Kumbe ni yule aliye kwenda Star tv akiwa uchi?Mgogoro wa wanafunzi UDOM na ule wa wahadhiri wao unabeba sura ya kisiasa tena siasa za kuangamiza taifa letu, Nasema haya nikisikitika kwa kinachoendelea katika uwanja wa siasa leo,
Hawa wanafunzi waliofukuzwa UDOM walichaguliwa baada ya kufaulu vizuri(alama A na B) masomo ya sayansi kidato cha nne kutokana agizo la serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete la kuitaka wizara ifanye njia za makusudi kupunguza tatizo la walimu wa sayansi katika shule za sekondari kidato cha 1-4.
Ilianzishwa mpango maalumu (Diploma Special Program) iliyozinduliwa na Rais kwa pesa zilizoombwa bungeni kisheria (bunge liliridhia) kuwasomesha vijana hao kwa gharama za serikali ili wakafundishe O-level katika shule za serikali kisha baadaye wakasome degree. Kazi ya kuwadahili vijana hawa ilifanywa na serikali yenyewe kupitia TCU.
Leo serikali ya chama kilekile na bunge lake lilelile wamekuja na waziri wa chama kilekile wanashindwa kuwalipa malipo wakufunzi wa wanafunzi hao na kupelekea mgomo wa wahariri, hawaishi hapo wanakwenda chuoni na kuwafukuza wanafunzi hao wasio na hatia, wanataka dunia iamini kuwa serikali iliyopita ni nyingine kabisa na haina mazuri iliyoyafanya na ilikua inaongozwa wajinga! Katika bunge lilelile na spika wa chama kilekile wanazuia hoja binafsi ya Mbunge wa upinzani anayetaka bunge lijadili mgogoro huu na kunusuru hatari inayowakumba watoto wetu hapo UDOM, na zaidi mbunge huyo ananyanyuliwa mzobemzobe na polisi na kutupwa nje ya lango la Bunge
Leo ni vijana hao hao kama wangeamua kwenda kidato cha tano wangemaliza form six mwaka jana lakini walijitolea na pamoja na kufaulu kwa division one na two zao kusaidia taifa. Leo wanafukuzwa kwa mabomu na mbwa wa polisi.
Unapowaondoa wanafunzi 7,802 ndani ya saa 24 sijui hii serikali ya CCM inawaza nini....
Ili waondoke wote hapo yanahitajika mabasi zaidi ya 150 ambayo ni karibu nusu ya mabasi yote yanayoondoka Ubungo kwa siku 1 kwenda nchi nzima, Haujafikiria watalala wapi...watakula wapi...
Na: Yericko Nyerere
Inasikitisha sana!Wadogo zangu mlioondoshwa UDOM kwa saa 24 poleni sana, mlienda kusomea ualim ili mje kufundisha au kuwa walim,ila ndoto zenu zimezimwa kama kibatari kwenye upepo mkali. Lakini huenda mmeepushwa na kadhia kubwa huko kwenye ajira,as long mlifaulu basi angalieni utaratibu mwingine wa kwenda kujiendeleza aidha advance level au kwenye vyuo vingine na si lazima msomee ualim hasa ualim huu unaolalamikiwa hapa nchini.
Pamoja na changamoto hii,napenda kuwaeleza hii si mara ya kwanza kwa vijana kutimuliwa vyuoni ndani ya saa 24, jana nilidokeza hapa kuwa wahanga wa hii issue ni wasichana, na madhara yanaweza yasionekane jana,leo au kesho ila kwa kadhia hii kuna mabinti watapata virus tu (HILI LITATOKEA).HAPA Wanafunzi wa Stashahda ya ualimu masomo ya Sayansi, Hesabu na Teknolojia UDOM warudishwa nyumbani
Poleni sana vijana,nenden mkahangaikie mipango yenu huko mbele ya safari mtazipata hizo degree
Kama wana kaidi amri ya spika hakuna namna wacha wafukuzwe..ili siku nyingine wajifunze adabu!Wabunge wote wa upinzani wameamuriwa kutoka nje ya Bunge kwasababu za kuhoji suala la wanafunzi wa UDOM kufukuzwa chuoni kinyama.
Kaandika Zitto kwenye ukurasa wake wa facebook.
.....seems ni mgonjwa....na sasa wabunge wote wanapata joto ya jiwe kwa kuchagua naibu spika kiitikadi na si kiutendaji...na wasubiri Ndalichako atakapoanza kuwachuguza vyeti vyao ndio watajua mbivu.....Hivi huyo spika wa bunge anakuwa na kazi gani kiasi kwamba anamwachia kiti naibu spika kila siku na matokeo yake bunge linaendeshwa kama kambi ya mafunzo ya umoja wa vijana wa ccm?
Kwa nini usioji?Acha fikira potofuhutakiwi kuoji maamuzi yalitoka juu hii mi sirikali ya magufuli ,hii ni awamu ya 5 ya hapa kazi tu
Daaah!! Sidhani kama una familia yoyote wala sidhani kama utawahi kuwa na familia yoyote hapa dunianiWafukuzwe tu maana hamna namna nyingine sasa.
Kazi yao imekuwa kudandia dandia tu hoja.
Hivyo kabisa
Hapo ndio napata maana ya ule wimbo wa john komba wa wataisoma namba, likija suala la vyeti feki hapo ndio wabunge wa ccm watajuta na kujikuta wanayaachia majimbo yao.....seems ni mgonjwa....na sasa wabunge wote wanapata joto ya jiwe kwa kuchagua naibu spika kiitikadi na si kiutendaji...na wasubiri Ndalichako atakapoanza kuwachuguza vyeti vyao ndio watajua mbivu.....
Hivi hao wanafunzi 7000 waliokatizwa ndoto zao kimaisha kwa ukatili hakuna watoto wa wanyonge? Au mnyonge ni yupi?Ndugu yangu, public policy hitekelezwi kwa kumwangalia mtu mmoja mmoja. hayo yalikuwa mambo ya Kikwete. ni marekebisho yanafanyika kwenye public policy, wengine wataumi ila mwishowe wanyonge wote watanufaika.
Cc😛hilipo BukililoKwa staili hii hili li nchi litakuwa masikini miaka 10000
Serikali ya kilevi imechukua hatua gani?Hivi mnataka kujadili nini hasa wakati hatua zimeishachukuliwa na serikali? ukawa tulieni bungeni mjadili bajeti ya taifa, acheni kurukia rukia mada na kuleta siasa kwa kila jambo
Uzuri wa wabunge wote wa ukawa wanajitambua, siyo wabunge wa ndiyooooooooo wa ccmHivi mnataka kujadili nini hasa wakati hatua zimeishachukuliwa na serikali? ukawa tulieni bungeni mjadili bajeti ya taifa, acheni kurukia rukia mada na kuleta siasa kwa kila jambo
Serkali ya kidhalimu na kifashist, imefanikiwa kulimiliki bunge na juling'oa meno yotehutakiwi kuoji maamuzi yalitoka juu hii mi sirikali ya magufuli ,hii ni awamu ya 5 ya hapa kazi tu
Endelea kutujuza uwezo wako wa kufikiriKumbe ni yule aliye kwenda Star tv akiwa uchi?
Uchumi wakati mtaendelea kuusoma kwenye magazeti ya uhuru na mzalendo tuKwa hivi vituko mgazete hayalali na njaa. Sasa cjui kama ndizo habari zitakazotufikisha kwenye uchumi wa kati