Wape Watoto fursa ya kujifunza masuala mengine katika maisha mbali na masomo ya darasani

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,316
Habari za wakati huu jamiiforums

Stories nyingi sana za KGB na zile zingine ambazo ninaandikaga kule jukwaa la jamii intelligence ni zile ambazo nilizisoma mwaka 2006 nikiwa kidato cha sita. Kipindi hicho hakuna smartphones lakini nilikuwa ninaiba muda kisha ninakwenda internet cafe moja iliyokuwa inamilikiwa na mama wa rafiki yangu maeneo ya Chang'ombe kule Keko wanapaita TAMECO.

dfrgbbb.jpg


Baba yangu alikuwaga ni mtumishi wa serikali. Alifanya kazi muda mrefu sana katika viwanda vilivyoanzisha na mwalimu nyerere ila kwa bahati mbaya akaja kupata redundancy baada ya kiwanda kile kufa mwaka 1993 kama sijakosea na kuamua kuingia katika kujiajiri hivyo na kuwa na muda mwingi sana wa kukaa na sisi watoto wake baada ya kazi.

Mzee alikuwa anatupigisha stories nyingi sana za masuala ya siasa za wakati huo wa ujamaa, ushawishi wa nchi ya Russia katika Africa hivyo nikatokea kuipenda sana USSR pamoja na sera zao za ujamaa.

Ilifika kipindi mzee alikuwa akitoka katika shughuli zake za kujiajiri alikuwa anakuja na magazeti kisha anatupa tuyasome alafu baadae kabla ya kulala anaanza kutuuliza maswali mmoja badala ya mwignine na hiyo ndio iliyonijengea mimi kupenda kusoma vitabu.

Nimeamua kuanzia mbali kwa kuwaelezea story fupi ya maisha yangu baada ya kukutana na statement hii ya huyu bilionea wa kichina bwana Jack Ma katika moja ya magazeti ya online. Jack anasema hivi "I told my son: you don't need to be in the top three in your class, being in the middle is fine, so long as grades are'nt too bad". Only this kind of person has enough free time to learn other skills.

Kwa kweli hii ni kinyume kabisa na mifumo mingi ya elimu katika nchi tofauti hapa duniani na Tanzania ikiwa moja wapo. Katika mifumo mingi ya elimu hapa duniani, lengo pekee ni kuweka kila kitu pembeni na kulenga tu kwa mwanafunzi kupata alama bora zaidi darasani. Kupata As pamoja na Bs.

Na katika hali nyingi ujuzi uliojifunza nje ya darasa hauhesabiwi hata wakati mwanafunzi anapotaka kujiunga na elimu ya vyuo vikuu. Kwa hivyo, dhana hii hutoa hitimisho kwa mwanafunzi ya kuwa stadi za maisha isipokuwa zile zinazofundishwa na shule sio muhimu kabisa na njia pekee wanayoweza kutumia katika kufaulu ni kupitia kupata alama bora za darasani pekee.

Mwaka juzi wa 2019 nilipata kusoma kitabu fulani kuhusiana na maisha ya huyu tajiri wa China (Hiki kitabu nilipewa kama zawadi tu). Licha ya ukweli kwamba Jack Ma hakuwahi kuwa miongoni mwa wanafunzi watatu wa juu (tatu bora) wakati wa maisha yake ya shule enzi hizo, lakini aliweza kuifanya Ali Baba kuwa moja ya kampuni ziliyofanikiwa zaidi kwenye masuala ya biashara za mtandaoni hapa ulimwenguni.

Na hiyo ni hadithi moja tu kati ya hadhiti nyingi sana zaidi ya mia moja kama hiyo ya wajasiriamali wengi wanaoongoza na wavumbuzi wakubwa hapa ulimwenguni ambao hawakuwahi kupata alama nzuri saaaana ila bado mpaka sasa wanaongoza makampuni makubwa na yenye mafanikio ulimwenguni.

Kulingana na taarifa nilizonazo ni kwamba Jack Ma mwenyewe anataja kwa nyakati tofauti kwamba yeye mwenyewe alishindwa mara 3 wakati wa mitihani ya kuingia chuoni.

Kwa hivyo haijalishi ni As au Bs ngapi mtoto wako anaweza kuzipata ila anapojifunza masuala mbalimbali mazuri pamoja na masomo yake mara kwa mara basi unakuwa unampa exposure nzuri ya kuja kuwa mtu wa maana hapo mbeleni! Na kumbuka stadi hizi zinaweza kuwa kitu chochote kuanzia kujifunza jinsi ya kuwasiliana na watu wa rika tofauti mpaka kujifunza lugha za kigeni kama kifaransa.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Sitaki mtoto wangu aje kuwa engineer ambaye hajui Rais wa Nigeria anaitwa nani. Dunia ya sasa inataka maarifa mengi hata kujua bargaining skills ni muhimu.
Itamsaidia nini kumjua?
Kwa nini isiwe "sitaki mtoto wangu asijue jinsi ya ku design jambo lolote hapa duaniani linalohusu fani yake! ".
Kama lengo lako mtoto wako awe raisi basi awajue wote wa dunia nzima na historia zao vinginevyo ni kupoteza muda tu.
 
Itamsaidia nini kumjua?
Kwa nini isiwe "sitaki mtoto wangu asijue jinsi ya ku design jambo lolote hapa duaniani linalohusu fani yake! ".
Kama lengo lako mtoto wako awe raisi basi awajue wote wa dunia nzima na historia zao vinginevyo ni kupoteza muda tu.
Ni busara kumwezesha mwanao kujua mambo mtambuka na yanayoendelea(current issues) itamjengea kujiamini, kupanua ubongo wake, kukabili changamoto mbalimbali mwenyewe na kumbuka hayo ndiyo hutafutwa kwenye usaili wa kazi(ubunifu,ujuvi wa mambo mtambuka na current issues)
 
Ni busara kumwezesha mwanao kujua mambo mtambuka na yanayoendelea(current issues) itamjengea kujiamini, kupanua ubongo wake, kukabili changamoto mbalimbali mwenyewe na kumbuka hayo ndiyo hutafutwa kwenye usaili wa kazi(ubunifu,ujuvi wa mambo mtambuka na current issues)
Mambo mtambuka ulipo kuwa na miaka 10 unayakumbuka.
Bill gate alikita kujua software akiwa mtoto, wewe unataka mtoto wako ajue mambo mtambuka, yamsaidie nini?
Life skill ndio muhimu kwa mtoto.
Kujua kila kitu ndio imetufanya tusiwe na watu waliobobea kwa undani. Tuige wazungu,wachina wanaanza kufundisha vitu kwa umakini matokea yake wanazalisha watu makini wanaokuja kututawala Africa.
Just imagine miradi mikubwa barani Africa inajengwa na wachina,wazungu na warabu,.why? .
Waandae watoto wko katika ulimwengu wa ushindani.
Iga Bill gate mkuu hakujua kla kitu zaidi ya business of cimputer.
 
Bill gate alikita kujua software akiwa mtoto, wewe unataka mtoto wako ajue mambo mtambuka, yamsaidie nini?
Mkuu, usifananishe mfumo wa elimu ya Marekani na Tanzania. Usimfananishe Bill Gates au mtoto wake na mtoto wangu mimi. Kumbuka wao walikuja kutuchukuwa watumwa ila sisi tulishindwa kufanya hivyo na mpaka leo tunatumia sababu hiyo kama kigezo moja wapo cha Afrika kuendelea kuza katika umasikini wa kutupwa...
 
Tupeane maujuzi hapa tufanye vitu vya skills kwa watoto wetu ili wawe vizuri.
Binafsi mimi huwa nawafundisha kidogo graphics design ingawa muda wangu ni mchache sana kuwa nao.
Usijali. A little goes a long way.
 
Tupeane maujuzi hapa tufanye vitu vya skills kwa watoto wetu ili wawe vizuri.
Binafsi mimi huwa nawafundisha kidogo graphics design ingawa muda wangu ni mchache sana kuwa nao.
Hata Kama Ni nusu saa kwa wiki, Mara mwaka Mara miaka 5 wataelewa tu.
Hili Jambo zuri Sana.
 
Mkuu, usifananishe mfumo wa elimu ya Marekani na Tanzania. Usimfananishe Bill Gates au mtoto wake na mtoto wangu mimi. Kumbuka wao walikuja kutuchukuwa watumwa ila sisi tulishindwa kufanya hivyo na mpaka leo tunatumia sababu hiyo kama kigezo moja wapo cha Afrika kuendelea kuza katika umasikini wa kutupwa...
Kwa hio nikufananishe na nini? Yani nisikufananishe na watu waliofanikiwa ,upo siliasi mkuu?
Wachina,wahindi, wakorea wote wanaiga wamarekani wanafanya nini af sisi tuige wakongo au wazuru(kuua waafrika wenzao) !!!!!!!
Bill gate aliwekeza muda wake kusoma software tu ili awe konki wewe unawekeza muda wa mtoto wako kusoma majina ya maraisi, hivi upo serious na hao watoto?
Si bora uwekeze wajue hata lugha tu kuliko mambo ambayo mtu anaweza kuyasoma binafsi hata akiwa mkubwa.
Kuna vitu unatakiwa uvijenge kwa mtoto angali mdogo,msome Terence Tao utajifunza kitu.
Shule zetu zonafundisha mambo mengi mengi(genaral knowledge ) bado nawe nyumbani unaiga mtindo ule wa shuleni sasa una fidia nini hapo?
mkuu unapoteza hao watoto watakulaumu.
Kumbuka tupo ktk ulimwengu wa teknolojia, wafunze watoto mahitaji ya sasa ya dunia.
Nenda soma how Elon musk teach his pupil then utajua what i imean.
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom