Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Leo nimeona na kumsikia mbunge mh Msambya anayetokea jimbo mojawapo huko Kigoma akitoa mchango wake kwa uchungu wakati wa kuchangia bajeti ya wizara ya sheria na katiba, kuwa kuna waraka ambao Kanisa limeusambaza kuhusu jinsi ambavyo waumini wanatakiwa kupiga kura, na eti wasichague wabunge ambao si wakristo. Akidai hii inaweza kuleta vurugu za kidini katika nchi yetu, huku akitolea mifano ya Nigeria n.k.

Pia ametaka kujua kuhusu hatima ya mahakama ya kadhi na OIC akitaka kujua kwa nini serikali haijapeleka sheria bungeni kuhusiana na mambo hayo.

Amelalamika kuwa anasikia kuna mpango wa sheria ya mahakama ya kadhi kuchanganywa na sheria zingine huku akikemea kuwa hivyo vitu ni kwa ajili ya waislamu na hakuna kupata maoni ya watu wengine wasio waislam.

Amesema hataunga mkono hoja kama hakupata ufafanuzi wa kuridhisha toka kwa waziri muhusika.

Swali ninalojiuliza je ni kweli kuna waraka wa aina hiyo? na kama upo mbona sikuona wanamtaka alete ushahidi? je kwa kutotaka alete ushahidi ni kweli serikali inakili kuwapo kwa waraka huo? Na kama upo basi mwenye kuwa nao naomba aulete hapa jf maana ni vema wote tuuone na kuujadili.

Naomba kuleta hoja.

Waraka wa Kanisa Katoliki uliopo unahusu Watanzania kutumia vizuri haki yao ya kupiga kura ili kuwachagua viongozi waleta maendeleo bila kujali dini ya mtu, kabila au chama. Waraka huo upendekeza baadhi ya vipa umbele ambavyo serikali ingefaa ivifanyie kazi - kuheshimu utu, haki za binadamu, mikakati ya kupunguza umaskini, kukuza uchumi, kuboresha huduma za jamii kama vile elimu, afya, ustawi wa jamii, nk.

Lakini waraka unaoongelewa na Mh Msambya siyo huo wa Kanisa Katoliki kwani wa Kanisa Katoliki hauna lengo lolote kutaka kuleta machafuko na udini nchini na pia kuwataka Wakatoliki wamchague kiongozi ambaye ni Mkatoliki tu kama anavyodai yeye.

Waraka wa aina hii sijawahi kuuona na sijui kama upo na nadhani ni wa kufikirika tu. Nina wasiwasi na tafsiri kama hizi za kupotosha mambo makusudi.

Kwa kweli mtu anayepinga waraka wa Kanisa Katoliki kwa jinsi jinsi ulivyo na malengo yake ana nia fulani ya kutaka kuingiza udini yeye mwenyewe. Mimi siamini kabisa kama Kanisa Katoliki halina haki ya kuwahamasisha waumini wake au Watanzania kwa ujumla kutumia vizuri kura yao kuliko kuwachagua viongozi wanaotuingiza kwenye ujinga, maradhi na umaskini.

Maana kama mtu anapinga waraka huo kuhusu namna ya kutumia uhuru wa kuchagua vizuri lazima pia apinge huduma au ushiriki wa Kanisa katika kuleta maendeleo ya nchi kwa ujumla - yaani utoaji elimu, huduma za afya na huduma nyingine za jamii.

Sijui wanaopinga wana nia gani hasa! Kuhusu Mahakama ya Kadhi hakuna Kanisa hata moja linalopinga Waislamu kuwa na hizo mahakama. Kinachopingwa ni kwamba ni kuzifanya mahakama hizo ziwe sehemu ya Katiba ya nchi wakati Katiba hiyohiyo inatoa uhuru wa kutosha wa kuabudu wa kila muumini wa dini yoyote ile ili mradi havunji sheria za nchi.

Sasa badala ya hao wanaopigia debe uanzishwaji wa Mahakama za Kadhi kama sehemu ya sheria mama wao kuonekana kama wanaleta udini, wanataka kujificha kwenye waraka ambao uko wazi kabisa na una lengo tu la kuwataka watu wote wawe waangalifu katika upigaji kura ili taratibu taratibu tuondokane na vitendo vya kununuliwa au kulaghaiwa kwa nia ya kuwachagua watu fulani wasio na uchungu na nchi yao kama baadhi ya viongozi walivyo.

Mimi ningetaka watu waseme kitu gani wanaona kilichosemwa kwenye waraka kina lengo la kuleta machafuko au udini kuliko kusema tu hata bila kujua waraka wenyewe unasema nini. Na wengi wa wanaolalamika ni wale ambao hawajausoma huo waraka au kama wameusoma wanaupindisha kwa sababu zao. Lakini hebu walete hoja hapa mstari kwa mstari au paragraph kwa paragraph na watuonyeshe jinsi usivyo waraka sahihi kwa maendeleo ya nchi.
 
nani aliyekurupuka? kama bado hujasoma hicho kitabu mbona unatoa hoja kuwa kinasema asipewe kura mgombea asiye Mkristo? picha iliyopo mbele ya gazeti la Raia Mwema haisemi hayo unayoyasema! Hiyo picha unaweza kuiona hata hapa: 100_1654.JPG (image)
.

Nziku,

Mi naona kuna lingine lakin sio hoja.

Nafikiri niliandika tokea awali kuwa mimi nimesoma habari hizo katika mada husika la Mchukia Fisadi

Swali ninalojiuliza je ni kweli kuna waraka wa aina hiyo? na kama upo mbona sikuona wanamtaka alete ushahidi? je kwa kutotaka alete ushahidi ni kweli serikali inakili kuwapo kwa waraka huo? Na kama upo basi mwenye kuwa nao naomba aulete hapa jf maana ni vema wote tuuone na kuujadili.
.

Nimesherehesha kwa kusema Yalioelezwa bungeni ni sawia na ndio maana hata wabunge hawakuomba MWONGOZO. kwani ndani ya bunge haipaswi kusema uongo.

Upande wangu nimekiagiza kitabu hicho nikisome kujiridhisha lakini sijakihukumu kijitabu hichi. Ebu nisome vizuri maandiko yangu
 
Nna mashaka sana na shule ya msambya...wadau tupeni data..na nadhan alishinda ubunge kidini kidini hivi..sasa anaongea utumbo mtupu..spika alitakiwa amfukuze huyu nje..sio kumtoa mtu ka zitto
 
Nziku,

Mi naona kuna lingine lakin sio hoja.

Nafikiri niliandika tokea awali kuwa mimi nimesoma habari hizo katika mada husika la Mchukia Fisadi

Dr. Barubaru, wala hakuna hoja nyingine. Naomba twende taratibu nadhani hukuelewa uzito wa ulichokiandika. Angalia hapa maneno ya mtoa hoja (rejea post ya kwanza

.... kuwa kuna waraka ambao Kanisa limeusambaza kuhusu jinsi ambavyo waumini wanatakiwa kupiga kura, na eti wasichague wabunge ambao si wakristo. ....

Majibu yako juu ya hiyo post ni haya

Hakika waraka huo upo. Ebu soma gazeti la Raia Mwema toleo la 088 la july1 - mpaka 7 utaona picha ya waraka huo.

sasa fikiria tena uzito wa maneno yako. Pole kama ulikosea and i beg your appology kama nimekuumiza kwa maneno yangu makali. Yote hayo yametokana na wewe kutoa uthibitisho wa jambo usilolijua, ndo maana unakana sasa.
 
Huyo Msambya ni kati ya Wabunge unaoweza kuwaita 'Makubwa Jinga'. Anapenda sana mambo ya udini. Nimemfuatilia kwa miaka mingi sana huyu, hana jipya. Mchango wake Bungeni kama sio kutetea mafisadi kama akina Manji, basi itakuwa ni kuhusu UDINI. Sasa watu wa aina hii itakuwa ajabu wakirudi tena Bungeni mwakani. BURE KABISA! Lazima awaombe radhi Maaskofu wa Kanisa Katoliki kwa upuuzi alioutamka Bungeni jana Jumanne.
 
Je unafahamu Vatican ina status ya nchi kama ilivyo Iran au Saudi Arabia? Na hao wenye jamuhuri za kiislamu balozi zao ni za nini TZ?

Ni kosa kubwa sana kuifananisha Iran au Saudia na Vatican. Hebu soma vizuri historia a Vatican . Mimi naweza kabisa kuifananisha VATICAN na MJI WA MAKKA. na kiongozi wa VATICAN PAPA kama Shekhe mkuu wa Msikiti mkuu wa Makka.
Lakin mind you Makka ipo ndani ya saudi arabiya kama ilivyo Vatican ipo ndani ya Italy.

Irani na Saudia na nyingine ningi kama Qatar, Yemen, Sudan Misri ni kama ilivyo Israel, marekani, UK, Sweden , France , Ital n.k. hizo ni nchi kamili.

Kisheria kuna mahusiano yanayoruhusiwa kwa nchi kuingia yaani ya nchi kwa nchi ndio hao wanaitwa mabalozi. Na vile vile kuna mahusiano ya miji kwa miji. kama unavyosikia Dar ina mahusiano na jiji la NY marekani n.k

Sasa kisheria nchi hairuhusiwi kuwa na mahusiano na miji , nchi inahusiana na nchi na sio majiji.

Sasa wacha nipate lunch ila pitia vizuri historia a vatican, ujue ina watu wangapi, atu hao wote wanafana kazi gani, jua eneo lao na hata viapo vyao nk.
 
Tatizo lako Dr. unatanguliza ushabiki badala la facts. Maneno yako yanakusaliti mwenyewe. Hivi kweli umesoma historia ya Vatican? unalinganisha hadhi ya utaifa kati ya Vatican na Makka? Mkuu give us a break. Unalinganisha mahusiano ya Dar na NY na mahusiano ya Vatican na wengine? LOL...

Mkuu soma hapa kidogo tu
Vatican City, officially the State of the Vatican City (Italian: Stato della Città del Vaticano), is a landlocked sovereign city-state whose territory consists of a walled enclave within the city of Rome, the capital city of Italy. At approximately 44 hectares (110 acres), and with a population of around 900, it is the smallest country in the world by both area and population.
The Vatican City is a city-state that came into existence in 1929 and is thus clearly distinct from the central authority of the Roman Catholic Church, known as the Holy See, which existed long before 1929. Ordinances of Vatican City are published in Italian; official documents of the Holy See are issued mainly in Latin. The two entities even have distinct passports: the state of Vatican City issues normal passports.
link: [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Vatican_City"]Vatican City - Wikipedia, the free encyclopedia[/ame]

Vatican ni sovereign city-state. Ina-issue passports. Sasa hiyo miji mingine unayosema ina-issue passport? ni sovereign states? Dr. vipi mkuu!
 
Nziku,Sasa usikurupuke kutoa hoja bila kufana tafiti. Sasa soma gazeti la leo la RAIA MWEMA utakiona kijitabu hicho picha yake ni kisha kitafute kwenye bookshop ( mimi nimemwagiza mtu aninunulie huko Dar kipo Cathedral bookshop pale opp forodhani sec ,posta.

