Wanawake wenzangu kujeni tutete kidogo!

Wanawake wenzangu kujeni tutete kidogo!

Habari za jumapili wapendwa!

Kuna tukio lilinitokea na through that nikapata funzo kubwa tu.

Nina rafiki yangu(class mate) tulikuwa marafiki tangu shule, ila baada ya kuhitimu tukapotezana na hatukuwa na mawasiliano. Tukaja kuonana tena baada ya kama miaka 9 akiwa katika mchakato wa kuoa, urafiki ukarudi na tukawa na mawasilianao ya karibu tu. Baada ya kufunga ndoa nilianza kuweka kadistance maana mazoea sana na waume za watu sio mazuri.

Kuna kipindi alikuwa na wazo fulani kuhusu biashara na alinishirikisha tukashauriana vizuri na biashara ikafunguliwa na ikawa ikienda vyema.
Alipenda kunipa updates za hiyo biashara, na baadae akamuachia mkewe(wifi) aiendeshe then akawa na wazo lingine la project nyingine kubwa zaidi ambayo ingekwenda vizuri alikuwa na plan ya kuacha kazi ya kuajiriwa na kuiendesha mwenyewe.

Kutokana na kunishirikisha kwa karibu sana mambo yake, nikagundua mazoea yanakolea zaidi, nikaanza kumpotezea nikitambua yeye mtu mzima ataelewa tu. Alianza kulalamika sana maana mara nyingi nilikuwa sipokei call zake wala kujibu text zake, ikabidi nimwambie tu ukweli kuwa nisingependa hayo mawasiliano ya karibu namna hiyo. Japo kwa uchungu alinielewa ila aliomba sana nisipoteze mawasiliano nae kabisa.

Baada ya kama mwezi hivi nilipokea simu kutoka kwa mkewe akilalamika sana na kunilaumu akihisi nina mahusiano na mumewe, ilibidi nimtulize munkari then tulonge taratibu kiutu uzima.
Alilalamika kuwa kuna mambo mengi ambayo emekuta ktk mawasiliano baina yangu na mumewe ambayo yeye binafsi hayajui na hajawahi kushirikishwa. Hapo sasa ndio ikabidi niongee nae na kumuuliza vizuri kuhusu mawasiliano baina yake na mumewe, nikagundua sio supportive kwa mumewe na huwa hayaamini mawazo ya mumewe.

Sasa nilichojifunza ni kwamba mwanaume anapenda sana kusikilizwa,kuheshimiwa na kuaminiwa. Anaweza akaja na wazo lake ambalo ukiliangalia harakaharaka unaona kabisa hapa hakuna kitu, sasa sisi wanawake huwa tuna tabia ya kuwakatisha tamaa, unaweza kuguna mguno classic au kucheka kabisa kwa dharau kumuonyesha kuwa wazo lake ni la hovyo kabisa, ilihali hata wazo mbadala pia hauna.

Mpe nafasi ya kumsikiliza, then kama atakuomba ushauri mpe kama hauna bora umshauri atafute ushauri pahali sahihi, mtie moyo na umuamini kuwa anaweza, hata kama alikuwa na hofu na wazo lake kwa kumtia moyo na kumuamini itampa ari ya kulifanyia kazi vizuri zaidi.

Wakati mwingine tunaweza kuwa tunazima ndoto za akina Mengi wengi tu bila kujua kuwa kwa support yetu wangefika mbali sana. Hata akishindwa kwa mara ya kwanza mtie moyo na mwambie ajaribu tena na tena na atafanikiwa. Sio ndio unaanza na maneno kama "nilijua tu usingefika kokote"!!

Kama ulimuamini na kumchagua yeye kati ya wengi,basi hauna budi kuyaamini mawazo yake pia. Kuwa msaidizi ambae kila wakati atajivunia kuwa nae, hata akikengeuka akikumbuka mazuri yako mengi hakika atajirudi tu.

Nakutakia kila la heri katika ndoa yako ila ukipata matatizo (hayaepukiki) nakuomba unitafute. Wanawake kama wewe ni wachache sana.
 
Mmmh I agree with you on this. Unapofunga ndoa na mtu, jua huyo mtu ni mume, ni baba, kaka, shemeji, mjomba, rafiki kwako na kwa watu wengine etc, at one point kuna watu watamuhitaji na yeye kuna muda atahitaji watu wengine.

I know unaweza ukawa good, but sometimes you can't be good in everything. Kama kuna vitu ambavyo najua me siwezi kumsaidia as much as anavyohitaji, I don't mind akitafuta msaada kwa mtu mwingine trustworthy. Sema ndo iwe ananishirikisha na ananipa updates inaendaje and if I can help in my own lil way, basi inakuwa pouwah zaidi. Honestly hakuna mtu atakayependa kugundua mumewe anamshirikisha mtu mwingine mambo yake, afu yeye mke haambiwi unless huyo mke ndo awe wa kukatisha tamaa. Unampa tu taarifa unamuacha zake
Ni kweli kabisa, lakini katika hii case ndoa ilikuwa changa na mke angeweza kuyamaliza na mume wake bila kuleta taharuki nje. Fikiria akiwa na shida na Espy sasa mke atajifikiria jinsi ya kumuanza kwani ameshalikoroga. Ukiwa kwenye ndoa inabidi uwe mwanadiplomasia, na psychologist wewe mwenyewe.
 
