Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Habari Leo:

Bakwata: Waraka wa Kanisa ni safi

WAKATI kukiwa na mjadala kuhusu mashirika ya dini kutoa elimu ya uraia, Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Shehe Suleimani Lolila, amesema elimu hiyo ni haki ya jamii na kwamba itasaidia kupatikana viongozi bora.

Amesema mpaka sasa, Bakwata imeshatoa elimu hiyo katika wilaya zipatazo 16 katika mikoa ya Pwani, Iringa, Dodoma na sasa elimu hiyo itaanza kutolewa mkoani hapa. Shehe Lolila alisema hayo juzi wakati akizungumza na viongozi wa Bakwata kutoka Nachingwea, Liwale, Ruangwa, Lindi Mjini, Lindi Vijijini na Kilwa.

Awali Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Larry Andre, ambaye alikuwa katika mazungumzo hayo, alisema Marekani imetoa msaada wa Sh milioni 38, kuisaidia Bakwata kutoa elimu hiyo kwa jamii mwaka huu. Balozi Andre alisema fedha hizo zilitolewa na watu wa Marekani ili kudumisha demokrasia ya kweli ambayo italeta amani ndani na nje ya nchi.

Alisema elimu hiyo inahusisha zaidi kufahamu utawala bora, sheria, Katiba, uwajibikaji na haki ya jamii kusikilizwa na kumchagua kiongozi bora atakayeonekana anafaa. Aliongeza kuwa nchi nyingi zinakuwa katika uchaguzi baada ya muda kunatokea vurugu, hali inayosababishwa na uelewa mdogo wa elimu hiyo.

“Mimi nimekaa nchi nyingi za Afrika, utaona mwananchi anakwenda kupiga kura akiwa mnyonge na hana furaha yoyote ile kutokana kutokuwa huru. Hali hiyo inasababishwa na ufahamu mdogo wa elimu ya uraia,” alisema Balozi huyo.

Kwa upande wa Shehe Lolila, alisema ni haki ya jamii kuelewa elimu hiyo kwa kuwa itaisaidia kufahamu haki zake. Alisema uelewa wa elimu ya uraia pia husaidia jamii kufahamu jinsi ya kumchagua kiongozi mwenye sifa hata kwenye uchaguzi kama wa Bakwata, kuanzia ngazi za wilaya hadi taifa na kuondokana na migogoro ndani ya taasisi ya kidini.

“Kwa kweli mimi ninafahamu kuwa mtu akiwa na elimu ya uraia, atakuwa na uwezo mzuri wa kuchagua viongozi wenye sifa za kutosha na ataleta maendeleo,” alisema Lolila. Alisema migogoro mingi inaanzia ngazi ya chini kwa kuchaguliwa watu ambao hawana uwezo wa kuongoza na mtu ambaye hana uelewa nini maana ya kiongozi, hayo yote ni ukosefu wa elimu ya uraia.

Hivi karibuni, uliibuka mjadala juu ya Waraka uliotolewa na Kanisa Katoliki Tanzania, ujulikanao kama Mpango wa Kichungaji Kuhamasisha Jamii kuelekea Uchaguzi ulioandaliwa na Chama cha Wanataaluma wa Kikatoliki (CPA) .

Mwanasiasa mkongwe nchini na Mbunge wa Kuteuliwa, Kingunge Ngombale-Mwiru, hivi karibuni akizungumza bungeni, aliasa na kutaka Kanisa hilo liondoe waraka wake kwa kile alichosema unahatarisha mshikamano wa taifa.
 
Haya sasa..
Nani ni Nani na Wapi na Wapi!
Akina Game Theory na X-Paster mnasemaje hapo, maana nyie ndo vinara wa `game` la masuala ya Dini!
Actually watu wote waliotuliza vichwa wanausifu ule waraka.
Ukikurupuka kuusoma kama akina Kingunge, ule waraka unakuwa tishio kwako.
 
Huu waraka wanaona ni mzuri kwa sababu na wao wametoa elimu kama hiyo! It will take time to understand these guys, they are double minded!
 
Ila ni kweli wa tz hatuna elimu ya uraia na kujua haki zetu hatujui demokrasia......bila hiyo elimu hakutakuja kuwa na mapinduzi ya kifikra....tujitambue...makanisa na wengine jamani watusaidie watu wetu wa vijijini....sina shaka sana na mijini media zinasaidia sana pia.....
 
Kingunge anaogopa kashfa ya makusanyo stendi ya ubungo itafichuliwa ndio maana waraka kama huo anaona ni tishio kwake
 
wanatuchanganya na mambo ya dini ili waendelee kumalizia nchi, hawana lolote!!!
Aibu tu zenyewe hawana!!

haijalishi demokrasia au diktetaship, mradi kiongozi awe na ujasiri wa kutetea watu wake, na kusimamia haki. nchi itakwenda vizuri tu.
 
Unaposema Bakwata imekubali inabidi iwe ni tamko rasmi la sivyo ni maoni binafsi.

Naona Kichwa cha habari na habari havioani!! Ipange upya
 
Haya sasa wale waliokuwa wanapiga kelele wako wapi,haya mambo bwana hayahitaji pupa.Mtu anapaswa kwanza kuupitia waraka wenyewe tena akiwa ametulia ndipo aamue kutoa comments zake hapa jamvini.Wengi walikurupuka tuu na kuanza kutoa matamshi tena mengine ya kashfa bila kujua wanachokipingani nini.

Tusiwe na mitazamo hasi pale tuu taasisi fulani inapotoa waraka au maelekezo fulani,tuwe na tabia ya kupitia kwanza waraka hizo au maelekezo hayo kabla ya kutoa maoni.Ninajua ya kwamba katiba ya Tanzania anatoa uhuru wa mtu kutoa maoni,lakini uhuru huo hauruhusu mtoa maoni kutukana au kukashifu wenzake.

Nashukuru kuwa BAKWATA wameweka msimamo sawa sasa mambo ni kwa kwenda mbele kuwaelimisha wananchi juu ya elimu ya uraia mpaka vijijini ili wachague viongozi bora na sio bora viongozi.
 
Niliwahi kusikia watu na udini wao wanasema Marekani ni adui wa Waislam .Nikadhani waislam sasa hawatenda UK wala Ulaya nyingine maana ni jamii ya wa Wamarekani , kuangalia pale balozini majina ya waislam yanaongoza kutaka kwenda Ulaya na Marekani .Nikapita Ubalozi w Iran na Saudia nikakuta wamepoa hata hawana muuliza visa .

Tumeona maneno mengi toka kwa akina GT lakini ukimwamia ondoka London uwele Iran ama Saudia atakuua maana moto wake anaujua .Leo waraka unapigiwa kelele kumbwa wa US wamesha toa pesa kubwa kuhusiana na Elimu hii leo wakristo watu mnawaka .

Jifunzeni nyie wadini wa hapa na acheni Tanzania ipewe somo wachague viongozi wote mwisho wa siku sisi wote ni Watanzania .
 
Amesema mpaka sasa, Bakwata imeshatoa elimu hiyo katika wilaya zipatazo 16 katika mikoa ya Pwani, Iringa, Dodoma na sasa elimu hiyo itaanza kutolewa mkoani hapa. Shehe Lolila alisema hayo juzi wakati akizungumza na viongozi wa Bakwata kutoka Nachingwea, Liwale, Ruangwa, Lindi Mjini, Lindi Vijijini na Kilwa.

Awali Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Larry Andre, ambaye alikuwa katika mazungumzo hayo, alisema Marekani imetoa msaada wa Sh milioni 38, kuisaidia Bakwata kutoa elimu hiyo kwa jamii mwaka huu. Balozi Andre alisema fedha hizo zilitolewa na watu wa Marekani ili kudumisha demokrasia ya kweli ambayo italeta amani ndani na nje ya nchi.

Wala sijasoma habari yote.... Lakini Achana na Pesa bwana. Hela ni kila kitu. Inaweza pasua miamba, badilisha fikra, nk nk nk...

Kazi kweli kweli...
 
Waseme tofauti wakose mamilioni ya wamarekani.....

Wakosefu wawili wakikubaliana haina maana kuwa walichokubaliana ni sawa...

Tuache ushabiki. Unaweza ukadhani kuwa misimamo/mitazamo ya Uongozi wa Kanisa la Katoliki na sasa Uongozi wa Bakwata ambayo uhalali wake miongoni mwa waislamu ni sawa na uhalali wa Wanasiasa wetu mioyoni mwenu itasaidia kufanikisha matamanio yako ya muda mfupi ya kuona kuwa ama UFISADI ama CCM ama Kikwete wanashughulikiwa na wananchi, lakini ukweli unabaki palepale kuwa haya yanayofanyika sasa kwa jina la ukombozi, demokrasia, mapambano ya ufisadi yanastawisha MBEGU ZA CHUKI miongoni mwa jamii yetu ambayo tayari imethibitika kuwa HATUAMINIANI kati ratio ya 1:9

Kuvunja misingi ni mwanzo wa kuvunja jamii/taifa....

omarilyas
 
Niliwahi kusikia watu na udini wao wanasema Marekani ni adui wa Waislam .Nikadhani waislam sasa hawatenda UK wala Ulaya nyingine maana ni jamii ya wa Wamarekani , kuangalia pale balozini majina ya waislam yanaongoza kutaka kwenda Ulaya na Marekani .Nikapita Ubalozi w Iran na Saudia nikakuta wamepoa hata hawana muuliza visa .

Tumeona maneno mengi toka kwa akina GT lakini ukimwamia ondoka London uwele Iran ama Saudia atakuua maana moto wake anaujua .Leo waraka unapigiwa kelele kumbwa wa US wamesha toa pesa kubwa kuhusiana na Elimu hii leo wakristo watu mnawaka .

Jifunzeni nyie wadini wa hapa na acheni Tanzania ipewe somo wachague viongozi wote mwisho wa siku sisi wote ni Watanzania .

Mkuu
unadhani kuna mdini Tz, hao wote unaosikia humu ni waongeaji tu, kama kawaida ya wtz tulio wengi.Leo ukioa mkeo lazima wapo wataongea tu na kupinga maamuzi yako ya kuoa,ukijenga kijijini nyumba nzuri watakwambia hiyo nyumba kwanini hujajemga mijini na ukijenga mjini watakwambia ona huyu kwanini hajajenga kwao kijijini.

Ni kama tu kaugonjwa fulani tulikonako tunapenda kuongea hasa kwa mitizamo hasi kwa kila kitu.Sasa viongozi uchwara lakini walio very keen ktk kumanipulate hii tabia yetu ndio wanachezeshea hii shere ikitoka huu mdundiko wanatia ule maana wanajuwa lazima tuongee tu.

Kule kwetu tungesema kila ikitoka dogoli ya nansio yaingie dogoli nyingine ya ukala
 
Hakuna mtu mwenye akili timamu na nia njema na Tanzania atakayepinga huu waraka.
 
Mkuu
unadhani kuna mdini Tz, hao wote unaosikia humu ni waongeaji tu, kama kawaida ya wtz tulio wengi.Leo ukioa mkeo lazima wapo wataongea tu na kupinga maamuzi yako ya kuoa,ukijenga kijijini nyumba nzuri watakwambia hiyo nyumba kwanini hujajemga mijini na ukijenga mjini watakwambia ona huyu kwanini hajajenga kwao kijijini.
Ni kama tu kaugonjwa fulani tulikonako tunapenda kuongea hasa kwa mitizamo hasi kwa kila kitu.Sasa viongozi uchwara lakini walio very keen ktk kumanipulate hii tabia yetu ndio wanachezeshea hii shere ikitoka huu mdundiko wanatia ule maana wanajuwa lazima tuongee tu.

Kule kwetu tungesema kila ikitoka dogoli ya nansio yaingie dogoli nyingine ya ukala
=========
Kusikia BAKWATA wamepokea fedha ya Wamarekani kuendesha elimu ya uraia ni hatua kubwa sana. Haya ni matunda ya Waislamu wanaoona mbali kama Marehemu Shehe Gorogosi. Kama alivyosema mmoja wetu hapa, wale wanaowalaani Marekani ndiyo wanaopenda kwenda huko. Hatuwezi kuendelea kudanganywa nao, tumewabaini.
 
GOOD MUSLIM, BUD MUSLIM....Prof Mahmoud Mamdani

Omarilyas
 
Tatizo la nchi hii, hatutaki kuongozwa kwa uyakinifu, tunapenda kuongozwa kidhanifu. Viongozi wetu wa sasa wanalifahamu hilo, ndio maana inapotokea kundi au watu wenye uelewa kama CPT (Catholic Episcope of Tanzania) akatoa mwelekeo wanang'aka! Ukweli waraka ule ukiusoma kwa makini unawataka watawala kujitathmini "kimaadili" na kuwataka wafahamu kuwa wao sio waamuzi wa mstakabali wa nchi, bali wananchi wenyewe kupitia vyombo vyao kama katiba na bunge lao huru na si serikali.
 
Tatizo hamkuwaelewa BAKWATA ,maana wanasema ukitaka kumuuwa mbwa mpe jina zuri ,msemo kama huo sijui kama nimeupatia.

Halafu Waislamu wako open kabisa ,hilo mnatakiwa nalo mlielewe ,wako tofauti kabisa na viongozi wa KANISA ambao roho zao mbaya haziwezi kujificha ,huu waraka umepiga mbali sana ,na BAKWATA wameuelewa ,ila ukiujua ule mwenzio anaujua ule.

Halafu niliweka mada hapa ya vyombo hivi vya kidini ikaondolewa mbio mbio ,kuwa ni vyombo ambavyo viongozi wake wanatumiwa na Sultani CCM katika kuleta vurugu mechi ,Bakwata ni tawi la CCM kama yalivyo makanisa.
 
Niliwahi kusikia watu na udini wao wanasema Marekani ni adui wa Waislam .Nikadhani waislam sasa hawatenda UK wala Ulaya nyingine maana ni jamii ya wa Wamarekani , kuangalia pale balozini majina ya waislam yanaongoza kutaka kwenda Ulaya na Marekani .Nikapita Ubalozi w Iran na Saudia nikakuta wamepoa hata hawana muuliza visa .

Tumeona maneno mengi toka kwa akina GT lakini ukimwamia ondoka London uwele Iran ama Saudia atakuua maana moto wake anaujua .Leo waraka unapigiwa kelele kumbwa wa US wamesha toa pesa kubwa kuhusiana na Elimu hii leo wakristo watu mnawaka .

Jifunzeni nyie wadini wa hapa na acheni Tanzania ipewe somo wachague viongozi wote mwisho wa siku sisi wote ni Watanzania .

Nimeipenda hiyo sasa ni somo kubwa sana. Kinachonishangza sana ni njisi nchi za magharibi zinavyoacha misingi yao Cchritsian foundation) iliyowafanya wawe hivyo walivyo na kuanza kukaribisha wageni wanokwenda kutaka kuharibu hiyo misingi, hapo ndipo utakapoona ile speech ya PM wa australia ilikuwa imesimama sana.

Anyway watampokeaje beast wasipokaribisha hayo........ kweli mambo yote yatapita ila neno litasimama!
 
Hivi misingi ya nchi za magharibi ni ya kikiristo ?
Hivi hebu tueleze wawe hivyo kwani huko walikotokea walikuwa vipi ? Ndugu unasoma historia za ulaya au unakurupuka tu ? Tutolee mfano wa hizo nchi za Magharibi unazozijua wewe ambazo zilikuwa na zinafuata misingi ya kikirsto ?

Halafu hebu tutajie hiyo misingi unayoijua wewe ya kikiristo ,mpaka tuone kuwa wao walikuwa na misingi mizuri ,maana kila nikiangalia naona misingi yao ni toto likishafika miaka kumi na tano likajitafutie makazi yake ? Mtu kumuachia mkewe mtu mwengine ,wanawake kuvaa nguo fupi na zinazobana na mambo kibao tu ,sasa hiyo misingi sijui walianza kuifuata lini hata leo ikawa wamebadilika.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom