Zee la shamba
Member
- Oct 17, 2007
- 55
- 4
Vyama vinne vya upinzani vilivyoanzisha ushirikiano, vinafanya utaratibu wa kumuomba radhi Rais Jakaya Mrisho Kikwete kutokana na kitendo chao cha kumuweka katika orodha ya mafisadi iliyotolewa katika viwanja vya Mwembe Yanga mapema mwezi uliopita.
Habari ambazo Rai imezipata kutoka kwa baadhi ya viongozi wa upinzani, zinaeleza kwamba kimsingi vyama hivyo vimegundua kwamba yalikuwa ni makosa ya kimkakati kumtaja Rais katika tuhuma hizo kwa sababu tuhuma walizotoa juu yake ni nyepesi.
Rai imeelezwa kwamba iwapo mambo yatakwenda vizuri, wataifanya kazi hiyo siku ya Jumamosi kwa kumuomba radhi rasmi Kikwete ikiwa ni pamoja na watu wengine wawili. Rai haikufanikiwa kupata jina la mtu wa tatu lakini mtu wa pili ameelezwa kuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Patrick Rutabanzibwa.
Katika tuhuma zilizosomwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Wilbroad Slaa, wapinzani walisema kuwa pamoja na mambo mengine, Agosti mwaka 1994, Kikwete aliingia katika mkataba na kampuni ya madini ya Kahama Mining Corporation Ltd.
Tuhuma hizo zilieleza kwamba ingawa mkataba ulionyesha kuwa ulikuwa unahusu eneo la Butobela Wilaya ya Geita Mkoani Mwanza, Agosti mwaka 1996 Kahama Mining Corporation walivamia eneo la Bulyanhulu, na kuwaondosha kwa nguvu watu waliokuwa wakiishi na kuchimba dhahabu katika eneo hilo. Baadaye Sutton Resources iliiuza Kahama Mining Corporation na Bulyanhulu kwa Kampuni ya Dhahabu ya Barrick Gold Corporation ya Toronto, Canada.
Mmoja kati ya viongozi wa kambi ya upinzani, ameiambia Rai kwamba baada ya kuangalia athari za tuhuma dhidi ya rais, wamegundua kwamba hilo lilikuwa kosa la kimkakati.
Strategically hilo lilikuwa kosa kumtaja Rais. Pia tuhuma dhidi yake zilikuwa nyepesi sana. Tunamtoa rais na wengine wawili, lakini tunaongeza wapya. Oktoba 27 tutamtoa na kumuomba radhi, alisema kiongozi huyo ambaye hata hivyo hakutaka jina lake litajwe.
Soorce Rai