Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Mjamaa Mpotevu, hakika Mchonga ilikuwa mashine nyingine, juzi nilikuwa namcheki kwenye mkanda mkali uliotengenezwa na TBC1 kuhusu miaka 30 ya Kumalizika kwa Vita vya Ukombozi dhidi ya Nduli Idi Amin Dada, we acha tu, itachukua sijui chaguzi ngapi kupata kiongozi makini kama yule - alafu kumbe Time Magazine ina nakala zote zinazomhusu Mwalimu toka enzi za Tanganyika kwenye mtandao wao, hebu cheki hii moja kutoka toleo la 26 Julai 1976 - yaani heri tungekuwa tunapata ujumbe mzito kama huu leo:

Message to America from Tanzania's President Julius K. Nyerere

As part of our Bicentennial observances TIME asked leaders of nations round the world to address the American people through the pages of TIME on how they view the U.S. and what they hope, and expect, from the nation in the years ahead. This message from Tanzania's President Julius K. Nyerere is the fourth in a series.

America is a society whose faults are the more glaring because of its admirable openness, because of the principles on which the nation was founded and because of the power which comes from its wealth and its size. It is an inspiration, and a warning, to the world. Poor nations aspire to emulate it, or else they fear it—and sometimes both.
For America is judged by the standards set out in imperishable language in the Declaration of Independence of 1776—which is one of the greatest documents of all time. And America now has a degree of wealth and power which could enable the ideals of its founding fathers to be translated into reality. It should now be possible for all Americans to live in dignity in a society which gives to all its citizens equal freedom and security and equal rights and responsibilities. Certainly, it should now be possible for America to "observe good faith and justice toward all nations" without having to fear for its own independence.
The continual struggle of Americans for the implementation of these principles within America, regardless of race or economic status, is a matter of history and contemporary politics. Much progress has been made over the past 200 years. In particular the Federal Government is now committed to fighting racial discrimination within the U.S. by laws, administrative acts and education. This we recognize; it is vital to the respect accorded to America.

But the gap between the principles and the potential on the one hand and the reality on the other is still frighteningly wide, even within America. Americans of non-European descent are still having to struggle to achieve for themselves their full rights as American citizens, equal with all others. Extreme poverty, and even hunger, exist among a sizable minority of American people. There appears to be almost a breakdown of many of the public and communal services which are vital to civilized life and in respect of which we would expect America to be an example to the rest of struggling humanity.

So countries like mine look at America in its Bicentennial year with admiration and respect, yet a feeling of disappointment for opportunities lost. But we also look at America with fear because of the use to which America's great power is often put, and the extent to which American principles have been flouted in the international exercise of American power.
Americans fought a war for their independence. They fought a civil war to maintain their unity despite the diverse social and cultural origins of Americans. The poor and oppressed of the world therefore expect Americans to understand and support the struggles of other peoples to be free and united, even if freedom and unity cannot be won peacefully. We expect that America will be the last nation, not the first, to try to thwart, pervert or destroy the real independence of other nations.

Instead, during the 15 years of our own national existence, we in Tanzania have witnessed American military power being used in an attempt to crush the national liberation struggles of Viet Nam and Cambodia. In some Latin American countries we have seen American economic power being used to frustrate the democratic will of the people about their own form of government. We have felt the effects of America's direct and indirect, but very powerful, support for the racist and colonialist forces of southern Africa. And we have seen American power time and again being used to fight freedom on the plea that it is fighting Communism.

Further, as poor nations like Tanzania struggle for those structural changes in the world economic system which are essential if our own efforts for development are not to be nullified, we find that American economic might is ranged on the other side—that is, on the side of our continued exploitation. Only minor reforms, or economic aid, are offered; sometimes even these are made conditional upon what America regards as our good political behavior in the United Nations and elsewhere. So the poor nations fear America and we struggle against America, even while we admire the great principles of America and her people's achievements.
We watch with respect, sympathy and anxiety—and sometimes almost with despair—as Americans endeavor to cope with the political and moral results of their own wealth-creating economic system, and to give international meaning to the principles laid down by the founding fathers of their nation.
For it is this one thing, above all, that really gives hope to the world. There are Americans of all colors and creeds who continue to struggle for equality and justice within America for all its peoples. There were Americans who used the time given by the dogged resistance of the Indochinese peoples in order to reassert the principles of democracy and equality and to oppose American imperialism in Southeast Asia. It was Americans who revealed, and who opposed, what was being done by their nation in Chile. And Americans are now working to get American support ranged on the side of national freedom and human equality in southern Africa.
Americans have created a power which is frequently abused internally and externally. But Americans continue to struggle against these abuses and for the survival of the universal principles enunciated in 1776. There is therefore still hope that America's great power will be used for human beings everywhere, rather than simply for the preservation and creation of American national wealth.
From Tanzania we salute America on its 200th anniversary. We send our good wishes for a future of American cooperation with the rest of the world on the basis of freedom, equality and justice, for all men and all nations.

Message to America from Tanzania's President Julius K. Nyerere - TIME


Kumbe babu aliisoma Declaration of Independence, lakini kwanini alikuwa mkiritimba sana?

WaAfrika bwana, wanasoma vitu lakini bado wanataka ku-reinvent the wheel.

Hila kosa lake kubwa ni kutomwashia Mrema kushinda uchaguzi wa 1995, yaani CCM wangejifunza sana.
 
Hiyo Declaration of Independence ni masterpiece. Wapi Afrika kuna nyaraka kama hiyo kwenye karne ya 18?
 
Hiyo Declaration of Independence ni masterpiece. Wapi Afrika kuna nyaraka kama hiyo kwenye karne ya 18?

Nyani Ngabu naona ushaanza, kasome juzuu ya Mtwa Mkwavinyika! Ukimaliza nenda kwenye nyaraka za Maktaba ya Chuo Kikuu cha Timbuktu. Alafu nenda Kushi ukasome urithi wa sharia za Malkia wa Sheba. Ukimaliza rudi Magharibi kwenye Himaya ya Yaa Asentewaa. Usisahau kupitia kwenye maktaba ya Alexandria. Haki na Sheria zilianzia Afrika sijui nini kimetusibu leo!
 
Charity begins at home, how many JF members are ready to come forward and participate on the JF members get together if its arranged? Can we stand by our IDs? or we are afraid of our selves? if we can not then we don't have aright to blem Tanzanians for not taking any action because we are part of them.
 
Nyani Ngabu naona ushaanza, kasome juzuu ya Mtwa Mkwavinyika! Ukimaliza nenda kwenye nyaraka za Maktaba ya Chuo Kikuu cha Timbuktu. Alafu nenda Kushi ukasome urithi wa sharia za Malkia wa Sheba. Ukimaliza rudi Magharibi kwenye Himaya ya Yaa Asentewaa. Usisahau kupitia kwenye maktaba ya Alexandria. Haki na Sheria zilianzia Afrika sijui nini kimetusibu leo!

Umejuaje kuwa huyo jamaa ni NN. Au nyie ni waarabu wa Pemba mnajuana kwa vilemba.

Anyway, mada ni kuhusu Einstein kutushangaa !!!. Kwanini watu waandike ilani, waraka, or whatever wakati wanawajua waharifu?

It seems to me kuwa viongozi wa kisiasa wanashindwa kusimama na kusema, na viongozi wa dini wanazunguka mbuyu tu.
 
Umejuaje kuwa huyo jamaa ni NN. Au nyie ni waarabu wa Pemba mnajuana kwa vilemba.

Anyway, mada ni kuhusu Einstein kutushangaa !!!. Kwanini watu waandike ilani, waraka, or whatever wakati wanawajua waharifu?

It seems to me kuwa viongozi wa kisiasa wanashindwa kusimama na kusema, na viongozi wa dini wanazunguka mbuyu tu.

Unaona komenti zako zimefanya waunganishe mada!

Kila shetani na mbuyu wake na kila nabii na kitabu chake!

Hizi ilani ni mwongozo wa kutusaidia tutumie nguvu ya umma!

Na hakika mwakani tutatumia nguvu ya watu kung'oa mzizi wa fitina!
 
Nyani Ngabu naona ushaanza, kasome juzuu ya Mtwa Mkwavinyika! Ukimaliza nenda kwenye nyaraka za Maktaba ya Chuo Kikuu cha Timbuktu. Alafu nenda Kushi ukasome urithi wa sharia za Malkia wa Sheba. Ukimaliza rudi Magharibi kwenye Himaya ya Yaa Asentewaa. Usisahau kupitia kwenye maktaba ya Alexandria. Haki na Sheria zilianzia Afrika sijui nini kimetusibu leo!

Nyani Ngabu ndio nani? Nitakuripoti kwa Invisible.

Huyo Mkwavinyika alijifunza wapi kuandika?
 
Nyani Ngabu ndio nani? Nitakuripoti kwa Invisible.

Huyo Mkwavinyika alijifunza wapi kuandika?

NN ni clone wa Nyani McCain, Ngwaninyami na pseudo-fraternity ya wyj.

Kuna aina nyingi za kuandika kama kulivyo na aina nyingi za herufi/sarufi.
 
Umefika wakati sasa kujua mchele na pumba katika mwelekeo wa Taifa hili. Ni dhahiri hali hiyo imeanza kujionyesha kwa Kingunge hata Msambya kukurupuka na kusema mwongozo huo haufai. Hakika hao wana lao jambo. Isitoshe wabunge wengine wanatoka sehemu ambazo kimaendeleo itachukua muda kupiga hatua. Sababu kubwa ni kuwa mafisadi wamepewa mwanya wa kuongoza nchi kwa kuwaibia wananchi. Mafisadi wamebaka uchumi wa Tanzania. Iweje leo Mbunge unaetegemewa kuwatetea wananchi uwakumbatie mafisadi? Waraka huu hata na mwingine ukiandikwa utaungwa mkono kama hauegemei kuwatenga/ kuwagawa wananchi. Kingunge una hofu gani????????????????????????????????????????????????????????????
 
Waraka wa Kanisa Katoliki wauzwa kama njugu nchini

Na Exuper Kachenje (Mwananchi)



UMAARUFU wa Waraka na Ilani vilivyotolewa na Kanisa Katoliki nchini, mauzo na bei yake yamezidi kuongezeka mara dufu, imebainika.

Kuongezeka kwa umaarufu wa waraka huo umekuja huku vijitabu hivyo vikiendelea kuzua mjadala na watu wa kada mbalimbali wakiwemo wabunge wakitofautiana kwa maoni.

Kanisa Katoliki nchini kupitia Chama Cha Wanataaluma Wakatoliki (CPT) kilitoa vijitabu hivyo vikieleza sifa za kiongozi anayefaa kuchaguliwa na vipaumbele vya Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi kwa siku kadhaa umebaini kuwa kiasi cha nakala 10,000 za waraka na ilani hiyo tayari zimechapwa na kununuliwa huku kukiwa na taarifa ya kuwepo mahitaji zaidi ya vijitabu hivyo kuongezeka kwa kasi.

Baadhi ya watu wameuunga mkono waraka huo na wengine kuupinga kupitia majukwaa na maeneo tofauti ikiwemo bungeni na kuchangia kuongeza umaarufu wake.

Uchunguzi huo umeonyesha kuwa vijitabu hivyo huuzwa kwa kati ya Sh2,000 hadi 5,000 wakati bei halali ni Sh1,500 kwa nakala.

Kanisa Katoliki limekuwa likitoa nyaraka za aina hiyo kama mwongozo kuelekea Uchaguzi Mkuu kila wakati wa uchaguzi tangu mwaka 1995.

Afisa Habari wa Idara ya Mawasiliano Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Modest Katonto aliliambia gazeti hili jana kwamba, nakala moja ya waraka huo huuzwa kwa Sh 1,500.

Hata hivyo, alisema wenye mamlaka ya kuzungumzia zaidi Waraka na Ilani hiyo na mauzo yake ni Chama cha Wanataaluma Wakatoliki (CPT).

“Ukitaka kujua zaidi kuhusu bei na kiasi cha nakala zilizochapwa na kuuzwa nenda CPT watakuambia vizuri, TEC iliidhinisha tu kutolewa kwa vijitabu hivyo,” alisema Padri Katonto.

Naye msemaji wa CPT, Merry Mushi alilithibitishia Mwananchi kuwa hadi kufikia sasa (Julai) chama hicho kilichapisha na kusambaza nakala 10,000 za vijitabu hivyo.

“Hatujafika mbali kama watu wanavyodhani, mpaka sasa tumesambaza nakala 10,000 tu,” alisema Kessy.

Alifafanua kuwa kati ya idadi hiyo ya Waraka au mpango, zimesambazwa nakala 6,000 ambapo nakala 4,000 za Ilani pia zimesambazwa.

Aliongeza kuwa Februari mwaka huu CPT ilitoa nakala 1,000 za waraka kwa kila mwezi kati ya mwezi Februari na Juni, huku ikichapa idadi kama hiyo ya Ilani kati ya Aprili na Juni.

Alibainisha kuwa kuna ongezeko kubwa la watu wanaohitaji vijitabu hivyo na hivyo kuwafanya waongeze uchapaji kwa zaidi ya nusu tofauti na awali.

Kessy alifahamisha kwamba, kutokana na ongezeko hilo, mwezi Julai walilazimika kuchapa nakala 2,000 za Waraka pia 2,000 za Ilani.

“Kweli tunaona ongezeko la hitaji, hivyo Julai hii tumechapa nakala 2,000 kwa Ilani na 2,000 kwa mpango,” alisema Kessy.

Alisema watu wote wanaruhusiwa kununua vijitabu hivyo huku akionyesha kushangazwa na idadi kubwa ya wanunuzi wa vijitabu hivyo ambao siyo Wakatoliki.


My Take:
Yaani waraka wa Wakatoliki unauzwa na hawatu hawalilii uwe wa bure? tena wa Kanisa linalochangiwa na sadaka za waumini wake?
 
My Take:
Yaani waraka wa Wakatoliki unauzwa na hawatu hawalilii uwe wa bure? tena wa Kanisa linalochangiwa na sadaka za waumini wake?

Trying to link to the Meremeta complaints mzee?

Ninavyofahamu mimi waraka pamoja na ilani vinavyosemwa hapa vimeandaliwa na CPT (Tanzania Catholic Professionals) na kupitishwa na TEC (Baraza la maaskofu).

Katika kuuandaa waraka huo, CPT hawakupewa mgao wowote wa sadaka, zaka kutoka kanisani, waligharimia wao wenyewe kutoka kwenye vyanzo vya mapato yao kama chama. Mapato yao si lazima yachangiwe na waumini wote wa katoliki kama ilivyo sadaka au zaka...labda wakifanya hivyo watakuwa wamefanya kwa kujitolea tu kwa mapenzi yao!

Point nayotaka kuonyesha hapa ni kuwa gharama za kutengeneza waraka hazikuchangiwa kwa sadaka au zaka za waumini bali zilitolewa na chama chao wenyewe ambazo zinaweza tokana na miradi mbalimbali wanayoibuni!

Kama ilivyo kwa report ya meremeta ni vizuri watz tukajifunza kuappreciate efforts za wanajamii katika kuleta mageuzi ya kweli tanzania sio kwa maneno tuuuuu bali kwa kuchangia kidogo hasa pale tunapoweza kufanya hivyo! Tukichangia hizi nguvu tutakuwa well assimilated kny mchakato mzima wa mageuzi ambapo tukijafanikiwa tutakuwa na sababu ya kujisifia na kujipongeza kwa hata kidogo chetu tulichotoa!
 
Padri Privatus Karugendo

amka2.gif

JAMBO linaloshangaza katika ulimwengu wa leo ni kwamba mambo yote aliyoyafanya Yesu wa Nazareti yamewekwa pembeni.
Yale ambayo hakufanya yanatangulizwa na kutukuzwa kwa nguvu zote. Yesu wa Nazareti hakuandika waraka; yeye alifundisha, aliponya na kuyaishi maisha ya watu wanyonge. Alikuja duniani kutengeneza mifumo mizuri ya kuishi utu wema.
Yesu wa Nazareti, aliishi kwenye ulimwengu unaofanana na wa kwetu. Ulimwengu uliokuwa umezongwa na matatizo mengi yaliyokuwa yakihitaji suluhu ya haraka.
Ulimwengu uliohitaji mfumo mzuri wa kuyaendesha maisha ya binadamu. Ingawa kuna maoni tofauti ya kwa vipi, kwa nini na lini, Wayahudi wengi wanakubaliana kwamba Yesu wa Nazareti, alipoanzisha utume wake, ulimwengu wao ulikuwa na matatizo makubwa. Hivyo mtu huyu alitengeneza mfumo mzuri wa kupambana na matatizo hayo.
Kristo wa Nazareti hakuandika waraka, pamoja na ushahidi wa kutosha kwamba wakati wa maisha yake watu walikuwa wanafahamu kusoma na kuandika. Hata yeye Yesu wa Nazareti alijua kusoma na kuandika:
"Akasimama ili asome maandiko matakatifu kwa sauti. Akapokea kitabu cha Nabii Isaya, akakifungua na kupata mahali palipoandikwa hivi: "Roho wa Bwana yu pamoja nami, kwani ameniteua rasmi niwaletee maskini habari njema. Amenituma niwatangazie wafungwa kwamba watapa uhuru, vipofu watapata kuona tena; amenituma niwakomboe wanaoonewa na niutangaze mwaka ambao Mungu atawaokoa watu wake."
"Baada ya kusoma akafunga kile kitabu, akampa mtumishi, kisha akaketi; watu wote wakamkodolea macho." (Luka 4: 16-20).
Huu ni ushahidi wa kutosha kwamba Yesu wa Nazareti, alifahamu kusoma! Kama alisoma inawezekana pia alifahamu kuandika. Lakini pia kuna ushahidi kwamba kuna wakati aliandika:
"Lakini Yesu akainama chini, akaandika ardhini kwa kidole……Kisha akainama tena, akawa anaandika ardhini." (Yohana 8: 6-8).
Inaonyesha wazi kwamba Yesu wa Nazareti, alifahamu kuandika, lakini hakuandika waraka wowote. Waraka wake yalikuwa maisha yake. Yeye alipambana na mifumo mibaya katika jamii na kujitahidi kuisimika mifumo mizuri. Aliyaishi maisha na si kuandika juu ya maisha; aliziishi sheria na sikuandika juu ya sheria; aliuishi upendo na si kuandika juu ya upendo; aliishi haki, wema na huruma na si kuandika juu ya haki, wema na huruma.
Tunahitaji mifumo mizuri ya kujenga maadili mema katika jamii. Huwezi kuufundisha waraka hewani. Ni lazima pawepo mfumo mzuri wa kuwafundisha watu. Mfumo huu hatuna! Yesu alipambana na mifumo mibovu. Hivyo na maaskofu wetu wapambane na mifumo mibovu na kutengeneza mifumo mizuri ya kumwezesha mwanadamu kuishi maadili mema.
Tofauti na Yohana Mbatizaji, ambaye alifanya kazi ya kubatiza tu, Yesu alikwenda mbali na kuanzisha harakati za kuwakomboa watu kutokana na unyonge wao, kutokana na kunyanyaswa na kutokana na umaskini.
Alianzisha harakati za ukombozi wa nyakati zote, nyakati zilizopo na nyakati zijazo. Ni lazima tukumbuke kwamba utume wa Yesu, ulielekezwa kwa watu wanyonge, watu waliokuwa wamepoteza matumaini. Watu hawa waliishi kwenye jamii yenye matabaka. Yesu, aliwarudishia matumaini, aliyafanya maisha yao yawe na maana. Aliwaelekeza kujiamini na kupambana na maisha. Aliwaelekeza kushirikiana na kugawana kila walichokuwa nacho, ili kupambana na maisha yenye matabaka.
Kwa kuponyesha na kufanya miujiza, Yesu alianzisha safari ya ukombozi wa Mwanadamu.
Kitu cha pekee, kinyume na manabii waliotangulia na wale tulionao sasa hivi ni kwamba Yesu, aliponya na kufanya miujiza bure. Hakutoza fedha wala kusubiri shukrani. Alitumia kipaji chake bure! Wagonjwa walipona, mamia ya watu walikula na kunywa kwa miujiza ya Yesu, bila malipo yoyote yale.
Leo hii wale wenye kipaji cha kuponya wanaogelea kwenye utajiri wa kutisha. Wanatoza fedha, wanataka shukrani na sifa nyingi. Wanataka kuheshimiwa na kuabudiwa – wanafanya kinyume kabisa na Yesu wa Nazareti.
Yesu, hakufanya miujiza kujionyesha, bali alikuwa na lengo la kuwasaidia watu, kuwatoa watu katika mateso ya umaskini, kunyanyaswa na kupuuzwa. Aliponya kwa vile aliwahurumia watu. Alitanguliza huruma, badala ya kutanguliza umaarufu na kuheshimika, alitanguliza wema badala ya kutanguliza kutumia vipaji vyake kujitajirisha na kujineemesha!
Kitu kingine kinachomtofautisha Yesu wa Nazareti na manabii wengine na hata Yohana Mbatizaji, ni kwamba Yohana Mbatizaji aliwahubiria wakosaji, alitaka watubu na kumgeukia Mungu. Lakini Yesu alikwenda kuishi na omba omba, watoza ushuru na malaya. Mbali na kazi ya kuhubiri, aliishi na kushiriki maisha ya wafuasi wake.
Vitabu vidogo vinne tunavyoviita Injili, si wasifu wa Yesu na wala havikuandikwa kwa ajili hiyo. Na wala hatuwezi kusema kwamba vitabu hivi vinaelezea historia ya Yesu. Hata hivyo havikuandikwa kwa lengo hilo! Lengo la vitabu hivi lilikuwa kuonyesha jinsi Yesu, anavyoweza kuwa muhimu kwenye maisha ya watu waliokuwa wakiishi nje ya Palestina, vizazi zaidi ya viwili baada ya kifo chake.
Vizazi hivi havikuhitaji wasifu wa Yesu, bali mwongozo na mfumo wa maisha wa kuwawezesha kuishi nje ya Palestina. Muhimu ni matendo ya Yesu, matendo ambayo hapana shaka hayakufanana na ya mtu mwingine.
Hata sisi leo hii hatuhitaji wasifu wa Yesu, bali tunahitaji mwongozo wake na mfumo wa maisha wa kutuwezesha kupambana na matatizo ya ulimwengu wa leo.
Hivyo maaskofu wetu wasituandikie waraka: Watutengenezee mifumo ya kuishi utu wema; waishi maisha ya wanyonge na wanaoonewa.
Mamilioni ya watu kwa miaka mingi wamekuwa wakilitaja jina la Yesu na kumwabudu, lakini wachache kati ya mamilioni ndio waliomwelewa Kristu na namba chache kabisa ndiyo waliofuata kile alichokitaka kitendeke. Maneno ya Yesu Kristu, yamebadilishwa na kupindishwa ili yatekeleze kile watu wanachokitaka, na wakati mwingine maneno yake yamebadilishwa na kupindishwa yasimaanishe kitu chochote!
Jina la Yesu, limetumiwa kubariki maovu ya kila aina, kama wale waliokuwa wakiongoza vita na kuua watu huku wakitanguliza msalaba na Biblia. Latini Amerika, mamilioni ya watu walipoteza maisha yao na sehemu nyingine kizazi kilifutika kabisa katika harakati za kueneza neno na mafundisho ya Yesu Kristu.
Lakini pia jina la Yesu, limetumiwa kuwashawishi na kuwaletea imani kubwa wanaume na wanawake wengi hata kufikia hatua ya kupumbazika na kufanya matendo ya kijinga, kama kujinyima chakula na kuitesa miili yao kufikia kiwango cha uwendawazimu. Yesu amekuwa akitukuzwa na kuabudiwa kwa yale ambayo hakuyalenga, yale aliyoyapinga na kuyakemea kuliko yale aliyoyalenga, aliyoyahubiri, aliyoyatetea na kuyafia.
Jambo la kushangaza ni kwamba mambo ambayo Yesu aliyapinga wakati wa uhai wake, yalifufuliwa, yalihubiriwa na kusambazwa dunia nzima kwa jina lake. Tatizo kubwa linaloisumbua jamii yetu, ambalo ni lazima maaskofu walielewe vizuri ni kutokuwa na mfumo unaoeleweka wa kuishi Ukristu ,utu wema na maadili mazuri. Mbali na ufisadi, kuna matatizo mengine mengi kama ukimwi, maadili mabovu, nk. Bahati mbaya hadi leo hii hakuna kanisa lenye mfumo wa kuwajibishana, kushauriana, kuelekezana na kujuliana hali. Hakuna mfumo wa kuhojiana, kama ni fisadi Mkristu na tunasali naye tukafahamu fedha anazipata wapi. Ukosefu wa mfumo unalifanya kanisa liendelee kuwakumbatia mafisadi. Fedha za mafisadi zimejenga makanisa, zimenunua vifaa vya kanisani, zimewasomesha mapadri na wachungaji, zimenunua chakula cha mapadri na wachungaji. Hivyo jambo muhimu na la haraka ni mfumo, vinginevyo tutaendelea kulumbana juu ya waraka hadi kufikia kuvuruga amani ya taifa letu!
Source: Tanzania Daima
 
Privatus Karugendo bado anafikiri kizamani sana....maisha ya Yesu wa Nazareth hata yeye hawezi kuyaishi, na alishindwa kuyaishi....ni kweli Yesu hakuandika nyaraka...so what ? je hizo haya anazotaja angetoa wapi kama kina Luka , Mathayo , Marko na Yohana wasingeandika....
Waraka wa kikatoliki kuelekea uchaguzi mkuu unATOA MWELEKEO SAHIHI WA NAMNA TUPASAVYO KUTOA MCHANGO WETU KUPITIA SANDUKU LA KURA HUKU TUKIMNG'OA FISADI MMOJA MMOJA KUANZIA mONDULI HAKI tABORA, UZARAMO HADI KWAWAHAYA.
Karugendo mgogoro wako na kanisa usifikie mahali pa wewe kutoona zuri hata moja dhidi ya kanisa katoliki.....
juu ya Kuchezewa kwa Biblia Takatifu ,ulikua wapi miaka yote kutokuyasema haya mpaka pale walipokukimbiza kwenye Upadri baada ya kanisa kugundua kua huna wito wa kufanya kazi za utume.
Ila mchango wako wa mawazo na uheshimu ila sikubaliani na namna ulivyowasilisha.
 
Pd. Karugendo wacha pumba zako! Kwenye Biblia tunasoma kwamba Paulo, ambaye alikuwa Mtume wake Yesu aliandika Waraka kwa wafuasi wake Yesu, wakiwemo Wagalatia, Waefeso, nk. Kwa mantiki hii, ni sawa kabisa kwa Kanisa Katoliki kutoa Waraka kwa waumini wa dhehebu lao.
 
Privatus karugendo naona sasa anachanganyikiwa kwa waatu tulioanza kusoma maandishi yake miaka ya tisini hatumini ninini kinakuja, ila amepwaya sana, hana mashiko tena watoto wa mjini wanaita KUFULIA..... mtu wa Mungu Priva rudi kanisani kaombe radhi maana mambo yako hayako sawa sawa.
 
Huyu Pd. Karugendo kasahau kuwa hata Yesu hakuwa Mwandishi wa Habari wa magazetini. Badala ya kuhubiri Injili na kufanya kazi ya kuokoa roho za waumini, Padiri mzima kaishia kujitafutia umaarufu kwa kutembeza pumba za kisiasa kwenye kijarida. Padiri hoja huna kwa hili!
 
Mchungaji na mwanasiasa Mtikila amedandia waraka wa Kanisa na sasa anazunguka nchi nzima akipita kwenye makanisa akisambaza sumu yake akiwaasa wanakondoo wamkatae kumchagua mchungaji wao Raisi Kikwete kwenye uchaguzi ujao pia kakamata bango la sakata la ile taasisi ya kupanda na kuvuna pasipo kulima DECI akiwashawishi waandamane kudai fedha zao

Hii sumu anayoimwaga makanisani je atafanikiwa??

Mida kaenda jiji la Mwanza
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom