Wapinzani watimuliwa tena Bunge la jioni

Wapinzani watimuliwa tena Bunge la jioni

Huu ni uthibitisho wa kutosha ile kauli ya Magufuli kwamba kautoa mwili wake kama sadaka kwa wanyonge ni unafiki wa hali ya juu. Hawa Wanafunzi ni baadhi ya wanyonge nchini na Magufuli yuko ndani ya Ikulu kimyaaa huku hawa Wanafunzi wakiendelea kuteseka kutokana na maamuzi ya hii Serikali dhalimu na Jipu naibu spika.
Mkuu BAK, hivi hakuna uwezekano wa rais akatengua nafasi ya naibu spika? Maana kwa hali inavyojionyesha ni kuwa tunaelekea kwenye kutumbukia kwenye ziwa rukwa ziwa linalo ongoza kwa kuwa na mamba wengi tena wenye njaa kali
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Unaelimu gani? Je hoja ya wanafunzi wewe hauoni kua in hoja?
Godfrey-K, kuna watu wa kupuuzwa humu jamnvini. Huyu Mwasita ni mmoja wao.

Mtu ambaye antoa hoja za maudhi katika kipindi ambacho vijana zaidi ya 7000 wanasimamishwa masomo bila sababu za msingi ni wa kupuuzwa na kuhurumiwa. Kwa bahati mbaya hata wengi wa wawakilishi wetu ni kama huyu kihio. Msamehe bure.
 
Hakika nimeamini vijana wa kitanzania hatujitambui tunashindwa kweli kutofautisha siasa na jambo la muhimu kama hili!. Tunashindwa kuonyesha uchungu kabisa kwa wadogo zetu.
 
Mkuu BAK, hivi hakuna uwezekano wa rais akatengua nafasi ya naibu spika? Maana kwa hali inavyojionyesha ni kuwa tunaelekea kwenye kutumbukia kwenye ziwa rukwa ziwa linalo ongoza kwa kuwa na mamba wengi tena wenye njaa kali
Mkuu unataka kusema hujui huyo mama yupo nyuma ya nani?
 
Mkuu huyu jamaa hawezi kufanya hivyo kwa sababu alimteua huyu bila ya kuwa mwanachama wa CCM hivyo anataka kuonyesha kwamba hakukosea kumteua huyu na si ajabu alimpa maelekezo kwamba mijadala yote ya kuisema vibaya Serikali aipige vita na hivyo kutoiruhusu. Nadhani katiba inampa uwezo rais wa kutengua uteuzi wa huyu lakini huyu jamaa alivyo mbishi na kutaka kuonyesha kwamba hakukosea hawezi kumtosa. Na huyu naibu mbona ana kaimu sana nafasi hiyo kila mara? Spika wa bunge yuko wapi? Nakumbuka miaka ya nyuma ilikuwa ni nadra sana kumsikia naibu spika wa Bunge.

Huo ndio ukweli kabisa mkuu maana kila siku utaona ni naibu spika tu, au ndio anaandaliwa kumdrop yule mzee wa kutembeza bakola kwenye mikutano ya ndani ya chama?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
mtu yeyote aliye soma elimu ya chuo kikuu hawezi jadili upuuzi kwenye thread kama hii inayogusa maisha ya watoto wa ndugu zako, nakumbuka siku tumefukuzwa chuo, kwanza mtandao wa simu ulikuwa haupatikani ulikuwa more than busy, usafiri wa kututoa chuo kwenda mjini ulikuwa ni shida, chakula ilikuwa ni shida malazi ilikuwa ni shida, MPESA vibanda vyote ilikuwa ni taabu, Tigo pesa ndio usiseme, nyumba za kulala wageni ilikuwa shida asikwambie mtu mateso yake
 
Hivi huyo spika wa bunge anakuwa na kazi gani kiasi kwamba anamwachia kiti naibu spika kila siku na matokeo yake bunge linaendeshwa kama kambi ya mafunzo ya umoja wa vijana wa ccm?
Afya mkuu!!! Maradhi yanasababisha uhitaji wa kupumzika muda wa kutosha.
 
Wabunge wa ccm hamnazo kabisa!naibu spika katili kama nini,watz,media zote kukemea haya.
 
Hapa ndiyo utaona unafiki wa Wabunge wa CCM, asubuhi baadhi ya Wabunge wa CCM waliamua kutoka bungeni ili kuwaunga mkono Wabunge wenzao wa upinzani, jioni hii baada ya kutishwa na ngazi za juu za chama chao wamekula ngumu bungeni utadhani si wao ambao asubuhi ya leo waliona umuhimu mkubwa wa mjadala kuhusu kufukuzwa Wanafunzi 7,802 UDOM.
 
Back
Top Bottom