Wanene kuongezewa marupurupu

Wanene kuongezewa marupurupu

Kuhusu kuvuruga ndoa ya Amina na Medi, mtu wa kumpa lawama zaidi nadhani ni yule Naibu Waziri aliyemwita Medi na kumshawishi amwache mke wake. Tumekua tukifundishwa kuwa ugomvi wa mme na mke usiuingilie, lakini bwana huyu aliingilia mambo ya unyumba wa wengine. Kama angekuwa na nia njema, angemwonya Amina kabla ya kufikisha taarifa hizo kwa mumewe.

Usanii at its best! Yaani uroda ale Zitto msalaba abebeshwe Nchimbi... tumekusikia mkuu keep it up..
 
Mkandara.

Mkandara unajua future ya Amina ameharibu huyu mpuuzi? wewe kama Amina angekuwa dada yako ungejisikiaje?

IF AT ALL something happened between the two Waheshimiwas, was the Lady raped? It takes two to tango, Au?

...just thinking aloud!
 
Mswahili: Kwanza, ni haki yako kumchukia Zitto. Lakini kusema kweli huna haki ya kumzushia mambo. Tunaomba basi chuki zako usizilete hapa kwenye forum. Binafsi nakuomba umtafute Zitto halafu ongea naye personally kumaliza chuki zako.

Pili, wanaforum naomba tusitumie nafasi ya Zitto kuja kwenye forum hapa kumvua nguo. Tushambulia hoja anazotoa Zitto na kama kuna jambo la ovyo amefanya, hilo ndilo tushughulike nalo, lakini tusizushiane au kuelezana jinsi mtu alivyokua na kulelewa. Pengine ndiyo maana viongozi wengine wanaweza wakawa wanasita kuingia kwenye hii forum. Hakuna mtu asiyependa kuheshimiwa. Kila mtu anataka heshima ya utu wake. It is too bad kwamba Mswahili unaongea habari za mamake Zitto hapa, na sijui hii imetoka wapi. Kwamba Zitto kalelewa na mzazi mmoja sio jambo la kumnyanyapaa, ni jambo la kumpongeza kwamba pamoja na matatizo yote aliyokuwa nayo ameweza kupambana hadi kufika hapo alipo.

Labda niweke jambo moja sawa japokuwa sipendi kuliongea hapa. Mswahili kazusha kwamba Zitto alifukuzwa Chuo Kikuu cha Zanzibar. Huu ni unazi wa hali ya juu, ndio maana nasema mswahi anamchukia Zitto sana, na sijui kwa nini!!? Habari ya Zitto kuacha chuo kikuu Zanzibar na kujiunga na UDSM naijua vizuri sana kama ninavyoisimulia hapa chini.

Nikiwa Rais wa DARUSO mwaka 1998/99, nilikutana na Zitto katika moja ya makongamano ya viongozi wa wanafunzi pale UCLAS, Zitto akiwakilisha serikali ya wanafunzi ya chuo kikuu cha Zanzibar. Tulikaa pale kwa siku tatu. Zitto alionyesha umahiri wake katika kuchangia mada mbalimbali. Binafsi nilivutiwa naye sana, na nikaa naye pembeni kumjua zaidi. Pamoja na mambo mengine, nilimuuliza ilikuwaje akaenda kusoma chuo kikuu Zanzibar na sio UDSM? Nikamweleza kuwa kwa uwezo alionao wa kujenga hoja alistahili kuwa pale UDSM ambapo ndiko kuna debates zaidi kuliko huko Zanzibar University. Akaniambia kuwa alikuwa hana uhakika kama angepata nafasi mlimani. Baada ya kuona marks zake za form six nikamhakikishia kuwa kwa marks hizo angeweza kuingia UDSM bila matatizo. Viongozi wengine wa DARUSO na vyuo vingine pia wakamshawishi sana Zitto aombe udahili UDSM mwaka uliofuta, kitu ambacho alifanya na hatimaye kuchaguliwa na akachukua uamuzi wa kuacha chuo kikuu Zanzibar. Kwa hiyo sio kweli kwamba Zitto alifukuzwa chuo kikuu cha Zanzibar. Huu ni uzushi wa kutisha.

