Wanawake wenzangu mnawezaje kumsamehe a cheating husband?

"Cheating" ni kama ndege imetua, usibakie hapo kujiuliza na kusikitika kwanini imetua hapo na korona.

Jaribu kutafuta ilipoondokea, Je ilikuwaje kuwaje mpaka iondoke huko na kuja na korona kwako? Labda itasaidia kujua chanzo na kudhibiti ndege nyingine nyingi zisije na korona na magonjwa mengine kwako.

Kushupaza shingo hapo kuwa tatizo liko kwa mmoja haikusaidii saana.

Sent from my HUAWEI LUA-L21 using JamiiForums mobile app
 
Pole sana nyakoo unachopitia ni kitu kigumu sana, mapenzi ni imani sasa kama imani yako imeshuka kiasi cha kumuona huyo mwanaume kama jirani ni hatari sana kwenu wote na kwa ndoa yenu.
Kama kweli mumeo anaona alikosea na inamuumiza nafsi basi atafanya anachoweza kukusaidia kupona katika maumivu uliyonayo
Unapoomba ushauri utapokea mengi sana ila suala la kwamba na wewe uanzishe mahusiano mimi siafiki na naamini hiyo haitakua suluhu kamwe kwani yatakua ni maamuzi ya kukurupuka kwa nia ya kulipiza kisasi na sio upendo.
Kuomba Mungu sana, fanya kazi zako kwa bidii, fanya vitu vinavyokupa furaha, ongeza muda wa kuonyesha upendo kwa wanaokupenda haswa watoto..... jitahidi sana usiwe mpweke maana hiyo inaweza kukuingiza kwenye mahusiano mabovu kuliko huyo mume ambae tayari mna watoto.
 
Ni bora mara 100 mtu kama amekuchoka avunje ndoa tu kuliko kujitia anakupenda saana kumbe anakupaka mafuta kwa mgongo wa chupa
Bibie kwa mwanamme hupaswi kutafsiri yeye kuchepuka kuwa ni kwa kuwa hakupendi uko wrong aisee. Anaweza akawa na mchepuko ila bado akipata taarifa na we una mahusiano mengine ukawa msala na usishangae hata ukabondwa au akakurudisha kwenu kwa muda. Kiukweli sijui tumeumbwaje.
 
Na wewe chepuka tu hapo kilichobaki nikulea watoto cheating haisameheki kabisa hasa mtu uliye mwamini, Hawa viumbe huua nyege za wake zao. Nakuhurumia maskini kiukweli na wewe chepuka tu ngoma droo wallah
A very destructive comment IMO, very destructive. Ingekuwa hivi ndoa zingebaki chache sana. Njia salama ni kuishi na kusameheana, ikishindikana basi talaka. Kulipiza kisasi sio maisha ya wanandoa.
 
Bibie kwa mwanamme hupaswi kutafsiri yeye kuchepuka kuwa ni kwa kuwa hakupendi uko wrong aisee. Anaweza akawa na mchepuko ila bado akipata taarifa na we una mahusiano mengine ukawa msala na usishangae hata ukabondwa au akakurudisha kwenu kwa muda. Kiukweli sijui tumeumbwaje.
Well kila mtu na jinsi anavyopokea, mimi natafsiri hivyo
 
A very destructive comment IMO, very destructive. Ingekuwa hivi ndoa zingebaki chache sana. Njia salama ni kuishi na kusameheana, ikishindikana basi talaka. Kulipiza kisasi sio maisha ya wanandoa.
Hata anayesoma ushauri naamini ni mtu mzima na akili zake, atachukua linalomfaa na kuacha lisilomfaa. Hebu tuache kila mtu atoe ushauri kulingana na kile anachofikiria
 
A wapi vile nimekiri hadharani wengi tu hi cheats kwa kushindana and I know couples zinashindana na hawajaachana kabisa. Cheating haisahauliki abadani na huua upendo
 
Mwanaume ku cheat nje ya ndoa hamanishi kuwa hakupendi, anakupenda Sana Tena Sana, Ila hiyo Ni kawaida kwa wanaume wote. Usithubutu kuvunja ndoa yako kisa Hilo Jambo utajuta badae.
Wabongo bhana, uliwahi fanya tafiti ukabaini wanaume wote wana cheat?

Unaishi kwa kukariri.

Kama unacheat wewe usidhani kila mwanaume yupo hivyo.

Wapo wanatosheka na mmoja na hawatoki nje kamwe.
 
Hata anayesoma ushauri naamini ni mtu mzima na akili zake, atachukua linalomfaa na kuacha lisilomfaa. Hebu tuache kila mtu atoe ushauri kulingana na kile anachofikiria
Na mimi nimetoa maoni yangu kama wengine, ku-object ushauri wa mwingine sio kosa, ndio maana option ya "quote" ikawekwa. cariha anaweza kuja na maoni yake ku-crash ya kwangu. Tuvumiliane katika hili.
 
A very destructive comment IMO, very destructive. Ingekuwa hivi ndoa zingebaki chache sana. Njia salama ni kuishi na kusameheana, ikishindikana basi talaka. Kulipiza kisasi sio maisha ya wanandoa.
Mbona nyie hamsamehi
 
Ni bora mara 100 mtu kama amekuchoka avunje ndoa tu kuliko kujitia anakupenda saana kumbe anakupaka mafuta kwa mgongo wa chupa

Khantwe Wana mambo mengi hawa bunadamu wenzetu wanayofata huko mengine hawawezi hata kuyahadithia. Laiti mkiwa kwenye ndoa ubongo na moyo vingekua transparent wenza wakaweza kusoma matendo wanayofanya huko wanakochepukia wengi tungekufa kwa cardiac attack.
 
Na mimi nimetoa maoni yangu kama wengine, ku-object ushauri wa mwingine sio kosa, ndio maana option ya "quote" ikawekwa. cariha anaweza kuja na maoni yake ku-crash ya kwangu. Tuvumiliane katika hili.
Sawa
 
A wapi vile nimekiri hadharani wengi tu hi cheats kwa kushindana and I know couples zinashindana na hawajaachana kabisa. Cheating haisahauliki abadani na huua upendo
Basi kama hausahauliki talaka inaweza kuwa best solution.
 
Back
Top Bottom