[emoji122] nimependa sana hapo pa kutafuta msaada kwa mtu mwingine 'trustworthy'
 
Bi mkubwa kuna a point umeitaja kuhusu friendship na nimekuelewa. Wengi wetu soon after getting married tunawish kucut off some old ties na jamaa/rafiki. But at some point I don't think kama it's good, coz for many years you have been using your friends to sustain, afu leo ndo unataka kuwatema mazima kisa you are married, nah. I understand kuna vitu vitapungua kidogo, maybe priorities etc, but isiwe reason ya kuwakacha Marafiki zetu, tena hii ni commonly between girls. Kila mmoja anamuona mwenzie lakini they don't fit in the same category, kumbe still kuna mambo mengi tu tunayoweza kushirikishana hata kama hayahusu ndoa Coz there is life apart from marriage

Bi mkubwa i guess uncle aliona possibly in the area of business unaweza ukamsaidia zaidi ya mkewe, was it wrong? Sio kila mtu ni mzuri kwenye biashara, I think mngesaidiana tu as long as you don't cross your limit, kuna a a certain distance that has to be maintained honestly.

Hiyo ya mke kumvunja moyo mume ni hatari kusema za ukweli. Kuna watu are naturally dream killers, Yani ukimshirikisha tu jambo lako atakukatisha tamaa huyo hadi ujute na unaweza kuacha kabisa kufanya jambo lako. Ndo unakuta mume anamtenga tu mkewe kwenye mambo yake afu akija kujua anajiliza, lia tu. Kumtia moyo mwenzio si hutaki, ngoja afanye tu vitu vyake kimya kimya ingawa ni vyema kuwa open na projects unazofanya, anything can happen anytime afu vitu vyako vikapotea bure
 
Mimi huwa najiamini sana na mawazo na fikra zangu.

Huwa nipo vizuri sana katika kuweka mipango na kufanya maamuzi.

Sijawahi kabisa kuhitaji msaada wa kimawazo toka kwa mwanamke.
Ngabu bwana!!
 
Ni kweli kabisa, lakini katika hii case ndoa ilikuwa changa na mke angeweza kuyamaliza na mume wake bila kuleta taharuki nje. Fikiria akiwa na shida na Espy sasa mke atajifikiria jinsi ya kumuanza kwani ameshalikoroga. Ukiwa kwenye ndoa inabidi uwe mwanadiplomasia, na psychologist wewe mwenyewe.
Hekima ni kitu cha msingi sana, unfortunately sio kila mtu amepewa. Me kwanza kuanza kumpigia mtu simu kumtuhumu anatembea na mtu wangu aiseeee
 
Mimi bwana nipo tofauti, hasa kwenye mambo ya kutake risk za biashara huwa namuambia mchumba wangu nataka kufanya hivi naomba usinishauri tofauti. Mpaka nakwambia wewe ujue nishaomba ushauri sana huko nje mpaka nimefikia uamuzi huu naomba support yako sio kunikwamisha.
Nilimuambia hivyo wakati nataka kuacha kazi....mimi huwa sisikilizi negatives ninapoamini pana njia ya kutoboa. Japo mara nyingi amenisaidia maamuzi mengi pia....huwa simtegemei sana. Zaidi akili yangu.
 
Fact, lkn kuna baadhi ya wanaume hawashirikishi kabisa wake zao kwenye mambo yao anahiyari ndg zake au rafiki. Anaona kumshirikisha mwanamke kwenye shughuli zake ni kujishusha coz atakua anajua nn kimeingia kwa siku na hapo atakua hana njia ya kumnyima hela akiwa anahitaji.
Kama mumeo hakushirikishi basi utambue haujampa sababu ya kukushirikisha, yawezekana alikushirikisha mambo fulani fulani haukuonyesha ushirikiano, au ulimkatisha tamaa, kwahiyo anaamua kushirikisha wale anaoona watamuelewa.
 
Mmmh I agree with you on this. Unapofunga ndoa na mtu, jua huyo mtu ni mume, ni baba, kaka, shemeji, mjomba, rafiki kwako na kwa watu wengine etc, at one point kuna watu watamuhitaji na yeye kuna muda atahitaji watu wengine.

I know unaweza ukawa good, but sometimes you can't be good in everything. Kama kuna vitu ambavyo najua me siwezi kumsaidia as much as anavyohitaji, I don't mind akitafuta msaada kwa mtu mwingine trustworthy. Sema ndo iwe ananishirikisha na ananipa updates inaendaje and if I can help in my own lil way, basi inakuwa pouwah zaidi. Honestly hakuna mtu atakayependa kugundua mumewe anamshirikisha mtu mwingine mambo yake, afu yeye mke haambiwi unless huyo mke ndo awe wa kukatisha tamaa. Unampa tu taarifa unamuacha zake
Kweli kabisa.
 
Back
Top Bottom