Joseverest
JF-Expert Member
- Sep 25, 2013
- 53,263
- 72,442
Aiseeh kumbe kuna watu wanakaa chini na kuandika vizuri hivi
Mimi huwa najiamini sana na mawazo na fikra zangu.
Huwa nipo vizuri sana katika kuweka mipango na kufanya maamuzi.
Sijawahi kabisa kuhitaji msaada wa kimawazo toka kwa mwanamke.
espy akuje ajibu hapa, could be..could not be!!Angekuwa naye ana mme mimi ningemwelewa vizuri lakini kama single hapo hapana halafu hizo sms alizokuwa akichart na huyo bwana hakutaja ni zipi yawezekana zilikuwa tata ndiyo maana mke akawa na kiulizo huyo mke sio mjinga kiasi hicho akute biashara partner halafu yy atibue hapana isije dada anajitetea
And...???????Hakuna binadamu mkamilifu hapa Duniani...
ha ha ha ha...Kama kunichunia umeambiwa ni dawa jitahidi umalizie dozi ili ugonjwa ukuishe
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]espy akuje ajibu hapa, could be..could not be!!
Hizo sms zaweza kuwa na utata, hakunaga chattings za me vs ke bila kuingiza michombezo. I've been there, I've flirted so much with ladies, I know!!
espy, hamkuwahi hata kutaniana na jamaa kuhusu migegedo, relationship, kwamba akikupata engo fulani ataku.....?[emoji12]
Sawa, ila sio kila mtu anahitaji mawazo ya mwanamke kufanya issues zake.Hakuna binadamu mkamilifu hapa Duniani...
Teh teh, kiongozi huyu jamaa alitaka experience ya espy! Lazima kuna kitu alitaka, alitumia mbinu ya biashara ili kumlengesha kimwana....Yaani katika rafiki zake wote waume kwa wake akuchague wewe espy tena mna ka historia?! Au anakujua ni mfanyabiashara mzuri?! Vinginevyo kuna namna....
Hii story iko edited.....hadi mke kumtafuta espy kuna kitu kakiona sio bure.Teh teh, kiongozi huyu jamaa alitaka experience ya espy! Lazima kuna kitu alitaka, alitumia mbinu ya biashara ili kumlengesha kimwana....
Tena na vi-sms vya michombezo, in the long run alikuwa apige kitu na biashara ingefia hapo hapo..
Mkuu, mimi sikutaka kuingiza ideologies zangu baada ya kuona mrengo wa wachangiaji wengi.Hii story iko edited.....hadi mke kumtafuta espy kuna kitu kakiona sio bure.
Wacha we!!Yaani katika rafiki zake wote waume kwa wake akuchague wewe espy tena mna ka historia?! Au anakujua ni mfanyabiashara mzuri?! Vinginevyo kuna namna....
Teh teh, kiongozi huyu jamaa alitaka experience ya espy! Lazima kuna kitu alitaka, alitumia mbinu ya biashara ili kumlengesha kimwana....
Tena na vi-sms vya michombezo, in the long run alikuwa apige kitu na biashara ingefia hapo hapo..
[emoji101] [emoji101] [emoji101] [emoji101]Hii story iko edited.....hadi mke kumtafuta espy kuna kitu kakiona sio bure.
Hakuwahi kumchafua mkewe hata!! Ni those kind of men ambae hawezi kumuongelea vibaya mkewe hata iweje. Hilo nililijua kupitia mke mwenyewe ktk chit chating.Mkuu, mimi sikutaka kuingiza ideologies zangu baada ya kuona mrengo wa wachangiaji wengi.
Kuna kitu dada zetu hawajui kuhusu wanaume, hasa wanapotafuta kitu. Mwanaume alitaka amlengeshe mdada, anaweza kutumia mbinu za ajabu, hata kumchafua mke wake ili mradi tu malengo yatimie.
Inawezekana kabisa jamaa ana washauri wazuri tu, akiwemo mkewe..lakini alimtaka huyu 'long time friend', akaona ni ngumu kumpata ndio akaja na mbinu za biashara.
Story ipo edited[emoji12]
Nimekuelewa sana aunt, najua ndoa pia inaanzia kwenye mahusiano yakikomaa ndo hatua ya ndoa. Nina mwanaume nnampenda huu ni mwaka wa pili hadi mtoto tunae anaelekea kujaza mwaka, yy amekuwa akinitia moyo hasa ktk bidii niyonayo maana tofauti na kufanya kazi yakuajiriwa najishughulisha na biashara ndgndg, lkn mm nimekuwa mckilizaji wa ndoto zake tu yy amesoma hajapata kazi lkn nilivyomsoma anaamini ktk kufanya kazi ya kuajiriwa Kwa suala lakujiajiri mmmh bado sioni mwitikio. Aunt nishauri mtu wa hivi ntamsapot vipi? Wkt Kwa suala LA kwenda Kwa wazazi anaona ni mapema kisingizio hana kazi wkt huo nawasiliana na mama yake kwamba kama familia wapo tayar kufuata taratibu tuoane lkn kijana wao yaani huyu baba mtoto ndo anawakwamisha niliumia sana na sikumwambia chchote. Hivi juzi kaja na wazo lakutaka kuanzisha biashara ya nguo za kike Kwa mtaji wa zaidi ya mill3 nilimwitikia ni nzuri lkn kiukweli sina mpango wakumpa hata elfu kumi yngu maana hata simuelewi mm naishi Kwa imani tu sasa. Nishauri mtu wa hivi namsapot nn na vipi?Habari za jumapili wapendwa!
Kuna tukio lilinitokea na through that nikapata funzo kubwa tu.
Nina rafiki yangu(class mate) tulikuwa marafiki tangu shule, ila baada ya kuhitimu tukapotezana na hatukuwa na mawasiliano. Tukaja kuonana tena baada ya kama miaka 9 akiwa katika mchakato wa kuoa, urafiki ukarudi na tukawa na mawasilianao ya karibu tu. Baada ya kufunga ndoa nilianza kuweka kadistance maana mazoea sana na waume za watu sio mazuri.
Kuna kipindi alikuwa na wazo fulani kuhusu biashara na alinishirikisha tukashauriana vizuri na biashara ikafunguliwa na ikawa ikienda vyema.
Alipenda kunipa updates za hiyo biashara, na baadae akamuachia mkewe(wifi) aiendeshe then akawa na wazo lingine la project nyingine kubwa zaidi ambayo ingekwenda vizuri alikuwa na plan ya kuacha kazi ya kuajiriwa na kuiendesha mwenyewe.
Kutokana na kunishirikisha kwa karibu sana mambo yake, nikagundua mazoea yanakolea zaidi, nikaanza kumpotezea nikitambua yeye mtu mzima ataelewa tu. Alianza kulalamika sana maana mara nyingi nilikuwa sipokei call zake wala kujibu text zake, ikabidi nimwambie tu ukweli kuwa nisingependa hayo mawasiliano ya karibu namna hiyo. Japo kwa uchungu alinielewa ila aliomba sana nisipoteze mawasiliano nae kabisa.
Baada ya kama mwezi hivi nilipokea simu kutoka kwa mkewe akilalamika sana na kunilaumu akihisi nina mahusiano na mumewe, ilibidi nimtulize munkari then tulonge taratibu kiutu uzima.
Alilalamika kuwa kuna mambo mengi ambayo emekuta ktk mawasiliano baina yangu na mumewe ambayo yeye binafsi hayajui na hajawahi kushirikishwa. Hapo sasa ndio ikabidi niongee nae na kumuuliza vizuri kuhusu mawasiliano baina yake na mumewe, nikagundua sio supportive kwa mumewe na huwa hayaamini mawazo ya mumewe.
Sasa nilichojifunza ni kwamba mwanaume anapenda sana kusikilizwa,kuheshimiwa na kuaminiwa. Anaweza akaja na wazo lake ambalo ukiliangalia harakaharaka unaona kabisa hapa hakuna kitu, sasa sisi wanawake huwa tuna tabia ya kuwakatisha tamaa, unaweza kuguna mguno classic au kucheka kabisa kwa dharau kumuonyesha kuwa wazo lake ni la hovyo kabisa, ilihali hata wazo mbadala pia hauna.
Mpe nafasi ya kumsikiliza, then kama atakuomba ushauri mpe kama hauna bora umshauri atafute ushauri pahali sahihi, mtie moyo na umuamini kuwa anaweza, hata kama alikuwa na hofu na wazo lake kwa kumtia moyo na kumuamini itampa ari ya kulifanyia kazi vizuri zaidi.
Wakati mwingine tunaweza kuwa tunazima ndoto za akina Mengi wengi tu bila kujua kuwa kwa support yetu wangefika mbali sana. Hata akishindwa kwa mara ya kwanza mtie moyo na mwambie ajaribu tena na tena na atafanikiwa. Sio ndio unaanza na maneno kama "nilijua tu usingefika kokote"!!
Kama ulimuamini na kumchagua yeye kati ya wengi,basi hauna budi kuyaamini mawazo yake pia. Kuwa msaidizi ambae kila wakati atajivunia kuwa nae, hata akikengeuka akikumbuka mazuri yako mengi hakika atajirudi tu.