Mapendekezo kwa JF management:

Kwa kuwa Mswahili amefikia hatua ya kuzusha kwa kiwango nilichoeleza hapo juu na kwa kuwa uzushi huu unaleta usumbufu mkubwa wa kisaikolojia kwa mhusika, jamaa zake na marafiki zake, na ili kulinda heshima ya forum hii kwa wanaforum na wageni wanaoitembelea, napendekeza mambo matatu yafuatayo:

(a) Mswahili apewe karipio na kemeo kali kuhusu mwenendo wake wa uchangiaji mada hapa
(b) Mswahili afungiwe uanachama na uchangiaji hapa JF kwa muda wa mwezi mmoja
(c) atakaporejeshewa uanachama wake, Mswahili amuombe radhi Ndugu Zitto na wana JF kwa uzushi na kutumia lugha isiyo ya uungwana katika michango yake

Naomba kuwasilisha.

PS: naomba mnisamehe kwa kuingia too personal kwenye habari ya shule ya Zitto, lakini nilitaka kuweka record sawasawa.
 
Kitila,

Si ungempa mswahili kwanza nafasi ya kutoa ushahidi wake na kujitetea kabla
ya kumhukumu kama ametenda kosa?

Kama akishindwa basi ndio JF management ichukue hatua ambazo wataona zitafaa.

Muhimu kwa JF wote ni kuwa waungwana na wakweli na kutumia kila juhudi ili tusichafue majina ya watu kwa facts ambazo tunajua sio ukweli au hatuna uhakika kama ni kweli.
 
MTZ,

Nakuunga mkono!! Mswahili hawezi kuandika habari bila kuwa na info. Ingawa hata kama zitto alifukuzwa chuo ZNZ sioni kama ni issue unless alifeli mitihani na kuwa discontinued!!!! DISCO ni dalili fulani za ukihyo wa mtu!!!
 
Baada ya kuwa safari nami nimerudi niweze kuungana nanyi tena na nasikia furaha kuwa hapa. Hata hivyo furaha yangu ilipata ukungu baada ya kusoma kile alichoandika Mswahili kumhusu mheshimiwa Zitto. Licha ya matatizo au udhaifu wowote au makosa yoyote aliyoyafanya Mhe. Zitto kumleta mama yake hapa na kumdhalilisha hivyo siyo uungwana hata chembe. Kama alichosema Mswahili kingekuwa na ukweli bado isingestahili kuzungumzwa hapa.

Nasikitika kuwa Mswahili kwa maneno yake anasema kana kwamba anajua kitu na baadhi ya watu wanampa hata benefit ya doubt. Bahati nzuri nawafahamu kina Zitto na ninamfahamu mama yake Mhe. Zitto. As a matter of fact nilikutana naye kwenye moja ya mikutano Dar wiki iliyopita. Niweke mambo fulani sawa.

Jina la Kabwe: Jina hilo si la upande wa mama yake bali upande wa baba yake. Jina kamili la mama yake Mhe. Zitto ni Shida Salum Bitariho.

Je mamake haji Dar? Kama nilivyosema hapo juu nimekutana na Mama Zitto wiki iliyopita. Mama Bitariho anakuja Dar karibu kila wiki kwani yeye ni mwenyekiti wa ushirikiano wa NGO pale Kigoma na anakuwa Dar mara nyingi tu. Sijui hili Mswahili kalipata wapi?

Je, Mhe. Zitto alifukuzwa UZ kwa ufuska?
Aliyosema Kitila ni hivyo ila nitaongeza jambo jingine. UZ walimnyima Zitto scholarship licha ya kuwa amepata scholarship pale. Nafasi hiyo akapewa kijana mwingine ambaye Zitto alimpita kwa alama, kwa vile kijana huyo anatoka Zanzibar. Hicho pia kilichangia uamuzi wa yeye kutafuta nafasi UDSM ambako alikubaliwa.

Inasikitisha kuona kuwa JF ni mahali pa kunyanyapaa wanawake hasa walio single na ambao kila kukicha wanajitahidi kuwalea vijana wao. Tumeona double standard na matusi anayorushiwa Amina na kina mama wengine hapa na watu wanayachukulia kama mzaha tu kejeli za kijiweni. Binafsi napenda kuchangia mengi labda nibadilishe jina na kuliweka jina la kiume ili niweze kuchangia bila ya jinsia yangu kuangaliwa. Ninachoomba ni kuwa Mswahili ambaye ni bingwa wa matusi na kashfa aombe radhi kwa kutudhalilisha kina mama kwa chuki zake binafsi! Kama wote mlioko hapa mlilelewa na baba na mama heri yenu, wengine hatukuwa na uchaguzi. Mimi mwenyewe nimelelewa na mama yangu tu baada ya baba kufariki vitani. Na mama yangu amejitahidi kunilea hadi hapo nilipo na milele nitamshukuru. Makosa yote ninayoyafanya sasa hivi siwezi hata chembe kumlaumu mama yangu!

Maandishi ya mswahili yamenitia kinyaa.
 
BI SENTI 50.
Huyu mama alifukuzwa chama cha walemavu Buguruni-Chawata na amefikishwa sana buguruni polisi file ziko pale sikutaka kwenda huko. na kama unasema simjui mwambie Zitto anipe ruksa nikaje wajihi wake au physical appearence yake ndio useme mimi simjui.
hiyo Ngo unayosema hata Dodoma anakuja nayo. ni ya ZITTO kamtumia mama yake kama mwenyekiti najua mengi ndugu yangu.
 
Mswahili nimekusikia vizuri. Je, jina la Kabwe ni la mama yake au la baba yake? Je, Mama Bitariho anakuja Dar au haji? Sina haja ya kumjadili mama wa watu, ulemavu siyo kitu mtu anaomba! Unaweza kuja na kila sifa na maelezo unayoyataka lakini kitendo chako cha kumshambulia mama wa watu ambaye hawezi kuja kujitetea hapa na hana sababu ya kufanya hivyo siyo cha kiungwana ni sawa na kumpiga mtu kwenye korodani wakati wa ndondi! Nakuomba umuache mama wa watu, kama unataka kuzungumza Zitto mzungumze lakini ya mama yake si ya kwake!!! uache ndugu na uone haya kuyaendeleza.
 
Haya ndio maajabu ya Jamboforums, wametukanwa marais wote wa Tanzania Nyerere, Mwinyi, Mkapa JK, mawaziri wakuu, mawaziri. Dini zimetukanwa mitume wameitwa malaya Mabalozi wameambiwa wamebaka na kila ya aina ya kashfa zimo humo. Hakukuwa na wito wa karipio, adhabu au kufungiwa.

Kwa bahati mbaya limemkuta kiongozi wa chama "M-badala" sitoshangaa mapendekezo yakafanyiwa kazi, why not after-all yametoka kwa kada Kitila.

Naomba nieleweke sitetei watu kutukanwa, kudhalilishwa nk bali consistency and equal treatment kwa watu wote bila kujali background za vyama vyao, makabila, dini, jimbo nk.

As we have broke the principles now the principles have found a way of breaking us....
 
Mswahili unakuwa kero; mwiba; kadhia; balaa; aibu na mambo yote unoweza yatamka yanayofanana na hayo. U mtu gani wewe usie na haya unathubutu kuongelea mambo ya mama za watu? wataka ya mama yako na dada zako nayo yawekwe hapa? we mwenyewe file lako chafu! hiyo kazi unofanya ya kupiga chabo maisha ya watu haifanani na umri wako, aibu kwako!
ustake watu wanze kuchimba data zako mana uwezo huo upo, au unafikiri wote unaofanya nao UT wanakusupport kwa uchafu huu? file lako tukilitaka tutalipata in no time, na uwe na hakika hatatupachikapachika ndani ya hoja, tutaifungulia thread yake nziima!
 
Masatu, sijui kuhusu wewe, lakini hilo la kumwingiza mama wa watu halina udhuru. Kama mswahili anataka kumtukana Mwanakijiji amtukane, kama anataka kumtukana Zitto amtukane, kama anataka kunitukana mimi na anitukane. Kwa sababu mimi nami ni mwanachama hapa JF. Kama huyo mama angempa sababu ya kumtukana au kufanya kitu ambacho kingemlazimisha atukanwe hapa hilo tungelijadili, viongozi wa dini ni fair game (matatizo mengi hapa duniani yametokana na imani hizo!), viongozi wa kisiasa (ni fair game), mabalozi ni fair game.. hata hivyo mama zao au watu wa familia zao ambao hawana hatia kwanini wawe sehemu ya mjadala? Mama Mkapa anajadilika kwani kuna issue, Mama Salma anajadilika kwani kuna issue...Regina wote wanazungumzika.

Hadi hivi sasa sijaona ni kwa nini mama Zitto amekuwa somo kisa cha makosa ya mwanae?
 
Masatu,
Nitukane mimi, sawa. Mtukane kiongozi, sawa. I draw the line inapofikia kwa mama yangu. Hapo nitakuvulia shati na kukunja misuli.
 
Masatu, sijui kuhusu wewe, lakini hilo la kumwingiza mama wa watu halina udhuru. Kama mswahili anataka kumtukana Mwanakijiji amtukane, kama anataka kumtukana Zitto amtukane, kama anataka kunitukana mimi na anitukane. Kwa sababu mimi nami ni mwanachama hapa JF. Kama huyo mama angempa sababu ya kumtukana au kufanya kitu ambacho kingemlazimisha atukanwe hapa hilo tungelijadili, viongozi wa dini ni fair game (matatizo mengi hapa duniani yametokana na imani hizo!), viongozi wa kisiasa (ni fair game), mabalozi ni fair game.. hata hivyo mama zao au watu wa familia zao ambao hawana hatia kwanini wawe sehemu ya mjadala? Mama Mkapa anajadilika kwani kuna issue, Mama Salma anajadilika kwani kuna issue...Regina wote wanazungumzika.

Hadi hivi sasa sijaona ni kwa nini mama Zitto amekuwa somo kisa cha makosa ya mwanae?

Bi Centi 50

Hapo sasa unapotoka! kumbuka suala hapa ni watu kutukanwa, kudhalilishwa na kuzushiwa mambo yasiyo ya kweli. Kwa vigezo vyovyote vile na kwa mtu yeyote hilo haliwezi kuwa fair game. Hilo ni kosa na litaendelea kuwa kosa, kumbuka hao wote uliwataja wana watoto, wajukuu, vilembwe nk kwa hiyo in away kuwatukana hao uliowataja hapo juu utakuwa unatukana either mama/baba wa mtu.

Kwa kifupi jambo hili halifai kwa wote na ninaposema wote nina maana bila kujali itikadi za vyama, kabila nk
 
Masatu,
Nitukane mimi, sawa. Mtukane kiongozi, sawa. I draw the line inapofikia kwa mama yangu. Hapo nitakuvulia shati na kukunja misuli.

Kwanini nikutukane in the 1st place?
 
Masatu,
Nitukane mimi, sawa. Mtukane kiongozi, sawa. I draw the line inapofikia kwa mama yangu. Hapo nitakuvulia shati na kukunja misuli.

Nikikutukana wewe mwanao/binti yako atakasirika atasema nitokane mimi sio baba yangu!... jawabu ni kuacha matusi alltogether
 
kwa hiyo wewe unafikiri vipi kuhusu kitendo cha Mswahili kumuingiza mama Zitto kwenye suala lisilohusika na kujaribu kumzulia mambo yasiyo ya kweli, ati jina la Zitto ni kutoka kwa mamake na ya kuwa mama yule hakanyagi Dar?!
 
kwa hiyo wewe unafikiri vipi kuhusu kitendo cha Mswahili kumuingiza mama Zitto kwenye suala lisilohusika na kujaribu kumzulia mambo yasiyo ya kweli, ati jina la Zitto ni kutoka kwa mamake na ya kuwa mama yule hakanyagi Dar?!

Comments reserved!
 
Haya ndio maajabu ya Jamboforums, wametukanwa marais wote wa Tanzania Nyerere, Mwinyi, Mkapa JK, mawaziri wakuu, mawaziri. Dini zimetukanwa mitume wameitwa malaya Mabalozi wameambiwa wamebaka na kila ya aina ya kashfa zimo humo. Hakukuwa na wito wa karipio, adhabu au kufungiwa.

Kwa bahati mbaya limemkuta kiongozi wa chama "M-badala" sitoshangaa mapendekezo yakafanyiwa kazi, why not after-all yametoka kwa kada Kitila.

Naomba nieleweke sitetei watu kutukanwa, kudhalilishwa nk bali consistency and equal treatment kwa watu wote bila kujali background za vyama vyao, makabila, dini, jimbo nk.

As we have broke the principles now the principles have found a way of breaking us....

Please tuwe wakweli, ni wapi hapo ambapo wanaCHADEMA tumewahi kuwafumshia viongozi au mtu yeyote matusi. Waliojitambulisha kuwa ni wana CHADEMA katika forum hii tunajulikana. Mtu asimame hapa aniwekee post kutoka kwa mwana CHADEMA ikimfurumshia mtu matusi. Please evidence. Au mtu asimame hapa anipe parallel ya mwana-CHADEMA aina ya Mswahili.

What I know CHADEMA members at least in this forum have always tried their level best to be constructively and objectively critical. Sisi ni mfano wa watu wanaopenda na wanaojua umuhimu wa debate. Hatuoni taabu wala kigugumizi kupingana na kuzodoana sisi kwa sisi hata katika forum hii. Lakini hatuamini katika matusi.

My message is, inawezekana kubishana na kutofautiana bila kuporomosheana matusi. We should learn to argue without shouting and swearing, it is possible!
 
Kitila kuna watu ambao bila kuongeza matusi au kashfa hoja zao haziwezi kusikika. Wanatumia matusi na kashfa ili kuzipa nguvu hoja zao. Kumbe uzuri wa hoja unatokana na nguvu zake yenyewe. Hata hivyo somo hilo kwa wengine bado ni gumu.
 
Back
Top Bottom