Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Mambo ndivyo yalivyo hasa pale unapogusa maslahi ya
mtu/kikundi fulani na ndicho kilichotokea kwa waraka
huu wa wakatoliki.Hii ina uafadhari kwa kuwa ni taasisi
iliyoamua kufanya hiovyo vinginevyo angekua mtu
binafsi yangetokea kama yaliyowapata watetezi wengi.
Ujumbe umefika kwa walengwa ambao wanataka kutufanya
watanzania tuendelee kuwa mbumbumbu ili hali 2kiendelea
kuibiwa.
Kingunge azidi kubanwa


na Hellen Ngoromera na Datus Bornface


amka2.gif

KAULI iliyotolewa bungeni hivi karibuni na mbunge wa kuteuliwa na rais, Kingunge Ngombale Mwiru, kwamba waraka wa Kanisa Katoliki, utaligawa taifa, jana iliendelea kukosolewa na kupingwa vikali na maaskofu wa kanisa hilo na la Kilutheri (KKKT).
Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania, Mhadhama Kardinali Polycap Pengo, akizungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Chuo cha Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam, alisema kama Kingunge hajui kusoma, ni vema akawauliza wanaojua, ili wamueleze hasa yale yaliyoandikwa katika waraka wa kanisa hilo.
Kauli hiyo ya Pengo dhidi ya mwanasiasa huyo mkongwe, ni mwendelezo wa majibu ya viongozi wa kanisa hilo, dhidi ya hatua ya mbunge huyo.
Aidha, Pengo alisema kuwa kanisa hilo halina mgombea na wala halitakipigia debe chama chochote cha siasa katika uchaguzi mkuu ujao, kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.
Alisema kuwa, anawashangaa baadhi ya watu wanaosema kwamba, kanisa hilo limeandaa waraka kwa wapiga kura ili kumpigia debe mgombea fulani au chama fulani.
“Kingunge kama hajui kusoma, basi awaambie wanaoujua wamueleze kilichoandikwa kwenye waraka wetu na sio kukurupuka kupinga kitu asichokijua vema. Narudia tena, kama Spika alivyosema, waraka uko sawa sawa kabisa.
“Sisi kama kanisa hatuungi mkono mgombea yeyote. Pia hutuungi mkono chama chochote na wala hatutakipigia debe chama chochote cha siasa katika uchaguzi ujao,” alisisitiza Pengo.
Naye, Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC), Mhashamu Askofu Juda Thaddaeus Ruwa’ichi, akizungumza na wanahabari mjini Dodoma, alisema wanaohoji waraka wa Kanisa Katoliki uliotolewa hivi karibuni wana uelewa finyu.
“Mkanganyiko wa mawazo na mawaidha yaliyotolewa na watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa unadokeza wazi kabisa kwamba wapo wanaoijadili ilani hiyo bila kujua kwanza yaliyomo ndani yake.
Hali hii inasababisha upotoshaji, kuwakanganya watu na hata kuzusha hisia za chuki katika jamii.
“Huu si uwajibikaji. Katika hili napenda kuwaasa Watanzania kuwa na tabia ya kuutafuta ukweli na kujenga hoja za msingi wa ukweli na uelewa sahihi,” alisema Ruwa'ichi ambaye pia ni Askofu wa Dodoma.
Alisema waraka huo ambao kwa maneno mengine unajulikana kama Upendo Katika Kweli, ni mhimili wa maendeleo ya kila mwanadamu na jamii.
Kwa mujibu wa Ruwa’ichi, mikataba kama ya rasilimali za madini lazima iangalie hali halisi badala ya kuigawa rasilimali hiyo bure na kukwamisha maendeleo ya taifa.
Alisema hati hiyo ambayo imejikita katika kutoa mafundisho juu ya masuala yanayohusu jamii, inaweka bayana kwamba ilani iliyotolewa na Kanisa Katoliki ni sehemu ya harakati zinazowataka watu wote kujenga uzalendo kwa njia ya elimu ya uraia, masuala ambayo ndiyo mhimili wa uwajibikaji.
Akiendelea kuutetea waraka wa kanisa hilo lenye wafuasi wengi hapa nchini, kiongozi huyo alibainisha kuwa, kanisa hilo lina nia njema ya kuwasaidia wananchi bila ubaguzi, kujizatiti kutambua na kushughulikia maslahi ya wote na pia kuhakikisha nchi na raia wake wanaishi kwa amani, haki, mshikamano, uwajibikaji na maendeleo endelevu.
Alisema viongozi waliochaguliwa na watu na kupewa dhamana, wana wajibu wa kutambua na kujali maslahi ya watu wote kwa kufanya juhudi za dhati na makusudi za kuvielewa na kuvishughulikia vipaumbele halali na sahihi vya wananchi, bila kujiruhusu kutumbukia katika mitego ya ubinafsi, ukabila, udini au ubaguzi wa aina yoyote.
Ruwa’ichi alisema shutuma zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa kuhusiana na hati hiyo iliyotolewa na Baba Mtakatifu Benedicto wa 16, Julai 7 mwaka huu, ni kielelezo cha wanasiasa hao kuwa na uelewa finyu kuhusiana na hati hiyo.
Alisema viongozi wa dini ni sehemu ya jamii na kwamba wao hawashughuliki na viumbe hewa, bali wananchi, hivyo ni lazima kuwapa mafundisho ambayo yanalenga katika kuwawezesha kufikia maendeleo ya kweli. Katika hatua nyingine, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Alex Malasusa, alisema kanisa hilo linaunga mkono waraka wa Kanisa Katoliki na kusema kuwa wanaoupinga ni mafisadi. Awali KKKT kupitia msemaji wake, ilisita kuuzungumzia waraka huo na kudai ingetoa msimamo wake baada ya kufanya vikao vya kuujadili.
 
Mbe!!!
kingunge bado ni kiongozi tu??? amezeeka yule nadhani mwakani atakuwa anatumia machela kuingia bungeni maana ni kwishney kila kitu amebakia kusema tu kwani hata kuwaza imekuwa ni adimu kwake.

Tumzomee ikibidi
 
Tatizo hamkuwaelewa BAKWATA ,maana wanasema ukitaka kumuuwa mbwa mpe jina zuri ,msemo kama huo sijui kama nimeupatia.

Halafu Waislamu wako open kabisa ,hilo mnatakiwa nalo mlielewe ,wako tofauti kabisa na viongozi wa KANISA ambao roho zao mbaya haziwezi kujificha ,huu waraka umepiga mbali sana ,na BAKWATA wameuelewa ,ila ukiujua ule mwenzio anaujua ule.

Halafu niliweka mada hapa ya vyombo hivi vya kidini ikaondolewa mbio mbio ,kuwa ni vyombo ambavyo viongozi wake wanatumiwa na Sultani CCM katika kuleta vurugu mechi ,Bakwata ni tawi la CCM kama yalivyo makanisa.
Huwezi kuwa fair na kumpenda mtu ambaye tayari umeshamtolea hukumu. Only truth will set us free na sio hisia zetu zinazoongozwa na matakwa yetu binafsi, ilhali hayako sawa.
 
LOL mnamchokoza Gametheory bureeeee! kwani hamjui Bakwata sio chombo cha waislamu bali ni chombo cha Serikali?!!!
 
Big up Bakwata! CPT sio (Catholic Episcope of Tanzania) bali ni Christian Professionals of TANZANIA kama alivyobainisha Nd Kazaimara
 
Mbona tayari tunalo, kwani JK anakaa wapi?, asiyemuislam kuingia IKULU tena msahau. 2015 mgombea wa CCM anatoka visiwani (Juma Shamhuna) ambako waislamu ni 99%, atakaa miaka 10 mpaka 2025, tunamuweka muislam tena kwani imeonesha wazi kuwa jengo lile likikaliwa na wasio lihusu linakuwa na mauzauza tu mara linakuwa ofisi ya ujasiriamali. Teh teh teh. Jengo lile linatakiwa kukaliwa na Khalifa (kiongozi). Si unamuona JK wetu anavyoongoza nchi sasa.

Wewe una uhuru zaidi wa hata kudai majengo ya shule zetu, wakati wa mjasiriamali thubutu!. Alikuwa anajua kuwa jengo lile si lenu, hivyo mkidai shule tu na yeye anatimuliwa kwenye jengo la waumini (muuminina). Hahahahahahaa, na ndiyo maana CCM wanaona ni bora kuanzisha mahakama ya kadhi kwa wenye jengo lao (IKULU). kwikwikwi! LOL!
sasa wewe rafiki,kama kikwete muislam akikaa ikulu akila kuku kwa mrija basi na wewe unakula kuku kwa mrija?wakati unakula dagaa wa mwanza kila siku hapo?hahahah, kama muislam mmoja yuko kwenye power, halafu wafanyakazi walio wengi wanakuwa wakristo, bado utasema uislam umeshika ikulu? ndo maana nasema mjitahidi kwenda shule, mtaweza kuwa na akili ya ku argue.

kwetu sisi wakristo, rais awe muislam au mkristo haijalishi,tunachotaka ni rais mwaminifu tu basi. angalia wewe bado una ukoko wa ugali wa juzi, ati kwasababu kikwete kakaa ikulu basi miaka yoote mtakuwa mnatawala nyie tu kule ikulu. halafu mfaidike nini? nendeni shule, angalia mlivyojaa huko uswahilini mnakaanga samaki wa kulumangia na kachumbari mchana kila siku. angalia watu wanaoishi uswahilini kuliko woote hapa bongo,ni waislam. kwenye slums ambazo hakika kuna nuka. hawasomi,vitoto vidogo tu wameshawaoza badala ya kupeleka shule. pole sana.

by the way, haujui kuwa sisi wakristo tusiofuga wala kutumia majini tunalo Jina la Yesu ambalo tukiomba tu, majini yote misikitini yanatetemeka, hivyo tunao uwezo kuomba hata uislam usiingie kule ikulu. hatujaamua tu. ni kwasababu sisi vita vyetu si vya damu na nyama,si vya kufundisha watu karate kwenye misikiti kama nyie,si vya kuhifadhi nondo na majambia kwenye misikiti kama ninyi. dini yetu na Mungu wetu ni tofauti na wenu. karibu kwenye ukristo uje uokoke.
 
Jumuiya ya Waislam nchini, Bakwata imeunga mkono waraka uliotolewa na kanisa Katoliki wa kutoa elimu ya uraia kwa wananchi.
 

Attachments

Good! Nawapenda sana hawa ndugu zetu! Huwa wanakuwa na jazba kali halafu wakielimishwa au wakipima upepo huwa wanaelewa. Pimeni basi na upepo wa mdudu kadhi na nyang'au oic muachane nao tafadhali!
 
Hii habari iliandikwa na Gazeti la Habari Leo. Lakini Gazeti hilo hilo likaandika tena kuwa lilifanya makosa kuandika hiyo habari. Soma chini,

Usahihi kuhusu Bakwata
Imeandikwa na mwadishi wetu; Tarehe: 24th July 2009
JANA gazeti hili katika ukurasa wake wa kwanza, liliandika habari iliyokuwa na kichwa kilichosema, 'Bakwata: Waraka wa Kanisa ni safi', ikikariri maelezo ya Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Shehe Suleiman Lolila.

Shehe Lolila Jumanne iliyopita aliwasilisha mada katika semina mkoani Lindi, kuhusu mashirika ya dini kutoa elimu ya uraia. Hata hivyo katika habari hiyo hakuna mahali Lolila anahusisha mada yake na Waraka huo wa Kanisa, ambao pia unatoa elimu ya uraia kuhusu uchaguzi.

Akifafanua hilo jana, Shehe Lolila alisema semina kama hizo zimekuwa zikitolewa nchini tangu mwaka jana kwa ufadhili wa Ubalozi wa Marekani nchini na wala hazina uhusiano wowote na Waraka wa Kanisa.

Kutokana na makosa yaliyofanyika ya kuhusisha semina hizo na Waraka huo, tunaiomba radhi Bakwata, Waislamu wote na Kaimu Katibu Mkuu Bakwata, Shehe Lolila kwa usumbufu wowote uliowapata. Mhariri.

Source: HabariLeo | Usahihi kuhusu Bakwata
 
Kadhi na Ilani ya CCM: Msekwa, Makamba waibuka Thursday, 23 July 2009 09:42 *Wasema CCM haijajenga msikiti wala kanisa
*Wabainisha kilichomo ndani ya andiko hilo
*Ngasongwa naye akana kuchomeka hoja hiyo

Na John Daniel, Dodoma


VIONGOZI wakuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wamepinga madai dhidi ya chama hicho kuvunja Katiba ya nchini kwa kuingiza suala la Mahakama ya Kadhi katika Ilani yake ya uchaguzi mwaka 2005 na kudai, wanaotafsiri hivyo, hawaielewi Ilani hiyo

Wakizungumza na gazeti hili jana kwa nyakati tofauti mjini hapa, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bw. Pius Msekwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Yusufu Makamba walipinga vikali jambo hilo na kulitolea ufafanuzi.


Bw. Makamba kwa upande wake, alisema CCM kama chama cha siasa kazi yake ni kusikiliza kelele za watu wanahitaji nini na kufanya kile kinachotakiwa na watu kama njia mojawapo ya kujijengea mazingira mazuri kisiasa.

Alisema haoni uvunjaji wowote wa Katiba kwani kuweka suala hilo ndani ya Ilani, ilikuwa muhimu kutokana na matakwa ya wananchi.

"Anayesema CCM ilivunja Katiba hakuelewa Ilani yetu, sisi kama chama cha siasa kazi
yetu ni kusikiliza kelele za watu, wanahitaji nini na kufanya kile wanachotaka.

"Ndio maana tulisikia watu wakitaka Mahakama ya Kadhi, waislam wanaamini Mahakama ya
Kadhi ni sehemu ya ibada, sasa ilibidi kama chama, tuchukue matakwa yao tulitafutie
ufumbuzi. Kutafutia ufumbuzi ni pamoja na kukataa au kulianzisha, yote mawili ni
kulitafutia ufumbuzi.

"CCM haijajenga msikiti wala Kanisa sasa anayesema tulivunja Katiba kwa vipi, hata
wewe mwandishi niambie ukitekeleza matakwa ya watu wako umevunja Katiba gani?

"Wanaodai hivyo hawajui,sasa kazi yetu ni kuchukua suala hilo na kuwapa Serikali
kwamba watu wanataka hiki na ndivyo tulivyofanya sisi, hatukuanzisha, sisi tumewapa Serikali, CCM haijaanzisha Mahakama ya kadhi, sisi tumeikabidhi Serikali mahitaji ya watu wake ili itekeleze, "alisema Bw. Makamba.

Alisema kitendo cha Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) kukubali kuunda Kamati
Maalum itakayosaidia na ile ya Serikali kuangali jinsi ya kuanzisha chombo hicho, ni
hatua kubwa kwao kama chama kwa kuwa tayari wametimiza wajibu wao wa kuimbia
Serikali kile kinachotakiwa na watu wake.

Alipoulizwa kama CCM itatoa kauli rasmi juu ya suala hilo, alisema; "Kauli yenyewe
ndiyo hii! Ninayokuambia, wewe ukiandika watu watasoma na hata huyo aliyesema
tumevunja Katiba atasoma! Nataka watu waelewe kwamba kutafutia jambo ufumbuzi si
kulianzisha tu hata kukataa ni kulitafutia ufumbuzi maana sasa watu wanajua
imefikia hapa,"alisema Bw. Makamba.

Alipoulizwa taarifa kwamba Mbunge wa Maswa Bw. John Shibuda (CCM) atachukuliwa hatua
ndani ya chama hicho ikiwa ni pamoja na kuonywa kwa kutoa maneno makali kutokana na
kuweka wazi kwamba chama hicho kilipotoka kuingiza suala hilo ndani ya
Ilani, alisema yeye hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa hayo ni maoni yake na aliyatoa kama Mbunge ambaye analindwa kisheria kutoa maoni yake.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Bw. Pius Msekwa alipoombwa kutoa maoni yake kuhusu suala hilo la CCM kuvunja Katiba kwa kuingiza ndani ya
Ilani ya CCM 2005, alisema anachojua ni kwamba chama hicho kiliahidi kulitafutia
ufumbuzi na kinachotakiwa ni watu kuelewa maana ya neno 'kulitafutia ufumbuzi' badala ya kuibua mambo mapya.

"Ebu ngoja niangalie Ilani yangu, au kama unacho soma hiyo sehemu, kilichotamkwa na
CCM ni 'kulitafutia ufumbuzi,'sasa kutafuta ufumbuzi juu ya suala lolote ni kutolea
uamuzi, sasa uamuzi unaweza kuwa tuanzishe au tusianzishe zote mbili ni kulipatia
ufumbuzi.

"Unajua hoja hiyo ilikuwa na swali kubwa kwamba tuanzishe au tusianzishe
sasa CCM iliposema tutalitafutia ufumbuzi maana yake ni kwamba tutoa jibu la
tuanzishe au la, hiyo ndiyo tafsiri sahihi ya kilichomo ndani ya Ilani.

"Sasa Serikali imeshatoa jibu kwamba haiwezi kulianzisha isipokuwa waislam wenyewe waanzishe, tayari hilo ni kulitafutia ufumbuzi, ujue suala hili lilianzishwa na Mhe. Mrema (Augustino Mwenyekiti wa TLP ), alisema CCM iliahidi Mahakama ya Kadhi sasa itekeleze, sasa watu walikuwa wanadai utekelezaji, ndio huo tayari umetekelezwa,"alisema Bw. Msekwa.

Kwa upande wake Mbunge wa Ulanga Magharibi Dkt. Juma Ngasongwa, amekanusha madai
kwamba ndiye aliyepenyeza kifungu hicho ndani ya Ilani alipoachiwa kama
mtaalam na kuifanyia mapitio ya mwisho.

Akizungumza na Majira nje ya ukumbi wa Bunge jana, Dkt. Ngasongwa alikiri kwamba yeye alikuwa mmoja katika Kamati ya chama iliyoandaa Ilani ya CCM na kwamba amekuwa
katika Kamati hiyo kwa vipindi vitatu mfululizo tangu mfumo wa vyama vingi ulipoanza nchini mwaka 1992 na mara zote amekuwa akiingia kwenye kamati hiyo
kama mtaalamu.

"Si kweli kwamba mimi ndiye niliingiza suala hilo ndani ya Ilani, wanaosema hivyo
watakuwa na chuki yao tu na mimi, nilirudi kuangalia kumbukumbu za nyuma suala la
Mahakama ya Kadhi liliwepo kwenye 'draft' (rasimu)

"Lakini suala hili si dogo maana linahusu karibu nusu ya Watanzania ambao ni waislam sasa ni lazima chama kishughulikie kwa kuwa hata wapinzani walianza kulizungumzia ilikuwa ni lazima CCM kulifanyia kazi,"alisema Dkt. Ngasongwa.


Alipoulizwa maoni yake kuhusu Ilani hiyo ya CCM kuvunja Katiba kwa kuingiza suala la Mahakama ya Kadhi na kuzuka malumbano, alisema suala hilo ni muhimu na kwamba chama hicho kilitimiza wajibu wake kwa kulichukua na kuikabidhi Serikali ili ilifanyie kazi na kwamba ni jinsi gani linafanyiwa kazi na Serikali, hilo halihusiani na chama tena.


Juzi chanzo chetu ndani ya Serikali na CCM kilidokeza kwamba, Dkt. Ngasongwa ndiye
alipenyeza suala hilo ndani ya Ilani na kwamba hata viongozi waandamizi wa chama
hicho walishtushwa walipoona kipengele hicho lakini hawakuwa na njia ya kuliondoa kutokana na muda na gharama za kurekebisha vitabu (Ilani).
 
Kingunge: Sigeuki waraka wa maaskofu Thursday, 23 July 2009 09:39 Na Reuben Kagaruki

MBUNGE wa Kuteuliwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Kingunge Ngombale Mwiru, ameendelea kushikilia msimamo wake wa kuamini kile alichokisema bungeni, kuhusu waraka uliotolewa na Kanisa Katoliki, kuwa unaweza kuhatarisha mshikamano na amani ya Taifa.

Akizungumza na gazeti hili, kwa njia ya simu, Dar es Salaam jana, Bw. Kingunge, alisema wanaotoa maoni yao kuhusu kile alichokisema, ni haki yao.

"Wanaosema ni haki yao, mimi siwezi kuwakataza. Maoni yangu nilishayatoa bungeni," alisisitiza Bw. Kingunge.

Alipoulizwa amepokeaje maoni yanayotolewa na watu mbalimbali wakiwemo maaskofu wa madhehebu mbalimbali, Bw. Kingunge alionekana kukwepa kujibu swali hilo.

Alipobanwa zaidi na gazeti hili kwa lengo la kutaka kujua kama ameridhishwa na majibu ya viongozi wa dini, hasa madai ya kumtuhumu kuwa hajasoma waraka huo alijibu;

"Wewe umeusoma? Waambie walioko huku (Dodoma) wakutafutie hansard uone nilisemaje," alisisitiza Bw. Kingunge na kisha kukata simu.

Akichangia mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Bw. Kingunge aliwajia juu maaskofu wa kanisa katoliki, na kuwataka kufuta waraka wao walioutoa unaolenga kuelimisha waumini wao, namna ya kuchagua viongozi bora. Bw. Kingunge alisema hatua hiyo inahatarisha mshikamano na amani ya Taifa.

"Nataka niseme jambo moja niseje nikatafsiriwa vibaya...kanisa katoliki wametoa waraka kwa ajili ya kuelekeza namna ya kupata viongozi wa kisiasa. Sasa tukifika huko KKKT (Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania) nao watataka, waanglikana bado, nao wakitoa, Wapentekoste nao watataka, Waislam bado."

"Viongozi wengi wa Katoliko nawaheshimu sana, wale wa juu nawafahamu, nawaheshimu sana, nawaomba sana warejeshe huo waraka wao, nchi hii tumeishi kwa umoja, mshikamano na udugu, hatutaki tufike kama Lebanon," alisema Bw. Kingunge.

Tangu atoe kauli hiyo Bungeni, Bw. Kingunge amepingwa na viongozi wengi wa kanisa, huku wengine wakidai alikuwa hajausoma.

Juzi, Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) Mhashamu Theddaeus Ruwaichi, alikaririwa akisema wanaojadili waraka wa kanisa lake bila kuusoma , ni masikini wa mawazo.

"Hali hii inasababisha upotoshaji , kukanyaga watu hata kuzusha hisia za chuki katika jamii," alisema alipozungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma
 
- Kingunge was wrong, kama viongozi wengi wa CCM on this ishu CCM walipaswa kuupokea waraka huu na kuufanyia kazi huku wakirekebisha sera zao ili somewhere zinakubaliane na baadhi ya mawazo ya huu waraka ambao hauna kosa lolote bali ni changamoto tu kwa CCM na sera zake kuelekea uchaguzi,

- CCM wamepoteza a golden political opportunity hapa kwa kujaribu kupingana na mawazo ya kanisa la Catholic, hatuna sheria inyaolikataza kanisa hilo kutoa mawazo yao kwa uongozi wa taifa, Tanzania bado tunaendelea kusumbiliwa sana na uongozi mbovu sana huko juu kumejaa viongozi ambao very quick to react negatively bila kusoma facts wala nyakati za kisiasa tulizonazo nationally! Ndio maana nimeamua politically ku-invest heavily kwa kiongozi mmoja ninayeamini kuwa ana nafasi kubwa sana ya kuwa rais 2015, na mwenye uwezo wa kuleta mabadiliko ya kweli.

Mungu Ibariki Tanzania.

Respect.

Kamanda FMEs!
 
Hata sijaelewa uoga wa CCM uko wapi na unatoka na kitu gani kwenye hii dokumenti ya wakatoliki.Wacha wasagwe wakiamka kuumbilia kama walivyo kimbilia mamnp ya OIC na Kazi Mkuu basi wajichanganye zaidi
 
Leon Bahati na Salim Said

VYAMA vya Siasa vya NCCR-Mageuzi na Chadema, vimesema waraka wa Kanisa Katoliki hauna matatizo na kwamba kama utasimamiwa, unaweza kuleta tija na maslahi kwa taifa.

Akitoa msimamo wa chama chake kuhusu mwongozo huo wa kanisa ambao katika siku za hivi karibuni, umeibua malumbano miongoni mwa wanasiasa, wasomi na viongozi wa madhehebu ya dini, Katibu Mkuu wa NCCR, Samuel Ruhuza, alisema chama chake kitaunga mkono waraka wowote, utakaotolewa na kikundi au madhehebu ya dini, ili mradi uwe umezingatia tija na maslahi kwa taifa. .

Hata hivyo chama hicho ambacho mwaka 1995, kilikuwa na nguvu kubwa kisiasa hapa nchini, kimesema kitapinga waraka wowote ambao utakuwa unapendelea mtu au kikundi fulani.

"Waraka au kauli ama msimamo wowote ambao una maslahi na nchi kwa jumla, NCCR wakati wowote itauunga mkono," alisema Ruhuza katika mahojiano na gazeti hili.

Ruhuza alisema kimsingi chama chake bado hakijaujadili mwongozo huo wa Kanisa Katoliki ambao unashauri wananchi kuwachagua watu safi, waadilifu na wacha Mungu.

Alipotakiwa kutoa msimamo wake, Ruhuza alisema ameusoma kwa makini na hajaona mahali popote ambapo Kanisa Katoliki, limekiuka maadili kiasi kwamba unaweza kuligawa taifa.

"Mimi kwa maoni yangu, sina matatizo na waraka huo wa Kanisa Katoliki kwa sababu haujaelekeza watu wamchague mtu fulani bali wamesema achaguliwe mwenye sifa hizi,"alisisitiza.

Alipoulizwa uwezekano wa mwongozo huo kusababisha taifa kusambaratika, Ruhuza alisemamara nyingi wanasiasa ndio wanaosababisha msambaratiko kwa kwa kuwapotosha wananchi, kwa maslahi binafsi.

Alisema wanasiasa wengi wana tabia ya kutahamaki na hata kueneza propaganda pale wanapoona kasoro zao zinawekwa wazi kiasi cha kutishia usalama wa maslahi yao.

Wakati huo huo, Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Victor Kimesera, alisema, waraka huo hauna tatizo kwa sababu unawataka Watanzania kuwa makini katika uchaguzi.

"Kwa maoni yangu waraka huo hauna tatizo, kwani kumtahadharisha mtu juu ya kitu fulani kuna udini au ukabila ndani yake," alihoji Kimesera.

Alisema, jambo la msingi ni kwa kila mtu kuusoma na kuuelewa waraka huo kabla ya kuanza kuujadili.


SOURCE: MWANANCHI.
 
Ndugu yangu Junius mimi naona hii ni kama misimamo yao binafsi. Hebu tusubiri tuone wakubwa kina Freeman na Mbatia wata react vipi kwa matamshi haya,si ajabu wakaitisha kamati kuu zao kuwajadili makatibu wao,ngoja tusubiri.
 
Hivi kwa nini Kardilnali Pengo asipewe kiti Bungeni, tumalize ubishi wote!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom