Wapinzani watimuliwa tena Bunge la jioni

Wapinzani watimuliwa tena Bunge la jioni

Mgogoro wa wanafunzi UDOM na ule wa wahadhiri wao unabeba sura ya kisiasa tena siasa za kuangamiza taifa letu, Nasema haya nikisikitika kwa kinachoendelea katika uwanja wa siasa leo,

Hawa wanafunzi waliofukuzwa UDOM walichaguliwa baada ya kufaulu vizuri(alama A na B) masomo ya sayansi kidato cha nne kutokana agizo la serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete la kuitaka wizara ifanye njia za makusudi kupunguza tatizo la walimu wa sayansi katika shule za sekondari kidato cha 1-4.

Ilianzishwa mpango maalumu (Diploma Special Program) iliyozinduliwa na Rais kwa pesa zilizoombwa bungeni kisheria (bunge liliridhia) kuwasomesha vijana hao kwa gharama za serikali ili wakafundishe O-level katika shule za serikali kisha baadaye wakasome degree. Kazi ya kuwadahili vijana hawa ilifanywa na serikali yenyewe kupitia TCU.

Leo serikali ya chama kilekile na bunge lake lilelile wamekuja na waziri wa chama kilekile wanashindwa kuwalipa malipo wakufunzi wa wanafunzi hao na kupelekea mgomo wa wahariri, hawaishi hapo wanakwenda chuoni na kuwafukuza wanafunzi hao wasio na hatia, wanataka dunia iamini kuwa serikali iliyopita ni nyingine kabisa na haina mazuri iliyoyafanya na ilikua inaongozwa wajinga! Katika bunge lilelile na spika wa chama kilekile wanazuia hoja binafsi ya Mbunge wa upinzani anayetaka bunge lijadili mgogoro huu na kunusuru hatari inayowakumba watoto wetu hapo UDOM, na zaidi mbunge huyo ananyanyuliwa mzobemzobe na polisi na kutupwa nje ya lango la Bunge

Leo ni vijana hao hao kama wangeamua kwenda kidato cha tano wangemaliza form six mwaka jana lakini walijitolea na pamoja na kufaulu kwa division one na two zao kusaidia taifa. Leo wanafukuzwa kwa mabomu na mbwa wa polisi.

Unapowaondoa wanafunzi 7,802 ndani ya saa 24 sijui hii serikali ya CCM inawaza nini....

Ili waondoke wote hapo yanahitajika mabasi zaidi ya 150 ambayo ni karibu nusu ya mabasi yote yanayoondoka Ubungo kwa siku 1 kwenda nchi nzima, Haujafikiria watalala wapi...watakula wapi...

Na: Yericko Nyerere
MH.YERICKO NYERERE nilitaraji uende mbali zaidi kueleza na kufafanua UKWELI
Kama nimeelewa sahihi wale wanafunzi wametakiwa kuondoka baada ya KUFUNGWA CHUO, kufuatia MGOMO WA WAKUFUNZI WAO. mgomo huu hauwahusu wanafunzi, hawadai boom wala malipo mengine bali waalimu hawaingii darasani. Isitoshe serikali imejua mchakato wa kumaliza mgogoro wake na WAKUFUNZI wao unaweza kuchukua muda mrefu, huenda pia haiingii akilini kuwaacha watu 7000 wakizagaa bila uangalizi na hatimae wao kuwa part and parcel ya mgogoro.
Ndio kusema serikali imefunga CHUO kwa muda usiojulikana mpaka watakapomaliza mgogoro na WAKUFUNZI wao ndipo wataitwa.
Now, what's the big deal..... mpaka watu wanashindwa kujadili issue mama ambayo ni MGOMO WA WAKUFUNZI na sasa mmeamua kugeukia WANACHUO 7000 kutakiwa kuondoka ndani ya siku moja?
 
Serikali hii hii ilitoa masaa 24 kwa wanafunzi wote wa St Joseph Arusha na Songea, hivi wale walifikaje makwao? Au wale walikuwa wanachuo na hawa ni wanafunzi. Wanaambiwa Lukuvi atakuja na tamko la serikali jioni ya kikao hiki hawataki wasaidiwaje?
Kwani bunge life likuwa Luna vikao au unataka kuleta za kuleta?
 
Serikali hii hii ilitoa masaa 24 kwa wanafunzi wote wa St Joseph Arusha na Songea, hivi wale walifikaje makwao? Au wale walikuwa wanachuo na hawa ni wanafunzi. Wanaambiwa Lukuvi atakuja na tamko la serikali jioni ya kikao hiki hawataki wasaidiwaje?
Daa!!wewe nisije kukutukana bure mbwa wewe!! Mdogo wangu tena wakike kalala stendi kwa kukosa usafilli wa kumfikisha nyumbsni mwanza afu we mngese unasema nini??[emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35]
 
Shida ni mbaya sana, kwa mwenenacho hawezi kuelewa. Na usiombe ikakukuta ( albert, 2016). Kutimuliwa gafla kwa wanafunzi kunaweza kuleta matatizo ya nauli kutokana na malengo aliyokuwa nayo mtu ikilinganishwa na familia za watanzania wengi ni wakipato cha chini Sana wanafunz weng watapata SHIDA Sana. Tuwaombee
 
Yani hapa kunawatu wanajitoa ufahamu kabisa na kuona eti ni sawa serikali inachokifanya. Hii inasikitisha sana
Sasa wanafunzi hawakuwa na kosa, serikali ilishindwa kuelewana na wahadhiri lakini mzigo wanabebeshwa wanafunzi hii sio sawa. Sasa kosa la kwanza ni kwa ndalichako na wapili ni tulia.
Prof Ndalichako angeweza kuliweka hili jambo vizuri bila kufika huku. Angewapa wanafunzi siku 10 za kuondoka tena kwa kauli ya upole kwakuwa hawajagoma wala kuleta vurugu. Hakupaswa kutoa muda mfupi namna hiyo kwa vijana wetu. Inauma sana kwakweli. Hizi ni.miongoni mwa njia mabilimbali zinazotumika kuudhalilisha ualimu
 
Mgogoro wa wanafunzi UDOM na ule wa wahadhiri wao unabeba sura ya kisiasa tena siasa za kuangamiza taifa letu, Nasema haya nikisikitika kwa kinachoendelea katika uwanja wa siasa leo,

Hawa wanafunzi waliofukuzwa UDOM walichaguliwa baada ya kufaulu vizuri(alama A na B) masomo ya sayansi kidato cha nne kutokana agizo la serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete la kuitaka wizara ifanye njia za makusudi kupunguza tatizo la walimu wa sayansi katika shule za sekondari kidato cha 1-4.

Ilianzishwa mpango maalumu (Diploma Special Program) iliyozinduliwa na Rais kwa pesa zilizoombwa bungeni kisheria (bunge liliridhia) kuwasomesha vijana hao kwa gharama za serikali ili wakafundishe O-level katika shule za serikali kisha baadaye wakasome degree. Kazi ya kuwadahili vijana hawa ilifanywa na serikali yenyewe kupitia TCU.

Leo serikali ya chama kilekile na bunge lake lilelile wamekuja na waziri wa chama kilekile wanashindwa kuwalipa malipo wakufunzi wa wanafunzi hao na kupelekea mgomo wa wahariri, hawaishi hapo wanakwenda chuoni na kuwafukuza wanafunzi hao wasio na hatia, wanataka dunia iamini kuwa serikali iliyopita ni nyingine kabisa na haina mazuri iliyoyafanya na ilikua inaongozwa wajinga! Katika bunge lilelile na spika wa chama kilekile wanazuia hoja binafsi ya Mbunge wa upinzani anayetaka bunge lijadili mgogoro huu na kunusuru hatari inayowakumba watoto wetu hapo UDOM, na zaidi mbunge huyo ananyanyuliwa mzobemzobe na polisi na kutupwa nje ya lango la Bunge

Leo ni vijana hao hao kama wangeamua kwenda kidato cha tano wangemaliza form six mwaka jana lakini walijitolea na pamoja na kufaulu kwa division one na two zao kusaidia taifa. Leo wanafukuzwa kwa mabomu na mbwa wa polisi.

Unapowaondoa wanafunzi 7,802 ndani ya saa 24 sijui hii serikali ya CCM inawaza nini....

Ili waondoke wote hapo yanahitajika mabasi zaidi ya 150 ambayo ni karibu nusu ya mabasi yote yanayoondoka Ubungo kwa siku 1 kwenda nchi nzima, Haujafikiria watalala wapi...watakula wapi...

Na: Yericko Nyerere

Kama aliyeleta hapa ni Yericko, inabidi nisome hapa kwa makini..zaidi kwani there is a possibility kuna exaggerations nyingi hapa..
 
Wafukuzwe tu maana hamna namna nyingine sasa.

Kazi yao imekuwa kudandia dandia tu hoja.

Hivyo kabisa

Kwa bahati mbaya nyie mnaojifanya mna hoja, nyingi ya hoja zenu ni za kulamisha na zinasonga mbele kwa nguvu ya dola. Matokeo yake kila siku ni ahadi tamu tamu kwa wananchi ila matokeo ni ya kutafuta kwa tochi.
 
Kama tuna ongelea Mti una matatizo unakauka hauna matunda mazuri na hauzalishi sawa sasa basi mara nyingi Tatizo ni Root yake...kule kwenye mizizi ndio kuna problem.
Mfano huu pia unatumika kwenye taasisi au organasation...ukiona idara zote zinayumba , haziwezi kutoa uamuzi wowote au unatoa maamuzi ya kufurahisha bodi ...huku hisa zinaporomoka basi ujue tatizo ni manager..manager aidha hana uwezo au haambiliki hivyo hawa wachini wanaogopa kufanya sahihi wana ogopa kufukuzwa...#hapahofutu
 
Daa!!wewe nisije kukutukana bure mbwa wewe!! Mdogo wangu tena wakike kalala stendi kwa kukosa usafilli wa kumfikisha nyumbsni mwanza afu we mngese unasema nini??[emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35]
Hayo matusi usije kuwa unajitukana mwenyewe, huyo hakuwa ndugu yako, utakubaliaje ndugu yako alale stand hali wewe upo. Na teknologia yote ya leo ukashindwa kumsaidia huyo siyo nduguyo
 
Hongera zake Dr.Kikwete kwa kuanzisha Special Diploma ya Masomo ya Sayansi.
 
Hayo matusi usije kuwa unajitukana mwenyewe, huyo hakuwa ndugu yako, utakubaliaje ndugu yako alale stand hali wewe upo. Na teknologia yote ya leo ukashindwa kumsaidia huyo siyo nduguyo

Unafahamu 7300 wanahitaji mabasi mangapi ? Au ndege ngapi ? Halafu uliza dodoma kuna mabasi mangapi yanayo ondoka hapo kwa siku.Fanya hesabu mwenyewe thn utapata jawabu kuwa kumbe mm mjinga
 
Iko siku tutaambiwa JF imefungiwa bila maelezo yoyote. Kulikua na ugumu gani wa hili jambo kujadiliwa bungeni na ufumbuzi kutafutwa? Kama kuna sababu za msingi walizonazo zinazopelekea wanafunzi hao kuondolewa chuoni kwanini zisiwekwe wazi, vinginevyo tutaamini kwamba hakuna sababu za maana nyuma ya hili zoezi.

Bunge kujadili suala hilo wakati serikali inalishughulikia ni kuingilia kati mhimili huo wa serikali.....tehtehtehtehteh (just a joke)
 
Mambo muhimu kama haya ni vizuri hekima kutumika ili kupata suluhisho la tatizo,kutumia askari na mbwa kuwaondoa wanachuo pale chuoni bado hujamaliza tatizo.
 
Kinachoendelea sasa bungeni ni nafasi wabunge kupiga kura kutokuwa na imani na naibu spika.
 
Unafahamu 7300 wanahitaji mabasi mangapi ? Au ndege ngapi ? Halafu uliza dodoma kuna mabasi mangapi yanayo ondoka hapo kwa siku.Fanya hesabu mwenyewe thn utapata jawabu kuwa kumbe mm mjinga

Hoja hapa ni unafiki wa wabunge, kwa kuwa wako bungeni na wataonekana kwa wapiga kura wanajifanya kuvimba mishipa ya shingo kutetea wanafunzi wa UDOM, walikuwa wapi vyuo viwili vya St Joseph Arusha na Songea kufungwa na wanafunzi wote kupewa masaa hayo hayo ishirini na nne, hakuna aliyesimama kutetea na kushinikiza serikali iwasadie kisa hakuna atakayewaona sababu hawapo bungeni
 
Serikali hii hii ilitoa masaa 24 kwa wanafunzi wote wa St Joseph Arusha na Songea, hivi wale walifikaje makwao? Au wale walikuwa wanachuo na hawa ni wanafunzi. Wanaambiwa Lukuvi atakuja na tamko la serikali jioni ya kikao hiki hawataki wasaidiwaje?
Ilikuwa inaigharimu nini wabunge kujadili jambo hilo la dharura? Eti Lukuvi atakuja na tamko jioni jioni ya kikao! Lisubiriwe tamko kutoka kwenye serikali ile ile iliyowatimua? Kwanini Serikali inafanya kazi kwa kuhofia wapinzani muda wote?
 
Hivi hao wanafunzi 7000 waliokatizwa ndoto zao kimaisha kwa ukatili hakuna watoto wa wanyonge? Au mnyonge ni yupi?
Ni wanafunzi 7802. Hakua aliyekatiza ndoto zao. wataendelea na masomo baada ya kurekebisha kasoro za BRN. Hizo ndizo garama za mabadiliko. Umesoma taarifa ya serikali?
 
Back
Top Bottom