Elewa kuwa ndio maana Hata spika hakuhitaji kuthibitisha kani kitabu bila shaka kitakua kimeeleza mengi.
'
Unaongea mambo ya kwenye kitabu kumbe hata hujakisoma? Hii ni ajabu sana. Soma kwanza mkuu ndiyo useme hayo unayotaka kuyasema
 
Watu wenye ufahamu lazima muelewe mahakama ya kadhi ni kwa ajili ya waislamu peke yao. Kwa nini kuanzishwa kwake kuwekwe kwenye katiba? Je mahakama hiyo ikianzishwa, mahakama hizo ni compulsory waislamu wote mashauri yao yasikilizwe na mahakama hizo? Je mahakama hizo zitasikiliza kesi za jinai zilizotendwa na waislamu?

Mimi kwa uelewa wangu mdogo nafikiri mahama za kadhi ni kwa ajili ya kusulukisha mashauri mbalimbali ya waislamu na hasa migogoro kati yao. Kama ni hivyo je kwa nini waislamu wasiwe na hizo mahakama bila kuwa na ulazima wa kuijumuisha katiba ya nchi? Iwepo kama NGO ambayo ina jukumu la kutatua migogoro ya waislamu. This is a secular state and all people regardless of their belief should be treated equally by the laws of the land.
 
Hakika waraka huo upo. Ebu soma gazeti la Raia Mwema toleo la 088 la july1 - mpaka 7 utaona picha ya waraka huo.

Labda kuna suala dogo napenda kuuliza. hivi kwanini Serikali ilipofuta misamaha a kodi kwa taasisi zote za kidini kwanini wakristu ndio waliolalama zaidi?

Nafikiri sasa Taifa linaelekea kubaya kwani wengi hawajui ruzuku Tuangalie kwene kijitabu cha bajeti ya 2007/2008 na 2008/2009 na pg 236 para iv ya bajeti 2009/2010 utaona ni nani kati ya waislamu na wakristu wanaochota ruzuku kubwa ( kwa hisabu zangu za kingumbaru aislamu wanachukua 7% tu ya pesa zote na zilizobaki zinakenda kanisani.

Sasa vp waislamu hawalalamiki kwa hilo? Nikiangalia hata kama serikali italipia fedha za ofisi a kadhi hawataeza kutumia zaidi ya 32% ya pesa wanazotumia aislamu katika ruzuku.

Inabidi watanzania wavumiliane na isiwe ile Kunya anye bata akinya kuku uchafu

Dr Hamza.
Mapumzikoni
Shanghani, Znz
Nafikiri kijita

Kwa hiyo ushahidi ni gazeti la RaiaMwema? Raiamwema ni gazeti la kanisa?

Halafu hiyo ruzuku unayoiongelea ni ruzuku gani?
 
Kwa hiyo ushahidi ni gazeti la RaiaMwema? Raiamwema ni gazeti la kanisa?

Halafu hiyo ruzuku unayoiongelea ni ruzuku gani?

Abu acha kupata shida ndugu yangu, hata hiyo Raia Mwema haijaandika hayo anayoyasema.
 
Abu acha kupata shida ndugu yangu, hata hiyo Raia Mwema haijaandika hayo anayoyasema.

Ahh ..kweli bana ngoja tumpumzishe ndg yetu..unajua hii mijadala inayohusisha dini watu wengi objectivity huwa wanaweka mfukoni..wanatanguliza jazba na hata mengine yasihusiana na mada yatachomekwa ili mradi busara isitawale..inabidi tuchukuliane ivoivo..
 
Kwa jinsi wakristo walivyokasirika kujadiliwa waraka na mapesa wanayopata kutoka serikalini naamini kwamba "kuna hidden agenda" kwenye waraka wao.
Kila anayewapinga hutukana ala! ukweli unauma eee

Wewe utakuwa unaota ndoto za mchana..serikali hiihii ya CCM itoe pesa kwa kanisa? lol..JF we cant have short of fun..!
 
naona huo waraka upelekwe misikitini ukajadiliwe kama kuna jambo lilo baya dhidi yao au mtu wao. kinachodaliwa ni ufisadi kwa maana ya kuchagua mtu asiyefaa kuwa kiongozi awe Nchimbi/Kapuya nakadhalika hata iwe Pinda ambye ni mkristo anaye waogesha mafisadi, maana walimtumia Kingunge sasa watu wameshtuka.
Labda mtu awe amepewa fedha mna mafisadi ndio atapotosha huu waraka wa Maaskofu/wakristo.
 
Wakati wakina Zitto wanazungumzia mambo ya maendeleo kwa nchi kiasi cha kupewa hata barabara za lami wakina Msambya wao wanaona mahakama ya Kadhi na OIC ndiyo maendeleo ya jimbo na taifa.

Huu ujinga utakwisha lini vichwani mwa watu hawa?

Nilisikia akisema Profesor Haroub (Marehemu) alikuwa mwalimu wake. Kumbe na yeye Msambya ni msomi? Lakini pamoja na elimu yake badala ya kutafuta maendeleo anatafuta mahakama ya kadhi? Ama kweli watu aina ya Msambya hata shule hawana sababu, si ajabu alikuwa ni zero tu hata huko university.
Kinachomtia wasiwasi Mh. Mbunge(hata na mm) ni kuwa waraka huo unawataka wakiristo wasiwachague viongozi wasiokuwa wakiristo, hili ww huoni kuwa ni tatizo kama ni kweli?
Na suala la mahakama ya kadhi na OIC, Mh. Msambya ana haki ya kuliulizia kwa kuwa chama chake kimetoa ahadi ya kulitekeleza katika ilani yake ya
uchaguzi,na pengine yy Mh. Msambya yupo hapo bungeni kwa kura za waislamu zilizotokana na ahadi hiyo, kitendo cha serikali ya CCM kupiga danadana masuala hayo ni kuonyesha kuwa CCM ni waongo, wasiotekeleza ahadi na wanatumia hadaa na ujanja kupata kura za wananchi.Mh. Msambya has a point on the topic.
 
Kinachomtia wasiwasi Mh. Mbunge(hata na mm) ni kuwa waraka huo unawataka wakiristo wasiwachague viongozi wasiokuwa wakiristo, hili ww huoni kuwa ni tatizo kama ni kweli?

Mkuu Junius onyesha umakini kidogo bro. wakati unasema waraka unasema kwa uhakika kama vile umeuona waraka wenyewe bado mwishoni unamalizia kwa kuuliza swali. Hii inashangaza, hivi jamani huoni kama madai hayo ni makubwa sana? Waraka huo unauzwa upo public mtu yeyote anaruhusiwa kuumiliki. So, just for common sense huoni kama hilo haliwezekani? kweli Watanzania tunamatatizo makubwa.

Waraka unasisitiza kuchagua viongozi pasipo ubaguzi. Zaidi ya hilo waraka unatoa rai ya kubadili kaatiba ili kuangalia ukubwa wa majukumu ya Rais na kuhusu wagombea binafsi.

Naomba mwenye huu waraka uturushie (soft copy).
https://www.jamiiforums.com/members/junius.html
 
Ni kosa kubwa sana kuifananisha Iran au Saudia na Vatican. Hebu soma vizuri historia a Vatican . Mimi naweza kabisa kuifananisha VATICAN na MJI WA MAKKA. na kiongozi wa VATICAN PAPA kama Shekhe mkuu wa Msikiti mkuu wa Makka.
Lakin mind you Makka ipo ndani ya saudi arabiya kama ilivyo Vatican ipo ndani ya Italy.

Irani na Saudia na nyingine ningi kama Qatar, Yemen, Sudan Misri ni kama ilivyo Israel, marekani, UK, Sweden , France , Ital n.k. hizo ni nchi kamili.

Kisheria kuna mahusiano yanayoruhusiwa kwa nchi kuingia yaani ya nchi kwa nchi ndio hao wanaitwa mabalozi. Na vile vile kuna mahusiano ya miji kwa miji. kama unavyosikia Dar ina mahusiano na jiji la NY marekani n.k

Sasa kisheria nchi hairuhusiwi kuwa na mahusiano na miji , nchi inahusiana na nchi na sio majiji.

Sasa wacha nipate lunch ila pitia vizuri historia a vatican, ujue ina watu wangapi, atu hao wote wanafana kazi gani, jua eneo lao na hata viapo vyao nk.

Kwani Vatican imezuia Makka kuwa na balozi Tanzania? Kama shida ni hiyo kwa nini asiwepo balozi kwa kuwakilisha Makka Tanzania?
 
Kinachomtia wasiwasi Mh. Mbunge(hata na mm) ni kuwa waraka huo unawataka wakiristo wasiwachague viongozi wasiokuwa wakiristo, hili ww huoni kuwa ni tatizo kama ni kweli?
Na suala la mahakama ya kadhi na OIC, Mh. Msambya ana haki ya kuliulizia kwa kuwa chama chake kimetoa ahadi ya kulitekeleza katika ilani yake ya
uchaguzi,na pengine yy Mh. Msambya yupo hapo bungeni kwa kura za waislamu zilizotokana na ahadi hiyo, kitendo cha serikali ya CCM kupiga danadana masuala hayo ni kuonyesha kuwa CCM ni waongo, wasiotekeleza ahadi na wanatumia hadaa na ujanja kupata kura za wananchi.Mh. Msambya has a point on the topic.
Unaweza kutuletea huo waraka tusome hapo palipo andikwa kwamba wakristo wasi wa chague waislamu? au ndio pesa za mafisa zinafnya kazi?
 
Kinachomtia wasiwasi Mh. Mbunge(hata na mm) ni kuwa waraka huo unawataka wakiristo wasiwachague viongozi wasiokuwa wakiristo, hili ww huoni kuwa ni tatizo kama ni kweli?
Na suala la mahakama ya kadhi na OIC, Mh. Msambya ana haki ya kuliulizia kwa kuwa chama chake kimetoa ahadi ya kulitekeleza katika ilani yake ya
uchaguzi,na pengine yy Mh. Msambya yupo hapo bungeni kwa kura za waislamu zilizotokana na ahadi hiyo, kitendo cha serikali ya CCM kupiga danadana masuala hayo ni kuonyesha kuwa CCM ni waongo, wasiotekeleza ahadi na wanatumia hadaa na ujanja kupata kura za wananchi.Mh. Msambya has a point on the topic.
weka ushaida tofauti ya hapo ni uchchoze wa kidini ambao maafa yake yaangalie ya kenya ingawa yao yalikuwa ya kikabila
 
Leo nimeona na kumsikia mbunge mh Msambya anayetokea jimbo mojawapo huko Kigoma akitoa mchango wake kwa uchungu wakati wa kuchangia bajeti ya wizara ya sheria na katiba, kuwa kuna waraka ambao Kanisa limeusambaza kuhusu jinsi ambavyo waumini wanatakiwa kupiga kura, na eti wasichague wabunge ambao si wakristo. Akidai hii inaweza kuleta vurugu za kidini katika nchi yetu, huku akitolea mifano ya Nigeria n.k.

Pia ametaka kujua kuhusu hatima ya mahakama ya kadhi na OIC akitaka kujua kwa nini serikali haijapeleka sheria bungeni kuhusiana na mambo hayo.

Amelalamika kuwa anasikia kuna mpango wa sheria ya mahakama ya kadhi kuchanganywa na sheria zingine huku akikemea kuwa hivyo vitu ni kwa ajili ya waislamu na hakuna kupata maoni ya watu wengine wasio waislam.

Amesema hataunga mkono hoja kama hakupata

Wakereketwa mko wapi ?sasa kama ni hivyo wale CCM zanzibar itabidi wapangiwe siku ya KUBABATIZWA kabla ya uchaguzi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom