Wapinzani kumwomba radhi JK

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2007
Messages
5,194
Points
0

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2007
5,194 0
Kadakadakada!

Usijimalize kwa udaku

Halafu CCM ya MAFISADI wako Tayari kuleta maendeleo Tanzania? Je ulisoma Mkataba wa BUZWAGI, ukiambiwa uliandikiwa pale darajani MAnzese utakataaa? Tuachane na propaganda za Rai na RA.Hakuna wa kumwomba radhi JK ni ndoto tu, mwambie afanye aliyoyaahidi.
Hiki ndicho hawataki kuona kikiendelea.

Ukiangalia hasira zote hapa zilianza baada ya mikataba ya Buzwagi, Tanesco, na Richmonduli kuwekwa hapa. Hasira imekuwa juu ya hasira kwa sababu hawakutegemea kama JF inaweza kumwaga lazi kiasi hiki!

Since then, watu wameanza kuipondea JF ili ionekane haifai. The same trick alotumia mwizi, mkoloni na mkwepa kodi Rostam Azizi dhidi ya wapinzani wa Kikwete wakati wa uchaguzi wa ccm 2005
 
John Mnyika

Verified Member
Joined
Jun 16, 2006
Messages
715
Points
225

John Mnyika

Verified Member
Joined Jun 16, 2006
715 225
Vyama vinne vya upinzani vilivyoanzisha ushirikiano, vinafanya utaratibu wa kumuomba radhi Rais Jakaya Mrisho Kikwete kutokana na kitendo chao cha kumuweka katika orodha ya mafisadi iliyotolewa katika viwanja vya Mwembe Yanga mapema mwezi uliopita.

Habari ambazo Rai imezipata kutoka kwa baadhi ya viongozi wa upinzani, zinaeleza kwamba kimsingi vyama hivyo vimegundua kwamba yalikuwa ni makosa ya kimkakati kumtaja Rais katika tuhuma hizo kwa sababu tuhuma walizotoa juu yake ni nyepesi.

Rai imeelezwa kwamba iwapo mambo yatakwenda vizuri, wataifanya kazi hiyo siku ya Jumamosi kwa kumuomba radhi rasmi Kikwete ikiwa ni pamoja na watu wengine wawili. Rai haikufanikiwa kupata jina la mtu wa tatu lakini mtu wa pili ameelezwa kuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Patrick Rutabanzibwa.

Katika tuhuma zilizosomwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Wilbroad Slaa, wapinzani walisema kuwa pamoja na mambo mengine, Agosti mwaka 1994, Kikwete aliingia katika mkataba na kampuni ya madini ya Kahama Mining Corporation Ltd.

Tuhuma hizo zilieleza kwamba ingawa mkataba ulionyesha kuwa ulikuwa unahusu eneo la Butobela Wilaya ya Geita Mkoani Mwanza, Agosti mwaka 1996 Kahama Mining Corporation walivamia eneo la Bulyanhulu, na kuwaondosha kwa nguvu watu waliokuwa wakiishi na kuchimba dhahabu katika eneo hilo. Baadaye Sutton Resources iliiuza Kahama Mining Corporation na Bulyanhulu kwa Kampuni ya Dhahabu ya Barrick Gold Corporation ya Toronto, Canada.

Mmoja kati ya viongozi wa kambi ya upinzani, ameiambia Rai kwamba baada ya kuangalia athari za tuhuma dhidi ya rais, wamegundua kwamba hilo lilikuwa kosa la kimkakati.

“Strategically hilo lilikuwa kosa kumtaja Rais. Pia tuhuma dhidi yake zilikuwa nyepesi sana. Tunamtoa rais na wengine wawili, lakini tunaongeza wapya. Oktoba 27 tutamtoa na kumuomba radhi,” alisema kiongozi huyo ambaye hata hivyo hakutaka jina lake litajwe.

Soorce Rai

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

VIONGOZI WA USHIRIKIANO WA VYAMA VYA UPINZANI KUZUNGUMZA NA WANANCHI KUHUSU UFISADI
• ‘Kuanika’ jinsi mabilioni mengine ‘yalivyochotwa’ benki kuu
• Kutaja viongozi wa serikali walivyohusika na ‘kampuni hewa’ ilivyotumika
• Kugawa mkataba wa Richmond kwa umma

Viongozi wa Ushirikiano wa Vyama Vya Upinzani vya CHADEMA, CUF, NCCR Mageuzi na TLP siku ya jumapili tarehe 28 Oktoba, 2007 watazungumza na wananchi katika mkutano wa ndani kutoa taarifa kwa umma kuhusu ufisadi.

Mazungumzo hayo ya ndani ambayo wananchi mbalimbali wanaalikwa kushiriki yatafanyika katika Ukumbi wa Urafiki uliopo Manispaa ya Kinondoni Jimbo la Ubungo Mkoani Dar e salaam kuanzia saa 4 mpaka saa 5 na nusu asubuhi.

Katika mazungumzo hayo viongozi wa Vyama vya Upinzani wataanika jinsi mabilioni mengine zaidi yalivyochotwa katika benki kuu ya Tanzania na kutaja viongozi wa serikali walivyohusika na ‘kampuni hewa’ ilivyotumika.

Itakumbukwa kwamba tarehe 15 Septemba, 2007 katika mkutano wa hadhara uwanja wa Mwembeyanga uongozi wa ushirikiano wa vyama vya upinzani ulitaja orodha ya mafisadi nchini yenye kueleza ufisadi, wizi na/au ubadhirifu au matumizi mabaya ya rasilimali za taifa.

Pamoja na viongozi wengine pia, Dr Wilbroad Slaa, Mbunge wa Karatu(CHADEMA) atazungumza katika mkutano huo. Dr Slaa ndiye aliyeibua hoja ya kutaka kuundwa kwa kamati teule ya kuchunguza tuhuma za ufisadi katika benki kuu na kupelekea kutangazwa kwa orodha ya mafisadi. Dr Slaa amerejea hivi karibuni kutoka Marekani ziarani nchini Marekani na Mkutano wa Bunge la Kusini mwa Afrika SADC nchini Malawi.

“ Katika mkutano huu hatutataja orodha nyingine ya mafisadi. Tutajenga katika orodha ya awali ya mafisadi. Katika mkutano huu kitakachotajwa ni ufisadi mwingine uliopelekea mabilioni mengine kuchotwa katika benki kuu. Pia katika Mkutano huo tutagawa mkataba wenye utata wa Richmond kama tulivyofanya kwa mkataba wa Madini wa Buzwagi ili umma”

Imetolewa na 26/10/2007:

John Mnyika
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi na
Mkurugenzi wa Vijana Taifa(CHADEMA)
0754694553
 
Mwanamalundi

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2007
Messages
3,129
Points
1,500

Mwanamalundi

JF-Expert Member
Joined Aug 30, 2007
3,129 1,500

Habari ambazo Rai imezipata kutoka kwa baadhi ya viongozi wa upinzani, zinaeleza kwamba kimsingi vyama hivyo vimegundua kwamba yalikuwa ni makosa ya kimkakati kumtaja Rais katika tuhuma hizo kwa sababu tuhuma walizotoa juu yake ni nyepesi.

Soorce Rai
....Wepesi wa tuhuma, haufuti tuhuma. Mwizi wa kuku, na mwizi wa ng'ombe, wote ni wezi. Huwezi kusema,aaah unajua huyu jamaa wizi wake hauna madhara eti kwa sababu ameiba kuku.

Rai imeelezwa kwamba iwapo mambo yatakwenda vizuri, wataifanya kazi hiyo siku ya Jumamosi kwa kumuomba radhi rasmi Kikwete ikiwa ni pamoja na watu wengine wawili. Rai haikufanikiwa kupata jina la mtu wa tatu lakini mtu wa pili ameelezwa kuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Patrick Rutabanzibwa.

Soorce Rai
Rutabanzibwa ndio amewapa pesa rai muandike hivyo. Mbona hajawapa taarifa ya pesa ya serikali aliyotumia kukarabati nyumba aliyouziwa. For your information, ametumia pesa ya walipa kodi (zaidi ya Shs millioni 300)kukarabati nyumba aliyonunua. Alianza kufanya huu ukarabati kabla ya kutangazwa rasmi zoezi la uuzaji wa nyumba za serikali. Kama hii habari sio ya kweli, tunamuomba akanushe.Katika tuhuma zilizosomwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Wilbroad Slaa, wapinzani walisema kuwa pamoja na mambo mengine, Agosti mwaka 1994, Kikwete aliingia katika mkataba na kampuni ya madini ya Kahama Mining Corporation Ltd.
.

Soorce Rai

I dont think, Dr. Slaa angeweza kuongea kitu ambacho hana uhakika nacho. Maana madhara yake ni makubwa.
Strategically hilo lilikuwa kosa kumtaja Rais. Pia tuhuma dhidi yake zilikuwa nyepesi sana. Tunamtoa rais na wengine wawili, lakini tunaongeza wapya. Oktoba 27 tutamtoa na kumuomba radhi,” alisema kiongozi huyo ambaye hata hivyo hakutaka jina lake litajwe.

Soorce Rai
mwizi wa kuku na mwizi wa ng'ombe wote ni wezi. Leo kaiba kuku, kesho ataiba ng'ombe. Wepesi wa tuhuma, haufuti tuhuma. Be serious RAI!!
 
KadaMpinzani

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2007
Messages
3,750
Points
0

KadaMpinzani

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2007
3,750 0
vizuri kwamba umesema kwamba wizi ni wizi, haujalishi kama umeiba kuku au umeiibia buzwagi ! Slaa mwenyewe ana tuhuma lakini hadi leo sijamsikia akijibu, au wafuasi wake hapa JF wakijibu ! woooote kimya !

Slaa jibu tuhuma, pesa za vilema ziko wapi ??
 
Mwanamalundi

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2007
Messages
3,129
Points
1,500

Mwanamalundi

JF-Expert Member
Joined Aug 30, 2007
3,129 1,500
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

VIONGOZI WA USHIRIKIANO WA VYAMA VYA UPINZANI KUZUNGUMZA NA WANANCHI KUHUSU UFISADI
• ‘Kuanika’ jinsi mabilioni mengine ‘yalivyochotwa’ benki kuu
• Kutaja viongozi wa serikali walivyohusika na ‘kampuni hewa’ ilivyotumika
• Kugawa mkataba wa Richmond kwa umma

Viongozi wa Ushirikiano wa Vyama Vya Upinzani vya CHADEMA, CUF, NCCR Mageuzi na TLP siku ya jumapili tarehe 28 Oktoba, 2007 watazungumza na wananchi katika mkutano wa ndani kutoa taarifa kwa umma kuhusu ufisadi.

Mazungumzo hayo ya ndani ambayo wananchi mbalimbali wanaalikwa kushiriki yatafanyika katika Ukumbi wa Urafiki uliopo Manispaa ya Kinondoni Jimbo la Ubungo Mkoani Dar e salaam kuanzia saa 4 mpaka saa 5 na nusu asubuhi.

Katika mazungumzo hayo viongozi wa Vyama vya Upinzani wataanika jinsi mabilioni mengine zaidi yalivyochotwa katika benki kuu ya Tanzania na kutaja viongozi wa serikali walivyohusika na ‘kampuni hewa’ ilivyotumika.

Itakumbukwa kwamba tarehe 15 Septemba, 2007 katika mkutano wa hadhara uwanja wa Mwembeyanga uongozi wa ushirikiano wa vyama vya upinzani ulitaja orodha ya mafisadi nchini yenye kueleza ufisadi, wizi na/au ubadhirifu au matumizi mabaya ya rasilimali za taifa.

Pamoja na viongozi wengine pia, Dr Wilbroad Slaa, Mbunge wa Karatu(CHADEMA) atazungumza katika mkutano huo. Dr Slaa ndiye aliyeibua hoja ya kutaka kuundwa kwa kamati teule ya kuchunguza tuhuma za ufisadi katika benki kuu na kupelekea kutangazwa kwa orodha ya mafisadi. Dr Slaa amerejea hivi karibuni kutoka Marekani ziarani nchini Marekani na Mkutano wa Bunge la Kusini mwa Afrika SADC nchini Malawi.

“ Katika mkutano huu hatutataja orodha nyingine ya mafisadi. Tutajenga katika orodha ya awali ya mafisadi. Katika mkutano huu kitakachotajwa ni ufisadi mwingine uliopelekea mabilioni mengine kuchotwa katika benki kuu. Pia katika Mkutano huo tutagawa mkataba wenye utata wa Richmond kama tulivyofanya kwa mkataba wa Madini wa Buzwagi ili umma”

Imetolewa na 26/10/2007:

John Mnyika
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi na
Mkurugenzi wa Vijana Taifa(CHADEMA)
0754694553
__________________
Kizazi Kipya, Maisha Mapya
New Generation, New Life

Mabadiliko ya Kweli, Uhuru wa Kweli
Real Change, Real Freedom

John Mnyika
Hivi nyie waandishi wa RAI source ya habari yenu ni nani hasa??
 
Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2007
Messages
5,194
Points
0

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2007
5,194 0
Hivi nyie waandishi wa RAI source ya habari yenu ni nani hasa??
Source ya habari yao kama ile email ya kumkandia Slaa ilowekwa hapa na wanamtandao ni spin master mwenyewe Rostam Aziz. Unashangaaa kusikia haya.

Subiri siku Dr Salim akirudi tena hapa kueleza jamaa waliyosema kuhusu yeye wakati wa kampeni za ccm! nchi inatawaliwa na mwizi na mkoloni Rostam kwa sasa.... I just give him few more days maana hii investigation inayoendelea juu yake inakaribia kufikia tamati
 
Mwakilishi

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2007
Messages
484
Points
195

Mwakilishi

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2007
484 195
Hiyo habari ya RAI imekaa kiudaku udaku kama siyo kiushabiki, lakini tusubiri hiyo siku ifike si ajabu tukaisikia "Mafisadi" reserve list ikitajwa.

Kudai Bwana Rutabanzibwa amewalipa RAI waandike hivyo bila ushahidi ni kuendeleza udaku vilevile.
 
Forum statistics

Threads 1,382,696
Members 526,441
Posts 33,834,192
Top