa anayeandaliwa ni Mkatoliki!
Wako wengine (akiwemo ofisa mwandamizi mmoja wa serikali aliyeandika makala kwa kujificha jina), waliohoji ni kwa nini mwongozo huu wa sasa wa Kanisa Katoliki ni tofauti na mingine iliyopata kutolewa na Kanisa hilo huko Dodoma, Bagamoyo nk. Wanasema huu wa sasa umekwenda mbali zaidi kwenye masuala ya uongozi wa kisiasa.

Jamani, hata hilo nalo ni la kushangaa? Nani asiyejua kwamba kutokana na uongozi dhaifu nchi yetu inapitia kipindi kigumu mno kuliko ilivyopata kutokea katika historia ya nchi yetu?

Ni nani asiyejua kwamba ufisadi ndani na nje ya serikali unaitafuna nchi yetu kuliko ilivyopata kutokea huko nyuma? Nani asiyejua kwamba kiasi cha pesa za umma zilizokwibwa katika EPA (na zinazoendelea kukwibwa) hakijapata kutokea tangu tupate uhuru kutoka kwa ukoloni wa Mwingereza?

Ni nani asiyejua kwamba – ama kwa sababu ya hila za CCM au kwa sababu nyingine zozote, idadi ya wapiga kura waliojitokeza katika chaguzi ndogo za ubunge za hivi karibuni, ni ndogo mno kulinganisha na idadi ya waliojiandikisha, na hilo linaashiria hatari kubwa mbeleni?

Ni nani asiyejua kwamba ingawa nchi yetu ni tajiri mno kwa maliasili, ufukara umekithiri kote nchini, na kwamba wageni ndiyo wanaonufaika zaidi na maliasili hizo kuliko wazawa?

Ni nani asiyejua kwamba ili kuirejesha nchi katika njia sahihi itakayoiwezesha kujipatia maendeleo endelevu ni muhimu kuwa na katiba mpya na ni muhimu vilevile kuwa na tume huru ya uchaguzi?

Ndugu zangu, kama mnayajua yote hayo, basi, mtakubaliana na mimi, na bila shaka mtakubaliana na Kanisa Katoliki, kwamba hizi ni nyakati tofauti zinazohitaji hatua tofauti. Na hiyo ndiyo asili ya Kanisa Katoliki kutoa hati (iite Ilani, Waraka, Mwangozo au vyovyote vile) ambayo ni tofauti na ilizozitoa huko nyuma. Ya sasa inaliangalia taifa katika mwanga mpya na kuziona changamoto mpya zinazotukabili kama taifa.

Na ndiyo maana (ingawa mimi si Mkatoliki) nakubaliana na yote yaliyomo katika hati hiyo ya Kanisa Katoliki, na ninalipongeza kwa hatua yake hiyo ya kuwapiga somo la uraia Watanzania.

Nalipongeza pia Kanisa Katoliki kwa sababu wakati wa mchakato wa kuandaa hati hiyo, halikuwashirikisha tu wanataaluma wake; bali bali pia wabunge kadhaa (waislamu na wakristo), wanasiasa kadhaa (waislamu na wakristo), viongozi kadhaa wa serikali (waislamu na wakristo), na hata wawakilishi kutoka vyama vya siasa nchini.

Ndiyo mana ukiisoma hati hiyo unaweza kufikiria kuwa imeandaliwa na NGO moja inayojishughulisha na masuala ya demokrasia na utawala bora, na si na kanisa.
Kwangu mimi, ndani ya hati hiyo ya Kanisa Katoliki siuoni Ukatoliki, wala Ulutheri, wala Ussuni, wala Ushia. Ninachokiona ni wito wa kuwaamsha Watanzania kuuona udhaifu wa uongozi wa taifa letu na kuchukua hatua kuwapata viongozi bora.

Hati hiyo inaposema: "Tunapendekeza kwamba huduma ya afya na elimu ziwe ndiyo kipaumbele namba moja katika kupanga uchumi wetu", siuoni ukatoliki, siuoni Ulutheri, siuoni Ussuni, siuoni Ushia wala siuoni Upagani. Ninachokiona ni changamoto kwa serikali yetu kuhusu upangaji wa bajeti hususan huduma za jamii.
Hati hiyo inapopendekeza " kuweka njia imara za marekebisho ya kifedha kwa ajili ya faida ya wawekezaji na kunufaika na upendeleo zaidi kwa watu wetu badala ya kuwajali zaidi wawekezaji wa kigeni", ninachokiona si Ukatoliki, si Ulutheri, si Ussuni, si Ushia na wala si Upagani. Ninachokiona ni utetezi kwa wazawa wa Tanzania dhidi ya wawekezaji wa kigeni.

Maalimu Seif anauliza: "Je, Waprotestanti, Wapentekoste, Shia, Sunni, Ibadhi, Ahmadia na wao wakisema wanatoa ilani zao, tutaelekea wapi?" Jibu langu kwake ni kwamba tutaelekea pazuri ilimradi tu ilani zao ziwe kama ya Wakatoliki; yaani zizungumzie masuala ambayo Watanzania tuna maslahi ya pamoja (common interest).

Mimi ni Mlutheri, na ninatamani mno kanisa langu hilo nalo lingeibuka na ilani yake, kama ambavyo ninatamani Waislamu nao wangeibuka na ilani yao, kama ninavyotamani pia NGOs nazo zingeibuka na ilani zao.

Nasema hivyo kwa sababu, mwisho wa yote, tutakuwa na mjadala wa kitaifa; mjadala ambao utatuwezesha kudonoa kila yaliyo mema katika kila ilani na hatimaye kuwa na hati (ilani) yenye common interest ambayo kwayo tunaweza kuishinikiza serikali kuleta mabadiliko tunayoyataka (the change we need, kama alivyopata kusema Barack Obama).

Matatizo yangu na Kanisa ni mawili. Kwanza, Kanisa linapaswa kuishia katika kutoa elimu ya uraia kwa Watanzania ili wachague viongozi bora, na si (Kanisa) kuwaelekeza waumini wake au wananchi wengine, nani wa kumpigia kura.

Haikuwa vyema katika uchaguzi uliopita (kwa mfano) kwa Kanisa kusema kwamba Kikwete ni chaguo la Mungu. Hivi leo baada ya Kikwete kukaa Ikulu zaidi ya miaka mitatu na watu kuona uendeshaji wake wa serikali ulivyo, ni wangapi bado wanaoamini kwamba ni chaguo la Mungu?

La pili, ni usafi wa Kanisa lenyewe kama taasisi. Kwa mfano, Kanisa haliwezi kunyoosha kidole na kukosoa kuhusu ufisadi wakati lenyewe linaogelea katika ufisadi na linawakumbatia mafisadi.

Hebu natujiulize: Ni kwa nini mtuhumiwa yule wa ufisadi wa Kagoda alikimbilia kanisani kujisafisha na Kanisa likamruhusu? Ni kwa nini Mkapa alilitumia Kanisa kujisafisha?

Je, si kweli pia kwamba baadhi ya hawa watuhumiwa wakubwa wa ufisadi ni Wakristo?

Je, huo sio ushahidi kwamba Kanisa linalegalega katika kufanya kazi yake kubwa hapa duniani; yaani kupigania usafi (purity) kwa waumini wake?
Hata hivyo, pamoja na madhaifu hayo ya kanisa kama taasisi, bado naiheshimu kazi iliyofanywa na Kanisa Katoliki ya kutoa hati hiyo inayotoa elimu ya uraia kwa Watanzania wote. Nataraji makanisa mengine yataliiga Kanisa Katoliki.

Einstein anasema: "Dunia ni mahali hatari pa kuishi si kwa sababu ya kuwepo watu waovu; bali kwa sababu ya kuwepo watu ambao hawataki kuchukua hatua zozote kubadilisha hali hiyo."

Kanisa Katoliki limekuwa la kwanza kuchukua hatua za kujaribu kubadilisha hali hiyo; lakini badala ya kulipongeza na kuzishawishi asasi nyingine nazo kutengeneza ilani zao ili hatimaye tuwe na mwafaka kuhusu mambo ambayo tuna maslahi ya pamoja, tunalikejeli na kukimbilia kwenye kisingizio cha udini.

Hakika, Einstein angelikuwa hai angetushangaa na pengine angetuita mabwege kwa kukejeli hatua hiyo ya Kanisa Katoliki inayolenga kutukomboa sote. Tunaikejeli eti tu kwa sababu imetolewa na kanisa!

Tafakari.
 
Last edited:
Sap Son!

Yes Einstein angetushangaa sio kwa sababu alizoandika mwandishi. Angetushangaa kwa sababu tunawaelewa mafisadi na bado tunatumia muda kuandika waraka au ilani ambayo itatumika baada ya mwaka mmoja kupita wakati watu wanaendelea kuboronga. Huku ni kusubiri ambako ni sawa na ku-do nothing kwa kipindi cha mwaka.
 
Sap Son!

Yes Einstein angetushangaa sio kwa sababu alizoandika mwandishi. Angetushangaa kwa sababu tunawaelewa mafisadi na bado tunatumia muda kuandika waraka au ilani ambayo itatumika baada ya mwaka mmoja kupita wakati watu wanaendelea kuboronga. Huku ni kusubiri ambako ni sawa na ku-do nothing kwa kipindi cha mwaka.

Tunahitaji wanasayansi wa roketi kama Babu yangu Einstein watushangae ndio tuamke?
 
Tunahitaji wanasayansi wa roketi kama Babu yangu Einstein watushangae ndio tuamke?

Sap Comandante !!

Tatizo mnazunguka mbuyu. Wezi mnawajua, wanakwenda makanisani na misikitini. Lakini bado mnataka kuandika waraka wa uchaguzi unaokuja. Afu mnajua kuwa wanaoteua wagombeaji ni wezi walewale.

Kwa mbali nimeanza kumuhusudu na kum-miss babu Mchonga AKA haambiliki.
 
Namaanisha kama hizo nyumba za udongo unazozisema kuwa zaweza kutuamsha zimetuamsha hadi tukajenga za magorofa mbona bado hazijatuamsha tukagundua kuwa kitulacho, yaani ufisadi, ki nguoni mwetu?

Tayari tunajua kuwa kitukulacho ki nguoni mwetu. Tatizo ni kwamba jinsi mtu ulivyo ni ndivyo ulivyo tu. Kwa mfano, kina dada wanaotumia mkorogo ili wawe weupe kama wazungu, hata wajimenye vipi hawatakuwa wazungu. Hata wazichomeje nywele zao na kuzinyoosha haziwezi kuwa kama za wazungu. Same principle applies here. Mafisadi tunawajua. Wako CCM. Sasa tatizo liko wapi? Kwa nini kila siku tunawachagua wao kuongoza nchi yetu? Kama tatizo mtu unalijua na linakukera na hufanyi chochote kuliondoa hilo tatizo lakini huachi kunung'unika BASI tatizo ni wewe mwenyewe kuliko hata hilo tatizo.
 
Sap Comandante !!
[...]
Kwa mbali nimeanza kumuhusudu na kum-miss babu Mchonga AKA haambiliki.

Mjamaa Mpotevu, hakika Mchonga ilikuwa mashine nyingine, juzi nilikuwa namcheki kwenye mkanda mkali uliotengenezwa na TBC1 kuhusu miaka 30 ya Kumalizika kwa Vita vya Ukombozi dhidi ya Nduli Idi Amin Dada, we acha tu, itachukua sijui chaguzi ngapi kupata kiongozi makini kama yule - alafu kumbe Time Magazine ina nakala zote zinazomhusu Mwalimu toka enzi za Tanganyika kwenye mtandao wao, hebu cheki hii moja kutoka toleo la 26 Julai 1976 - yaani heri tungekuwa tunapata ujumbe mzito kama huu leo:

Message to America from Tanzania's President Julius K. Nyerere

As part of our Bicentennial observances TIME asked leaders of nations round the world to address the American people through the pages of TIME on how they view the U.S. and what they hope, and expect, from the nation in the years ahead. This message from Tanzania's President Julius K. Nyerere is the fourth in a series.

America is a society whose faults are the more glaring because of its admirable openness, because of the principles on which the nation was founded and because of the power which comes from its wealth and its size. It is an inspiration, and a warning, to the world. Poor nations aspire to emulate it, or else they fear it—and sometimes both.
For America is judged by the standards set out in imperishable language in the Declaration of Independence of 1776—which is one of the greatest documents of all time. And America now has a degree of wealth and power which could enable the ideals of its founding fathers to be translated into reality. It should now be possible for all Americans to live in dignity in a society which gives to all its citizens equal freedom and security and equal rights and responsibilities. Certainly, it should now be possible for America to "observe good faith and justice toward all nations" without having to fear for its own independence.
The continual struggle of Americans for the implementation of these principles within America, regardless of race or economic status, is a matter of history and contemporary politics. Much progress has been made over the past 200 years. In particular the Federal Government is now committed to fighting racial discrimination within the U.S. by laws, administrative acts and education. This we recognize; it is vital to the respect accorded to America.

But the gap between the principles and the potential on the one hand and the reality on the other is still frighteningly wide, even within America. Americans of non-European descent are still having to struggle to achieve for themselves their full rights as American citizens, equal with all others. Extreme poverty, and even hunger, exist among a sizable minority of American people. There appears to be almost a breakdown of many of the public and communal services which are vital to civilized life and in respect of which we would expect America to be an example to the rest of struggling humanity.

So countries like mine look at America in its Bicentennial year with admiration and respect, yet a feeling of disappointment for opportunities lost. But we also look at America with fear because of the use to which America's great power is often put, and the extent to which American principles have been flouted in the international exercise of American power.
Americans fought a war for their independence. They fought a civil war to maintain their unity despite the diverse social and cultural origins of Americans. The poor and oppressed of the world therefore expect Americans to understand and support the struggles of other peoples to be free and united, even if freedom and unity cannot be won peacefully. We expect that America will be the last nation, not the first, to try to thwart, pervert or destroy the real independence of other nations.

Instead, during the 15 years of our own national existence, we in Tanzania have witnessed American military power being used in an attempt to crush the national liberation struggles of Viet Nam and Cambodia. In some Latin American countries we have seen American economic power being used to frustrate the democratic will of the people about their own form of government. We have felt the effects of America's direct and indirect, but very powerful, support for the racist and colonialist forces of southern Africa. And we have seen American power time and again being used to fight freedom on the plea that it is fighting Communism.

Further, as poor nations like Tanzania struggle for those structural changes in the world economic system which are essential if our own efforts for development are not to be nullified, we find that American economic might is ranged on the other side—that is, on the side of our continued exploitation. Only minor reforms, or economic aid, are offered; sometimes even these are made conditional upon what America regards as our good political behavior in the United Nations and elsewhere. So the poor nations fear America and we struggle against America, even while we admire the great principles of America and her people's achievements.
We watch with respect, sympathy and anxiety—and sometimes almost with despair—as Americans endeavor to cope with the political and moral results of their own wealth-creating economic system, and to give international meaning to the principles laid down by the founding fathers of their nation.
For it is this one thing, above all, that really gives hope to the world. There are Americans of all colors and creeds who continue to struggle for equality and justice within America for all its peoples. There were Americans who used the time given by the dogged resistance of the Indochinese peoples in order to reassert the principles of democracy and equality and to oppose American imperialism in Southeast Asia. It was Americans who revealed, and who opposed, what was being done by their nation in Chile. And Americans are now working to get American support ranged on the side of national freedom and human equality in southern Africa.
Americans have created a power which is frequently abused internally and externally. But Americans continue to struggle against these abuses and for the survival of the universal principles enunciated in 1776. There is therefore still hope that America's great power will be used for human beings everywhere, rather than simply for the preservation and creation of American national wealth.
From Tanzania we salute America on its 200th anniversary. We send our good wishes for a future of American cooperation with the rest of the world on the basis of freedom, equality and justice, for all men and all nations.

Message to America from Tanzania's President Julius K. Nyerere - TIME
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom