Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
makwaia hajawahi kuwakilisha nguvu ya hoja bali ni hoja ya nguvu siku zote. simfahamu sana but naamini elimu yake,uelewa wke kama mwandishi una walakini,huwa anapandisha jazba kabisa kutetea anachikitaka yeye. anaiga kina Tim ebastian au Lary King, but haoni kuwa wale wanachokoa hoja toka kwa wanaohojiwa anadhani wanaweka mawazo yao. namshauri awasikilize kwa makini na kutafakari, ya udini sijui actually.
 
H soma mkataba wa Serikali na Makanisa, Serikali inawakopea hela kufungua na kuhudumia mashule, hospitali nk, na Serikali ndio inalipa. Mbona Waislam wasipewe hilo. .
Kila siju huu umekuwa wimbo utadhani ni ukweli. Tunaomba kama unayo hii MOU ya kanisa na serikali tafadhali tuwekeeni hapa. La sivyo hii itabaki ni bla bla yenu waislamu kama kawaida.

Unapozungumzia shule za Waislam nilizotaja unasema chache. Nimesema hiyo ni Dar tu.
Taja wewe zingine kama zipo! tunajua kama zipo ni hizo ulizotaja tu.
 
Nafikiri IKULU KAMA UNADAI MZEE, CHUKUENI TU. KWANZA MMEJAZA MIZIMU NA MAZINDIKO TU. kwani wakristo wanafaidika nini na ikulu, ni mara ngapi kwanza tumewaambia waihamishe iyo iende dodoma. hatuathiriki mzee.

Kama kweli ilijengwa kwa misingi ya kiislam ndiyo maana hatuna mafanikio mengi, ni laana maana kule ni matambiko mengi sana na mashetani ya kupalinda!!!! Tunaomba ing'olewe na mchanga kifusi kihamishwe tujenge nyingine. Mi nitatoa shamba langu bure kwa ajili ya kujenga Ikulu. Haliko mbali. Kwani ni lazima Ikulu ikae katikati ya mji???

Hivi siku ile moto lizuka usikute mashetani yalikasirika yalisahaliwa kulishwa dose??? Tehe tehe!!

Kujenga kwa design ya kiarabu maana yake si mali ya kiislam??!!!! Kwani ni watu wangapi wamejenga nyumba zoa kwa art ya kiarabu hata vitanda vyao na samani nyingine ndani wakati ni wakristu?? Basi na nyumba hizi ni mali zenu, draft a claim!!!! Yaani bwana,tufikirie mbali.
 
Hapo sasa tutakuwa tumefikia hatua mbaya maana mapanga kama ya algeria yatakua yananukia kabisa.
 
Nafikiri IKULU KAMA UNADAI MZEE, CHUKUENI TU. KWANZA MMEJAZA MIZIMU NA MAZINDIKO TU. kwani wakristo wanafaidika nini na ikulu, ni mara ngapi kwanza tumewaambia waihamishe iyo iende dodoma. hatuathiriki mzee.

Mbona tayari tunalo, kwani JK anakaa wapi?, asiyemuislam kuingia IKULU tena msahau. 2015 mgombea wa CCM anatoka visiwani (Juma Shamhuna) ambako waislamu ni 99%, atakaa miaka 10 mpaka 2025, tunamuweka muislam tena kwani imeonesha wazi kuwa jengo lile likikaliwa na wasio lihusu linakuwa na mauzauza tu mara linakuwa ofisi ya ujasiriamali. Teh teh teh. Jengo lile linatakiwa kukaliwa na Khalifa (kiongozi). Si unamuona JK wetu anavyoongoza nchi sasa.

Wewe una uhuru zaidi wa hata kudai majengo ya shule zetu, wakati wa mjasiriamali thubutu!. Alikuwa anajua kuwa jengo lile si lenu, hivyo mkidai shule tu na yeye anatimuliwa kwenye jengo la waumini (muuminina). Hahahahahahaa, na ndiyo maana CCM wanaona ni bora kuanzisha mahakama ya kadhi kwa wenye jengo lao (IKULU). kwikwikwi! LOL!
 
Last edited:
kANISA LISHARUDISHIWA NYINGI TU KAMA FORODHANI,MAGAMBA,MAZENGO.
 
Niliwahi kulizungumzia hli tatizo la dini ila kuna watu waliniona huyu ni mpotea njia wa uchinani,Sasa munajionea.Africa kwa ujumla hizi dini ndio chanzo cha umasikii wetu kwa 70%,sio tu kwa kubaguana bali pia tumeletewa miutamaduni ambayo hatuendani nayo then tamaduni yetu ikaitwa uchawi.Kama hii mijamaa(Ukiristu na Uisilamu) isingeingia nina imani tungemature katika mila zetu na tungekuwa na mila ya taifa,uakumbuka China walikuwa mila elfu kadhaa na kwa sasa wameziunganishana kuwa na mila mja ya Taifa.
Shame to dini zote na hao vikalagosi wenu munaowaita Jesus(Jasusi),Mohamedi(aka Allah) hehe.
I will e mail my mom,BB to Jasusi ,CC o Allah niwaambie vitabu vyao ndio source ya umasikini na tengano Africa.
Jamani,tukae pamoja na tufanye mambo ya maana.Achaneni na hii midini.
 
kANISA LISHARUDISHIWA NYINGI TU KAMA FORODHANI,MAGAMBA,MAZENGO.



Utaratibu wa kuzirudisha zote unafatiliwa kwa karibu na timu maalum na Wizara ya Elimu, Afya na Ustawi wa Jamii kwa zile Hospital kubwa na Local Government kwa zile dispensaries!!!!. Safi sana.
 
..sikubaliani na mwenendo wa Prof.Lipumba lakini namuunga mkono kuhusu uchambuzi wake wa waraka wa Kanisa Katoliki.

..binafsi nilisema kwamba ingependeza kama waraka huo ungeliepuka kujadili suala la Mahakama ya Kadhi na OIC.

..hata hapa jamii forums mmejionea jinsi hoja hizo mbili zinavyotutafuna mpaka tunashindwa kujadili masuala mengine muhimu yanayotuunganisha kama WATANZANIA.
 
Niliwahi kulizungumzia hli tatizo la dini ila kuna watu waliniona huyu ni mpotea njia wa uchinani,Sasa munajionea.Africa kwa ujumla hizi dini ndio chanzo cha umasikii wetu kwa 70%,sio tu kwa kubaguana bali pia tumeletewa miutamaduni ambayo hatuendani nayo then tamaduni yetu ikaitwa uchawi.Kama hii mijamaa(Ukiristu na Uisilamu) isingeingia nina imani tungemature katika mila zetu na tungekuwa na mila ya taifa,uakumbuka China walikuwa mila elfu kadhaa na kwa sasa wameziunganishana kuwa na mila mja ya Taifa.
Shame to dini zote na hao vikalagosi wenu munaowaita Jesus(Jasusi),Mohamedi(aka Allah) hehe.
I will e mail my mom,BB to Jasusi ,CC o Allah niwaambie vitabu vyao ndio source ya umasikini na tengano Africa.
Jamani,tukae pamoja na tufanye mambo ya maana.Achaneni na hii midini.

Sasa wewe mchina africa twambie upagani wako umeleta maendeleo yapi? Hadi sasa katika huu upagani una hali njema ipi?
 
Kuhusu mahakama ya kadhi hili pia linazungumzika,matatizo ninayo yaona hapa ni mawili

1.Wasio waislamu hawaamini kama mahakama hii haitaleta usumbufu kwa imani yao-Hawa wako sawa 100%.
Sasa njia kuu ni mazungumzo hakuna watu wenye uelewa kama mapadri na maaskofu,ni kukaa nao kujua wasiwasi wao ni nini hasa na kuwaeleza,hata ikichukua miaka 10,lakini pia wana haki ya kujiridhisha kwa sababu pia nao wana haki ya kulinda imani zao.

