Wanawake wenzangu kujeni tutete kidogo!

Wanawake wenzangu kujeni tutete kidogo!

Aiseee uko kama mimi yani hata nikute mnasifiana kuhusu game yenu yani siwezi shika simu nikupigie kukuuliza.Ila kuna wadada wamejaaliwa midomo yani wasione japo message tu ya kusalimiana basi utapigiwa simu na msg za vitisho juu hadi unabaki umeduwaa tu
Hahahaaa unachambwa kichambo matata!!
Unahangaika kugombana na huyu mwenzio anahamia kwa mwingine, sasa utatukana wangapi!!
 
Eeh unashangaa zinaanza na zile, unakula nini leo, umevaaje weeeee

Hahaha!, acha tu. And then mwisho zinaanza dose, lazima muongee mara 3 kwa siku ku make amekula na yuko okay kama hakuna wa kukatisha uhusiano wa hivyo mapema inahitaji maturity.

Kuepuka hayo yote, nimem salute espy
 
Hahahaaa unachambwa kichapo matata!!
Unahangaika kugombana na huyu mwenzio anahamia kwa mwingine, sasa utatukana wangapi!!
Na michepuko huwa ina ngebe jamani, utadhani inaendaga kusomea ngebe. Na inakuvuruga kweli kweli hadi unapata kichaa cha ndoa
 
Habari za jumapili wapendwa!

Kuna tukio lilinitokea na through that nikapata funzo kubwa tu.

Nina rafiki yangu(class mate) tulikuwa marafiki tangu shule, ila baada ya kuhitimu tukapotezana na hatukuwa na mawasiliano. Tukaja kuonana tena baada ya kama miaka 9 akiwa katika mchakato wa kuoa, urafiki ukarudi na tukawa na mawasilianao ya karibu tu. Baada ya kufunga ndoa nilianza kuweka kadistance maana mazoea sana na waume za watu sio mazuri.

Kuna kipindi alikuwa na wazo fulani kuhusu biashara na alinishirikisha tukashauriana vizuri na biashara ikafunguliwa na ikawa ikienda vyema.
Alipenda kunipa updates za hiyo biashara, na baadae akamuachia mkewe(wifi) aiendeshe then akawa na wazo lingine la project nyingine kubwa zaidi ambayo ingekwenda vizuri alikuwa na plan ya kuacha kazi ya kuajiriwa na kuiendesha mwenyewe.

Kutokana na kunishirikisha kwa karibu sana mambo yake, nikagundua mazoea yanakolea zaidi, nikaanza kumpotezea nikitambua yeye mtu mzima ataelewa tu. Alianza kulalamika sana maana mara nyingi nilikuwa sipokei call zake wala kujibu text zake, ikabidi nimwambie tu ukweli kuwa nisingependa hayo mawasiliano ya karibu namna hiyo. Japo kwa uchungu alinielewa ila aliomba sana nisipoteze mawasiliano nae kabisa.

Baada ya kama mwezi hivi nilipokea simu kutoka kwa mkewe akilalamika sana na kunilaumu akihisi nina mahusiano na mumewe, ilibidi nimtulize munkari then tulonge taratibu kiutu uzima.
Alilalamika kuwa kuna mambo mengi ambayo emekuta ktk mawasiliano baina yangu na mumewe ambayo yeye binafsi hayajui na hajawahi kushirikishwa. Hapo sasa ndio ikabidi niongee nae na kumuuliza vizuri kuhusu mawasiliano baina yake na mumewe, nikagundua sio supportive kwa mumewe na huwa hayaamini mawazo ya mumewe.

Sasa nilichojifunza ni kwamba mwanaume anapenda sana kusikilizwa,kuheshimiwa na kuaminiwa. Anaweza akaja na wazo lake ambalo ukiliangalia harakaharaka unaona kabisa hapa hakuna kitu, sasa sisi wanawake huwa tuna tabia ya kuwakatisha tamaa, unaweza kuguna mguno classic au kucheka kabisa kwa dharau kumuonyesha kuwa wazo lake ni la hovyo kabisa, ilihali hata wazo mbadala pia hauna.

Mpe nafasi ya kumsikiliza, then kama atakuomba ushauri mpe kama hauna bora umshauri atafute ushauri pahali sahihi, mtie moyo na umuamini kuwa anaweza, hata kama alikuwa na hofu na wazo lake kwa kumtia moyo na kumuamini itampa ari ya kulifanyia kazi vizuri zaidi.

Wakati mwingine tunaweza kuwa tunazima ndoto za akina Mengi wengi tu bila kujua kuwa kwa support yetu wangefika mbali sana. Hata akishindwa kwa mara ya kwanza mtie moyo na mwambie ajaribu tena na tena na atafanikiwa. Sio ndio unaanza na maneno kama "nilijua tu usingefika kokote"!!

Kama ulimuamini na kumchagua yeye kati ya wengi,basi hauna budi kuyaamini mawazo yake pia. Kuwa msaidizi ambae kila wakati atajivunia kuwa nae, hata akikengeuka akikumbuka mazuri yako mengi hakika atajirudi tu.
Nadhani umezungumzia upande mwingine wa mapenzi ambao wengi huwa hawauoni!
Ndoa haiishii kwenye kitanda tu!
Ndoa ina eneo jingine la uwekezaji - kwanza watoto (familia) na pia uzalishaji mali.
ukiwa mzuri kitandani/kwenye mahaba bila ya kuwa na mchango kwenye uzalishaji ni tatizo, na kinyume chake pia yaani kuwa mzalishaji bila ya kuinvest kwenye mahaba nako ni tatizo!
wake na waume tujifunzeni kupitia somo hili!
 
Blessed darling, umesaidia ndoa ya mtu. Hiyo opportunity ingempata mtu mwingine weeee
Haya mambo wanawake tunaweza kuyakomesha, maana ukimkataa hakubaki, sasa why uharibu kwa mwenzio wakati kesho yako huijui!!
 
Hahaha!, acha tu. And then mwisho zinaanza dose, lazima muongee mara 3 kwa siku ku make amekula na yuko okay kama hakuna wa kukatisha uhusiano wa hivyo mapema inahitaji maturity.

Kuepuka hayo yote, nimem salute espy
Sasa ukute Ke naye yupo lonely, khaa mbona perfect chance to cure her loneliness. Bi mkubwa hapo kacheza kama Ronaldo (atanunaje)
 
Hahha sasa unakuta huko unakopiga simu ndo mwenzako mchambaji zaidi, unachambwa wimawima na baby anaendelea naye
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Eti unachambwa wima wima, hadi kiranga choote kinakuisha, kuna watu walishajichoka jamani!!
 
Hahahaaa hawajawahi kunifanya chochote.

Kwani vipi? Unaona mimi ni anti-wanawake au?

Kwani Kisura siyo mwanamke? Si nimesema yeye sapoti yake inatosha....au hujaona?
Mmmmh!! Haya bwana.
Siku ukimuumba huyo wifi yangu naomba taarifa tafadhali.
 
Hahaha!, acha tu. And then mwisho zinaanza dose, lazima muongee mara 3 kwa siku ku make amekula na yuko okay kama hakuna wa kukatisha uhusiano wa hivyo mapema inahitaji maturity.

Kuepuka hayo yote, nimem salute espy
Mara mbona kama hauko sawa leo just tell me am here for you!! Ohoooooo
[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Eti unachambwa wima wima, hadi kiranga choote kinakuisha, kuna watu walishajichoka jamani!!
Kuna this friend of mine, aligundua mumewe anachepuka akautafuta huo mchepuko. Afu worse enough mumewe ni one of those idiots ambao wanatoa siri za wake zao kwa michepuko. Kichambo alichokula + kumwagiwa siri zake, presha ilipanda hapo hapo
 
Na michepuko huwa ina ngebe jamani, utadhani inaendaga kusomea ngebe. Na inakuvuruga kweli kweli hadi unapata kichaa cha ndoa
Yaani anakuchamba kama wewe ndio umetembea na mumewe, akili lazima zikurudi.
 
Nadhani umezungumzia upande mwingine wa mapenzi ambao wengi huwa hawauoni!
Ndoa haiishii kwenye kitanda tu!
Ndoa ina eneo jingine la uwekezaji - kwanza watoto (familia) na pia uzalishaji mali.
ukiwa mzuri kitandani/kwenye mahaba bila ya kuwa na mchango kwenye uzalishaji ni tatizo, na kinyume chake pia yaani kuwa mzalishaji bila ya kuinvest kwenye mahaba nako ni tatizo!
wake na waume tujifunzeni kupitia somo hili!
Huo upande mwingine wa mahaba huwa unaongelewa sanaaaaa, huu upande kama tumeusahau hivi wakati nao ni muhimili muhimu tu ktk familia.
 
Sasa ukute Ke naye yupo lonely, khaa mbona perfect chance to cure her loneliness. Bi mkubwa hapo kacheza kama Ronaldo (atanunaje)
Dota hivi muda wa kulala haujafika tu!! Kitoto kinaongea hiki, Nalendwa naomba umchukue kwa muda tafadhali. Angalau siku moja tu.
 
Nilichojifunza huyo jamaa ulikuwa na hisia nae za kimapenzi kdg ...ila ushaur nzuri
 
Back
Top Bottom