Wapinzani watimuliwa tena Bunge la jioni

Wapinzani watimuliwa tena Bunge la jioni

Mgogoro wa wanafunzi UDOM na ule wa wahadhiri wao unabeba sura ya kisiasa tena siasa za kuangamiza taifa letu, Nasema haya nikisikitika kwa kinachoendelea katika uwanja wa siasa leo,

Hawa wanafunzi waliofukuzwa UDOM walichaguliwa baada ya kufaulu vizuri(alama A na B) masomo ya sayansi kidato cha nne kutokana agizo la serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete la kuitaka wizara ifanye njia za makusudi kupunguza tatizo la walimu wa sayansi katika shule za sekondari kidato cha 1-4.

Ilianzishwa mpango maalumu (Diploma Special Program) iliyozinduliwa na Rais kwa pesa zilizoombwa bungeni kisheria (bunge liliridhia) kuwasomesha vijana hao kwa gharama za serikali ili wakafundishe O-level katika shule za serikali kisha baadaye wakasome degree. Kazi ya kuwadahili vijana hawa ilifanywa na serikali yenyewe kupitia TCU.

Leo serikali ya chama kilekile na bunge lake lilelile wamekuja na waziri wa chama kilekile wanashindwa kuwalipa malipo wakufunzi wa wanafunzi hao na kupelekea mgomo wa wahariri, hawaishi hapo wanakwenda chuoni na kuwafukuza wanafunzi hao wasio na hatia, wanataka dunia iamini kuwa serikali iliyopita ni nyingine kabisa na haina mazuri iliyoyafanya na ilikua inaongozwa wajinga! Katika bunge lilelile na spika wa chama kilekile wanazuia hoja binafsi ya Mbunge wa upinzani anayetaka bunge lijadili mgogoro huu na kunusuru hatari inayowakumba watoto wetu hapo UDOM, na zaidi mbunge huyo ananyanyuliwa mzobemzobe na polisi na kutupwa nje ya lango la Bunge

Leo ni vijana hao hao kama wangeamua kwenda kidato cha tano wangemaliza form six mwaka jana lakini walijitolea na pamoja na kufaulu kwa division one na two zao kusaidia taifa. Leo wanafukuzwa kwa mabomu na mbwa wa polisi.

Unapowaondoa wanafunzi 7,802 ndani ya saa 24 sijui hii serikali ya CCM inawaza nini....

Ili waondoke wote hapo yanahitajika mabasi zaidi ya 150 ambayo ni karibu nusu ya mabasi yote yanayoondoka Ubungo kwa siku 1 kwenda nchi nzima, Haujafikiria watalala wapi...watakula wapi...

Na: Yericko Nyerere
Yeriko, unashangaa masaa 24, wenzako tulikuwa tunaondolewa ndani ya masaa 2 tu!! Usiulize wapi, ni hapa hapa Bongo
 
Hivi huyo spika wa bunge anakuwa na kazi gani kiasi kwamba anamwachia kiti naibu spika kila siku na matokeo yake bunge linaendeshwa kama kambi ya mafunzo ya umoja wa vijana wa ccm?
Tatizo lenu bawacha uelewa shida mnadhani kila jambo mtapeleka kibawacha tu.
 
Mimi siyo CDM wala CCM ila siwezi kuvumilia mambo yanavyofanywa ya kunyanyasa na kudhalilisha km yalivyofanywa leo.Nikikumbuka msoto wa chuoni pale boom likikata natamani kulia,tulikua tunashindia mkate na maji tu ila leo wanafunzi na vijana wenzetu wanafanyia uhuni kama huu...yaani hapa hamna cha LUMUMBA wala UFIPA we have to join to fight against this humilation.Haiwezekani Spika atoe maamuzi ya hovyo hivi na waziri wa elimu atoe majibu ya marahisi hivyo..Haiwezekani kabisa.Huyu Naibu spika atakua amesoma kwa shule za juu hajui uchungu na machungu ya vyuoni,pia atakua hana mtoto anayesomea shule za serikali ndio maana hana ubinadam ndani ya nafsi yake.Vijana wote tulaani kabisa maamuzi ya Naibu spika,haki lazima itendeke
Tupo pamoja kabisa mkuu!
 
Wadogo zangu mlioondoshwa UDOM kwa saa 24 poleni sana, mlienda kusomea ualim ili mje kufundisha au kuwa walim,ila ndoto zenu zimezimwa kama kibatari kwenye upepo mkali. Lakini huenda mmeepushwa na kadhia kubwa huko kwenye ajira,as long mlifaulu basi angalieni utaratibu mwingine wa kwenda kujiendeleza aidha advance level au kwenye vyuo vingine na si lazima msomee ualim hasa ualim huu unaolalamikiwa hapa nchini.
Pamoja na changamoto hii,napenda kuwaeleza hii si mara ya kwanza kwa vijana kutimuliwa vyuoni ndani ya saa 24, jana nilidokeza hapa kuwa wahanga wa hii issue ni wasichana, na madhara yanaweza yasionekane jana,leo au kesho ila kwa kadhia hii kuna mabinti watapata virus tu (HILI LITATOKEA).HAPA Wanafunzi wa Stashahda ya ualimu masomo ya Sayansi, Hesabu na Teknolojia UDOM warudishwa nyumbani
Poleni sana vijana,nenden mkahangaikie mipango yenu huko mbele ya safari mtazipata hizo degree
 
Kwa taarifa yako kati ya wabunge walio onyesha kukerwa na hayo maamuzi ya huyo naibu spika ni kutoka ndani ya ccm pia, jifunze kuwa mzalendo kwenye mambo ya msingi!
Kwa taarifa yako kati ya wabunge walio onyesha kukerwa na hayo maamuzi ya huyo naibu spika ni kutoka ndani ya ccm pia, jifunze kuwa mzalendo kwenye mambo ya msingi!
Dogo pole kwa ban.
 
Wabunge wote wa upinzani wameamuriwa kutoka nje ya Bunge kwasababu za kuhoji suala la wanafunzi wa UDOM kufukuzwa chuoni kinyama.

Kaandika Zitto kwenye ukurasa wake wa facebook.
Mungu ailaani ccmmm na viongozi wake wote na wanaoishangilia
 
Huu ni uthibitisho wa kutosha ile kauli ya Magufuli kwamba kautoa mwili wake kama sadaka kwa wanyonge ni unafiki wa hali ya juu. Hawa Wanafunzi ni baadhi ya wanyonge nchini na Magufuli yuko ndani ya Ikulu kimyaaa huku hawa Wanafunzi wakiendelea kuteseka kutokana na maamuzi ya hii Serikali dhalimu na Jipu naibu spika.
 
Back
Top Bottom