Wape Watoto fursa ya kujifunza masuala mengine katika maisha mbali na masomo ya darasani

Kujua kila kitu kwa mtoto haiwezekani ila anaweza akajua mambo mengi nje ya mfumo rasmi wa elimu...
Shule zetu zinafundisha watoto kujua kila kitu, unabisha mkuu? Tuanze kuorodhesha hapa masomo ya s/m.
Watoto mashileni wanafundishwa:
Dini,Sayansi, jografia,uraia, sanaa,muziki,michezo, stadi za kazi(ufundi),Lugha, tehama, haiba nk .
Je hapo hawafundishwi kila kitu, je kwa ufundishwaji huo wanaweza kujua vitu kwa undani?
Je kuna watoto wanaweza kusuka ungo huko mashuleni?
Vipi kutumia kompyuta, kugonga misumari je wanaweza?
Vipi kuongea kingereza ?
 
Kuna ya kukumbuka na kusahahu. Hata waliosom physics form six baada ya miaka 10 ukiwapa tena mtihani ule ule ni lazima waombe kujikumbusha kwanza kabla ya kuufanya...
Mkuu kwa dunia ya sasa ya utandawazi mambo ya mtambuka watoto wanajifunza automatic tu, bila hata kumpa vitabu au magazeti.
Fundisha watoto mambo ya sanaa(ubunifu, mziki, mpira nk), sayansi,teknolojia lugha na ujasiliamali ndio vinavyolipa kwa sasa.
Achana na mambo ya kutaja majina ya viongozi sijui vita ya libya na utopolo mwingine atavijua tu kupitia tv.
Tupo katika kipindi ambacho watoto wetu tunaweza kuwandaa vizuri zaidi kuliko wakati wowote ule.
Mfano hapa JF yu ajifunza mambo mengi mtambuka ambayo hatikuwahi kujifunza.
Wazazi wa sasa tujifunze the power of internet and harvest from it.
 
Sidhani kama upo sahihi
 
Shule zetu zinafundisha watoto kujua kila kitu, unabisha mkuu?
Kumfundisha mtoto kila kitu na yeye kujua kila kitu hayo ni mambo mawili tofauti kabisa mkuu. Bila shaka wewe pia ulipita katika mfumo wetu huu wa elimu. Je, unajua kila kitu?...
 
Je kuna watoto wanaweza kusuka ungo huko mashuleni?
Vipi kutumia kompyuta, kugonga misumari je wanaweza?
Vipi kuongea kingereza ?
Sio mbaya kama mtoto akijua mambo mengi lakini sio kujua kila kitu. Hata hawa professors wetu bado hawajui kila kitu...
 
Mkuu kwa dunia ya sasa ya utandawazi mambo ya mtambuka watoto wanajifunza automatic tu, bila hata kumpa vitabu au magazeti.
Hakuna kujifunza "automatically" mkuu, ni lazima mtoto apewe muda wa kujifunza pamoja na support kutoka kwa wazazi. Kama unasema mtoto anaweza kujifunza pasipo kumpa vitabu wala magazeti, je ni wangapi wanamudu gharama za vifaa vya kisasa vya mawasiliano kama smartphones na laptops?...
 
Achana na mambo ya kutaja majina ya viongozi sijui vita ya libya na utopolo mwingine atavijua tu kupitia tv.
Mtoto atayajua kupitia TV gani sasa wakati ukifika muda wa kutazama taarifa za habari unaangalia peke yako wakati wao bado wapo nje wanacheza au wapo busy na homeworks zisizoisha?
 
Tupo katika kipindi ambacho watoto wetu tunaweza kuwandaa vizuri zaidi kuliko wakati wowote ule.
Mfano hapa JF yu ajifunza mambo mengi mtambuka ambayo hatikuwahi kujifunza.
Wazazi wa sasa tujifunze the power of internet and harvest from it.
Kwa hapa umeongea point ya maana
 
Mtoto atayajua kupitia TV gani sasa wakati ukifika muda wa kutazama taarifa za habari unaangalia peke yako wakati wao bado wapo nje wanacheza au wapo busy na homeworks zisizoisha?
Hapa kila mtu anazungumzia jinsi ya kulea famila yake nyumbani kwake.Kama wewe unaangalia taarifa ya habari peke yako sio wazazi wote, usijumlishe mkui.
Kila mtu achague njia inayofaa ila kuilamu serikali tuache, kuna njia mbadala nyingi sana kujifunza mambo.
 
Engineers wazuri sana wapo bongo tatizo mitaji mikubwa hawana...
Waafrika hatukosi visingizio.
Kusaka mtaji ni sehemu ya kuelimika, kama huwezi pata mtaji badi hujaelimika bado unatakiwa uongeze mtaji.
Bill gate hakurithi mtaji leo tajiri ika kuna wazungu wengi tu wenye akili kumzidi hawajawahi kumiliki kampuni.
Elon musk kazaliwa Afrika alipogundua hatawezeshwa kule kwai akajiongeza leo ana mtaji mkubwa tu.
 
Kuna Silicon Dar pale kijitonyama na kuna Hub za watoto kama ile ya nani Ndoto Hub.

Pia unaweza mtengenezea Hub mwanao humohumo geto kwake kama wazungu
Kama wazungu na kama ana pesa nyingi ya kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom