Wapinzani watimuliwa tena Bunge la jioni

Mgogoro wa wanafunzi UDOM na ule wa wahadhiri wao unabeba sura ya kisiasa tena siasa za kuangamiza taifa letu, Nasema haya nikisikitika kwa kinachoendelea katika uwanja wa siasa leo,

Hawa wanafunzi waliofukuzwa UDOM walichaguliwa baada ya kufaulu vizuri(alama A na B) masomo ya sayansi kidato cha nne kutokana agizo la serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete la kuitaka wizara ifanye njia za makusudi kupunguza tatizo la walimu wa sayansi katika shule za sekondari kidato cha 1-4.

Ilianzishwa mpango maalumu (Diploma Special Program) iliyozinduliwa na Rais kwa pesa zilizoombwa bungeni kisheria (bunge liliridhia) kuwasomesha vijana hao kwa gharama za serikali ili wakafundishe O-level katika shule za serikali kisha baadaye wakasome degree. Kazi ya kuwadahili vijana hawa ilifanywa na serikali yenyewe kupitia TCU.

Leo serikali ya chama kilekile na bunge lake lilelile wamekuja na waziri wa chama kilekile wanashindwa kuwalipa malipo wakufunzi wa wanafunzi hao na kupelekea mgomo wa wahariri, hawaishi hapo wanakwenda chuoni na kuwafukuza wanafunzi hao wasio na hatia, wanataka dunia iamini kuwa serikali iliyopita ni nyingine kabisa na haina mazuri iliyoyafanya na ilikua inaongozwa wajinga! Katika bunge lilelile na spika wa chama kilekile wanazuia hoja binafsi ya Mbunge wa upinzani anayetaka bunge lijadili mgogoro huu na kunusuru hatari inayowakumba watoto wetu hapo UDOM, na zaidi mbunge huyo ananyanyuliwa mzobemzobe na polisi na kutupwa nje ya lango la Bunge

Leo ni vijana hao hao kama wangeamua kwenda kidato cha tano wangemaliza form six mwaka jana lakini walijitolea na pamoja na kufaulu kwa division one na two zao kusaidia taifa. Leo wanafukuzwa kwa mabomu na mbwa wa polisi.

Unapowaondoa wanafunzi 7,802 ndani ya saa 24 sijui hii serikali ya CCM inawaza nini....

Ili waondoke wote hapo yanahitajika mabasi zaidi ya 150 ambayo ni karibu nusu ya mabasi yote yanayoondoka Ubungo kwa siku 1 kwenda nchi nzima, Haujafikiria watalala wapi...watakula wapi...

Na: Yericko Nyerere
 
Serikali hii hii ilitoa masaa 24 kwa wanafunzi wote wa St Joseph Arusha na Songea, hivi wale walifikaje makwao? Au wale walikuwa wanachuo na hawa ni wanafunzi. Wanaambiwa Lukuvi atakuja na tamko la serikali jioni ya kikao hiki hawataki wasaidiwaje?
 
Wabunge wote wa upinzani wameamuriwa kutoka nje ya Bunge kwasababu za kuhoji suala la wanafunzi wa UDOM kufukuzwa chuoni kinyama.

Kaandika Zitto kwenye ukurasa wake wa facebook.
Wafukuzwe tu maana hamna namna nyingine sasa.

Kazi yao imekuwa kudandia dandia tu hoja.

Hivyo kabisa
 
Iko siku tutaambiwa JF imefungiwa bila maelezo yoyote. Kulikua na ugumu gani wa hili jambo kujadiliwa bungeni na ufumbuzi kutafutwa? Kama kuna sababu za msingi walizonazo zinazopelekea wanafunzi hao kuondolewa chuoni kwanini zisiwekwe wazi, vinginevyo tutaamini kwamba hakuna sababu za maana nyuma ya hili zoezi.
 
Mimi siyo CDM wala CCM ila siwezi kuvumilia mambo yanavyofanywa ya kunyanyasa na kudhalilisha km yalivyofanywa leo.Nikikumbuka msoto wa chuoni pale boom likikata natamani kulia,tulikua tunashindia mkate na maji tu ila leo wanafunzi na vijana wenzetu wanafanyia uhuni kama huu...yaani hapa hamna cha LUMUMBA wala UFIPA we have to join to fight against this humilation.Haiwezekani Spika atoe maamuzi ya hovyo hivi na waziri wa elimu atoe majibu ya marahisi hivyo..Haiwezekani kabisa.Huyu Naibu spika atakua amesoma kwa shule za juu hajui uchungu na machungu ya vyuoni,pia atakua hana mtoto anayesomea shule za serikali ndio maana hana ubinadam ndani ya nafsi yake.Vijana wote tulaani kabisa maamuzi ya Naibu spika,haki lazima itendeke
 
Serikali hii hii ilitoa masaa 24 kwa wanafunzi wote wa St Joseph Arusha na Songea, hivi wale walifikaje makwao? Au wale walikuwa wanachuo na hawa ni wanafunzi. Wanaambiwa Lukuvi atakuja na tamko la serikali jioni ya kikao hiki hawataki wasaidiwaje?
Kama huna elimu kamwe huwezi kuwathamini wanao tafuta elimu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ukiwekwa mahali, utalipa fadhila kwa kutetea maslahi ya aliyekuweka hata kama inabidi ujitoe ufahamu.
Kuna wati serikali ya Magufuli sina Imani nao hata huyu dada...sina Imani na utendaji wake kabisa
 
Back
Top Bottom