Mzee MMJ,
Nimeshitushwa kuhusu unafiki wako wa kuwatafuta kuwahoji viongozi wa CCM, na kulia kuhusu wanafunzi, kumbe viongozi wa Chadema huwagusi ila unawatetea?
Unakumbuka tulipokuambia kuwa hatuhitaji mahojiano kati yako na Freeman, kwa sababu wewe sasa umekuwa compromise? Sasa kama hizi ndio standard zenyewe hapa forum, then tunafanya nini? Sasa unashangaa kina Msolla wanavyokukatia simu?
What a joke? Bravo kwa wale wote mnao-raise hell keep it up, Mtanzania, Masatu, endeleeni kumkoma nyani giladi, asiogopwe mtu hapa, eboo!
Mheshimiwa Zitto, it is about time sasa ukajibu maswali kuhusu kashfa yako na Amina Chifupa, mbunge mwenzio na mke wa mwananchi kama sisi unaotuwawakilisha bungeni, I mean sasa tutawatumaje wake zetu ofisini kwako tukiwa na shida zinazohitaji msaada wako kama mbunge?
Kwa wale mnaotaka kutubabaisha na maneno ya ujanja ujanja, tunasema sisi sio watoto wadogo hapa, ni haki yetu wananchi kujua kilichotokea kati ya waheshimiwa Zitto, na Amina Chifupa, kama ilivyo haki yake, Zitto hapa kuwatukana viongozi wazembe wa serikali na tunamuunga mkono mara nyingi, kama hawezi kujibu basi aache kabisaaa kuwagusa viongozi wa serikali na siasa kwa ujumla, kwa sababu hana moral ground ya kumkosoa kiongozi yoyote wa serikali na hasa wanaoingia bungeni kama yeye!
Kwa mara ya kwanza I am ashamed kuwa member wa hii forum, maana huu ni utoto na kumfukuza mwenda wazimu tukiwa uchi, mheshimiwa Zitto, rudisha heshima ya hii forum kwa kujibu na kutueleza ukweli wa kilichotokea mkuu, sisi wote hapa ni watu wazima, hakuna mtoto mdogo hapa wa kuambiwa habari za uroda, then hata Richmond pia ni uroda bro if that is the case of uroda,
Wazee tuacheni unafiki hapa, sio mahali pake, mizimu ya BCS itatushitaki ndio maana kunaanza balaa za mitambo hapa, acheni utoto mambo yawekwe hadharani hapa, lakini tuisgeuzane kuwa watoto hapa, na sisi ni watu wazima tena wenye akili timamu za kuona uozo wa viongozi wetu kwa makini, sasa itakuwaje tunataka kupromote usaniii tunaoukataa kutoka kwa serikali yetu?
Ndio maana ninasema kuwa sisi wananchi hatuna vision wala busara, na pia ni wasanii wa kutupwa?