2.Wasio waislamu hawaoni sababu ya taasisi isio na maslahi kwao,iendeshwe kwa pesa za kodi yao=Pia wako sawa 100%
Inaweza kuangaliwa jinsi ya kuanzisha chombo hiki nje ya wigo wa serikali,halafu mtu akienda na hukumu yake pale Kisutu ipokelewe na kukazwa.

Nadhani tuepuke malumbano ya hizi hoja,tujiegemeze zaidi kushughulikia mafisadi uchaguzi haupo mbali,tukijisahau tutastukia uchaguzi upo mlangoni,jama wanarudi tena kwa kishindo huku tukijuliza tumeibiwa au karatasi zimejibadilisha?[/QUOTE]
=====

Yaani hii hoja murua kabisa. Watu watulize bori ili akili zifanye kazi.

Mpaka sasa hata katika mfumo wa mahakama zetu, mashauri ya ndoa, dini na mirathi, bado mahakimu wanapenda kusikia dini ya mhusika inasemaje kabla hawajaamua kesi hizo. Kwa hiyo sisi Waislam tukikubali kuanzisha Mhakama ya Kadhi nje ya serikali, tuna nafasi nzuri ya kuhakikisha kuwa hukumu zake, zinaheshimika katika mahakama za nchi.

Afterall, hata tungeruhusiwa kuanzishiwa ndani ya dola, bado kuna maandalizi mengi yanahitajika kufanyika. Nionavyo mimi, kuna wenzetu wanasukuma hili jambo kwa lengo la kupata ajira na wala si Uislam unaowasukuma. Serikali ile ile tunayoilaumu kwa kuiteka BAKWATA leo tunataka ituanzishie mahakama!
 
Wakatoliki mbona wameshaanza hiyo move ya kurudisha shule zao kitambo, na kusema kweli hata kama wachangiaji mnasema wakizichukua elimu itakayotolewa itakuwa bora ila watoto wa wakulima hawataweza kutia mguu kusoma kwano Ada ni kubwa sana.
Wameshaichukua shule yetu ya Forodhani (4RAWDHAN ) pale pwani ya Bahari karibia na St. Joseph, shule ambayo ilikuwa na masista duu na mabrazaman wa nguvu ( kusaga, Jack Msomali( dem wa p. Funk, ) K.Lynn, Irene Kiwia, Bonanza, lilian, na masela kibao tuliokuwa tunaibuka upande wa pili kula mihogo na wengine kibao na ndio maconcert yalipochumbukia tulikuwa tunasoma wakutoka kijichi mbagala, mburahati, manzese kwa mfugambwa, tandale kwa mtogole mpaka wa Masaki, Obay , Mikocheni, sasa watasoma wa masaki tu, kwani primary school tu pale sasa hv ( Forodhani ) ada kwa mwaka ni Tshs 2M.
Vp kuhusu Azania, Tambaza,pugu, Minaki, Kisutu, zanaki, Mtendeni Smsingi nazo zitachukuliwa
Historia zetu za Shule zinaibiwa Baba wa Taifa hakuwa Mjinga kuzipeleka hizi shule Serikalini aliepuka mengi likiwemo hili la Udini.
Tafukuri.....tafakari, tahayari.....?
 
Wataalamu wa siasa hii wanaita PROPAGANDA.

Katika kipindi hiki cha kuelekea 2010, kuna 'spin masters' wanatengeneza jambo la kushughulisha mijadala ya wananchi na kuwasahau watawala na mapungufu yao. Na likiisha hili la Kadhi na Waraka wa Kanisa, zengwe jingine litatengenezwa na ikiwezekana baadhi ya watu watajaribu kuandamana, wazuiliwe na kelele ziendelea.

Zimeishia wapi hoja za kupiga vita ufisadi? Vyama vya upinzani mbona kimya (??!!) Inashangaza hata JF tumefuata mkumbo.
 
Aisee kweli humu jamvini hv sasa pananuka moshi wa Kadhi na Maaskofu na sio uvundo wa mafisadi tena!
Mara Nov 2010 mafisadi ndani ya nyumba tumeliwa, mazee noma kiaina.
 
Jamii yoyote ikianza kuchanganya siasa na dini hupoteza mwelekeo wa maendeleo ya wananchi wake, haswa pale jamii ya Taifa lenyewe linapokuwa ni ya dini mbili kubwa. Ikiwa Taifa ni la dini moja au moja ina zaidi ya pasenti 75, basi huwa rahisi ku-handle.
Mwalimu aliona mbali sana alipoonya kuwa serikali yetu isiwe na dini bali wananchi ndiyo waruhusiwe kuabudu yoyote waitakayo au hata kubakia bila dini.

Kanisa Kotoliki linatakiwa lishauriwe kuondoa kipengele chochote kihusucho udini ndani ya waraka ili kuuhalalisha zaidi, na Bunge letu linatakiwa kuacha kabisa na kokomesha mara moja hoja zinazohusu dini Bungeni.

Na Wananchi tunaoipenda Tanzania tusiwapigie kura viongozi ambao wana hisia za udini maana hawa siyo Wantanzania halisi, ama hawalitakii mema Taifa letu.
 
Sasa wewe mchina africa twambie upagani wako umeleta maendeleo yapi? Hadi sasa katika huu upagani una hali njema ipi?
Utaleta wapi maendeleo wakati mumeshikilia midini yenu,China,Japan,Korea wote wameendelea kwakuwa hakuna midini,angalia Sri Lanka,Nepal jinsi wanavyokufa kwa ajili ya midini hiyo.
Dini(Ukoloni uliopita) na Demokrasia(Ukoloni wa kisasa) ndio chawi wa maendeleo yetu Africa,Unakumbuka Mchina alisema kuwa Africa wameruka stages na watataabika mno.
KIla mtu achuku chake mapema tuu
 
Bwana Philemon ukitakak umjua mtu mwenye akili na busara mwangalie anapozumza mbele za watu. Huyu mchungaji namsikiliza siku moja moja na nilishaconclude mbele ya familia kwamba huyu jamaa nimbabaishaji na hana akili kabisa kwanza sijui kama kamaliza std vii. I doubt kwa sababu ni mara nyingi amekuwa akikandia wachungaji wengine na kuona kuwa yeye ni bora kuliko wengine. Kuhusu wajibu wa viongozi wa dini yeye kama kiongozi hajui wajibu wake wa kuhakikisha kuwa waumini wake wanatakiwa wawe na maisha bora ndo waweze kumtumikia Mungu. Je anajua uongozi mbovu unaharibu uchumi kitu ambacho kinaweza kumpelekea yeye akakosa sadaka za waumini wake watakapo kuwa wamekataa tamaa na maisha. Anataka kuona waumini wake wanashindwa kwenda kanisani kwa kukosa lishe na nguo. Hana akili kabisa narudia tena.


hujakosea ...sipendage tabia ya watumishi wa Mungu wanaoshambulia wenzao au kushambuliana ..badala ya kukazania kazi ya kuvua samaki....[uchungaji]..,nadhani ni huyu nilimsikia siku akisema kuwa ....atashinda hata kama wanaopambana naye wako na makanisa pembeni ya barabara....sasa nadhani alikuwa akiwalenga watumishi wenzake.....

...anyway siku za mwisho zikifika ...wengi watakuja kwa jina lake....nikuomba Mungu atupe mwanga wa kujuwa sauti yake ya kweli....kama wanadamu hatuwezi kujuwa labda na yeye anaweza akawa ananena sauti ya Mungu au la....la muhimu tuombe Mungu tu...

......NDIO maana siku hizi wappo wanaokuja kwa jina la Mungu kumbe vibwetere...,mara gea ya DECI...etc ...nasangaa sana kwa nini baadhi ya watumishi wa Mungu wanangangania kuhubiria ... mjini tu ...au kwa kuwa tuna pesa za mishahara za kutoa sadaka...MUNGU ALIAGIZA NENO LA MUNGU NI KWA WATU WOTE....Lakini watu wanangangania kutumia TELEVISHENI na kutuwekea akauti namba ....wakati wanajuwa wazi asilimia 10 tu ya watanzania ndio wanamiliki umeme,,...sembuse wenye TV....mahubiri yanawalenga kina nani...kama si wenye uwezo???

nafagilia watu kama mwakasege ambaye hanganganii TV ...yeye anatumia radio ambayo asilimia kubwa wanazo .....na anafanya mikutano....ya hadhara...,waenezaji wa dini iwe kiislamu au kikristo wa mwanzo ....walienda vijijini....na kufuata watu walipo...sasa uinjilishaji usilenge matajiri pekeeeee!!!...matokeo yake ndio haya ...siku tukikosa pesa za kulipia nyenzo za mawasiliano kama tv ...unatekwa nyara....na kulishwa maneno...tu au ukajilisha ili kumfurahisha mfadhili..!!
 
Utaleta wapi maendeleo wakati mumeshikilia midini yenu,China,Japan,Korea wote wameendelea kwakuwa hakuna midini,angalia Sri Lanka,Nepal jinsi wanavyokufa kwa ajili ya midini hiyo.
Dini(Ukoloni uliopita) na Demokrasia(Ukoloni wa kisasa) ndio chawi wa maendeleo yetu Africa,Unakumbuka Mchina alisema kuwa Africa wameruka stages na watataabika mno.
KIla mtu achuku chake mapema tuu
Culture yetu ni midini hiyo. Culture ya wazungu na waarabu ni midini unayosema. Wao wameendelea na midini.
Lakini nchi ikiwa chini ya wakina Kingunge wapagani kama wewe, ni laana na hatuwezi kupata maendeleo kamwe.
Shida ni hao wapagani waliovaa ngozi ya dini walio juu ndio shida.
Tukilogwa kuwapa wapagani nchi hii tumekwisha.
 
Kingunge azidi kubanwa


na Hellen Ngoromera na Datus Bornface


amka2.gif

KAULI iliyotolewa bungeni hivi karibuni na mbunge wa kuteuliwa na rais, Kingunge Ngombale Mwiru, kwamba waraka wa Kanisa Katoliki, utaligawa taifa, jana iliendelea kukosolewa na kupingwa vikali na maaskofu wa kanisa hilo na la Kilutheri (KKKT).
Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania, Mhadhama Kardinali Polycap Pengo, akizungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Chuo cha Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam, alisema kama Kingunge hajui kusoma, ni vema akawauliza wanaojua, ili wamueleze hasa yale yaliyoandikwa katika waraka wa kanisa hilo.
Kauli hiyo ya Pengo dhidi ya mwanasiasa huyo mkongwe, ni mwendelezo wa majibu ya viongozi wa kanisa hilo, dhidi ya hatua ya mbunge huyo.
Aidha, Pengo alisema kuwa kanisa hilo halina mgombea na wala halitakipigia debe chama chochote cha siasa katika uchaguzi mkuu ujao, kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.
Alisema kuwa, anawashangaa baadhi ya watu wanaosema kwamba, kanisa hilo limeandaa waraka kwa wapiga kura ili kumpigia debe mgombea fulani au chama fulani.
“Kingunge kama hajui kusoma, basi awaambie wanaoujua wamueleze kilichoandikwa kwenye waraka wetu na sio kukurupuka kupinga kitu asichokijua vema. Narudia tena, kama Spika alivyosema, waraka uko sawa sawa kabisa.
“Sisi kama kanisa hatuungi mkono mgombea yeyote. Pia hutuungi mkono chama chochote na wala hatutakipigia debe chama chochote cha siasa katika uchaguzi ujao,” alisisitiza Pengo.
Naye, Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC), Mhashamu Askofu Juda Thaddaeus Ruwa’ichi, akizungumza na wanahabari mjini Dodoma, alisema wanaohoji waraka wa Kanisa Katoliki uliotolewa hivi karibuni wana uelewa finyu.
“Mkanganyiko wa mawazo na mawaidha yaliyotolewa na watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa unadokeza wazi kabisa kwamba wapo wanaoijadili ilani hiyo bila kujua kwanza yaliyomo ndani yake.
Hali hii inasababisha upotoshaji, kuwakanganya watu na hata kuzusha hisia za chuki katika jamii.
“Huu si uwajibikaji. Katika hili napenda kuwaasa Watanzania kuwa na tabia ya kuutafuta ukweli na kujenga hoja za msingi wa ukweli na uelewa sahihi,” alisema Ruwa'ichi ambaye pia ni Askofu wa Dodoma.
Alisema waraka huo ambao kwa maneno mengine unajulikana kama Upendo Katika Kweli, ni mhimili wa maendeleo ya kila mwanadamu na jamii.
Kwa mujibu wa Ruwa’ichi, mikataba kama ya rasilimali za madini lazima iangalie hali halisi badala ya kuigawa rasilimali hiyo bure na kukwamisha maendeleo ya taifa.
Alisema hati hiyo ambayo imejikita katika kutoa mafundisho juu ya masuala yanayohusu jamii, inaweka bayana kwamba ilani iliyotolewa na Kanisa Katoliki ni sehemu ya harakati zinazowataka watu wote kujenga uzalendo kwa njia ya elimu ya uraia, masuala ambayo ndiyo mhimili wa uwajibikaji.
Akiendelea kuutetea waraka wa kanisa hilo lenye wafuasi wengi hapa nchini, kiongozi huyo alibainisha kuwa, kanisa hilo lina nia njema ya kuwasaidia wananchi bila ubaguzi, kujizatiti kutambua na kushughulikia maslahi ya wote na pia kuhakikisha nchi na raia wake wanaishi kwa amani, haki, mshikamano, uwajibikaji na maendeleo endelevu.
Alisema viongozi waliochaguliwa na watu na kupewa dhamana, wana wajibu wa kutambua na kujali maslahi ya watu wote kwa kufanya juhudi za dhati na makusudi za kuvielewa na kuvishughulikia vipaumbele halali na sahihi vya wananchi, bila kujiruhusu kutumbukia katika mitego ya ubinafsi, ukabila, udini au ubaguzi wa aina yoyote.
Ruwa’ichi alisema shutuma zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa kuhusiana na hati hiyo iliyotolewa na Baba Mtakatifu Benedicto wa 16, Julai 7 mwaka huu, ni kielelezo cha wanasiasa hao kuwa na uelewa finyu kuhusiana na hati hiyo.
Alisema viongozi wa dini ni sehemu ya jamii na kwamba wao hawashughuliki na viumbe hewa, bali wananchi, hivyo ni lazima kuwapa mafundisho ambayo yanalenga katika kuwawezesha kufikia maendeleo ya kweli. Katika hatua nyingine, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Alex Malasusa, alisema kanisa hilo linaunga mkono waraka wa Kanisa Katoliki na kusema kuwa wanaoupinga ni mafisadi. Awali KKKT kupitia msemaji wake, ilisita kuuzungumzia waraka huo na kudai ingetoa msimamo wake baada ya kufanya vikao vya kuujadili.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom